Kitabu
Kitabu
القواعد الأربع
يهدف "متن القواعد الأربعة" للعلامة محمد بن عبد الوهاب إلى توضيح أربعة قواعد أساسية في فهم التوحيد والشرك.
NJIA ZENYE FAIDA KWA MAISHA YENYE FURAHA
Kitabu "Njia zenye Faida kwa Maisha yenye Furaha" cha Sheikh, mwanachuoni Abdur-Rahman bin Naasir As-Sa'adiy – Mwenyezi Mungu amrehemu – kinashughulikia sababu zinazopelekea furaha ya kweli kutoka katika mtazamo wa kiimani wa kina, na kinamwongoza msomaji kufikia utulivu wa moyo kupitia imani na matendo mema, kumtaja Mwenyezi Mungu, kuridhika, kutafakari neema zake, kufanya ihsani, kutegemea Mwenyezi Mungu, kuwa na subira, na kuyapima mambo ipasavyo; kwa mtindo mzuri unaoweka mbele yako ramani ya maisha yenye utulivu, yenye uwiano, na yenye furaha licha ya misukosuko ya maisha.
Misingi Mitatu na Ushahidi wake:
Kitabu hiki kinazungumzia mambo ya msingi ambayo yampasa Muislamu kujifunza: Kumjua Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuijua dini ya Uislamu, na kumjua Mtume Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake-, na kinaweka mkazo juu ya umuhimu wa mambo haya ya msingi katika kujenga imani na matendo mema kwa kutegemea ushahidi kutoka katika Qur'an tukufu na Sunna za Mtume.
MASOMO MUHIMU KWA UMMA WOTE
Kitabu cha “Masomo Muhimu Kwa Umma Wote” cha Sheikh Abdulaziz bin Baaz - Mwenyezi Mungu amrehemu - ni risala fupi yenye manufaa makubwa. Aliiandika imamu huyu ili iwe akiba ya kielimu kwa umma wote wa Waislamu. Amezungumzia ndani yake misingi ya Dini na nguzo zake, kuanzia kumpwekesha Mwenyezi Mungu, Imani na Uislamu, hadi hukumu za tahara na swala, adabu za Uislamu, na kueleza suala la kujitahadhari na ushirikina na maasi; kwa mbinu rahisi iliyo wazi, iliyojengeka juu ya Kitabu na Sunna; ili kuifanya itikadi ya Kiislamu na ibada sahihi viwe karibu na wazi kwa kila Muislamu.
DONDOO KUHUSU ITIKADI YA KIISLAMU
Kitabu hiki kinafafanua misingi ya imani inayojumuisha kumuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na mipango ya Mwenyezi Mungu ya heri yake na ya shari yake; na kinaonyesha kanuni za msingi zilizo wajibu kwa Muislamu kuziamini na kuzifanyia kazi, kikisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano na Mwenyezi Mungu kupitia kuielewa kwa kina itikadi ya Kiislamu.
Makala kuhusu damu za maumbile za wanawake
Kitabu “Risala kuhusu damu za maumbile za wanawake” cha Sheikh, mwanachuoni mkubwa, Muhammad bin Swaleh Al-Uthaimiin, Mwenyezi Mungu amrehemu, ni Makala ya kielimu iliyo thabiti iliyochunguza kwa utafiti na uhakiki wa damu za maumbile za wanawake: Hedhi, damu ya ugonjwa, na Nifasi, ikiegemea kwenye Qur’ani Tukufu na Sunna za Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ikiambatana na ufahamu makini wa kauli za wenye elimu katika masuala haya. Ndani yake zimebainishwa hukumu za damu hizo, zikifafanua kwa makini tofauti zilizopo kati ya hali mbalimbali, na ikitoa muongozo wa kisheria…
Itikadi sahihi na mambo yanayopingana nayo.
Mtunzi Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Utangulizi Kila sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu peke yake, na rehema na amani ziwe juu ya yule ambaye hakuna nabii atakayekuja baada yake, na ziwe juu ya watu wa familia yake na maswahaba wake.
كتاب التوحيد
Kitabu cha Tauheed {upwekeshaji} Ambayo ndiyo haki ya ALLAH juu ya waja Utunzi wa Shekh wa kiislam. MUHAMMAD IBN ABDUL WAHAAB ATTAMIIMY. 1206H Kimetiliwa umuhimu na.
آداب المشي إلى الصلاة
(Kitabu cha Adabu za kwenda katika Swala) Mtunzi: Sheikh Al- islaam na alama miongoni mwa alama, kiongozi aliyerudisha upya elimu ya dini, Sheikh Muhammad bin Abdulwahhab Allah Mtukufu amrehemu. Wamefanya kazi ya kusahihisha na kulinganisha Nakala iliyoandikwa kwa mkono katika Maktaba ya Saudia kwa namba 269/86 na nakala nyingine nyingi zimechapishwa na masheikh wafuatao: Abdul karim bin Muhammad Al-laahim. Naasir bin Abdillahi Al- Twariim, Suud bin Muhammad Al- bashar. Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu: (Mlango wa adabu za kwenda katika Swala) Ni Sunna kutoka…
الإمام محمد بن عبد الوهاب دعوته وسيرته
Imamu Muhammad Bin Abdul Wahaab ulinganizi wake na Historia yake. Utunzi wa Shekh Abdul Aziz Bin Abdillahi Bin Baaz Sifa zote njema anastahiki ALLAH Mola wa viumbe wote, sala na salam na baraka ziwe juu ya mja wake na Mtume wake mbora wa viumbe bwana wetu na kiongozi wetu Muhammad bin Abdillahi, na watu wake na Swahaba zake na wenye kufuata nyayo zao. Ama baada ya hayo: Enyi ndugu zangu watukufu, Enyi wanangu watukufu, muhadhara huu mfupi nauleta mbele yenu ili kuzinawirisha fikra, pamoja na kuweka wazi uhakika wa mambo, na kuwanasihi waja kwa ajili ya ALLAH, na kutekeleza baadhi ya mambo…
شروط الصلاة وأركانها وواجباتها
Sharti za swala na nguzo zake na wajibu wake Kimetungwa na Sheikhul Islam Al Mujaddid Imamu Muhammadi bin Abdil Wahhab -Mwenyezi Mungu amrehemu- Mwaka 1115-1206 H Amekihakiki na akashughulika nacho na akazichambua hadithi zake fakiri kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Dr. Saidi bin Ally bin Wahfu Al Qahtwaaniy Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema na Mwenye kurehemu.
فضل الإسلام
Ubora wa uislamu Imamu Muhammad Ibnu Abdil Wahaab. Mlango wa Ulazima wa Kuufuata Uislamu. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na Mwenye kutafuta dini isiyokuwa dini ya Kiislamu, ambayo ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kumpwekesha na kumfuata kwa kumtii na kumdhalilikia, na kwa Mtume wake aliye Nabii wa mwisho Muhammad, Rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa kumuamini na kumfuata na kumpenda kwa dhahiri na kwa siri, basi hiyo haitakubaliwa kwake, na yeye Akhera atakuwa ni miongoni mwa wenye kupata hasara ambao walizifanyia ubahili nafsi zao kwa kuzinyima mambo yenye…
الإسلام - نبذة موجزة عن الإسلام (مشتملة على الأدلة)
Uislamu Dondoo fupi kuhusu uislamu kama ilivyokuja katika Qur'an tukufu na mafundisho ya Mtume rehema na amani zimfikie. Ni kitabu muhimu kinachokusanya maana fupi ya uislamu kina bainisha misingi yake mafundisho yake, na mazuri yake kutoka katika vyanzo vyake asili navyo ni Qur'an tukufu na mafundisho ya Mtume, na kitabu kina wahusu watu wazima waislamu na wasiokuwa waislamu kwa lugha zao na katika kila zama na maeneo kwa kutofautiana mazingira na hali. (Nakala iliyokusanya ushahidi kutoka katika Qur'an tukufu na mafundisho matukufu ya Mtume -rehema na amani ziwe juu yake. 1- Uislamu ndio…
المختصر المفيد للمسلم الجديد
Muhutasari wenye faida kwa Muislamu mpya. Muandaaji Muhammad Al-shihriy 2020-1441 Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu Utangulizi
يومي الأول في الإسلام
SIKU YANGU YA KWANZA KATIKA UISLAMU Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu: Utangulizi Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyemtuma Nabii wake Muhammadi -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa ni huruma kwa walimwengu wote, na ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika wake, Mola mlezi wa mwanzo na wa mwisho, na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, ndiye wa mwisho katika manabii na Mitume, Rehema na Amani ziwe juu yake, na salamu nyingi mpaka siku ya kiyama, Ama baada ya hayo:…
المنتقى من المتجر الرابح في ثواب العمل الصالح - المعتمد
كتاب جامع لجملة من أحاديث النبي -صلى الله عليه وسلم- الصحيحية في ثواب الأعمال الصالحة كطلب العلم والطهارة والصلاة، وصلاة التطوع، والجمعة والجنائز، والصدقات والصوم والحج والجهاد، وقراءة القرآن، وذكر الرحمن وغيرها.
Imani aliyowafaradhishia Mwenyezi Mungu waja wake kutoka katika yale yaliyokuja katika Qur'ani Tukufu na Sunna za Mtume.
Hii ni ensaiklopidia inayojumuisha misingi yote na mambo muhimu ya itikadi na masuala yake. Ina sifa maalumu ya kufungamanisha masuala ya itikadi na Qur'ani Tukufu, na Sunna za Mtume zilizosafika, huku ikifanya juhudi kubwa katika kuweka msingi madhubuti wa itikadi kwa njia fupi na ya kujumuisha mambo yote, kwa kutumia maneno rahisi kueleweka wakati wa kubainisha na kuweka wazi masuala ya itikadi. Ensaiklopidia hii pia imesalimika kutokana na mijadala ya kimantiki na kifalsafa, na inalenga kubainisha maudhui mbalimbali ya itikadi kwa mbinu inayowezesha watu wa viwango vyote vya kielimu…
الأذكار التي تقال صباحًا ومساءً
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu adhkaari ambazo husemwa Asubuhi na Jioni. Mwenyezi Mungu hakuna mola isipokuwa Yeye,(na) ndiye Mwenye uhai wa maisha, Msimamia kila jambo, Kusinzia hakumshiki wala kulala. Ni Vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, Na nani huyo awezaye kuombea mbele Yake (Mungu) bila idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, hawalijui lolote katika elimu Yake (Mwenyezi Mungu) isipokuwa kwa alipendalo (Mwenyezi Mungu).Kiti chake cha Enzi kimeenea mbingu na na ardhi, wala kuvilinda hivyo hakumshindi, na Yeye (peke yake)…
من خلقني؟ ولماذا؟
Ni nani aliyeniumba? Na ni kwa nini aliniumba? Kila kitu kinaashiria kuwepo Muumba. Ni nani aliziumba mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake, miongoni mwa viumbe vikubwa ambavyo havijulikani ukubwa wake? Ni nani aliyetengeneza mpangilio huu mzuri zaidi katika mbingu na ardhi? Ni nani aliyemuumba mwanadamu kisha akampa usikivu, uoni na akili, na akamjalia uwezo wa kujifunza maarifa na kufahamu uhakika wa mambo? Vipi unafasiri uumbaji huu wa kiwango cha juu sana katika wa viungo vya mwili wako, na miili ya viumbe vilivyo hai? Na ni nani aliyeviumba kwa ustadi huu mkubwa? Ni namna gani…
الإسلام دين رسل الله
Uislamu ni dini ya Mitume wa Mwenyezi Mungu Uislamu ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu Muumba wa dunia na Mwenye kuiendesha dunia, na kujifungamanisha kwake kwa mapenzi na kumtukuza, na msingi wa Uislamu ni kumuamini Mwenyezi Mungu, na kuwa Yeye Mwenyezi Mungu ni Muumbaji, na kila kisichokuwa Mwenyezi Mungu kimeumbwa, na kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anastahiki kuabudiwa peke yake asiye na mshirika, hakuna wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, majina mazuri yote ni yake na sifa za juu zote ni zake, na ni Mwenye ukamilifu wa moja kwa moja bila ya upungufu, hakuzaa wala hakuzaliwa wala hakuna wa…
الإسلام دين رب العالمين
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu Uislamu ni Dini ya Mola Mlezi wa viumbe Nani Mola wako? Hili ni swali zito katika maswali yote: Nalo ni swali muhimu, ni lazima kwa kila mtu kufahamu majibu yake. Mola wetu Mlezi ni Yule aliyeziumba Mbingu na Ardhi, na akateremsha kutoka mawinguni maji kisha akaotesha kutokana na maji hayo matunda na miti ikiwa ni chakula kwetu sisi na kwa ajili ya wanyama tunaowatumia kama chakula, na ni Yeye ambaye amewaumba baba zetu, na akaumba kila kitu, na ni Yeye aliyeuweka usiku na mchana, na ni Yeye pia aliyeuweka usiku kuwa wakati wa kulala…
مقدمة وغلاف المنتقى من موسوعة الأحاديث النبوية
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu Utangulizi Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu, na rehema na amani zimfikie Nabii Muhammadi, na watu wake na Maswahaba zake wote, na wote watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya malipo, ama baada ya hayo: Hakika katika mambo anayotakiwa kuyapa kipaumbele muislamu ni kusoma kwa umakini na kuzingatia, nakutafuta elimu na kuifanyia kazi -hii iwe baada kujifunza kitabu cha Mwenyezi Mungu- yafuate mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake "Nimeacha kwenu…
الشهادتين
Utakapotaka kuingia katika Uislamu, ni wajibu kwako utamke Shahada ifuatayo kwa sauti yenye kusikika, na kufahamu maana yake na kuiamini: Ash-hadu an-laa ilaaha illa-llahu (Maneno haya yanamaanisha kuwa: Ninashuhudia (kwa moyo na kutamka kwa ulimi) kwamba hapana yeyote anayestahili kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake). Na ninashuhudia (kwa moyo na kutamka kwa ulimi) kwamba Muhammad ni mtume wa Mwenyezi Mungu, na Issa mwana wa Mariamu ni mja wa Mwenyezi Mungu na ni mtume wake. Ninashuhudia (kwa moyo na kutamka kwa ulimi) kwamba hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki…
NAMNA YA SWALA YA MTUME, REHEMA NA AMANI ZIWE JUU YAKE
Mheshimiwa, Sheikh, Abdulaziz bin Baaz - Mwenyezi Mungu amrehemu - ameeleza ndani ya kitabu cha "Namna ya Swala ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake", kwa ufupi namna ya swala ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, kwa mbinu rahisi na njia nzuri kabisa, huku akitegemea ushahidi wa kimaandiko yaliyo sahihi; ili kiwe muongozo kwa Muislamu katika swala yake. Alibainisha ndani yake nguzo za swala na sunna zake na namna yake, kuanzia wudhu mpaka kutoa salamu ya kumaliza swala, akikusanya ndani yake kati ya ushahidi na upambanuzi, akilingania watu kumuiga kikamilifu Mtume, rehema na amani ziwe…
UCHAMBUZI NA UFAFANUZI WA MASUALA MENGI YA HIJA, UMRA NA ZIARA KWA MUJIBU WA MUONGOZO WA QUR'ANI NA SUNNA
Kitabu kinafafanua hukumu za Hija, Umra na Ziara kwa mujibu wa Qur'ani na Sunna, na kinaeleza mambo ya wajibu katika Hija na Umra. Vile vile kinaeleza mambo yaliyokatazwa wakati wa Ihramu na adabu za kuutembelea Msikiti wa Mtume, huku kikihadharisha dhidi ya uzushi (Bid'aa) katika ibada hizi.
Adabu za safari na hukumu zake
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, na rehema na amani ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad, na watu wake na Maswahaba zake wote. Ama baada ya hayo: Hii ni makala fupi kuhusu adabu za safari na hukumu zake. Tumepupia ndani yake kuweka wazi mambo ambayo aghalabu anayahitajia msafiri. Na tunamuomba Mwenyezi Mungu aufanye ujumbe huu uwe kwa ajili ya kutafuta uso wake mtukufu, na awanufaishe kwao Waislamu wote. Kwanza: Adabu za safari
MUHTASARI WA NAMNA YA KUFANYA UMRAH NA HUKUMU ZAKE
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, na rehema na amani ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad, na watu wake na Maswahaba zake wote. Ama baada ya hayo: Hii ni makala fupi juu ya namna ya kufanya Umra, hukumu zake na adabu zake. Tumejitahidi kubainisha ndani yake mengi katika yale anayohitaji mtu anayefanya ‘Umra. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aifanye iwe kwa ajili ya uso wake mtukufu, na kwamba anufaishe kwayo Waislamu wote.
Wasia wangu
Kila sifa njema anazistahiki Mwenyezi Mungu, na rehema na amani ziwe juu ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na baada ya hayo: Mimi (............................................................) Mwenye namba ya kitambulisho cha uraia: Nimetoa Wasia huu nikiwa katika hali inayozingatiwa kisheria, kwanzia kuwa na akili timamu na uwezo wa kupambanua mambo, ya kwamba mimi ninashuhudia ya kuwa, hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake, asiye na mshirika, na kwamba Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, na kwamba Issa ni mja wa Mwenyezi Mungu na ni Mtume wake, na ni neno…
NAMNA YA KUFANYA UMRAH
Kijitabu "Namna ya kufanya Umrah" cha Sheikh, Abdulaziz bin Baaz, Mwenyezi Mungu amrehemu, kinaeleza ibada za Umrah kwa mtindo ulio wazi na unaoeleweka kwa urahisi; ili kitumike kama mwongozo wa kivitendo katika kusaidia Waislamu kutekeleza ibada zao za Hija au Umra kwa unyenyekevu na urahisi, kikiambatana na dua na nyiradi zilizopokelewa kutoka kwa Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, katika kila hatua.
MAKOSA YANAYOFANYIKA KATIKA HIJA, UMRAH NA KUTEMBELEA MSIKITI WA MTUME
Makosa na ukiukaji unaohusiana na Umra Kwanza: Ukiukaji wa watu na makosa yao katika Ihram 1. Kuacha kufanya ihlaal, kwa kutoinua juu sauti yake mwanzoni mwa kuhirimia ibada aliyokusudia sawa iwe Hija au Umra. Na Sunna: Ni kunyanyua sauti katika hilo.
FATWA ZA HIJA, UMRA NA KUTEMBELEA MSIKITI WA MTUME
Ambayo yalichaguliwa kutoka katika Mkusanyiko wa Fatwa za Kamati ya Kudumu ya Fatwa katika Ufalme wa Saudi Arabia, huku maswali yakiwa yamefupishwa ili kuendana na kila hali. Kwanza: Majibu (Fatwa) ya kiujumla Swali: Je, inaruhusiwa kwa baba yangu kufanya Umra kwa pesa alizokopa benki? Jibu: Ni lazima kwa anayetaka kuhiji au kufanya Umra kwa niaba yake au kwa niaba ya mtu mwingine achague pesa nzuri kwa ajili ya matumizi katika Hija yake na Umra. Kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mzuri na hakubali isipokuwa yaliyo mazuri tu.
Muhtasari wa namna ya kufanya Hija
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, na rehema na amani ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad, na aali zake na Maswahaba zake wote. Ama baada ya hayo: Hii ni Makala fupi katika namna ya kufanya Hija, tumefanya hima kubwa katika kubainisha mambo mengi ya msingi anayoyahitaji Mwenye kuhiji. Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye ninayemuomba aifanya kazi hii iwe ni kwa ajili ya uso wake mtukufu, na awanufaishe kwayo Waislmu wote. Utangulizi
Miongoni mwa alama za Tauhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu)
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, na mwisho mwema ni wa wachamungu. Na ninashuhudia kwamba hakuna mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu peke yake, asiye na mshirika, na ninashuhudia kwamba Muhammad ni mja wake na Mtume wake. Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na jamaa zake na Maswahaba wake. Ama baada ya hayo: Hakika, Tauhidi ndiyo mwanzo na mwisho wa Dini, na ndiyo ndani yake na nje yake. Nayo ndiyo (Daa'wa) wito wa kwanza na wa mwisho wa Mitume. Nayo ndiyo maana ya…
HUKUMU ZA AL-HADYU, AL-ADHWAHI NA NAMNA YA KUCHINJA.
Hukumu za Al-hadyu (wanyama wachinjwao kama zawadi ya Msikiti Mtukufu wa Makka) na Al-adhwahi (wanyama wachinjwao siku ya Idi) na Namna ya Kuchinja. Huu ni Ujumbe mfupi uliokusanya mambo muhimu zaidi kwa Muislamu katika hukumu za wanyama wachinjwao kama sadaka, na vichinjwa vya siku ya Idi; ili Muislamu awe na elimu na uelewa wa wazi kuhusu mambo ya dini yake.
Nani aliyeumba Dunia? na ni nani aliyeniumba? na kwa ajili gani?
Kitabu "Nani aliyeumba Dunia? na ni nani aliyeniumba, na kwa ajili gani? kinajadili asili ya uwepo wa Dunia na Mwanadam, kwa kutilia mkazo kuwa Dunia haijaja kwa kuzuka na kwa kuja bila uwepo wa aliyeileta, isipokuwa inamuumbaji aliye mkubwa ambaye ni Allah, ambaye ameweka kanuni za ndani zaidi zinazoongoza maisha na dunia, kitabu kinaweka wazi sifa za Allah na umuhimu wa kuamini mitume na vitabu vya mbinguni, na kinahimiza kuwa Uislamu ni dini ya kweli ambayo imekusanya ujumbe wa mitume, kinawaita watu katika imani na kwa ajili ya kuhakikisha utukufu wa kweli duniani na akhera.
Mimi ni Muislamu
Makala hii imebainisha maana ya Uislamu, na ni nani Muislamu, na vipi utakuwa Muislamu wa kweli, kama ilivyosheheni kwa kutaja uzuri wa Uislamu na baadhi ya adabu na tabia za hali ya juu, na nafasi ya mwanamke, na haki za ndugu wa karibu na jirani na jamii, inabainisha kuwa Uislamu unaamrisha na unaita watu kwenye kila jambo zuri, na haukatazi isipokuwa kila kilicho kibaya.
KUZURU PANGO LA HIRAA
Kitabu cha Kuzuru Pango la Hiraa, kinazungumzia mahali hapa ambapo ndipo mahali pa mwanzo wa Ujumbe wa Utume na mahali pa mwanzo pa kuteremkia aya za mwanzo za Qur'ani tukufu, na kinatanabahisha kuwa ibada zilizofanywa kuwa katika sheria huwa kule Makka katika Msikiti Mtukufu pekee na maeneo matakatifu yaliyotengwa kwa ajili ya Hija, na kinapinga kila uzushi wa kutaka kuokolewa na kutaka baraka kutoka katika maeneo au vitu visivyokuwa vya kisheria, kama vile Pango la Hiraa. Vile vile, kinatahadharisha dhidi ya kwenda kinyume na sunna ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, na kinawaita watu…
Mtume wa Uislamu, Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake
Kitabu "Mtume wa Uislamuz Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake" kinaweka wazi maisha ya Nabii Muhammad kuanzia kwenye nasaba yake na kuoa kwake kulikobarikiwa mpaka kuanza kuteremka kwa ufunuo na kuanza kwa utume wake ambao ndio wa mwisho, na kinabainisha alama za unabii wake na alama za ukweli wake, na kinaweka wazi sheria aliyokuja nayo na nafasi yake katika kuhifadhi haki za mwanadamu na heshima yake, kama ambavyo kinaweka wazi misimamo ya mahasimu wake na kutoa kwao ushahidi wa kumuunga mkono, pamoja na kutia mwangaza juu ya tabia zake nzuri ambazo sheria imeziweka kuwa ni kiigizo kwa…
Ufafanuzi wa matamshi ya Adhana
Kitabu cha Ufafanuzi wa Matamshi ya Adhana kinashughulikia maneno ya adhana na kuyafafanua kwa ufafanuzi wa kiimani, kikidhihirisha vipengele vyake vya kiitikadi na kimalezi, na kubainisha kuwa Adhana si wito tu wa swala, bali ni wito wa kila siku wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu na mafanikio. Kinachambua maneno ya Adhana na kufafanua maana zake kwa kina, kuanzia kumtukuza Mwenyezi Mungu, shahada ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na suala la Utume, hadi wito kwa ajili ya swala na mafanikio, na kuhitimishwa kwa kumtukuza Mwenyezi Mungu na kumpwekesha. Hayo yote kwa mtindo wenye kugusa nyoyo,…