ستون سؤالا في أحكام الحيض والنفاس
*
These files are generated automatically from the book's text; their layout may differ from the printed edition.
*
*
Swali la 1:
Jawabu la 1:
Swali la 2:
Jawabu la 2:
Swali la 3:
Jawabu la 3:
Swali la 4:
Jawabu la 4:
Swali la 5:
Jawabu la 5:
Swali la 6:
Jawabu la 6:
Swali la 7:
Jawabu la 7:
Swali la 8:
Jawabu la 8:
Swali la 9:
Jawabu la 9:
Swali la 10:
Jawabu la 10:
Swali la 11:
Jawabu la 11:
Swali la 12:
Jawabu la 12:
Swali la 13:
Jawabu la 13:
Swali la 14:
Jawabu la 14:
Swali la 15:
Jawabu la 15:
Swali la 16:
Jawabu la 16:
Swali la 17:
Jawabu la 17:
Swali la 18:
Jawabu la 18:
Swali la 19:
Jawabu la 19:
Swali la 20:
Jawabu la 20:
Swali la 21:
Jawabu la 21:
Swala la 22:
Jawabu la 22:
Swali la 23:
Jawabu la 23:
Swali la 24:
Jawabu la 24:
Swali la 25:
Jawabu la 25:
Swali la 26:
Jawabu la 26:
Swali la 27:
Jawabu la 27.
Swali la 28:
Jawabu la 28:
Swali la 29:
Jawabu la 29.
Swali la 30:
Jawabu la 30:
Swali la 31:
Jawabu la 31:
swali la 32:
jawabu la 32:
swali la 33:
Jawabu la 33:
swali la 34:
Jawabu la swali la 34:
Swali la 35:
Jawabu la swali la 35:
Swali la 36:
Jawabu la 36:
Swali la 37:
Jawabu la 37:
Swali la 38:
Jawabu la 38:
Swali la 39:
Jawabu la 39:
Swali la 40:
Jawabu la 40:
Swali la 41:
Jawabu la 41:
Swali la 42:
Jawabu la 42:
Swali la 43:
Jawabu la 43:
Swali la 44:
Jawabu la 44:
Swali la 45:
Swali la 45:
Swali la 46:
Jawabu la 46:
Swali la 47:
Jawabu la 47
Kwa sababu Mtume- rehema na amani ziwe juu yake- alimuamrisha Asmaa bint Umeisi, mke wa Abubakari -radhi za Allah ziwe juu yao- pindi alipopata damu ya nifasi katika eneo la Dhul-Hulaifa, akamuamrisha akoge na aweke nguo sehemu inayotoka damu, na ahirimie, na hivi pia anafanya mwanamke mwenye hedhi, anabakia katika ibada yake aliyohirimia mpaka atwaharike, kisha azunguke nyumba ya Allah na azunguke Swafa na Marwa.
Swali la 48:
Jawabu la 48:
Swali la 49:
Jawabu la 49:
Swali la 50:
Jawabu la 50:
Swali la 51:
Jawabu la 51:
Swali la 52:
Jawabu la 52:
Swali la 53:
Jawabu la 53:
Swali la 54:
Jawabu la 54:
Swali la 55:
Jawabu la 55:
Swali la 56:
Jawabu la 56:
Swali la 57:
Jawabu la 57:
Swali la 58:
Jawabu la 58:
Swali la 59:
Jawabu la 59:
Swali la 60:
Jawabu la 60:
kwa sababu Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alimkataza mwenye hedhi kuzunguka Kaaba, na mwanamke mwenye nifasi ni sawa na mwanamke mwenye hedhi.
Neno "Khumra" lililotumika katika hadithi: Ni Mswala unaotumika kuswalia. Na Mswala huo umeitwa hivyo kwa sababu unafunika uso.
MASWALI SITINI KATIKA HUKUMU ZA HEDHI NA NIFASI
*
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.
UTANGULIZI:
Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimuendee Mtume wa Allah, Muhammad bin Abdillah na wafuasi wake na maswahaba wake na kila atakayepita katika njia yake mpaka siku ya malipo, baada ya hayo:
Dada yangu Muislam!
Kutokana na maswali mengi ambayo wanaulizwa wanachuoni kuhusiana na hukumu za hedhi katika ibada, tukaona tuyakusanye maswali yote yanayojirudia mara nyingi, na mara nyingi yanatokea bila kurefusha, na hilo ni katika kutaka kufupisha.
Dada yangu Muislamu!
Jitihada zetu za kuyakusanya maswali haya, ni ili yawe mikononi mwako daima, hilo linatokana na umuhimu wa utambuzi wa sheria ya Allah, ili uweze kumuabudu Allah kwa ujuzi na maarifa.
Angalizo: Inaweza kuonekana kuwa baadhi ya maswali yemejirudia kwa yule atakayekipitia kitabu hiki kwa mara ya kwanza, lakini baada ya mazingatio ataona katika maswali hayo kuna ziada ya elimu katika jibu moja ziada ambayo haipatikani katika jibu lingine, tukaona tusiyaache maswali hayo.
Kwa utangulizi huu: Tunaomba -Rehema na amani ziwe juu- ya Muhammad na wafuasi wake wote na Maswahaba wake wote.
MIONGONI MWA HUKUMU ZA HEDHI KATIKA SWALA NA SWAUMU:
Akitwaharika mwanamke baada ya swala ya Alfajiri, je ajizuie na afunge swaumu siku hiyo?, na je siku hiyo itahesabika kwake kuwa kafunga au atatakiwa kuilipa siku hiyo?
Akitwaharika mwanamke baada ya kuchomoza Alfajiri, wanachuoni wana kauli mbili juu ya mwanamke huyu katika kujizuia kula na kunywa na tendo la ndoa mchana wa siku hiyo.
Kauli ya kwanza: Atalazimika kujizuia kula, kunywa, na tendo la ndoa katika masaa yaliyobakia kwa siku hiyo, lakini haitohesabika kwake siku hiyo, bali atawajibika kuilipa, na hii ndio kauli ya wanachuoni wengi katika madhehebu ya Imam Ahmad -Allah amrehemu-
Kauli ya pili: Hatolazimika kujizuia kula, kunywa, na tendo la ndoa mchana wa siku hiyo, kwa sababu haikubaliki funga kwa siku hiyo, kwa sababu mwanzo wa siku alikuwa kwenye hedhi, na aliye katika hedhi hafai kufunga, na kwakuwa swaumu yake si sahihi, basi hakuna faida ya kujizuia kula, kunywa, na tendo la ndoa, na wakati wa siku hiyo si wakati wa kuheshimiwa kwa upande wake, kwa sababu ameamrishwa kula mwanzo wa mchana, bali ni haramu kwake kufunga mwanzo wa mchana, Na swaumu ya kisheria: Ni kujizuia na vyote vyenye kufunguza kwa lengo la kumwabudu Allah toka kuchomoza Alfajiri mpaka kuzama kwa jua.
Na kauli hii -kama unavyoiona- ina nguvu zaidi kuliko kauli ya kwanza ya kujizuia, lakini kwa kauli zote hizi mbili itamlazimu kulipa siku hii.
Atakapotwaharika aliyekuwa na hedhi, na akaoga josho kubwa baada ya swala ya Alfajiri, na akaswali, na akaikamilisha swaumu ya siku yake ile, je anawajibika kulipa siku hiyo?
Atakapo twaharika Mwanamke aliyekuwa katika hedhi kabla ya kuchomoza Alfajiri hata kwa dakika moja, lakini akapata yakini kuwa ametwaharika, ikiwa ni katika Ramadhani basi atalazimika kufunga, na inakuwa funga yake siku hiyo ni sahihi, na wala halazimiki kuilipa siku hiyo, kwa sababu amefunga akiwa ametwaharika, hata kama hakuoga josho kubwa ila baada ya Alfajiri basi hakuna tatizo. Kama vile Mwanaume akiwa katika janaba lililotokana na tendo la ndoa au kujiotea, na akala daku na wala hakuoga janaba ila baada ya Alfajiri, funga yake itakuwa sahihi.
Kwa mujibu wa hili, napenda kutoa angalizo la jambo lingine kwa wanawake, pindi mwanamke atakapo ijiwa na hedhi, na alikuwa kafunga siku hiyo, baadhi ya wanawake hudhania kwamba hedhi itakapowajia baada ya kufungua kabla ya kuswali swala ya Ishaa funga yao ya siku hiyo inakuwa imeharibika, jambo hilo halina dalili katika sheria, bali hedhi itakapomuijia mwanamke baada ya Magharibi walau kwa muda mchache basi funga yake inakuwa imetimia na ni sahihi.
Je ni lazima kwa wanawake wenye Nifasi kuswali na kufunga wakitwaharika kabla ya siku arobaini?
Naam; muda wowote atakapotwaharika mwanamke mwenye nifasi kabla ya siku arobaini basi ni lazima juu yake kufunga ikiwa ni ndani ya mwezi wa Ramadhani, ni lazima juu yake kuswali, na inafaa kwa mume wake kumuingilia; kwa sababu yuko twahara, hakuna kitu kinachomzuia kufunga na hakuna kinachomzuia kuswali wala kufanya tendo la ndoa.
Ikiwa mzunguko wa mwezi wa mwanamke ni siku nane au siku saba, kisha mzunguko wake ukaendelea mara moja au mara nyingine zaidi ya siku hizo, ni ipi hukumu yake?
Ikiwa mzunguko wa mwanamke huyu ni siku sita au saba, kisha muda wa kuwa na damu ukarefuka, ukawa siku nane, au saba, au kumi, au kumi na moja, basi hatoswali mwanamke huyu mpaka atwaharike, Na hilo ni kwa sababu Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- hakuweka ukomo maalumu wa siku za mzunguko wa hedhi. Na amesema Allah Mtukufu: "Na wanakuuliza kuhusu hedhi, sema: Huo ni uchafu" [Al-baqara: 222], Muda wowote damu hii ikiwepo basi mwanamke atabaki katika hali hiyo mpaka atwaharike, na aoge josho kubwa, kisha aswali, na ukija mwezi wa pili siku zimepungua ukilinganisha na mwezi wa kwanza, basi akitwaharika ataoga hata kama mwezi huu haukuwa kama ule uliopita.
Na jambo la msingi nikuwa; Muda wowote mwanamke akiwa katika mzunguko wa hedhi basi hatoswali, uwe mzunguko huo una siku kama mzunguko uliopita, au zimezidi au zimepungua, atakapotwaharika ataswali.
Je mwanamke mwenye nifasi anakaa siku arobaini haswali na hafungi, au kinachozingatiwa ni kukatika ile damu, muda wowote ikikatika anakuwa katwaharika na ataswali, na ni upi muda mchache wa kutwaharika?
Damu ya uzazi haina wakati maalumu, muda wowote damu ikiwepo atakaa, hatoswali, hatofunga, na hatoingiliwa na mumewe.
Na pindi akiona katwaharika -hata kabla ya siku arobaini, hata kama hakukaa isipokuwa siku kumi au tano- basi ataswali, atafunga, na ataingiliwa na mumewe, wala hakuna tatizo katika hilo.
Na jambo la msingi nikuwa; Nifasi ni jambo linahisika, linafungamana na hukumu za kisheria kwa kuwepo kwake na kutokuwepo kwake, muda wowote ikiwepo basi zinathibiti hukumu zake, na muda wowote akitwaharika basi hukumu za nifasi hatohusika nazo.
Lakini lau zikizidi zaidi ya siku sitini basi damu hiyo itakuwa ni damu ya ugonjwa, atakaa muda ule ambao unawafikiana na muda wake wa hedhi pekee, kisha ataoga, na ataswali.
Litakapodondoka tone dogo la damu ya hedhi mchana wa Ramadhani, na ikaendelea damu hii kumtoka mwanamke ndani ya mwezi wa Ramadhani naye anafunga, je funga yake ni sahihi?
Ndio, swaumu yake ni sahihi, ama haya matone si chochote, yanatokana na mishipa ya damu, imepokewa kutoka kwa Ally bin Abi twalib -Allah amridhie- amesema: "Hakika matone haya ambayo yanakuwa mithili ya damu inayotoka puani si hedhi" hivyo ndivyo alivyosema radhi za Allah ziwe juu yake.
Mwanamke mwenye hedhi au nifasi akitwaharika kabla ya Alfajiri, je swaumu yake iko sahihi au la?
Naam, iko sahihi swaumu ya mwanamke mwenye hedhi atakapotwaharika kabla ya Alfajiri, na hakuoga josho kubwa la kujitwaharisha isipokuwa baada ya Alfajiri, na hukumu hii ni pamoja na wanawake walio katika nifasi, kwa sababu kwa wakati huo ni katika watu wanaotakiwa kufunga, na huu ni mfano wa aliyepatwa na janaba, na ikachomoza Alfajiri akiwa na janaba, swaumu yake ni sahihi; Kutokana na kauli yake Allah -Mtukufu-: "Na sasa hivi waingilieni na tafuteni yale aliyowaandikieni Allah kwa ajili yenu, na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu nyinyi weupe wa Alfajiri ya kweli itokanayo na giza la usiku" (Al baqara: 187) Na akiruhusu Allah kumuingilia mwanamke mpaka ibainike Alfajiri ya kweli basi inamlazimu katika hilo kusiwe na kuoga josho kubwa isipokuwa baada ya kuchomoza Alfajiri, kutokana na hadithi ya Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akiamka asubuhi akiwa na janaba kutokana na kumuingilia mkewe naye akiwa katika swaumu. Yaani: Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa haogi janaba isipokuwa baada ya kuchomoza Alfajiri.
Mwanamke akihisi damu ya hedhi, na damu hiyo haikutoka kabla ya Magharibi, au akahisi maumivu ya mzunguko wake, je inafaa swaumu yake siku hiyo, au ni wajibu kwake kuilipa?
Pindi akihisi mwanamke aliyetwaharika kuja kwa damu ya hedhi akiwa amefunga, lakini haikutoka mpaka baada ya kuzama kwa jua, au alihisi maumivu kwa sababu ya hedhi, lakini haikutoka isipokuwa baada ya kuzama kwa jua, basi swaumu yake siku hiyo ni sahihi, hatoirudia swaumu ile ikiwa ni swaumu ya lazima, na wala haziharibiki thawabu zake kwa hilo ikiwa ni swaumu ya sunna.
Pindi mwanamke atakapoona damu, na hakuwa na uhakika kama ni damu ya hedhi, je ni ipi hukumu ya swaumu yake siku hiyo?
Swaumu yake siku hiyo ni sahihi; Kwa sababu asili ni kutokuwa na hedhi mpaka ibainike kwake kwamba ile ni hedhi.
Baadhi ya wakati, mwanamke anaona athari ya damu chache ikiwa katika hali ya matone yakimtoka katika nyakati tofauti tofauti ndani ya siku moja, baadhi ya wakati anaziona wakati wa mzunguko wake wa kisheria na mzunguko ukiwa bado haujamtoka, na mara nyingine anaziona wakati ambao sio wa mzunguko wake, ni ipi hukumu ya swaumu yake katika hali hizo mbili.
Limetangulia jawabu linalofanana na swali hili muda si mrefu lakini kilichobaki nikuwa ikiwa matone haya yanatokea katika siku za mzunguko yatazingatiwa kama ni hedhi ambayo unaijua, na itakuwa ni hedhi.
Je mwanamke aliye katika mzunguko wa hedhi na nifasi anakula na kunywa mchana wa Ramadhani?
Ndio, wanakula na kunywa katika mchana wa Ramadhani, lakini bora ikawa kula huko ni kwa siri ikiwa ana watoto ndani ya nyumba kwa sababu jambo hilo huleta tatizo kwa watoto wakiona mtu anakula mchana wa Ramadhani.
Akitwaharika mwenye hedhi au nifasi muda wa Alasiri, je analazimika kuswali swala ya Adhuhuri na Alasiri, au halazimiki kuswali isipokuwa Alasiri peke yake?
Kauli yenye kutegemewa katika swala hili nikuwa: Analazimika kuswali swala ya Alasiri pekee kwa sababu hakuna dalili juu ya ulazima kwake kuswali Adhuhuri, na asili ni kutokuwa na dhima ya jambo na Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeupata wakati wa swala ya Alasiri kwa kiwango cha rakaa moja kabla jua halijazama basi ameipata Lasiri", Na hakutaja kwamba amediriki Adhuhuri, ingekuwa swala ya Adhuhuri ni lazima kwa mtu huyu basi angebainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- na mwanamke akitokwa na damu ya hedhi, baada ya kuingia wakati wa Adhuhuri basi haimlazimu akitwaharika kulipa isipokuwa swala ya Adhuhuri pekee na hatolipa Alasiri pamoja na kwamba swala ya Adhuhuri hujumuishwa na swala ya Alasiri na wala hakuna tofauti kati yake na sura iliyoulizwa katika swali.
Na kuhusu suala hili, kauli ya kutegemewa nikwamba halazimiki isipokuwa swala ya Alasiri pekee kutokana na dalili ya kisheria na kiyasi (Kuoanisha mambo), na hivyo hivyo ikiwa ametwaharika kabla ya kutoka wakati wa swala ya Ishaa, basi halazimiki isipokuwa kuswali swala ya Ishaa peke yake, wala halazimiki kuswali swala ya Magharibi.
Baadhi ya wanawake ambao huporomosha ujauzito, hali zao huwa katika moja kati ya hizi: Ujauzito ukitoka kabla mtoto hajaumbwa tumboni, au mimba ikatoka baada ya kuumbwa kiumbe na ukadhihiri muundo wa umbile lake, ni ipi hukumu ya swaumu siku hiyo ambayo katokwa na mimba ile, na swaumu za siku ambazo ataiona damu inatoka?
Ikiwa mtoto hajaumbika tumboni basi damu itakayomtoka si damu ya uzazi, na juu ya hili basi atafunga na kuswali na swaumu yake ni sahihi.
Na ikiwa mtoto ameumbika basi damu itakayomtoka ni damu ya nifasi, haifai kwake kuswali katika hali hiyo, wala haruhusiwi kufunga swaumu.
Na kanuni na kigezo katika swala hili ni kuwa; Ikiwa mtoto ameumbika basi damu itakayomtoka ni damu ya uzazi (nifasi), na ikiwa hajaumbika basi damu itakayomtoka siyo damu ya nifasi, na ikiwa damu itakayomtoka ni damu ya uzazi (nifasi) haitofaa kwake yote yale yasiyofaa kwa wanawake wanaotokwa na damu ya uzazi (nifasi) na ikiwa si damu ya uzazi (nifasi) basi hatoharamishiwa juu yake anayoharamishiwa mwanamke mwenye nifasi.
Mwanamke mjamzito akitokwa na damu mchana wa Ramadhani, je jambo hili lita athiri swaumu yake?
Itakapotoka damu ya hedhi na mwanamke akiwa amefunga basi funga yake itaharibika, kutokana na kauli ya Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hivi haikuwa wakati alipokuwa katika mzunguko wake wa hedhi haswali wala hafungi?" Na kwa ajili hii tunazingatia hili ni katika mambo yanayofunguza swaumu, na damu ya uzazi ni mfano wake, na kutoka damu ya hedhi na nifasi vinaharibu funga ya mtu.
Na mwanamke mjamzito akitokwa na damu mchana wa Ramadhani basi ikiwa ni hedhi basi hiyo ni hedhi kama ilivyo hedhi ya mwanamke asiye mjamzito, na inaathiri swaumu yake, na ikiwa siyo hedhi basi haiathiri funga yake.
Na damu ya hedhi ambayo inaweza mtokea mwanamke mwenye mimba ni damu ya hedhi ambayo haikatiki kwake tangu kubeba ujauzito huo, bali inamjia katika zile nyakati zake alizozizoea kuwa damu ya hedhi humuijia, basi hedhi hii kwa kauli yenye kutegemewa inathibiti kwake na inachukua hukumu za hedhi ya kawaida.
Ama ikikatika damu hiyo ya hedhi naye bado mjamzito, kisha ikawa baada ya hapo anaona damu katika wakati ambao siyo wa mzunguko wake wa kisheria, hili haliathiri funga yake, kwa sababu hii si hedhi.
Ikiwa mwanamke anaona damu siku moja akiwa katika mzunguko wake, na siku inayofuata haoni damu mchana kutwa, ni kipi juu yake anatakiwa kufanya?
Linalo onekana ni kwamba, hii twahara au ukavu (katika sehemu za siri) uliopatikana wakati wa siku zake za hedhi, utafuata (hukumu za) hedhi, hautohesabika kama ni twahara, pamoja na hilo ataendelea kujizuia kwa yale anayojizuia kwayo mwanamke aliye katika hedhi.
Na wamesema baadhi ya wanachuoni: Mwanamke mwenye kuona damu siku moja, na siku nyingine akaona yuko twahara, basi ile damu (aliyoiona) ni hedhi, na ule usafi (aliouona) ni twahara mpaka zifike siku kumi na tano. Na ikifika siku ya kumi na tano, inakuwa damu itokayo baada ya hapo ni damu ya ugonjwa (Istihadhwa). Na hili ndilo limetajwa kuwa ni sahihi na wanachuoni wengi katika madhehebu ya Imam Ahmad ibn Hanbali (Allah amrehemu).
Katika siku za mwisho za hedhi au kabla ya kutwaharika, mwanamke ikiwa haoni athari ya damu ya hedhi, je anaruhusiwa kufunga siku hiyo? Ikiwa haoni maji maji meupe yakitoka katika tupu yake, au afanye nini?
Ikiwa ni kawaida ya mwanamke, haoni maji maji meupe kama ilivyo kwa baadhi ya wanawake basi mwanamke huyu atafunga swaumu yake, na ikiwa kawaida yake anaona maji maji meupe, basi hatofunga mpaka aone maji maji hayo yamekatika.
Ni ipi hukumu ya mwanamke mwenye hedhi na anayetokwa damu ya uzazi (Nifasi) kusoma Qur'ani akiwa anatizama au kile alichohifadhi katika hali ya dharura, mfano yeye ni mwanafunzi au ni mwalimu?.
Hakuna tatizo kwa mwanamke aliye katika hedhi au damu ya uzazi (Nifasi) kusoma Qur'ani ikiwa ni kwa hitajio, kama vile mwalimu wa kike, au mwanafunzi wa kike ambaye anasoma uradi wake (kiwango anachohitaji kusoma katika Qur'ani) usiku au mchana.
Ama kisomo -Namaanisha: Kusoma Qur'ani kwa ajili ya kutafuta ujira na thawabu za kisomo -jambo bora asisome; kwa sababu wanachuoni wengi au wengi wao wanaona kwamba mwanamke aliye katika hedhi haifai kwake kusoma Qur'ani.
Je analazimika mwanamke aliye katika hedhi kubadili nguo zake baada ya kutwaharika, pamoja na kuwa nguo hizo hazikudondokewa na damu yoyote wala uchafu wowote?.
Haimlazimu yeye kufanya hivyo, kwa sababu hedhi haichafui (hainajisi) mwili, bali damu ya hedhi inachafua inachokutana nacho pekee na kwa hili Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- aliamrisha wanawake pindi zinapogusa damu za hedhi nguo zao wasafishe pale palipopatwa na damu kisha waswalie nguo zao.
Mwanamke amefungua katika mwezi wa Ramadhani siku saba, alikuwa akitokwa damu ya uzazi, na hakulipa siku hizi mpaka akajiwa na Ramadhani ya pili, na akazungukiwa katika Ramadhani ya pili na siku saba ambazo alikuwa ananyonyesha (hakufunga) kwa hoja alikuwa na maradhi, na imekaribia kuingia Ramdhani ya tatu, tupeni faida, Allah awalipeni thawabu.
Ama akiwa mwanamke huyu kama alivyojieleza -kuwa yeye ni mgonjwa na wala hawezi kulipa-, basi wakati wowote akiweza kulipa basi na afunge; kwa sababu yeye ana udhuru hata kama ikija Ramadhani ya pili.
Ama ikiwa mwanamke huyu hana udhuru wowote ule, alikuwa akijifanya mgonjwa na anafanya uzembe, huyu hairuhusiwi kwake kuchelewesha kulipa Ramadhani mpaka Ramadhani ya pili. Amesema Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nikidaiwa swaumu ambayo natakiwa kulipa, basi siwezi kuilipa isipokuwa katika mwezi wa Shaaban.
Na kwa namna hiyo, ni juu ya mwanamke huyu ajitazame mwenyewe, ikiwa hana udhuru basi anapata dhambi, na juu yake kutubia kwa Allah, na apupie kulipa swaumu zilizo juu yake, ikiwa ana udhuru hakuna shida juu yake, hata kama ikichelewa mwaka au miaka miwili.
Baadhi ya wanawake wanaingiwa na Ramadhani ya pili wakiwa hawajafunga baadhi ya siku katika Ramadhani iliyopita, ni lipi jambo la lazima juu yao kufanya?.
Jambo la lazima juu yao: Kutubia kwa Allah juu ya jambo hili; kwa sababu haifai kwa mwenye deni la swaumu za Ramadhani akachelewesha mpaka Ramadhani ya pili bila udhuru; kutokana na kauli ya Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake-: "Ilikuwa ninakuwa na deni la swaumu natakiwa kulipa, basi siwezi kuzilipa isipokuwa katika mwezi wa Shaaban".
Na hii inaonyesha ya kwamba haiwezekani kuchelewesha kulipa mpaka Ramadhani ya pili, ni juu yake atubie kwa Allah -Mshindi Aliyetukuka- kwa yale aliyoyafanya, na alipe siku alizoziacha baada ya Ramadhani ya pili.
Mwanamke atakapotokwa na damu ya hedhi Adhuhuri, akiwa hajaswali swala ya Adhuhuri, je analazimika kuilipa swala ile baada ya kutwaharika?
Katika hili kuna tofauti baina ya wanachuoni, wapo wanaosema haimlazimu mwanamke huyu kuilipa swala hii, kwa sababu hakufanya uzembe na wala hatopata dhambi; na kwakuwa anaruhusiwa kuichelewesha swala mpaka ukikaribia mwisho wa wakati wa swala.
Wengine wanasema: Analazimika kuilipa, namaanisha kuilipa swala ile iliyompita kabla ya hedhi kutoka, kutokana na ujumla wa maneno ya Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakaye idiriki rakaa katika swala basi amediriki swala"
Na kwa kujiepusha kuingia katika madhambi: Bora ailipe, maana ni swala moja, hakuna ugumu katika kuilipa.
Atakapoona mjamzito damu kabla ya kujifungua kwa siku moja au siku mbili, je ataacha kufunga na kuswali kwa ajili ya damu hiyo au lipi afanye?
Mjamzito atakapoiona damu siku moja au siku mbili kabla ya kujifungua, huku akiwa na uchungu wa kujifungua, basi damu hiyo ni damu ya uzazi (Nifasi), kwa ajili ya damu hiyo hatoswali na wala hatofunga, isipoambatana damu hiyo na uchungu wa kujifungua, basi damu hiyo iliyoharibika haizingatiwi, na wala haimzuii mwanamke kufunga wala kuswali.
Ni yapi maoni yako kuhusu kumeza vidonge vya kuzuia mzunguko wa mwezi wa damu ya hedhi kwa ajili ya kufunga pamoja na watu?
Mimi ninatahadharisha kuhusu hilo, na hilo ni kwa sababu vidonge hivi vina madhara makubwa, limethibiti hilo kwangu kupitia madakatari, na anaambiwa mwanamke: Jambo hilo ameliandika Allah kwa mabinti wa Adam, basi tosheka kwa lile alilokuandikia Allah Mtukufu, na ufunge siku ambazo hakuna kizuizi, kitakapo patikana kizuizi basi fungua kwa kuridhia yale ambayo Allah Mtukufu amekadiria.
Mwanamke baada ya miezi miwili tangu kukatika kwa damu ya uzazi (Nifasi), akaanza kuona vitone vidogo vya damu, je atafungua, na wala hatoswali? au ni kipi atafanya?.
Matatizo ya wanawake katika damu ya hedhi na damu ya uzazi (Nifasi) ni bahari isiyo na ufukwe, na katika sababu za matatizo hayo: Matumizi ya vidonge vya kuzuia mimba au kuzuia damu ya hedhi, na zamani watu hawakuwa wakijua matatizo haya mengi, Sahihi, haya matatizo yalikuwepo tangu alipopewa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Utume, bali yalikuwepo tangu alipopatikana mwanamke, lakini kwa wingi wake katika sura hii ambayo anafikia mwanadamu haelewi namna ya kutatua matatizo haya, hili ni jambo la kuhuzunisha sana.
Lakini kanuni ya ujumla: Mwanamke akitwaharika, akaona kutwaharika baada ya damu ya hedhi na damu ya uzazi: Yakatoka maji maji meupe wanayajua wanawake- basi baada ya mwanamke kutwaharika ukitoka uchafu, unjano, au tone, au unyevu, hivi vyote si hedhi, na havimzuii vitu hivyo kuswali, kufunga na wala havizuii tendo la ndoa baina ya mwanaume na mwanamke kwa sababu vitu hivyo si damu ya hedhi. Alisema Ummu Atwiya: "Tulikuwa hatuoni unjano na uchafu kuwa ni kitu" amesimulia Bukhari na akazidisha Abuu Daud: (wakiona vitu hivyo) Baada ya kutwaharika. Mtiririko wa wapokezi wake ni sahihi.
Na kuhusu hili tunasema: Kila kitakachotokea katika vitu hivyo baada ya kutwaharika kwa uhakika, vitu hivyo havimdhuru mwanamke na wala havimzuii kuswali swala zake, na kufunga swaumu zake, na havimzuii kuingiliwa na mume wake lakini ni lazima kwa mwanamke huyu asifanye haraka asubiri mpaka aone kuwa katwaharika. Kwa sababu baadhi ya wanawake damu ikikauka, hufanya haraka na hujitwaharisha kwa kuoga kabla hawajaona kule kutwaharika kunakotakiwa. Na kwa hivyo, walikuwa wanawake walioishi kipindi cha Mtume wakiagiza Kursuf yaani; pamba yenye damu, iende kwa mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake, alikuwa akiwaambia: Msifanye haraka mpaka muone maji maji meupe ambayo hutoka baada ya hedhi kumalizika.
Baadhi ya wanawake damu inaendelea, na wakati mwingine inakatika siku moja au siku mbili kisha inarejea, je ni ipi hukumu katika hali hii kuhusu swaumu yake na swala yake na ibada zingine?.
Linalofahamika kwa wanachuoni walio wengi ni kwamba: Mwanamke anapokuwa katika siku zake, zikiisha siku zake, basi anajitwaharisha kwa kuoga, na ataswali na kufunga na atakachokiona baada ya hapo siku moja au siku mbili si hedhi kwa sababu siku chache za kutwaharika baina ya hedhi mbili kwa wanachuoni hawa ni siku kumi na tatu.
Na wamesema wanachuoni wengine kwamba: Bali kwa mwanamke huyu atakapoona damu basi hiyo ni hedhi, na wakati wowote akitwaharika basi ametwaharika, hata kukiwa hakuna baina ya hedhi ya kwanza na ya pili siku kumi na tatu.
Lipi bora kwa mwanamke: Akaswali usiku ndani ya mwezi wa Ramadhani nyumbani kwake, au msikitini, hasa hasa msikitini kukiwa na mawaidha na ukumbusho? Ni upi muongozo wako kwa wanawake ambao wanaswali msiktini?.
Bora akaswali katika nyumba yake, kutokana na ujumla wa kauli ya Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Na Nyumba zao ni bora kwao wao" Na ni kwa sababu mwanamke kutoka nyumbani kwake hakujasalimika na fitina katika nyakati nyingi, na kuwa mwanamke kubakia nyumbani kwake ni bora kwake, kuliko kutoka kwenda msikitini, ama mawaidha na mazungumzo ya kheri inawezekana akayapata kupitia kanda.
Na muongozo wangu kwa wanawake ambao wanaswalia msikitini: Watoke katika nyumba zao wakiwa hawajajipamba kwa mapambo, wala kujipulizia manukato.
Ni ipi hukumu ya mwanamke kuonja chakula mchana wa Ramadhani akiwa amefunga.
Hukumu yake: Hakuna shida juu ya jambo hilo, akiwa na haja ya jambo hilo, lakini akiteme kile alichokionja (asimeze).
Mwanamke kapata ajali, na alikuwa mwanzoni mwa mimba yake, mimba ikatoka baada ya kutokwa na damu nyingi, je inajuzu kwake kufungua, au anaendelea kufunga? Akifungua je atapata dhambi?
Tunasema: Hakika mjamzito hatokwi na damu ya hedhi, kama anavyosema Imam Ahmad: Wanawake wengi hujua ujauzito kwa kukatika hedhi, na hedhi kama walivyosema Wanachuoni, ameiumba Allah -Mtukufu- kwa hekima ya kuwa ni chakula cha mtoto aliye tumboni, mimba itakapoanza hedhi hukatika.
Lakini baadhi ya wanawake inaweza ikaendelea kwake damu ya hedhi kama kawaida kama ilivyokuwa kabla ya mimba, huyu atahukumiwa kuwa hedhi yake ni hedhi ya kawaida, kwa sababu hedhi kwake iliendelea na wala haikuathirika na mimba, hedhi hii itamzuia na yale yote ambayo yanayozuiwa na hedhi ya siku zote ya mwanamke asiyemjamzito, hivyo, itawajibisha yale ambayo yanawajibika kwa mwenye hedhi, na itadondosha yale yote ambayo yanadondoshwa na hedhi ya kawaida (ikiwemo swala n.k)
Na kwa ufupi ni kwamba: Damu inayomtoka mjamzito iko katika aina mbili:
Aina moja wapo inahukumiwa kuwa ni hedhi, nayo ni ile ambayo inaendelea kutoka kwake kama ilivyokuwa ikitoka kabla ya mimba, basi maana ya jambo hili ni; Mimba haijamuathiri, hii itakua ni hedhi ya kawaida.
Na aina ya pili, ni damu inayotoka wakati wa mimba, ima kwa sababu ya ajali, au alibeba kitu kizito, au kudondoka toka juu ya kitu fulani na mfano wake, damu hii si hedhi, bali ni damu ya ugonjwa. kwa hiyo, haimzuii damu hii kuswali, wala kufunga, bali anakuwa katika hukumu ya wanawake waliotwaharika.
Lakini ajali ikisababisha mtoto kushuka au mimba ambayo iliyokuwa tumboni, atakuwa kama walivyosema wanachuoni: Mimba ikitoka na imebainika kwake umbile la mwanadamu, basi damu itakayotoka baada ya kutoka mtoto itahesabika kuwa ni damu ya uzazi, ataacha kuswali, na kufunga, na mumewe atajitenga naye mpaka atwaharike.
Na akitoka mtoto ambaye hajakamilika basi haizingatiwi kuwa ni damu ya uzazi, bali ni damu iliyoharibika, haimzuii mwanamke kuswali, wala kufunga, wala kingine chochote.
wamesema Wanachuoni: Muda mchache ambao kinabainika kiumbe: Ni siku themanini na moja; kwa sababu mtoto yupo tumboni kwa mama yake. Kama alivyosema Abdullah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- Ametuhadithia mkweli mwenye kusadikishwa, akisema: "Hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake katika tumbo la mama yake siku arobaini, kisha linakuwa pande la damu mfano wa siku hizo, kisha linakuwa pande la nyama mfano wa siku hizo, kisha hutumwa Malaika na anaamrishwa kuandika mambo manne; kuandika riziki yake, kifo chake, muovu au mwema". Na wala haiwezekani kuumbwa kabla ya siku hizo, mara nyingi kiumbe hakibainiki kabla ya siku tisini, kama walivyosema baadhi ya Wanachuoni.
Mimi ni mwanamke ilitoka mimba ikiwa katika mwezi wa tatu, mwaka umepita sasa, na sikuswali mpaka nilivyotwaharika, waliniambia, ulikuwa unatakiwa kuswali, basi kipi natakiwa kufanya, na mimi sifahamu idadi ya siku maalumu?.
Jambo linalofahamika kwa wanachuoni ni kwamba: Mwanamke pindi itakapotoka mimba yake ikiwa imetimiza miezi mitatu basi hatoswali, kwa sababu aliyetoka ni mtoto aliyebainika umbile lake na damu inayotoka inakuwa ni damu ya uzazi hivyo hatoswali ikiwa inatoka damu hiyo.
wanasema wanachuoni: Inawezekana kubainika umbile la mtoto tumboni zikitimia siku 81 na hizi ni chini ya miezi mitatu, akiwa na yakini kwamba mimba imetoka ikiwa na miezi mitatu, damu itakayomtoka inakuwa damu iliyoharibika, haachi swala kwa sababu hiyo.
Na jambo hili ni juu ya mwanamke kukumbuka, ikiwa mtoto aliyetoka ilikuwa kabla ya siku 80 basi atazilipa swala zile, ikiwa hajui ni swala ngapi kaziacha? Basi akadirie, na ajitahidi kujua idadi, kisha dhana yake kubwa ikiwa katika idadi fulani ya swala zilizompita, basi azilipe kwa idadi hiyo.
Muulizaji wa kike anauliza: Yeye tangu awajibikiwe na swaumu anafunga Ramadhani, lakini halipi siku zake alizofungua kwa sababu ya mzunguko wa damu ya hedhi, na kwa sababu ya kutokujua idadi ya siku alizofungua, kwa hiyo, yeye hivi sasa, anaomba muongozo lile la lazima juu yake kulifanya.
Inasikitisha kutokea hili baina ya wanawake wa waumini, hakika huko kuacha- namaanisha: Kuacha kulipa siku ambazo ni lazima kwao kufunga -ima ni kwa sababu ya kutokujua, na ima ni kwa sababu ya uzembe, yote mawili ni msiba, kwa sababu ujinga dawa yake ni kusoma na kuuliza, ama kuzembea, dawa yake ni kumcha Allah Mshindi Aliyetukuka, na kujichunga kujua Allah anakuona, na kuogopa mwisho wa mambo, na kupupia yale ambayo Allah anayaridhia.
Juu ya mwanamke huyu, atubie kwa Allah kwa yale aliyoyafanya, na aombe msamaha, ajitahidi kuzijua siku alizoacha kadiri ya uwezo wake kisha atazilipa, na kwa kufanya hili hatolaumiwa, natarajia Allah atakubali toba yake.
Ni ipi hukumu ya mwanamke kafikiwa na mzunguko wa hedhi baada ya kuingia wakati wa swala, je inawajibika kwake yeye kulipa akitwaharika? Na hivyo hivyo pindi akitwaharika kabla ya kutoka muda wa swala?
Kwanza: Mwanamke akiingia katika mzunguko wa damu ya hedhi baada ya kuingia wakati wa swala basi inawajibika kwake akitwaharika alipe swala ambazo alipatwa na mzunguko katika wakati wake, ikiwa hajaswali kabla ya kuingiwa na hedhi. Na hili ni kwa mujibu wa kauli yake Mtume rehema na amani za Allah zimfikie: "Mwenye kuipata rakaa moja ya swala basi kwa hakika atakuwa ameipata swala". Ikiwa mwanamke ataupata muda wa swala kiasi cha rakaa moja, kisha akaingia katika hedhi kabla hajaswali, itamlazimu kukidhi (kulipa) swala hiyo pindi atakapo twaharika.
Pili: Ikiwa mwanamke atatwaharika kutokana na hedhi kabla muda wa swala haujatoka, basi itamuwajibikia kulipa swala hiyo. Na lau atatwaharika kabla ya jua kuchomoza kwa kiasi cha rakaa moja itamuwajibikia kulipa swala ya Alfajiri, na lau atatwaharika kabla ya jua kuzama kwa kiasi cha rakaa moja itamuwajibikia kuswali swala ya Alasiri, na lau atatwaharika kabla ya usiku kufikia katikati itamuwajibikia kulipa swala ya Ishaa, na ikiwa atatwaharika baada ya nusu ya usiku, haitamuwajibikia swala ya Ishaa, Allah Mtukufu anasema: "...Na mtakapopata amani mkawa katika salama, hapana vita, basi simamisheni swala, kwa hakika swala kwa waumini ni faradhi iliyopangiwa wakati maalumu" [Annisai: 103], Yaani: Ni faradhi iliyopangiwa wakati maalumu, haifai kwa mtu kuitoa swala nje ya wakati wake (akaswali baada ya kutoka muda wake), wala kuiswali kabla ya kuingia wakati wake.
Iwapo imeingia kwangu desturi ya mwezi (hedhi) na hali nikiwa katikati ya swala, nitatakiwa kufanya nini? Na je, nitawajibika kulipa swala hiyo baada ya muda wa hedhi?
Ikiwa mwanamke itamtokea hedhi baada ya kuingia wakati wa swala; kwa mfano mwanamke akafikwa na hedhi baada ya kupinduka jua kwa nusu saa, basi bila shaka baada ya kutwaharika kutokana na hedhi yake atailipa swala hii ambayo uliingia muda wake na hali akiwa na twahara. Na hiyo ni kwa mujibu wa kauli ya Allah Mtukufu: "..Kwa hakika swala imekuwa juu ya waumini ni faradhi iliyopangiwa wakati maalumu" [An-Nisai: 103]
Na wala mwanamke hatolipa swala zilizomkuta akiwa ndani ya hedhi; kwa mujibu wa kauli ya Mtume rehema na amani za Allah zimfikie - katika hadithi ndefu: "Je, si pale mwanamke anapoingia katika hedhi haswali na wala hafungi?" Na wanachuoni wamekubaliana kuwa mwanamke halipi swala ambayo ilimpita akiwa katika hedhi.
Ama ikiwa atatwaharika, na hali ilikuwa imebaki katika muda wa swala kiasi cha rakaa moja na zaidi, basi ataswali swala hiyo ambayo ni ya wakati aliotwaharika ndani yake, na hii ni kwa mujibu wa kauli yake Mtume rehema na amani za Allah zimfikie: "Mwenye kupata rakaa moja katika swala ya Alasiri kabla jua halijazama, basi kwa hakika atakuwa ameipata swala ya Alasiri". Na ikiwa mwanamke atatwaharika ndani ya wakati wa Alasiri, au kabla ya kuchomoza jua, na ikawa imebaki kabla ya kuzama jua au kuchomoza jua kwa kiasi cha rakaa moja, basi ataswali Alasiri kwa mnasaba wa swala la kwanza, na ataswali Alfajiri kwa mnasaba wa swala la pili.
Mimi nina mama mzazi ambaye anafikia umri wa miaka sitini na tano, na yeye katika kipindi cha miaka kumi na tisa hajapata mtoto, na hivi sasa ana kipindi cha miaka mitatu akiwa na ugonjwa wa kutokwa na damu, -na inavyoonekana nikuwa- maradhi hayo yalimpata katika wakati huo vile vile anakabiliwa na ibada ya swaumu, je ni nini nasaha zenu kwake, na je, nini atakachotakiwa kufanya?
Hukumu ya mfano wa mwanamke kama huyu aliyefikwa na ugonjwa wa kutokwa na damu: Anatakiwa aache kuswali na kufunga katika kipindi cha desturi yake iliyotangulia kabla ya kufikwa na ugonjwa huu. Hivyo basi iwapo ilikuwa kawaida yake anapata hedhi katika mwanzo wa kila mwezi kwa muda wa siku sita kwa mfano, basi atakaa katika mwanzo wa kila mwezi kwa muda wa siku sita na hali ya kuwa haswali wala hafungi, na zitakapoisha siku hizo basi ataoga na ataswali na atafunga.
Na namna ya swala ya mwanamke kama huyu na mfano wake: Ataosha tupu yake kwa ukamilifu, halafu ataifunga na atatawadha, na atakuwa akifanya hivyo baada ya kuingia wakati wa kila swala ya faradhi, na atafanya hivyo hivyo atakapokuwa anataka kuswali swala za suna zisizokuwa faradhi.
Na katika hali kama hii, na kutokana na tabu anazopitia, itakuwa inajuzu kwake kukusanya swala ya Adhuhuri na Laasiri, na swala ya Magharibi na Ishaa: Kwa kufanya kwake hivi ataswali swala mbili kwa mara moja; Yaani swala ya Adhuhuri na Alasiri. Na twahara moja pia kwa ajili ya swala mbili: Yaani swala ya Magharibi na Ishaa, na Alfajiri itakuwa pekee. Hivyo basi badala ya kuswali mara tano ataswali mara tatu tu.
Na hapa nitarudia maelezo mara ya pili, ninasema: Pindi atakapotaka kujitwaharisha ataosha tupu yake, na ataifunga kwa kitambaa au mfano wa kitambaa, ili ipungue ile hali ya kutoka damu. Kisha atatawadha, na ataswali Adhuhuri rakaa nne na Alasiri rakaa nne. Na Magharibi rakaa tatu na Ishaa rakaa nne, na Alfajiri rakaa mbili, kwa maana kwamba asipunguze rakaa hizo kama wanavyodhania baadhi ya watu wasiokuwa na elimu na maarifa. Lakini inajuzu kwake kukusanya kati ya swala ya Adhuhuri na Alasiri, na kati ya swala ya Magharibi na Ishaa, ima kwa kutanguliza au kwa kuchelewesha, na ikiwa atataka kuswali swala ya sunna kwa udhu huo huo aliyoswalia swala hizo za faradhi, hapana ubaya kufanya hivyo.
Nini hukumu ya mwanamke kukaa katika msikiti mtukufu wa Makka au msikiti wa Madina, na hali akiwa na hedhi; kwa nia ya kusikiliza mafunzo ya hadithi za Mtume rehema na amani za Allah zimfikie, na kusikiliza hotuba?
Haijuzu kwa mwanamke mwenye hedhi kukaa ndani ya msikiti wa Makka au msikiti mwingine wowote, lakini inajuzu kwake kupita na kukatisha ndani ya msikiti kwa nia ya kutimiza haja yake humo, na mfano wa hilo; kama alivyosema Mtume rehema na amani za Allah zimfikie, alipomuamrisha mama Aisha alete Msala, mama Aisha akasema: Msala uko msikitini na mimi nina hedhi. Mtume wa Allah rehema na amani zimfikie akasema: "Hedhi yako haiko mkononi mwako", Na ikiwa mwanamke mwenye hedhi atakatisha msikitini, na hali ya kuwa damu yake haichuruziki ndani ya msikiti, basi hapana ubaya wowote juu yake.
Ama ikiwa mwanamke huyo anataka tu kukaa msikitini hilo halitajuzu kisheria.
Na dalili ya hilo: Ni kuwa Mtume rehema na amani za Allah zimfikie aliwaamrisha wanawake kutoka katika swala ya iddi ili kuhudhuria mahala pa tukio la swala ya iddi (wanawake walioachwa huru kutokana na utumwa na mabinti wanaotawa na wanawake wenye hedhi) isipokuwa tu akaamrisha wenye hedhi wajitenge na mahala pa kuswalia. Hivyo hilo linajulisha kuwa mwanamke mwenye hedhi haijuzu kwake kukaa msikitini kwa nia ya kusikiliza hotuba au kusikiliza darasa na hadithi.
*
MIONGONI MWA HUKUMU ZA TWAHARA KATIKA SWALA:
Je kinachotoka kwa kuchuruzika toka kwa mwanamke (katika sehemu zake za siri)- kikiwa ni rangi nyeupe au ya njano- ni najisi au twahara, na je unawajibika udhu kwa hicho kinachotoka, pamoja na kujuwa kwamba kinaendelea kutoka bila kukatika, na ipi hukumu ikiwa kitaacha kutoka? hususani ni kwamba wengi katika wanawake wasomi wanazingatia kile kinachotoka ni unyevunyevu wa kawaida na wa asili, hailazimiki kuchukua Udhu?
Kinachodhihiri kwangu baada ya utafiti ni kuwa: Kinachochuruzika kutoka kwa mwanamke ikiwa hakitoki kwenye kibofu basi kinatoka katika mfuko wa uzazi na kitakuwa ni twahara, lakini kinatengua udhu pamoja na kuwa ni twahara: Kwa sababu kitu kinachotengua udhu si sharti kiwe najisi, kwani huoni upepo unaotoka sehemu ya nyuma hauna umbo, lakini pamoja na hivyo unatengua udhu.
Na kwa ajili hiyo tu, ikiwa damu hiyo itamtoka mwanamke na hali akiwa na udhu basi damu hiyo itatengua udhu wake, na itamuwajibikia kutawadha udhu mpya.
Na ikiwa damu hiyo inaendelea kutoka haitatengua udhu wake, lakini atatawadha kwa ajili ya swala pindi utakapoingia muda wake, na kwa udhu huo huo ataswali swala ya sunna na atasoma Qur'ani, na atafanya lolote katika mambo ya halali kwake. Na hivi ni kama walivyosema wasomi kuhusu mtu mwenye ugonjwa wa kutokwa na mkojo mfululizo, hii ndiyo hukumu ya mwenye kutokwa na damu katika kadhia ya twahara, anakuwa twahara, na katika swala la kutenguka udhu wake, mkojo huo unatengua udhu ila tu ikiwa unatoka mfululizo wakati huo hautatengua udhu. Lakini mwanamke hatatawadha kwa ajili ya swala ila baada ya kuingia muda, na awe muangalifu.
Ama ikiwa damu hiyo inakatika, na ikawa desturi yake haikatiki katika nyakati za swala, basi ataahirisha swala mpaka wakati ambao damu inakatika, madhali tu hahofii kupitwa na kipindi cha swala. Ikiwa atahofia kupitwa na kipindi cha swala basi itambidi atawadhe na atajifunga na kujihifadhi na kuswali.
Na hapana tofauti kati ya damu ndogo na damu nyingi; Kwa sababu zote hizo zinatokea katika njia moja; hivyo basi ikiwa ni nyingi au kidogo zote hizo zinatengua udhu. Hii ni tofauti na damu inayotoka katika maeneo mengine ya mwili kama damu au matapishi, vitu hivyo havitengui udhu vikiwa kidogo au vikiwa vingi.
Ama itikadi ya baadhi ya wanawake kuhusu damu hiyo kwamba haitengui udhu hili mimi sijui linatokana na asili ipi, isipokuwa kauli ya Ibn Hazmi Allah amrehemu yeye anasema: Damu hii haitengui udhu, lakini hakuleta dalili yoyote juu ya kauli yake hii na lau angetaja dalili yoyote kutoka katika kitabu na sunna na kauli za Maswahaba hiyo ingelikuwa ni hoja.
Na ni juu ya mwanamke kumcha Allah na apupie kujitwaharisha; kwa sababu swala haikubaliwi bila ya twahara, hata akiswali mara mia, kwani baadhi ya wanachuoni wanasema: Mtu anayeswali bila ya twahara anafanya kufuru; kwa sababu kufanya hivyo ni kuzifanyia kejeli aya za Allah -Aliyetakasika na Kutukuka.
Atakapotawadha mwanamke ambaye anatokwa na kinachomtoka katika sehemu zake za siri bila kukatika kwa ajili ya swala ya faradhi, je ni sahihi kwake akaswali swala za sunna anazotaka na kusoma Qur'ani kwa ule udhu aliouchukua kwa ajili ya ile swala ya faradhi mpaka swala ya faradhi nyingine inayofuata?
Atakapochukua udhu mwanamke kwa ajili ya swala ya faradhi katika mwanzo wa wakati wake basi ni juu yake akaswali swala za sunna anazotaka na kusoma Qur'ani mpaka utakapoingia wakati wa swala nyingine.
Je ni sahihi kwa mwanamke huyo kuswali swala ya dhuha kwa udhu wa swala ya Alfajiri?
Hilo si sahihi, kwa sababu swala ya dhuha ni swala ya wakati maalumu, ni lazima kuchukua udhu kwa ajili ya swala ya dhuha ukiingia wakati wake, kwa sababu mwanamke huyu ni mfano wa yule mwanamke anayetokwa na damu ya ugonjwa, na alimuamrisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- mwanamke anayetokwa na damu ya ugonjwa achukue Udhu kwa kila swala (anayotaka kuswali).
Na wakati wa swala ya Adhuhuri: Ni toka kupinduka kwa jua (kuelekea Magharibi) mpaka wakati wa swala ya Alasiri.
Na wakati wa swala ya Alasiri: Ni toka wakati wa kutoka swala ya Adhuhuri mpaka jua likiwa la njano, (na wakati wa) dharura (kwa ajili ya swala ya Lasiri) ni mpaka kuzama kwa jua.
Na wakati wa Magharibi: Ni toka kuzama kwa jua mpaka kupotea kwa wekundu unaotokea angani wakati wa kuzama kwa jua.
Na wakati wa swala ya Ishaa: Ni kutoka wakati umepotea ule wekundu unaotokea angani wakati wa kuzama kwa jua mpaka nusu ya usiku.
Je ni sahihi kwa mwanamke huyu kuswali kisimamo cha usiku itakapopita nusu ya usiku kwa udhu ule wa Ishaa?
Hapana, itakapopita nusu ya usiku inawajibika kwa mwanamke huyu kuchukua udhu tena, na pamesemwa kuwa: Sio lazima kuchukua udhu mpya na hii ndio kauli yenye nguvu yenye kufanyiwa kazi.
Ni upi muda wa mwisho wa swala ya Ishaa, na vipi utautambua?.
Wakati wa mwisho wa swala ya Ishaa ni nusu ya usiku, na hilo hutambuliwa kwa kugawa mara mbili baina ya kuzama kwa jua na kuchomoza Alfajiri, nusu ya kwanza inaisha muda wa mwisho wa swala ya Ishaa, na inabakia nusu ya mwisho haina wakati bali ni kizuizi baina ya Ishaa na Alfajiri.
Atakapochukua udhu mwanamke anayetokwa na chenye kutoka kwa kukatikakatika (hakitoki mfululizo sehemu za siri) na baada ya kumaliza kuchukua udhu na kabla ya swala yake, kikatoka mara nyingine, nini afanye mwanamke huyu?
Ikiwa kile kinachotoka kiliacha kutoka basi asubiri mpaka ule muda ambao kinaacha kutoka, ama ikiwa hana hali inayofahamika, muda wa kutoka na muda wa kuacha kutoka, basi atachukua udhu baada ya kuingia wakati wa swala, ataswali, na halazimiki juu yake chochote.
Kipi kinalazimu pindi hicho kinachotoka (sehemu za siri) kikigusa mwili au nguo?
Ikiwa kile kinachotoka ni twahara (kisafi) basi hakuna kinachomlazimu, na kikiwa ni najisi -nacho ni kile kinachotoka katika kibofu- basi inawajibika juu yake akoshe (mwili au nguo hizo)
kuhusu kutia udhu kutokana na kile chenye kutoka, je inatosha akaosha vile viungo vya udhu peke yake?
Ndio, inatosha hilo, ikiwa kinachotoka ni twahara, nacho ni kile kinachotoka katika mfuko wa uzazi na sio kinachotoka katika kibofu.
Ni ipi sababu ya kutonukuliwa kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- hadithi yoyote yenye kuonyesha juu ya kutenguka kwa udhu kwa kile kinachotoka, pamoja na kwamba Maswahaba wa kike walikuwa wakipupia juu ya kutaka kujua mambo katika dini yao?
Kwa sababu kinachotoka hakimjii kila mwanamke.
Yule mwanamke ambaye alikuwa hachukui udhu kwa kutokujua hukumu yake, anawajibika nini juu yake mwanamke huyo?
Juu yake mwanamke huyo ni kutubu kwa Allah (Mshindi Aliyetukuka) na awaulize wanazuoni juu ya hilo.
kuna wanaonasibisha kwako kauli ya kutochukua udhu kwa kutoka kile chenye kutoka (sehemu za siri)?
Mwenye kuninasibishia kauli hii sio mkweli, jambo linalodhihiri ni kwamba yeye kafahamu kutoka katika kauli yangu: Kwamba hakitengui Udhu.
Ni ipi hukumu ya uchafu unaomtoka mwanamke kabla ya hedhi kwa siku moja au zaidi au chini ya hapo, na kinaweza kuwa chenye kutoka kikawa mfano wa uzi laini mweusi au kahawia au mfano wa hiyo? Ni ipi hukumu lau ikiwa baada ya hedhi?
Hiyo ikiwa ni mwanzo wa hedhi basi hiyo ni hedhi, na hutambuliwa hilo kwa maumivu ambayo yanamkuta aliye na hedhi kwa kawaida.
Ama uchafu baada ya hedhi, atasubiri mpaka uondoke; kwa sababu uchafu unaoungana na hedhi nao ni hedhi; kutokana na kauli ya Aisha- radhi za Allah ziwe juu yake: Msifanye haraka mpaka muone twahara baada ya hedhi. Na Allah ndiye Mjuzi zaidi.
*
MIONGONI MWA HUKUMU ZA HEDHI KATIKA HIJA NA UMRA:
Vipi anaswali rakaa mbili za baada ya kuhirimia mwanamke anayetokwa na damu ya hedhi? Na je inafaa kwa mwanamke mwenye hedhi kusoma na kurudia rudia Adhkari ndani ya nafsi yake, au haifai?
Jambo la kwanza: Tunapaswa kujua kwamba Ihram (Nia ya kuanza Hija au Umra) haina swala yoyote; kwa sababu haikuja kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kwamba ameweka sheria kwa umma wake kuwe na swala maalum kwa ajili ya Ihram, si kwa kauli yake, au kitendo chake, au kufanyika kitu mbele yake akakipitisha.
Jambo la pili: Mwanamke huyu mwenye hedhi ambaye ameingia katika hedhi kabla hajahirimia, anaweza kuhirimia akiwa katika hedhi.
Na ama kauli yake katika swali: Je anaweza kusoma Qur'ani? Basi jawabu ni ndio, na mwanamke mwenye hedhi anaruhusiwa kusoma Qur'ani akiwa na haja au akiona kuna masilahi juu ya hilo, ama kama hakuna haja wala masilahi, bali anasoma tu kama ibada na kujikurubisha kwa Allah, lililo bora asisome.
Amesafiri mwanamke kwenda katika Hijja, na akajiwa na mzunguko wa mwezi (Hedhi), toka siku tano kabla ya safari yake, lakini baada ya kufika katika sehemu ya kuhirimia, akaoga na akaingia katika ibada ya Hijja kwa kuhirimia, lakini yeye hajatwaharika na mzunguko wake wa hedhi, alipofika katika mji wa Makka akabakia nje ya eneo tukufu, hakufanya chochote katika metendo matukufu ya Hijja na Umra, na akakaa siku mbili katika mji wa Mina, kisha akatwaharika, akajitwaharisha kwa kukoga, na akatekeleza matendo yote ya Umra akiwa ametwaharika, kisha ikamrudia damu akiwa katika Twawaf ya Hija (kuzunguka Al-Kaaba kwa ajili ya Hija) isipokuwa aliona haya na akakamilisha matendo ya Hija, hakumwambia msimamizi wake mpaka baada ya kufika katika mji wake, ni ipi hukumu ya hilo?
Hukumu ya hilo: Damu iliyompata wakati anazunguka Al-Kaaba wakati wa Hija, ikiwa ni damu ya hedhi ambayo anaijua kwa ile kawaida yake na maumivu yake basi hakika kule kuzunguka kwake Kaaba kwa ajili ya Hija (Twawaful ifadha) hakuko sahihi, inamlazimu arudi katika mji wa Makka; ili aweze kutufu twawaful Ifadha (kuzinguka Kaaba kwa ajili ya Hija), ahirimie kufanya ibada ya Umra katika maeneo ya kuhirimia kisha atekeleze ibada ya Umra kwa kutufu (Kuzunguka Kaaba) na kuzunguka swafa na Marwa na apunguze nywele kisha ndio atufu twawaful Ifadha (kuzunguka Kaaba kwa ajili ya Hija)
Ama ikiwa damu hii sio damu ya hedhi, ni damu ya kawaida inayojulikana, bali imetokana na msongamano mkubwa au hofu na yanayofanana na hayo, basi kuzunguka kwake kuko sahihi kwa wale wasioshurutisha twahara (katika wanazuoni) mtu akiwa anazunguka Kaaba.
Ikiwa ameshindwa kurudi, katika swala la mwanzo, kiasi kwamba yuko katika miji ya mbali, basi Hija yake ni sahihi, kwa sababu hana uwezo wa kufanya zaidi ya vile alivyofanya.
Amefika mwanamke amehirimia kwa ajili ya Umra, na alipofika katika mji wa Makka akapata hedhi, na msimaizi wake analazimika kusafiri kwa haraka, na hana msimamizi mwingine katika mji wa Makka, ni ipi hukumu yake?
Atasafiri pamoja naye, na atabakia katika ibada yake akiwa amehirimia, kisha atarejea akitwaharika, na hili ikiwa atakuwa Saudia; kwa sababu kurejea akiwa hapo ni jambo jepesi, na wala halina tabu ndani yake jambo hilo, hahitaji hati za kusafiria na mengineyo.
Ama akiwa anatoka nje ya Saudia, na ni tabu kwake kurudi, basi atajihifadhi, atazunguka Al-Kaaba, atazunguka Swafa na Marwa na amalize ibada yake ya Umra katika safari hiyo hiyo, kwa sababu kuzunguka kwake Kaaba wakati huo ni dharura, na dharura huruhusu mambo yaliyokatazwa.
Ni ipi hukumu ya mwanamke wa kiislamu ambaye amepatwa na damu ya hedhi katika siku za Hija, je ile Hija itamtosheleza (Itakubalika)?
Hili haliwezekani kulijibu mpaka ijulikane ni muda gani mwanamke huyu kapatwa na damu ya hedhi, na hilo ni kwa sababu baadhi ya matendo ya Hija hayazuiliwi na hedhi kufanyika, na mengine yanazuiliwa, mfano: Kuzunguka Kaaba, hawezi kuzunguka mpaka awe na udhu (Twahara), na mengine katika matendo ya Hija anaweza kuyafanya akiwa na hedhi.
Nilikuja kufanya Hija yangu ya lazima mwaka jana, nilifanya matukio yote ya Hija isipokuwa Twawaful Ifadha (kuzunguka Kaaba kwa ajili ya Hija) na Twawaful wadaa (Kuzunguka kaaba kwa ajili ya kuaga), nilizuiwa na udhuru wa kisheria, nikarudi nyumbani kwangu katika mji wa Madina nikiazimia kurudi siku katika masiku ili nizunguke Kaaba mizunguko niliyoiacha, kutokana na mimi kutojuwa mambo ya dini, nimehalalika na kila kitu, nimefanya mambo yote ambayo nakatazwa katika ihraam, nikaulizia kurudi ili nizunguke Kaaba nikaambiwa: Hauwezi tena kurudi, kwani tayari umeharibu ibada yako, inakulazimu kurudia Hija mara nyingine mwaka unaokuja, pamoja na kuchinja Ngamia au Ng'ombe, je fatwa hii ni sahihi? Je kuna njia nyingine, ni ipi hiyo, na je Hija yangu imeharibika? Na je natakiwa kurudia? Nipe faida kwa yale ninayotakiwa kuyafanya, Allah awabariki.
Na hili pia ni katika balaa, kutolewe Fatwa bila ya elimu, na wewe katika hali hiyo unawajibika kurudi katika mji wa Makka, na ukatufu Twawaful ifadha pekee (Kuzunguka Kaaba kwa ajili ya Hija).
Ama kuzunguka Al-Kaaba kwa lengo la kuaga (Twawaful Wadaa) hulazimiki kufanya hivyo madamu ulikuwa na hedhi wakati unatoka katika mji wa Makka, kwa sababu mwenye hedhi halazimiki kufanya mzunguko huo; kutokana na hadithi ya bin Abbas -radhi za Allah ziwe juu yao- Aliwaamrisha watu jambo lao la mwisho katika ibada ya Hija liwe ni kuzunguka Kaaba, isipokuwa aliwafanyia wepesi waliopatwa na hedhi. Na katika riwaya ya Abuu Daudi: Jambo lao la mwisho katika ibada ya Hija liwe ni kuzunguka Kaaba. Na ni kwa sababu Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alipoambiwa kwamba Swafia ametufu (amezunguka Kaaba kwa mzunguko wa Hija) basi akasema: (Na arudi basi). Imeonyesha hadithi hiyo kwamba mzunguko wa Kaaba kwa kuiaga Kaaba unadondoka kwa mwanamke mwenye hedhi.
Ama mzunguko wa Kaaba kwa ajili Hija huo ni lazima, na kwa kuwa amehalalika na kila kitu kwa kutojua, hilo halimdhuru kitu, kwa sababu asiyejua anapofanya katazo katika makatazo ya Ihiramu, hana dhambi. Kutokana na kauli ya Allah Mtukufu: "Ewe Mola wetu Mlezi usituadhibu ikiwa tutasahau au kukosea" [A-Baqara: 286], Akasema Allah Mtukufu: "Hakika nimefanya hivyo". Na kauli yake Allah: "Hakuna tatizo juu yenu katika yale mliyokosea lakini tatizo liko kwa yale yaliyokusudiwa na nyoyo zenu". [Al-Ahzab:5] Yote aliyoyakataza Allah Mtukufu kutoyafanya kipindi cha ibada ya Hija au Umra kwa yule mwenye kufanya ibada hiyo, akiyafanya katika hali ya kutokujua au kusahau au kwa kulazimishwa hana dhambi, lakini udhuru wake ukiondoka anawajibika juu yake ajivue katika lile aliloshikama nalo na kurudi katika asili.
Mwanamke anayetokwa na damu ya uzazi, ikianza damu yake siku ya Tarwiya (Tarehe 8 Dhul Hija), na akakamilisha nguzo za Hija isipokuwa Twawafu na Sa'i (Kukimbia baina ya Safa na Marwa), isipokuwa akaona ametwaharika twahara za mwanzo mwanzo baada ya siku kumi, je atasubiri? Na akoge, na atekeleze nguzo iliyobakia ambayo ni mzunguko wa Kaaba kwa ajili ya Hija?
Haifai kwake kuoga, na kuzunguka Kaaba mpaka apate uhakika wa kutwaharika, jambo linalofahamika tokana na neno -mwanzo mwanzo- hii inamaana kwamba hajaona twahara iliyokamilika, lazima aone twahara iliyokamilika, muda wowote atakapotwaharika basi atakoga na atatekeleza Twawaf na Sa'i (Kukimbia baina ya Safa na Marwa).
Na akizunguka Swafa na Marwa (Sa'i) kabla ya kuzunguka Kaaba hakuna neno, kwa sababu Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- aliulizwa kuhusu mtu kuzunguka Swafa na Marwa kabla ya kuzunguka Kaaba wakati wa Hija akasema: "Hakuna tatizo".
Mwanamke ameweka nia ya kufanya Hija akiwa katika Sail (Sehemu ya kuhirimia kwa watu wa pande za Najid) akiwa yuko katika hedhi, na alipofika katika mji wa Makka akaenda katika mji wa Jidda, kwa ajili ya haja zake, na akatwaharika akiwa Jidda, na akaoga, na akachana nywele zale, kisha akaikamilisha Hija yake, je Hija yake ni sahihi? Na je analazimika chochote juu yake?
Hija yake iko sahihi na wala hana chochote juu yake.
Mimi nilikwenda Umra, nilipita katika eneo la kuhirimia na kutia nia ya ibada hiyo nikiwa katika hedhi, sikuhirimia, nikabakia katika mji wa Makka mpaka nikatwaharika, nikahirimia katika mji wa Makka, je jambo hili linafaa? na nini natakiwa kufanya, na ni lipi ninawajibika kwalo?
Kitendo kilichofanyika hakiko sahihi, mwanamke anayetaka kufanya Umra, haifai kwake kupita eneo la kuhirimia mpaka atie nia ya kufanya ibada ya Umra/Hija hata akiwa na hedhi, kutia nia kwake kuna hesabika na ni sahihi. Na dalili ya hilo ni kwamba: Alijifungua Asmaa bint Umaisi, mke wa Abubakari -radhi Allah ziwe juu yao- na Mtume- rehema na amani ziwe juu yake- akiwa anashuka katika mji wa Dhul-Hulaifa, alikuwa akikusudia kufanya Hija ya kuaga, akaagiza ujumbe Asmaa kwenda kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- nini anatakiwa afanye katika hali kama hiyo? Akasema:" Koga, kisha zuia na nguo, na hirimia (Tia nia ya ibada ya Hija). Na damu ya hedhi ni kama damu ya nifasi.
Basi tunasema kwa mwanamke mwenye hedhi atakapopita eneo la kuhirimia (kutia nia), akiwa anataka kufanya Hija au Umra, tunamwambia: Koga, zuia na nguo sehemu ya damu, na hirimia. Na kujistiri maana yake ni: Aweke vizuri kipande cha nguo katika sehemu yake ya siri ya mbele, na aifunge vizuri nguo hiyo, kisha ahirimie sawa sawa iwe ni ibada ya Hija au Umra, lakini akihirimia na akafika Makka haruhusiwi kuizunguka Kaaba mpaka atwaharike. Na kwa hili alisema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia Aisha pindi alipopata hedhi akiwa katika Umra: "Fanya yote anayoyafanya mwenye kufanya Hija isipokuwa usizunguke Kaaba mpaka Utwaharike", na hii ni riwaya ya Bukhari na Muslim. Na pia katika -Sahihi Bukhari- ametaja Aisha kwamba alipotwaharika alizunguka Kaaba, na akazunguka mlima wa Swafa na Marwa, hii ikaonyesha kwamba mwanamke akihirimia kufanya ibada ya Hija au Umra, naye akiwa katika hedhi, au ilimjia hedhi kabla hajazunguka Kaaba, basi hatozunguka Kaaba na kuzunguka Swafa na Marwa mpaka atwaharike na akoge.
Ama akitufu hali ya kuwa ametwaharika, baada ya kumaliza kuzunguka Kaaba ndio ikamjia hedhi, basi ataendelea, na atazunguka Swafa na Marwa hata kama akiwa na hedhi, na atapunguza nywele zake, na Umra yake itamalizika, kwa sababu kuzunguka Swafa na Marwa hakushurutishwi kutwaharika.
Nimefika toka Yanbu'i kwa ajili ya Umra mimi na familia yangu, lakini nilivyofika Jidda, akapambazukiwa na asubuhi mke wangu akiwa na hedhi, nikakamilisha Umra peke yangu bila ya mke wangu kufanya Umra yake, ni ipi hukumu kuhusu mke wangu?
Hukumu kwa kumzingatia mke wako, ni kusubiri mpaka atwaharike, kisha akamilishe Umra yake; Kwa sababu Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-pindi Swafia- radhi za Allah ziwe juu yake- alipopata hedhi akasema: "Je itatuzuia sisi hiyo?", Wakasema: Hakika yeye alikwisha zunguka kaaba kwa ajili ya Hija, akasema: "Basi na aendelee". Kauli yake -rehema na amani ziwe juu yake-: "Je itatuzuia sisi hiyo?", Hii ni dalili ya kuwa mwanamke anatakiwa abakie akipata damu ya hedhi kabla ya kuzunguka Kaaba kwa ajili ya Hija, mpaka atwaharike kisha azunguke.
Hivyo hivyo kuzunguka Kaaba kwa ajili ya Umra ni mfano wa kuzunguka Kaaba kwa ajili ya Hija (Al-ifadhah), kwa sababu mzunguko huo ni nguzo, anapopata hedhi anayefanya ibada ya Umra kabla ya kuzunguka Kaaba basi atasubiri mpaka atwaharike kisha azunguke Kaaba.
Je eneo la kuzunguka Swafa na Marwa ni eneo takatifu? Je mwenye hedhi atasogelea eneo hilo? Je anawajibika yule atakayeingia katika eneo takatifu la kuzunguka Swafa na Marwa aswali rakaa mbili za kusalimia msikiti?
Ambalo linadhihiri eneo la kuzunguka Swafa na Marwa sio katika msikiti mtukufu, na ndio maana wameweka ukuta wenye kutenganisha baina ya msikiti na eneo la kuzunguka Swafa na Marwa, lakini ni ukuta mfupi, na hakuna shaka kwamba jambo hili ni bora kwa watu, kwa sababu lau eneo hilo lingeingizwa na kuwa katika Msikiti, angekuwa mwanamke akipata damu ya hedhi na kamaliza kutufu bado kuzunguka Swafa na Marwa angezuiliwa kuzunguka kwa sababu eneo la kuzunguka ni katika Msikiti, na mwanamke mwenye hedhi haruhusiwi kuwa humo.
Jambo ambalo ninalitolea Fatwa katika hili ni: Akipata hedhi baada kuzunguka Kaaba na kabla ya kuzunguka Swafa na Marwa, basi anaruhusiwa kuzunguka, kwa sababu sehemu ya kuzunguka Swafa na Marwa haizingatiwi kama ipo ndani ya msikiti.
Ama rakaa mbili za kuusalimia msikiti kunaweza kusemwa kuwa: Mtu akizunguka Swafa na Marwa baada ya kuzunguka Kaaba, kisha akarudi msikitini, basi ataziswali, na akiacha kuswali hana dhambi. Na lililo bora ni kuitumia fursa vizuri, na aswali rakaa mbili, kwa sababu kuswali maeneo kama hayo kuna fadhila kubwa.
Nimehiji na nikajiwa na mzunguko wa kisheria wa mwezi, nikaona haya kumwambia mtu yeyote, nikaingia katika mji mtukufu, nikaswali, nikatufu, na kuzunguka Swafa na Marwa, lipi lilo juu yangu, na ifahamike ulinijia mzunguko huo baada ya nifasi.
Haifai kwa mwanamke akiwa katika siku zake iwe ni damu ya hedhi au damu ya uzazi kwa yeye kuswali, akiwa katika mji wa Makka au mji wake au sehemu yoyote ile atakayokuwa. Hii ni kutokana na kauli ya Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kwa mwanamke: "Je hakuwa pindi akiwa katika hedhi haswali na hafungi?". Na wamekubaliana waislamu ya kuwa mwanamke mwenye hedhi haruhusiwi kufunga wala kuswali.
Na kwa mwanamke huyu aliyefanya hilo, anatakiwa atubie kwa Allah, na aombe msamaha kwa yale yaliyotokea.
Ama Twawafu yake kipindi cha hedhi sio sahihi, ama kuzunguka kwake Swafa na Marwa ni sahihi, kwa sababu kauli yenye nguvu ni kufaa kutanguliza mzunguko wa Swafa na Marwa kabla ya kuzunguka Al-Kaaba katika Hija, na juu ya hili inawajibika juu ya mwanamke huyu akazunguke Kaaba tena, kwa sababu kuzunguka Kaaba kwa ajili ya Hija ni nguzo katika nguzo za Hija, na wala hakutimii kujihalalisha kwa mara ya pili isipokuwa kwa jambo hilo.
Na juu ya hilo, mwanamike huyu haruhusiwi kuingiliwa na mumewe,-ikiwa ameolewa- mpaka azunguke Kaaba, na wala haifungiki ndoa kwakwe ikiwa hajaolewa- mpaka azunguke Kaaba- Na Allah ndiye Mjuzi zaidi.
Akipata hedhi mwanamke siku ya Arafa nini anatakiwa kufanya?
Mwanamke atakapoingia katika hedhi siku ya Arafa ataendelea kufanya Hija, na atafanya yale wanayofanya watu, na wala hatozunguka Kaaba mpaka atwaharike.
Akipata hedhi mwanamke baada ya kutupa mawe ambayo ni nguzo kubwa, na kabla ya kuzunguka Kaaba kwa ajili ya Hija, akiwa ameambatana yeye na mumewe na waliokuja nao, afanye nini, pamoja na kujua kuwa haiwezekani kurudi baada ya safari hiyo?
Ikiwa hawezi kurudi tena basi atajihifadhi na kuzunguka kwa dharura, na wala hana chochote juu yake, na atakamilisha matendo mengine ya Hija yaliyobakia.
Pindi wakitwaharika wanawake wenye damu ya nifasi (Damu ya uzazi) kabla ya siku arobaini, je Hija yao inaswihi? na wasipoona twahara ni kipi wanafanya? pamoja na kufahamu ya kuwa wametia nia ya Hija.
Wakitwaharika wanawake walio katika damu ya uzazi kabla ya siku arobaini basi wataoga, na wataswali, na watafanya yote wanayoyafanya wanawake waliotwaharika mpaka kuzunguka Kaaba; kwa sababu damu ya nifasi haina ukomo wa uchache wake.
Ama asipoona twahara basi Hija yake ni sahihi pia, lakini hatatufu kuzunguka Kaaba mpaka atwaharike;
*
Related books
All books
من أحكام الصيام
HUKUMU ZA AL-HADYU, AL-ADHWAHI NA NAMNA YA KUCHINJA.26 lughaHUKUMU ZA AL-HADYU, AL-ADHWAHI NA NAMNA YA KUCHINJA.
Hukumu za Al-hadyu (wanyama wachinjwao kama zawadi ya Msikiti Mtukufu wa Makka) na Al-adhwahi (wanyama wachinjwao siku ya Idi) na Namna ya Kuchinja. Huu ni Ujumbe mfupi uliokusanya mambo muhimu zaidi kwa Muislamu katika hukumu za wanyama wachinjwao kama sadaka, na vichinjwa vya siku ya Idi; ili Muislamu awe na elimu na uelewa wa wazi kuhusu mambo ya dini yake.
Ni nani aliyeniumba? Na ni kwa nini aliniumba?75 lughaNi nani aliyeniumba? Na ni kwa nini aliniumba?
Kila kitu kinaashiria kuwepo Muumba. Ni nani aliziumba mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake, miongoni mwa viumbe vikubwa ambavyo havijulikani ukubwa wake? Ni nani aliyetengeneza mpangilio huu mzuri zaidi katika mbingu na ardhi? Ni nani aliyemuumba mwanadamu kisha akampa usikivu, uoni na akili, na akamjalia uwezo wa kujifunza maarifa na kufahamu uhakika wa mambo? Vipi unafasiri uumbaji huu wa kiwango cha juu sana katika wa viungo vya mwili wako, na miili ya viumbe vilivyo hai? Na ni nani aliyeviumba kwa ustadi huu mkubwa? Ni namna gani inajipanga vizuri na kutulia Dunia hii iliyo kubwa,…
Sharti za swala na nguzo zake na wajibu wake11 lughaSharti za swala na nguzo zake na wajibu wake
Kimetungwa na Sheikhul Islam Al Mujaddid Imamu Muhammadi bin Abdil Wahhab -Mwenyezi Mungu amrehemu- Mwaka 1115-1206 H Amekihakiki na akashughulika nacho na akazichambua hadithi zake fakiri kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Dr. Saidi bin Ally bin Wahfu Al Qahtwaaniy Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema na Mwenye kurehemu.