Dua kutoka katika Qur'ani na Sunna
Mtunzi Mhitaji kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu "Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopindukia mipaka katika majina yake. Watakuja lipwa yale waliyokuwa wakiyatenda." Suratul-Araaf: 180. Allah (Mwenyezi Mungu), Al-Awwaal (Wa Mwanzo), Al-Aakhir (Wa Mwisho), Adh-Dhwaahir (Wa Dhahiri), Al-Baatwin (Wa Siri), Al-'Aliy (Mtukufu), Al-A'alaa (Wa juu zaidi), Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
These files are generated automatically from the book's text; their layout may differ from the printed edition.
Dua kutoka katika Qur'ani na Sunna
Mtunzi
Mhitaji kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu
Dkt. Sa'id bin Ali bin Wahf Al-Qahtwaani "Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopindukia mipaka katika majina yake. Watakuja lipwa yale waliyokuwa wakiyatenda." Suratul-Araaf: 180.
Allah (Mwenyezi Mungu), Al-Awwaal (Wa Mwanzo), Al-Aakhir (Wa Mwisho), Adh-Dhwaahir (Wa Dhahiri), Al-Baatwin (Wa Siri), Al-'Aliy (Mtukufu), Al-A'alaa (Wa juu zaidi), Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
Utangulizi
Al-Muta'aal (Mtukufu Aliye juu), Al-'Adhwiim (Mkuu), Al-Majiid (Mtukufu), Al-Kabiir (Mkubwa), As-Samii'u (Mwenye kusikia), Al-Baswiir (Mwenye kuona), Al-'Aliim (Mwenye kujua mno),
Al-Khabiir (Mwenye habari zote), Al-Hamiid (Msifiwa zaidi), Al'Aziiz (Mwenye nguvu, Mtukufu), Al-Qadiir (Muweza mno), Al-Qaadir (Mwenye uwezo), Al-Muqtadir (Mwenye uwezo juu ya kila kitu), Al-Qawiyy (Mwenye nguvu), Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, tunamsifu na tunamtaka msaada, na tunamtaka msamaha, na tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na uovu wa nafsi zetu na kutokana na ubaya wa matendo yetu. Atakayeongolewa na Mwenyezi Mungu, basi hakuna wa kumpoteza. Na atakayempoteza, basi hakuna wa kumuongoa. Na ninashuhudia kwamba hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake, bila ya mshirika, na ninashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja wake na Mtume wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na juu ya watu wa familia yake na Maswahaba wake na wote wanaomfuata kwa wema mpaka siku ya Malipo. Ama baada ya hayo:
Al-Matiin (Aliye Madhubuti), Al-Ghaniyy (Aliyejitosheleza), Al-Hakiim (Mwenye hekima), Al-Haliim (Mstahamilivu), Al-'Afuww (Msamehevu), Al-Ghafuur (Mfuta dhambi zote), Al-Ghaffaar (Mwingi wa kufuta madhambi), Huu ni muhtasari wa kitabu changu kiitwacho Adh-Dhikru wad-Du'aa wal-'ilaaju birruqaa minal-kitabi wassunnati. [3] Nimeifanyia ufipisho sehemu yake ya Dua (maombi), ili iwe rahisi kunufaika kwacho, na nimezidisha ndani yake Dua (maombi) mbalimbali, na faida zenye manufaa, akipenda Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ninamuomba Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu, Mtukufu kwa majina yake mazuri kabisa na sifa zake zilizo juu zaidi akifanye (Kitabu hiki) kiwe ni kwa ajili ya kutafuta uso wake mtukufu. Hakika Yeye ndiye msimamizi wa hilo na ndiye Mwenye uweza juu yake. [3] Na kimeshachapishwa kitabu asili kilichotajwa - na kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu - pamoja na kuelezea upokezi wa Hadithi zake kwa kina katika juzuu nne: Al-Adhkaaru (Hisnul-Muslim) katika juzuu ya kwanza na ya pili, na Dua katika juzuu ya tatu, na tiba na kisomo cha ruqya katika juzuu ya nne.
Attawwaabu (Mwingi wa kukubali Msamaha), Ar-Raqiibu (Msimamizi), Ash-Shahiidu (Mwenye kushuhudia mambo yote), Al-Hafiidhu (Mwenye Kuhifadhi), Al-Latwiifu (Mpole), Al-Qariibu (Aliye karibu), Al-Mujiibu (Mwenye kuitikia), Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu na baraka zake ziwe juu ya Nabii wetu Muhammad, na juu ya watu wa familia yake na Maswahaba wake, na wote wanaomfuata kwa wema mpaka siku ya Malipo.
Al-Waduudu (Mwenye kupenda), Ash-Shaakiru (Mwenye kushukuru), Ash-Shakuuru (Mwingi wa kushukuru), Assayyidu (Bwana), Asswamadu (Mkusudiwa), Al-Qaahiru (Mshindi wa vyote), Al-Qahhaaru (Mshindi zaidi juu ya kila kitu), Amekiandika (kitabu hiki) Sa'id bin Ali bin Wahf Al-Qahtwaani
Al-Jabbaaru (Anayefanya analolitaka), Al-Hasiibu (Mwenye kuhesabu matendo ya waja), Al-Haadii (Muongozaji), Al-Hakamu (Mwenye kuhukumu), Al-Qudduusu (Aliyetakasika), Assalaamu (Mwenye amani), Al-Barru (Mwema), Kiliandikwa mwezi Shaban 1408 Hijria
Ubora wa maombi (dua)
Al-Wahhabu (Mpaji Mkuu), Ar-Rahmaani (Mwingi wa rehema), Ar-Rahiimu (Mwingi wa kurehemu), Al-Kariimu (Mtukufu, Mkarimu), Al-Akramu (Mkarimu zaidi), Ar-Rauufu (Mpole), Al-Fattaahu (Mwingi wa kufungua),
Ar-Razzaaqu (Mwingi wa kutoa riziki), Al-Hayyu (Aliye Hai milele), Al-Qayyuumu (Msimamia yote milele), Ar-Rabbu (Mola Mlezi), Al-Maliku (Mfalme), Al-Maliiku (Mfalme Mkuu), Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na Mola wenu Mlezi amesema: 'Niombeni, nitakuitikieni. Kwa hakika wale wanaojivuna kuniabudu Mimi, wataingia Jahannam wadhalilike." [4] Surat Ghafir: 60. Na akasema Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka: "Na waja wangu watakapokuuliza kuhusu mimi, basi Mimi niko karibu. Naitika maombi ya muombaji anaponiomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka." Suratul-Baqarah: 186 Na alisema Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Dua ndiyo ibada." Kisha akasoma: "Na Mola wenu Mlezi amesema: Niombeni, nitawaitikia." [3] Na amesema Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakika Mola wenu Mlezi aliyetakasika na kutukuka ni Mwenye staha, Mkarimu. Anastahi mja wake anaponyanyua mikono yake kumuelekezea kwamba airejeshe mitupu." [4] Na amesema Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakuna Muislamu yeyote atakayeomba maombi yasiyokuwa na madhambi ndani yake wala kukata udugu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa kwa maombi hayo moja kati ya mambo matatu haya: Ima amuharakishie maombi yake, au amuwekee akiba ili amlipe akhera, au amuondoshee katika mabaya mfano wake." (Maswahaba) Wakasema: "Kwa hivyo tuzidishe?" Akasema: "Mwenyezi Mungu ni mwenye kuzidisha zaidi." [5] Abuu Daudi, 2/78, kwa nambari 1481, na At-Tirmidhiy, 5/211, kwa nambari 2959, na Ibn Majah, 2/1258, kwa nambari 3828, na Al-Albaani alisema kwamba ni hadithi sahihi katika Sahiih Al-Jaami'i Asswaghiir, 3/150 naye Ibn Majah pia akasema kwamba ni hadithi sahihi, 2/324. Imepokelewa na Abuu Daudi, 2/78, kwa nambari 1488, na Tirmidhiy, 5/557, kwa nambari 3556 na Ibn Majah, 2/1271, kwa nambari 3865. Alisema Ibn Hajar: "Mlolongo wa wasimulizi wake ni mzuri", na Al-Albaani akasema kwamba ni hadithi sahihi katika Sahih At-Tirimidhiy, 3/179. Ameipokea At-Tirmidhiy, 5/566, na 5/462, kwa nambari 3573, na Ahmad, 3/18, kwa nambari 11150. Alisema Al-Albaani kwamba ni Hadithi sahihi katika Sahih Al-Jaami'i Asswaghiir, 5/116, na katika Sahih Sunan At-Tirmidhi, 3/140.
Al-Waahidu Al-Ahadu (Aliye Mmoja wa Pekee), Al-Mutakabbiru (Mkubwa), Al-Khaaliqu (Muumbaji), Al-Khallaaqu (Mwingi wa Uumbaji), Al-Baariu (Mtengenezaji), Al-Muswawwiru (Mtia sura), Miongoni mwa adabu za dua na sababu za kujibiwa kwake [9] Tazama adabu hizi na sababu za kujibiwa kwake pamoja na ushahidi wake katika kitabu asili kiitwacho "Adhdhikru waddu'aa wal-'ilaaju birruqaa minal-kitabi wassunnati", 3-927-975.
Al-Mu-uminu (Mtoaji wa amani), Al-Muhaiminu (Mwenye kuyaendesha mambo peke yake), Al-Muhiitu (Mwenye kuzingira kila kitu), Al-Muqiitu (Mwenye kuhifadhi), Al-Wakiilu (Msimamizi Mtegemewa), Al-Kaafii (Mwenye kutosheleza), Al-Waasi'u (Mwenye Wasaa), 1. Kutakasa matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Al-Haqqu (Wa Haki), Al-Jamiilu (Mzuri), Ar-Rafiiqu (Mpole), Al-Hayiyyu (Mwenye staha), As-Sittiiru (Mwingi wa kusitiri), Al-Ilaahu (Mungu), Al-Qaabidhu (Mwenye kuzuia), 2. Aanze kwa kumsifu Mwenyezi Mungu na kumtaja kwa uzuri, kisha amuombee rehema na amani Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na vile vile amalizie kwa kumtakia rehema na amani.
Al-Baasitu (Mkunjufu), Al-Mu'utwi (Mwenye kutoa), Al-Muqaddimu (Mwenye kutanguliza), Al-Muakhkhiru (Mwenye kuchelewesha), Al-Mubiinu (Mwenye kubainisha), Al-Mannaanu (Mpaji kwa wingi), Al-Waliyyu (Msimamizi wa kila kitu), 3. Kuyapa uzito maombi hayo na kuwa na yakini kwamba yatajibiwa.
Al-Maulaa (Mola), An-Naswiiru (Mwenye kunusuru), Ash-Shaafii (Mponyaji), Maalikul-Mulki (Mmiliki wa ufalme wote), Jaami'un-naas (Mwenye kuwakusanya watu). 4. Kukithirisha maombi na kutofanya haraka ya kuitikiwa.
Nuurus-samaawaati wal-ardhi (Nuru ya Mbinguni na Ardhini), Dhul-jalaal Wal-Ikraam (Mwenye Utukufu na Ukarimu), Badii'us-samaawaati wal-ardhi (Mwanzilishi wa Mbingu na Ardhi baada ya kutokuwepo kabla).[2] 5. Moyo kuhudhuria katika dua. Tazama majina haya pamoja na ushahidi wake kutoka kwenye Qur'ani na Sunnah katika kitabu kiitwacho "Sharhu Asmaaillahil-husnaa fii dhwau-ilkitaabi wassunnah, cha Mtunzi huyu huyu.
6. Kuomba katika kipindi cha faraja na dhiki.
7. Asiombwe isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake.
8. Kutomuapiza mke, mali, mtoto na mtu binafsi.
9. Kushusha chini sauti wakati wa maombi, iwe baina ya kuishusha chini na kuidhihirisha.
10. Kukiri makosa, na kutaka msamaha wa makosa hayo, na kukiri neema, na kumshukuru Mwenyezi Mungu juu yake.
11. Kutojisumbua kuomba maombi yaliyopangika kwa vina.
12. Kujishusha chini, na kunyenyekea, na kuwa na hamu na hofu.
13. Kurejesha vitu vilivyochukuliwa kwa dhuluma pamoja na kutubia.
14. Kuomba mara tatu tatu.
15. Kuelekea kibla.
16. Kunyanyua mikono wakati wa kuomba.
17. Kushika udhu kabla ya kuomba kama hilo litakuwa jepesi.
18. Asivuke mipaka katika maombi.
19. Aanze kujiombea mwenyewe pindi atakapomuombea mtu mwingine.[10] Imethibiti kutoka kwa Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kuwa alianza kujiombea mwenyewe, na vile vile imethibiti kuwa hakuanza kujiombea mwenyewe, kama alivyomuombea Anas, na bin Abbas, na Ummu Ismail na wengineo. Tazama ufafanuzi wa kina katika mambo haya ndani ya kitabu kiitwacho "Sharh Annawawiy liswahih muslim", 15/144, na "Tuhfatul-ahwadhii sharh sunan Attirmidhiy", 9/328, "Fat-hul-baari sharh sahih Al-bukhaari", 1/281.
20. Atumie majina mazuri kabisa ya Mwenyezi Mungu na sifa zake zilizo za juu kabisa kufika kwa Mwenyezi Mungu, au atumie matendo mema aliyoyafanya muombaji, au kwa kuombewa na mtu mwema aliye hai na aliyepo.
21. Kiwe chakula chake, kinywaji chake na mavazi yake ni vya halali.
22. Asiombe ubaya au kukata udugu.
23. Aamrishe mema na akataze maovu.
24. Ajiweke mbali na kila aina ya maasi.
Nyakati, hali na sehemu zinazojibiwa ndani yake dua [11] Tazama nyakati hizi na hali na sehemu pamoja na ushahidi wake kwa ufafanuzi wa kina katika kitabu asili kiitwacho "Sharh Annawawiy liswahih muslim", 3/975-1117.
1. Usiku wa Cheo (unapatikana ndani ya siku kumi za mwisho za Mwezi wa Ramadhani).
2. Masaa ya mwisho ya usiku karibu na Alfajiri.
4. Baada ya swala za lazima.
4. Baina na adhana na kusimama kwa swala
5. Wakati maalumu katika kila usiku (ni muda wa kujibiwa).
6. Wakati wa adhana ya swala za lazima.
7. Mvua inaponyesha.
8. Wakati jeshi linapotembea kwenye safu kupigania njia ya Mwenyezi Mungu.
9. Wakati maalumu katika siku ya Ijumaa.
Na kauli yenye nguvu zaidi kuhusu wakati huo ni kwamba ni wakati wa mwisho katika nyakati za Alasiri siku ya Ijumaa, na inaweza ikawa ni wakati wa hotuba na swala ya Ijumaa.
10. Wakati wa kunywa maji ya Zamzam pamoja na kuwa na nia ya ukweli.
11. Katika sijida.
12. Wakati unapozinduka kutoka kwenye usingizi wa usiku, na kuomba maombi yaliyothibiti katika wakati huo.
13. Atakapolala akiwa katika hali ya twahara kisha akazinduka usiku na akaomba.
14. Wakati wa kuomba: Laa ilaha illa anta sub-haanaka inni kuntu mina dhaalimin (Hakuna mungu isipokuwa Wewe. Hakika mimi nilikuwa katika madhalimu).
15. Maombi ya watu baada ya kifo cha mtu.
16. Kuomba baada ya kumsifia Mwenyezi Mungu na kumtakia rehema Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake katika kikao cha Tahiyyatu ya mwisho.
17. Wakati wa kumuomba Mwenyezi Mungu kwa jina lake kuu zaidi ambalo akiombwa dua kwalo, huitikia, na akihitajiwa kwalo, hutoa. [12] Tazama jina kuu zaidi la Mwenyezi Mungu kwenye hadithi nambari 203, na nambari 104, na nambari 105 katika kitabu hiki.
18. Muislamu anapomuombea ndugu yake Muislamu bila ya yeye kuwepo.
19. Maombi ya siku ya Arafa katika uwanja wa Arafa.
20. Maombi ndani ya Mwezi wa Ramadhani.
21. Maombi pindi wanapojikusanya Waislamu katika vikao vya kumtaja Mwenyezi Mungu.
22. Wakati wa kuomba pindi mtu anapopatwa na matatizo kwa kusema: Inna lillaahi wa innaa ilaihi raaji'uuni. Allaahumma ajurnii fii muswiibatii, wa akh-lif lii khairan minha (Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika kwake tutarejea. Ewe Mwenyezi Mungu, nilipe katika msiba wangu huu na unipe badala bora kuliko hilo).
23. Kuomba wakati moyo unapokuwa umemuelekea Mwenyezi Mungu, na wakati mtu anapofanya matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake.
24. Maombi ya aliyedhulumiwa dhidi ya mwenye kumdhulumu.
25. Maombi ya mzazi kumuombea mtoto wake, na mzazi anapomuapiza mtoto wake.
26. Maombi ya msafiri.
27. Maombi ya mtu mwenye funga mpaka atakapofungua.
28. Maombi ya mtu mwenye funga wakati anapofungua.
29. Maombi ya mtu mwenye dhiki kubwa sana.
30. Maombi ya imamu muadilifu.
31. Maombi ya mtoto mwema kwa wazazi wake.
32. Maombi baada ya kutawadha pindi anapoomba dua iliyothibiti katika hilo.
33. Maombi baada ya kutupa vijiwe kwenye Jamrat assughraa wakati wa Hija.
34. Maombi baada ya kutupa vijiwe kwenye Jamrat alwustwaa wakati wa Hija.
35. Maombi wakati unapokuwa ndani ya Al-ka'aba. Na atakayeswalia ndani ya uzio wa Ismail (unaoambatana na Al-ka'aba), kwani huo ni sehemu katika Al-ka'aba.
36. Maombi anapokuwa mtu juu ya Swafa (kwa wafanyao ibada ya Hija au Umra).
37. Maombi anapokuwa mtu juu ya Marwa (kwa wanaofanya ibada ya Hija au Umra).
38. Maombi ya mtu anapokuwa Muzdalifa (sehemu inayofuata baada ya kutoka Arafa).
Na Muumini anafaa kumuomba Mola wake Mlezi daima popote atakapokuwa. Amesema Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka: "Na waja wangu watakapokuuliza kuhusu Mimi, basi Mimi kwa hakika nipo karibu. Ninaitikia maombi ya muombaji anaponiomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka." [13] Suratul-Baqarah: 186. Lakini nyakati hizi, na hali, na sehemu hizi zinafaa kupewa kipaumbele wakati wa kuomba.
Dua kutoka katika Qur'ani na Sunna
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, na rehema na amani ziwe juu ya yule ambaye hakuna nabii baada yake.
1. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu 2. Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote 3. Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu 4. Mmiliki wa siku ya Malipo 5. Ni wewe peke yako tunayekuabudu na ni wewe peke yako tunayekutaka msaada 6. Tuongoe njia iliyonyooka 7. Njia ya wale uliowaneemesha. Siyo ya wale waliokasirikiwa, wala waliopotea. [14] Suratul- Faatiha: 1-7
2. Ewe Mola wetu Mlezi! Tukubalie! Hakika Wewe ndiye Msikivu, Mwenye kujua yote.[15] Suratul-Baqarah: 127
3. Na tusamehe makosa yetu, hakika Wewe ni mwenye kukubali zaidi msamaha, Mwingi wa kurehemu.[16] Suratul-Baqarah: 128
4. Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema na akhera tupe mema na utukinge kutokana na adhabu ya Moto.[17] Suratul-Baqarah: 201
5. Tumesikia na tumetii. Tunakutaka maghufira Mola wetu Mlezi! Na marejeo ni kwako. [18] Suratul Baqara: 285
6. Mola wetu Mlezi! Usituchukulie ubaya tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama uliyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi! Usitutwike tusiyoyaweza, na uyatupilie mbali mabaya yetu, na utusamehe na uturehemu. Wewe ndiwe Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi dhidi ya kaumu ya makafiri. [19] Suratul Baqara: 286
7. Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kutuongoa, na tutunuku rehema itokayo kwako. Hakika, Wewe ndiwe Mwenye kutunuku mno." [20] Surat Al Imraan: 8
8. "Mola wetu Mlezi! Hakika, sisi tumeamini. Basi tusamehe dhambi zetu, na tuepushe na adhabu ya Moto." [21] Surat Al-Imran: 16
9. "Mola wangu Mlezi! Nitunuku kutoka kwako dhuria (kizazi) chema. Hakika, Wewe ndiye unayesikia maombi." [22] Surat Al-Imran: 38
10. "Mola wetu Mlezi! Tuliyaamini uliyoyateremsha, na tulimfuata Mtume huyu, basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia." [23] Surat Al-Imran: 53
11. "Mola wetu Mlezi! Tufutie dhambi zetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na isimamishe imara miguu yetu na utunusuru dhidi ya kaumu ya makafiri." Surat Al-Imran: 147
12. "Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Sub-haanaka (umetakasika)! Basi tukinge kutokana na adhabu ya Moto. 192. Mola wetu Mlezi! Hakika, yule unayemuingiza Motoni, basi umemhizi (umemfedhehesha). Na waliodhulumu hawana wasaidizi wowote. 193. Mola wetu Mlezi! Hakika, sisi tumemsikia muitaji akiita kwenye Imani kwamba: Muaminini Mola wenu Mlezi; kwa hivyo, tukaamini. Basi tufutie dhambi zetu, na utufunikie makosa yetu, na utufishe pamoja na walio wema. 194. Mola wetu Mlezi! Na utupe yale uliyotuahidi kwa Mitume wako, wala usituhizi (usitufedheheshe) Siku ya Kiyama. Hakika, Wewe huvunji miadi." [25] Surat Al Imraan: 191-194
13. "Mola wetu Mlezi! Tuliamini, basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia." [26] Surat Al-Maaidah: 83
14. "Mola wetu Mlezi! Tumezidhulumu nafsi zetu, na kama hutatufutia dhambi na ukaturehemu, hakika tutakuwa katika waliohasirika." [27] Suratul A'araaf: 23
15. "Mola wetu Mlezi! Usitujaalie kuwa pamoja na kaumu madhalimu." [28] Suratul A'araaf: 47
16. Ewe Mwenyezi Mungu, "Wewe ndiye rafiki mlinzi wetu. Basi tusitiri dhambi na uturehemu. Na Wewe ndiwe Mbora zaidi wa wasitirio dhambi. Na utuandikie mema katika dunia hii na katika Akhera." [29] Suratul A'araaf: 155-156
17. "Mwenyezi Mungu ananitosha. Hakuna mungu isipokuwa Yeye tu. Mimi ninamtegemea Yeye, na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi." [30] Surat At-Taubah: 129
18. "Mola wetu Mlezi! Usitufanye wenye kutiwa majaribio na hao kaumu madhalimu. 86. Na utuokoe kwa rehema yako kutokana na kaumu hawa makafiri." [31] Surat Yuunus: 85-86
19. "Mola wangu Mlezi! Hakika mimi ninajikinga kwako kutokukuomba nisilo na elimu nalo. Na kama hunisamehe na kunirehemu, nitakuwa katika waliopata hasara." [32] Surat Hud: 47
20. Ewe Mwenyezi Mungu, ewe "Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ndiye Mlinzi wangu katika dunia na Akhera. Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu na niunganishe na walio wema." [33] [Surat Yusuf: 101] [10]. [10] Angalia kwa ajili ya faida: Kitabu Al-Fawaaidi cha Ibn Qayyimi, Ukurasa wa 436-437.
21. "Ewe Mola wangu Mlezi! Ujalie mji huu uwe wa amani, na uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu." [34] Surat Ibrahim: 35
22. "Mola wangu Mlezi! Nijalie niwe mwenye kusimamisha Swala, na katika dhuria yangu pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu." [35] Surat Ibrahim: 40
23. "Mola wetu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku itakaposimama hesabu." [36] Surat Ibrahim: 41
24. "Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uongofu katika jambo letu." [37] Suratul-Kahf: 10
25. "Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu. 26. Na nirahisishie kazi yangu hii. 27. Na lifungue fundo lililo katika ulimi wangu." [38] Surat At-Twaha: 25-28
26. "Mola wangu Mlezi! Nizidishie elimu." [39] Surat Twaha: 114
27. "Hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Wewe, utakasifu ni wako. Hakika mimi nilikuwa katika madhalimu." [40] Surat Al-Anbiya: 87
28. "Mola wangu Mlezi! Usiniache peke yangu, na Wewe ndiye Mbora wa wanaorithi." [41] Surat Al-Anbiya: 89
29. "Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashetani. 98. Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie." [42] Suratul-Muuminun: 97-98
30. "Mola wetu Mlezi! Tumeamini; basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanaorehemu." [43] Suratul-Muuminun: 109
31. "Mola wangu Mlezi, Samehe na urehemu nawe ni Mbora wa wanaorehemu."[44] Suratul-Muuminun: 118
32. "Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannam. Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimuachi." 66. Hakika hiyo ni kituo na makao mabaya."[45] Surat Al-Furqaan: 65-66
33. "Mola wetu Mlezi! Tupe katika wake zetu na wana wetu yaburudishayo macho, na utujalie tuwe viongozi kwa wacha Mungu." [46] Surat Al-Furqaan: 74
34. "Mola wangu Mlezi! Nitunuku hukumu na uniunganishe na walio wema. Na unijalie nitajwe kwa wema na watu watakaokuja baadaye. Na unijalie katika warithi wa Bustani za neema." [47] Surat Ash-shu'araa: 83-85
35. "Wala usinihizi (usinifedheheshe) Siku watakapofufuliwa. 88. Siku ambayo mali haitafaa kitu wala wana. 89. Isipokuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi." [48] Surat Ash-shu'araa: 87-89
36. "Ewe Mola wangu Mlezi! Nizindue niishukuru neema yako uliyonineemesha mimi na wazazi wangu, na nipate kutenda mema uyapendayo, na uniingize kwa rehema yako katika waja wako wema." [49] Surat An-Naml: 19
37. "Mola wangu Mlezi, hakika mimi nimejidhulumu mwenyewe. Basi nisamehe." [50] Surat Al-Qasas: 16
38. "Mola wangu Mlezi, niokoe kutokana na watu madhalimu."[51] Surat Al-Qasas: 21
39. "Huenda Mola wangu Mlezi akaniongoa njia iliyo sawa." [52] Surat Al-Qasas: 22
40. "Mola wangu Mlezi, hakika mimi ni mhitaji wa heri utakayoniteremshia." [53] Surat Al-Qasas: 24
41. "Ewe Mola wangu Mlezi, ninusuru kutokana na watu waharibifu hawa!" [54] Suratul-Ankabuut: 30
42. "Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunuku aliye miongoni mwa watenda mema." [55] Surat Asswaafaat: 100
43. "Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizonineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayoyapenda. Na unitengenezee dhuria zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu."[56] Suratul-Ahqaaf: 15
44. "Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani, wala usijalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu mno." [57] Suratul-Hashr: 10
45. "Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea na kwako tunajikurubisha na kwako ndio marejeo." [58] Suratul-Mumtahina: 4
46. "Mola wetu Mlezi! Usitufanyie mtihani kwa waliokufuru. Na tusamehe, Mola wetu Mlezi. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima." [59] Suratul-Mumtahinah: 5
47. "Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliyeingia nyumbani mwangu akiwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake." [60] Surat Nuuh: 28
48. "Mola wetu Mlezi! Tukamilishie nuru yetu na utusamehe. Hakika Wewe ni muweza wa kila kitu." [61] Surat At-Tahriim: 8
49. "Ewe Mwenyezi Mungu! Niongoze mimi kwa yale ambayo watu hutofautiana kwayo katika haki kwa idhini yako. Hakika Wewe humuongoa umtakaye katika njia iliyonyooka." [62] Haya yametoholewa kutoka katika Suratul-Baqarah: 213.
50. Ewe Mwenyezi Mungu! Nipe hekima ambazo mwenye kupewa hekima hizo, basi hakika atakuwa amepewa heri nyingi. [63] Haya yametoholewa kutoka katika Suratul-Baqarah: 269.
51. Ewe Mwenyezi Mungu, niimarishe mimi kwa kauli iliyo thabiti katika maisha ya duniani na maisha ya Akhera. [64] Haya yametoholewa kutoka katika Surat Ibrahim: 27.
52. Ewe Mwenyezi Mungu, tupendezee imani na uipambe ndani ya nyoyo zetu, na utufanye tuuchukie ukafiri, uovu, upotovu na uasi, na utujalie kuwa miongoni mwa walioongoka. [65] Haya yametoholewa kutoka katika Suratul-Hujraat: 7.
53. Ewe Mwenyezi Mungu! Nikinge na choyo ya nafsi yangu, na unijalie kuwa miongoni mwa waliofaulu. [66] Haya yametoholewa kutoka katika Surat At-Taghaabun: 16.
54. "Ewe Mwenyezi Mungu! Tupe hapa katika Dunia (mambo) mazuri, na Akhera utupe mazuri na utukinge kutokana na adhabu ya Moto." [67] Bukhari, kwa nambari 4522, na nambari 6389, na Muslim, kwa nambari 2690.
55. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na majaribu ya Moto na adhabu ya Moto, na kutokana na majaribu ya kaburi na adhabu ya kaburi, na kutokana na uovu wa majaribu ya utajiri, na uovu wa majaribu ya umasikini. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na uovu wa Masihi Dajali. Ewe Mwenyezi Mungu, usafishe moyo wangu kwa maji ya theluji na barafu, na utakase moyo wangu kutokana na makosa kama jinsi ulivyoitakasa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na uweke mbali baina yangu na baina ya makosa yangu kama ulivyoweka mbali baina ya Mashariki na Magharibi. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na uvivu, madhambi na vitu vitakavyonigharimu (madeni). [68] Bukhari, kwa nambari 832, na Muslim, kwa nambari 589.
56. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa, na uvivu, na woga, na ukongwe, na ubahili, na ninajikinga kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na kutokana na majaribu ya uhai na kifo. [69] Bukhari, kwa nambari 2823, na Muslim kwa nambari 2706.
57. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na balaa nzito, na kupatwa na upotofu, na hukumu mbaya, na furaha ya maadui (juu ya msiba wangu).[70] Bukhari kwa nambari 6347, na Muslim kwa nambari 2707, na matamshi yake ni: Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akijikinga kutokana na kupatwa na ugumu wa balaa, na kupatwa na ususuwavu, na hukumu mbaya na furaha ya maadui (juu ya msiba wangu)."
58. Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu, na unitengenezee dunia yangu ambayo kunapatikana maisha yangu, na unitengenezee Akhera yangu ambako kunapatikana kuishi kwangu milele, na unijalie ziada ya uhai kwenye kila lenye heri, na ujalie kifo ni kitulizo changu kutokana na kila shari. [71] Imepokelewa na Muslim, kwa nambari 2720.
59. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba uongofu, ucha Mungu, kujizuia na machafu na kuwa ni mwenye kutosheka. [72] Imepokelewa na Muslim, nambari (2721).
61. Ewe Mwenyezi Mungu, niongoze na unipe msimamo wa sawasawa. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba uongofu na msimamo wa sawasawa. [74] Imepokelewa na Muslim, nambari (2725).
62. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kuondokewa neema zako, na kubadilika kwa salama yako, na kufikiwa ghafla na adhabu zako, na kila aina ya hasira zako.[75] Imepokelewa na Muslim, nambari (2739).
63. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na uovu wa yale niliyofanya, na kutokana na uovu wa yale nisiyoyafanya. [76] Imepokelewa na Muslim, nambari (2716).
64. Ewe Mwenyezi Mungu, ziongeze mali zangu, na watoto wangu, na unibariki mimi kwa kile unachonipa. [77] [Na refusha maisha yangu katika kukutii Wewe. Na yafanye matendo yangu kuwa mazuri], na nisamehe. [78] Haya yanaashiriwa na maombi ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, aliyomuombea Anas: "Ewe Mwenyezi Mungu, muongezee mali zake, na watoto wake, na mbariki katika kile ulichompa." Ameipokea hadithi hii Bukhari kwa nambari 1982, na Muslim kwa nambari 660. Ameipokea Bukhari katika kitabu chake kiitwacho "Al-Adabu Al-Mufrad" kwa nambari 653. Al-Albaaniy alisema kwamba ni hadithi sahihi katika kitabu kiitwacho "Silsilatul-Ahaadiithi As-Swahiihaa" kwa nambari 2241, na katika "Swahih Al-Adabil-Mufrad" ukurasa 244. Na yale yaliyo baina ya mabano yanaashiriwa na kauli yake Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alipoulizwa: Ni watu gani walio bora? Akasema: "Ni yule ambaye umri wake utakuwa mrefu na matendo yake yakawa mazuri." Ameipokea hadithi hii At-Tirmidhiy kwa nambari 2329 na Ahmad kwa nambari 17716. Al-Albaaniy alisema kwamba ni hadithi sahihi katika "Swahih At-Tirmidhiy" 2/271. Nilimuuliza shekhe wetu Ibn Baaz, Mwenyezi Mungu amrehemu, juu ya kuomba kwa maombi hayo, je ni sunnah? Akasema: "Ndiyo."
65. Hapana mungu apasaye kuabadiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Mkuu, Mpole. Hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi. Hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mbingu na Mola Mlezi wa ardhi, na Mola Mlezi wa Kiti Kitukufu cha Enzi.[79] Bukhari nambari 6345, na Muslim nambari 2730.
66. Ewe Mwenyezi Mungu, rehema zako ndizo ninazozitarajia. Basi usiniache kujitegemea mwenyewe kwa kiasi cha mpepeso wa jicho, na unitengenezee mambo yangu yote. Hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe. [80] Ameipokea Abu Daud kwa nambari 5090, na Ahmad 5/42, na Al-Albaaniy akasema kwamba ni nzuri katika "Swahih Abi Daud" 3/250, na katika "Swahih Al-Adabil-Mufrad, kwa nambari 260, na vilevile mwanazuoni mkubwa Ibn Baaz alisema kwamba mlolongo wa wasimulizi wake ni mzuri katika kitabu kiitwacho "Tuhfatul-Akhyaar" ukurasa wa 24.
67. Hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Wewe, utakasifu ni wako. Hakika mimi nilikuwa katika madhalimu. [81] Tirmidhi nambari 3505, na Al-Hakim na akasema kwamba ni hadithi sahihi, na Imam Adh-Dhahaby akakubaliana naye katika hilo 1/505. Vile vile, Al-Albaaniy alisema kwamba ni hadithi sahihi katika "Swahih At-Tirmidhi 3-168, na matamshi yake ni: Maombi ya dhin nuun pindi alipomuomba Mwenyezi Mungu ilhali yuko ndani ya tumbo la chewa: An laa ilaha illa anta sub-haanaka inni kuntu minadhdhwaalimiin (Hapana mungu ila Wewe. Hakika mimi nilikuwa katika madhalimu). Kwani, hataomba mtu Muislamu kwa maombi haya katika kitu chochote kile isipokuwa Mwenyezi Mungu atamuitikia maombi yake.
68. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mja wako, mtoto wa mja wako, mtoto wa kijakazi wako. Nywele zangu za utosi zipo mkononi mwako. Hukumu zako kwangu ni zenye kupita, na maamuzi yako kwangu ni ya uadilifu. Ninakuomba kupitia kila jina lako, ulilojiita kwalo mwenyewe, au uliloteremsha ndani ya Kitabu chako, au ulilomfundisha yeyote katika viumbe wako, au ulilificha ndani ya elimu ya ghaibu iliyo kwako, kwamba uifanye Qur'ani ndiyo kitulizo cha moyo wangu, na mwangaza wa kifua changu, na kiondoshaji cha huzuni yangu, na kimalizaji cha msongo wa mawazo yangu. [82] Ahmad nambari 1/391-452, Al-Haakim nambari 1/509, na Al-Haafidh Ibn Hajar akasema kwamba ni hadithi nzuri katika "Takhriij Al-Adhkaar", na vile vile Al-Albaaniy akasema kwamba ni hadithi sahihi katika "Takhriij Al-Kalim At-Twayyib" ukurasa wa 73.
69. Ewe Mwenyezi Mungu, Mwenye kuzigeuza nyoyo, geuza nyoyo zetu kwenye utiifu wako. [83] Ameipokea Muslim kwa nambari 2654.
70. Ewe Mwenye kuzigeuza nyoyo, uimarishe moyo wangu katika Dini yako. [84] At-Tirmidhi kwa nambari 3522, na Ahmad 4/182, na Al-Haakim 1/525-528 na akasema kwamba ni Hadithi sahihi, na Adhdhahabiy akakubaliana naye, na Al-Albaaniy akasema kwamba ni hadithi sahihi "Swahiih Al-Jaamii", 6/309, na katika "Swahiih At-Tirmidhi" 3/171. Alisema Ummu Salama, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Haya ndiyo maombi aliyokuwa Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akiyaomba sana.
71. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba unipe salama Duniani na Akhera. [85] Ameipokea At-Tirmidhi kwa nambari 3514, na Bukhari katika "Al-Adabul-Mufrad" kwa nambari 726, na tamshi lake kwa upokezi wa Tirmidhi ni: "Muombeni Mwenyezi Mungu salama katika dunia na akhera." Na katika tamshi lingine: "Muombeni Mwenyezi Mungu msamaha na salama, kwani mmoja wenu hakupewa baada ya yakini kilicho bora kuliko kuwa salama." Al-Albani alisema kwamba ni hadithi sahihi katika "Swahiih Ibn Majah" 3/180 na 3/185, na 3/170, na ina ushahidi mbalimbali, utazame ushahidi huo katika "Musnad Imam Ahmad" kwa upangiliaji wa Ahmad Shaakir, 1/156-157.
72. "Ewe Mwenyezi Mungu, ufanye mwisho wetu kuwa mzuri katika mambo yetu yote, na tukinge kutokana na hizaya ya dunia na adhabu za akhera." [86] Ahmad 4/181, na Twabaraniy katika kitabu kiitwacho "Al-Kabiir" 2/33/1169, na katika "Dua" kwa nambari 1436, na Ibn Hibaan kwa nambari 2424, 2425 katika (Mawaarid). Alisema Al-Haafidh Al-Haithamiy katika "Majmaa Az-Zawaaid" 10/178: "Wapokezi wa Ahmad na moja ya mtiririko wa wasimulizi wa Twabaraniy ni wa kuaminika."
"Mola wangu Mlezi, nisaidie na wala usiwasaidie wengine dhidi yangu. Na ninusuru na wala usiwanusuru wengine dhidi yangu. Na wafanyie vitimbi kwa niaba yangu (maadui zangu), na wala usifanye vitimbi dhidi yangu. Na niongoze na ufanye wepesi uongofu kwangu. Na ninusuru dhidi ya kila aliyevuka mipaka dhidi yangu. Mola wangu Mlezi, nifanye niwe ni mwenye kukushukuru, mwenye kukutaja, mwenye kukuogopa, mwingi wa utiifu kwako, niwe mwenye kukunyenyekea, kurudi kwako sana. Mola wangu Mlezi, nikubalie toba yangu, na yatakase madhambi yangu, na niitikie maombi yangu, na imarisha hoja zangu, na uongoze moyo wangu, na upe ulimi wangu msimamo wa sawasawa, na niondoshee husuda ndani ya moyo wangu." [87]. Bukhari katika "Al-Adabul-Mufrad" nambari 664-665, na Abu Daud nambari 1510-1511, Tirmidhiy nambari 3551, na Ibn Maajah nambari 3830, na Ahmad 1/127 na Al-Haakim na akasema kwamba ni sahihi, na Adh-Dhahabiy akakubaliana naye katika hilo, 1-519, naye Al-Albaniy akasema pia kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahih Abi Daud" 1/414, na katika "Sahih At-Tirmidhiy" 3/178.
74. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika sisi tunakuomba heri alizokuomba kwazo nabii wako Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - na tunajikinga kwako kutokana na shari alizojikinga kwako nabii wako Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na Wewe ndiye mwenye kutakwa msaada, na ni juu yako kufikisha tu, na hapana uwezo wala nguvu isipokuwa ni kwa Mwenyezi Mungu." [88] At-Tirmidhiy nambari 3521, na Ibn Maajah nambari 3846 kwa maana yake. Alisema At-Tirmidhiy: Hadithi hii ni nzuri, na si ya kawaida (Hasanun Ghariib). Na Al-Albaani akasema kwamba ni hadithi dhaifu katika kitabu kiitwacho "Dhaif At-Tirmidhiy" ukurasa wa 387.
75. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na shari za masikio yangu, na kutokana na shari za macho yangu, na kutokana shari za ulimi wangu, na kutokana na shari za moyo wangu, na kutokana na shari za matamanio yangu." [89] Abu Daud kwa nambari 1551, na Tirmidhiy kwa nambari 3492, na Nasaai kwa nambari 5470, na wengineo. Alisema Al-Albaaniy kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahih At-Tirmidhiy" 3/166, na katika "Sahih An-Nasaai" 3/1108.
76. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na ukoma, na mbaranga, na wendawazimu, na kutokana na maradhi mabaya." [90] Abu Daud kwa nambari 1554, na Nasaai kwa nambari 5493, na Ahmad 3/192, na Al-Albaaniy alisema kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahihi An-Nasaai" 3/1116, na katika "Sahih At-Tirmidhiy" 3/184.
77. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na tabia mbovu, na matendo mabaya, na matamanio mabaya." [91] At-Tirmidhiy kwa nambari 3591, na Ibn Hibaan kwa nambari 2422 (Mawaarid), na Al-Haakim 1/532, na Twabaraaniy katika kitabu kiitwacho "Al-Kabiir" 36/19/19, na Al-Albaaniy akasema kwamba ni hadithi sahihi katika kitabu kiitwacho "Sahih At-Tirmidhiy" 3/184.
78. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika Wewe ni Msamehevu, Mkarimu, unapenda kusamehe, basi nisamehe." [92] At-Tirmidhiy kwa nambari 3513, na An-Nasaai katika kitabu cha "Al-Kubraa" kwa nambari 7712, na Al-Albaaniy alisema kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahih At-Tirmidhiy" 3/170.
79. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba kufanya matendo yenye heri, na kuacha mambo yenye kuchukiza, na kuwapenda masikini, na unifutie madhambi yangu, na unirehemu. Unapokusudia kuwajaribu watu, basi nifishe hali ya kuwa si mwenye kutiwa katika majaribu hayo. Na ninakuomba kukupenda, na kumpenda anayekupenda, na kupenda matendo yanayonisongeza kwenye mapenzi yako."[93] Ameipokea Ahmad kwa tamko la Hadithii hii 5/243, na At-Tirmidhiy kwa nambari 3235 kwa mfano wa Hadithi hii, na akasema kwamba ni hadithi nzuri, na akasema: "Nimemuuliza Muhammad Ibn Ismail - akimkusudia Bukhari - akasema: 'Hadithi hii ni nzuri tena sahihi (Hasanun Sahih)." Na mwisho wa Hadithi akasema Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hayo ni haki, basi yasomeni na mjifunze." Na Al-Haakim 1/521, naye Al-Albaaniy akasema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih At-Tirmidhiy" 3/318.
80. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba (unipe) katika heri zote; zile za haraka na zinazochelewa, kwa ninayoyajua na nisiyoyajua. Na ninajikinga kwako kutokana na shari zote zinazokuja haraka na zinazochelewa, ninazozijua na nisizozijua. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba (unipe) miongoni mwa heri alizokuomba kwazo mja wako na nabii wako, na ninajikinga kwako (uniepushe) kutokana na shari alizojikinga kwako mja wako na nabii wako. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba Pepo, na yanayomtia mtu karibu yake miongoni mwa kauli au matendo, na ninajikinga kwako kutokana na Moto na yanayomtia mtu karibu yake miongoni mwa kauli au matendo, na ninakuomba ujalie kila hukumu utakayonihukumia iwe ni heri." [94] Ameipokea Abu Daud kwa nambari 3846 kwa matamshi ya Hadithi hii hii, na Ahmad 6/134 na matamshi ya ziada ya pili, imepokelewa na Al-Haakim na akasema kwamba ni sahihi, na Adh-Dhahaby akakubaliana naye 1/521, na matamshi ya ziada ya kwanza ni mapokezi yake. Vile vile Al-Albaaniy alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih Ibn Maajah" 2/327.
81. "Ewe Mwenyezi Mungu, nihifadhi kwa Uislamu nikiwa nimesimama. Na nihifadhi kwa Uislamu nikiwa nimekaa. Na nihifadhi kwa Uislamu nikiwa nimelala. Na usinijalie kuwa ni mwenye kufurahikiwa na adui zangu au hasidi wangu kwa sababu ya misiba yangu. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba (unipe) kutoka katika kila heri ambayo hazina zake ziko mkononi mwako. Na ninajikinga kwako kutokana na kila shari ambayo hazina zake ziko mkononi mwako." [95] Al-Haakim 1/525 na akasema ni hadithi sahihi, na Adh-Dhahabiy akakubaliana naye. Vile vile, Al-Albaaniy alisema ni hadithi nzuri (Hasan) katika "Sahihi Al-Jaamii" 2/398, na katika "Silsilat Al-Ahaadiith Asswahiiha" 4/54 kwa nambari 1540.
82. "Ewe Mwenyezi Mungu, tugawie sehemu katika kukuogopa ambayo kwayo utazuia baina yetu na kukuasi. Na katika kukutii ambako kwa hilo utatufikisha katika Pepo yako. Na yakini ambayo kwayo utatupunguzia matatizo ya dunia. Ewe Mwenyezi Mungu, tustareheshe kupitia masikio yetu na macho yetu na nguvu zetu kwa muda ambao utatupa uhai. Na uvijalie viwe ni vyenye kubakia. Na ujalie kisasi chetu juu ya wenye kutudhulumu. Na utunusuru dhidi ya aliyetufanyia uadui. Na usijalie matatizo yetu kuwa katika dini yetu. Na usiifanye dunia kuwa ndiyo jambo muhimu zaidi kwetu, wala kuwa ndiyo kiwango cha juu zaidi cha elimu yetu, wala usimpe mamlaka juu yetu mtu asiyetuhurumia." [96] At-Tirmidhiy kwa nambari 3502, na Al-Haakim 1/528 na akasema kwamba ni sahihi, na Adh-dhahabiy akakubaliana naye, vile vile Ibn Sunniy kwa nambari 446. Na Al-Albaaniy akasema kwamba ni Hadithi nzuri (Hasan) katika "Sahih At-Tirmidhiy" 3/168 na katika kitabu kiitwacho "Sahih Al-Jaamii" 1/400.
83. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na uoga, na ninajikinga kwako kutokana na ubahili, na ninajikinga kwako kutorudi kwenye umri wenye udhalili, na ninajikinga kwako kutokana na majaribu ya dunia na adhabu za kaburi." [97] Bukhari kwa nambari 2822.
84. "Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe makosa yangu, na ujinga wangu, na kupindukia kwangu mipaka katika mambo yangu, na kwa yale ambayo Wewe unayafahamu zaidi kuliko mimi. Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe mambo ninayoyafanya kwa mzaha, na kwa kuyapa uzito, na kwa kukosea, na kwa kukusudia, na yote hayo ni juu yangu."[98] Wamekubaliana juu ya usahihi wa Hadithi hii, Bukhari kwa nambari 6398 na Muslim kwa nambari 2719.
85. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu dhuluma nyingi, na hakuna wa kufuta madhambi isipokuwa Wewe. Basi nisamehe msamaha utokao kwako, na unihurumie. Hakika Wewe ni Msamehevu, Mwingi wa kurehemu." [99] Wamekubaliana juu ya usahihi wa Hadithi hii, Bukhari kwa nambari 834, na Muslim nambari 2705.
85. "Ewe Mwenyezi Mungu, nimejisalimisha kwako, na kwako nimeamini, na juu yako nimetegemea, na kwako nimejisogeza, na kwa ajili yako ninapambana. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwa utukufu wako, hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe, kwamba usije nipoteza. Wewe ndiye uliye hai ambaye hafi, na majini na watu wanakufa." [100] Wamekubaliana juu ya usahihi wa Hadithi hii, Bukhari kwa nambari 6398 na Muslim kwa nambari 2719.
87. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika sisi tunakuomba sababu za kupata rehema zako, na sababu zitakazotia nguvu kupata msamaha wako, na kupata salama kutokana na kila dhambi, na kupata faida katika kila wema, na kufaulu kuipata Pepo na kuokoka kutokana na Moto." [101] Ameipokea Al-Haakim 1/525 na akasema kwamba ni sahihi, na Adh-Dhahabiy akakubaliana naye, na Al-Baihaqi katika "Ad-Da'awaat" kwa nambari 206. Pia angalia kitabu "Al-Adhkaar" cha imamu Annawawiy ukurasa wa 340. Mhakiki Abdul-Qaadir Al-Arnaautu alisema kwamba ni hadithi nzuri (Hasan).
88. "Ewe Mwenyezi Mungu, wasamehe Waumini wa kiume na wa kike." [102] Haya yatokana na Hadithi ya Ubadah - radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwamba alisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani ziwe juu yake - akisema: "Atakayewatakia msamaha Waumini wanamume na wanawake, Mwenyezi Mungu atamuandikia jema kwa kila Muumini wa kiume na wa kike." Ameipokea At-Twabaraany katika kitabu "Al-Kabiir" 5/202 kwa nambari 5092, na 3/334 na kwa nambari 2155. Al-Haithamy alisema kwamba mtiririko wa mapokezi yake ni mzuri katika kitabu "Majmaa' Az-zawaaid", 10/210. Na Al-Albaaniy akasema kwamba ni hadithi nzuri (Hasan) katika "Sahihi Al-Jaamii" kwa nambari 5902, 5/242.
89. "Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe madhambi yangu, na unipanulie katika nyumba yangu, na unibariki kwa kile unachoniruzuku." [103] Ameipokea Ahmad, kwa nambari 16599, na kwa nambari 23114, na kwa nambari 23188, naye At-Tirmidhiy kwa nambari 3500, na wamesema waliokihakiki kitabu kiitwacho "Al-musnad" kwamba ni Hadithi nzuri (hasan) kwa sababu ya hadithi nyinginezo na mfano wake, 27/144, na katika 38/197, na katika 38/145.
90. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba katika fadhila zako na rehema zako. Hakika hakuna anayemiliki hayo isipokuwa Wewe." [104] Ameipokea Hadithi hii At-Twabaraniy. Na amesema Al-Haithamiy katika kitabu "Majmau Az-zawaaid", 159/10: "Wapokezi wake ni wapokezi wa vitabu vya hadithi sahihi isipokuwa Muhammad Ibn Ziad, naye anaaminika". Vile vile, Al-Albaaniy amesema kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahih Al-Jaamii", 404/1, kwa nambari 1278.
91. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na ukongwe (uzee uliopindukia), na kuporomoka kutoka sehemu za juu, na kudondokewa na jengo, na huzuni, na kuzama majini, na kuungua kwa moto. Na ninajikinga kwako kutochezewa na shetani wakati wa kifo. Na ninajikinga kwako nisife kwenye njia yako hali ya kuwa ni mwenye kurudi nyuma. Na ninajikinga kwako nisife kwa kuumwa na nyoka au mfano wake." [105] Ameipokea Hadithi hii Abuu Daud kwa nambari 1552, na An-Nasaai kwa nambari 5531, na kwa nambari 5532, na Al-Albaani alisema kwamba ni sahihi katika "Sahihi An-Nasaai", 3/1123, na katika "Sahihi sunan Abi Daud" 1/425.
92. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na njaa. Kwani njaa ndiyo mwenza mbaya wa kulala naye. Na ninajikinga kwako kutokana na hiyana. Kwani hiyana ndiyo rafiki mbaya zaidi."[107] Ameipokea Hadithi hii Abuu Daud kwa nambari 1547, na An-Nasaai kwa nambari 5483. Albaani alisema kwamba ni hadithi nzuri (Hasan) katika "Sahih An-Nasaai" 1112/3.
93. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa, na uvivu, na uoga, na ubahili, na ukongwe, na ugumu wa moyo, na kughafilika, na umasikini, na udhalili, na ufukara uliopindukia, na ukafiri, na kuvuka mipaka, na kutotii, na unafiki, na kutaka kusikika, na kujionyesha, na ninajikinga kwako kutokana na uziwi, na ububu, na wendawazimu, na ukoma, na mbaranga, na maradhi mabaya." [107] Ameipokea Hadithi hii An-Nasaai kwa nambari 5493, na Al-Haakim 1/530. Albaani alisema kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahih Al-Jaami'i" 406/1, na katika kitabu "Irwaaul-Ghaliil" kwa nambari 852.
94. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na ufakiri (umasikini uliopindukia), na uchache, na udhalili, na ninajikinga kwako kutodhulumu au kudhulumiwa." [108] Ameipokea Hadithi hii Abu Daud kwa nambari 1544, na An-Nasaai kwa nambari 5475, na amesema Albani kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahihi An-Nasaai" 3/1111, na katika "Sahihi Al-Jaami'i" 1/407, na yaliyo kwenye mabano yamepokelewa kwa Ibn Hibaan (Mawaarid), vile vile Albaaniy amesema ni Hadithi sahihi katika "Sahih Mawaarid Adh-Dhamaan 2/455.
95. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na jirani muovu katika makazi yangu ya kudumu, kwani jirani wa kijijini (safarini) huhama (humalizika ujirani wake)." [109] Bukhari katika "Al-Adab Al-Mufrad" kwa nambari 117, na Al-Haakim 1/532 na akasema kwamba ni Hadithi sahihi, na Adh-Dhahabi akakubaliana naye. Vile vile ameipokea Hadithi hii An-Nasaai kwa nambari 5517, na Albaaniy akasema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih Al-Jaami" 1/408 na vile vile katika "Sahih An-Nasaai" 3/1118.
96. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na moyo usiokuwa na hofu, na kutokana na maombi yasiyojibiwa, na kutokana na nafsi isiyotosheka, na kutokana na elimu isiyo na manufaa, na ninajikinga kwako na mambo haya manne." [110] Ameipokea Hadithi hii At-Tirmidhi kwa nambari 3482, na Abu Daud kwa nambari 1549, na Albaani akasema kwamba ni Hadithi sahihi katika kitabu "Sahih Al-Jaami'i" kwa nambari 1295, na vile vile katika "Sahih An-Nasaai" 3/1113.
97. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na siku mbaya, na usiku mbaya, na wakati mbaya, na mwenza mbaya, na kutokana na jirani muovu katika makazi yangu ya kudumu."[111] Ameipokea hadithi hii At-Twabarani na akasema Al-Haithami katika kitabu "Az-Zawaaid" 144/10 kwamba: "Wapokezi wake ni wapokezi wa vitabu vya hadithi sahihi", na Albaaniy akasema kwamba ni hadithi nzuri (Hasan) katika kitabu "Sahih Al-Jaami" 1/411, kwa nambari 1290.
98. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba Pepo, na ninajikinga kwako kutokana na Moto" (utayasema mara tatu)[112]. Ameipokea Hadithi hii At-Tirmidhi kwa nambari 2572, na Ibn Majah kwa nambari 3340, na An-Nasaai kwa nambari 5536, na Albaani akasema kwamba ni hadithi sahihi katika kitabu "Sahih At-Tirmidhiy" 2/319, na katika kitabu "Sahih An-Nasaai" 3/1121, na matamshi ya Hadithi yake ni: "Atakayemuomba Mwenyezi Mungu Pepo mara tatu, Pepo itasema: 'Ewe Mwenyezi Mungu, muingize Peponi.' Na atakayejikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Moto mara tatu, Moto utasema: 'Ewe Mwenyezi Mungu, mkinge kutokana na Moto.'"
99. "Ewe Mwenyezi Mungu, nipe ufahamu wa dini."[113] Hili linaashiriwa na Hadithi ya upokezi wa Bukhari na Muslim katika maombi ya Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - aliyomuombea bin Abbas, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na juu ya baba yake. Ameipokea Bukhari kwa nambari 143, na Muslim kwa nambari 2477.
100. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako nisije kukushirikisha kwa jambo ninalolijua, na ninakutaka msamaha kwa nisilolijua." [114] Ameipokea Hadithi hii Ahmad 4/403, na Ibn Abi Shaibah 10/337, na At-Twabaraniy katika "Al-Muujamul-Ausatwi" 4/284, na Albaani akasema kwamba ni Hadith nzuri (Hasan) katika "Sahih At-Targhiib wat-Tarhiib" 1/19.
101. "Ewe Mwenyezi Mungu, ninufaishe kwa uliyonifundisha, na unifundishe yenye manufaa kwangu, na unizidishie elimu." [115] Ameipokea Hadithi hii At-Tirmidhi kwa nambari 3599, na Ibn Maajah kwa nambari 259, na Albaani amesema kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahih Ibn Maajah" 1/47.
102. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba elimu yenye manufaa, na riziki nzuri, na matendo yenye kukubalika." [116] Ameipokea Hadithi hii Ibn Maajah kwa nambari 925, na An-Nasaai katika "Amali al-yaumi wal-lailah" kwa nambari 102, na Ahmad 6/294, na 305, na Albaani alisema kwamba ni hadithi sahihi katika kitabu "Sahih Ibn Maajah" 1/152.
103. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba Ewe Mwenyezi Mungu kwa kuwa Wewe ni Mmoja, wa Pekee, Mkusudiwa, ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hana yeyote wa kufananishwa naye, kwamba unisamehe madhambi yangu. Hakika Wewe ni Msamehevu, Mrehemevu." [117] Ameipokea Hadithi hii An-Nasaai kwa nambari 1300, na matamshi ya Hadithi hii ni yake, na vile vile An-Nasaai katika "Al-Kubraa" kwa nambari 7665, na Abu Daud kwa nambari 985, na Albaani akasema kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahih Sunan An-Nasaai", 1/147.
104. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba kwa kuwa sifa njema zote ni zako, hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe [uliye mpweke usiye na mshirika], Mwenye kuneemesha mno. [Ewe] Muumbaji mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Ewe mwenye utukufu na ukarimu. Ewe uliye Hai, ewe Msimamia yote milele. Hakika mimi ninakuomba Pepo na ninajikinga kwako kutokana na Moto."[118] Ameipokea Abu Daud kwa nambari 1495, na Ibn Majah kwa nambari 3858, na An-Nasaai kwa nambari 1299, na At-Tirmidhiy kwa nambari 3544, na Albaani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih An-Nasai" 1/279, na katika "Sahih Ibn Majah" 2/329.
105. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba kwa kuwa ninashuhudia kuwa Wewe ni Mwenyezi Mungu, hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe, uliye wa Pekee, Mkusudiwa, ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hakuna yeyote wa kufananishwa naye." [119] Abuu Daud kwa nambari 985, na At-Tirmidhy kwa nambari 3475, na Ibn Majah kwa nambari 3857, na Ahmad 5/360, na Albaani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih Sunan At-Tirmidhiy" 3/163.
106. "Ewe Mola wangu Mlezi, nisamehe, na nikubalie toba yangu. Hakika Wewe ni Msamehevu, Mfuta madhambi." [120] Abu Daud kwa nambari 1518, na At-Tirmidhi kwa nambari 3434, na matamshi haya ni ya hadithi yake, na ameipokea An-Nasai katika "Al-Kubraa" kwa nambari 10292, na Ibn Majah kwa nambari 3814, na Albaani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih Ibn Majah" 2/321, na "Sahih At-Tirmidhiy" 3/153.
107. "Ewe Mwenyezi Mungu, kwa elimu yako ya mambo yaliyojificha, na kwa uwezo wako juu ya viumbe, nipe uhai maadamu unajua kuwa uhai ni heri kwangu, na unifishe maadamu unajua kuwa kifo ni heri kwangu. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba unifanye kukuhofu kwa wazi na kwa siri, na ninakuomba neno la haki katika hali ya kuridhia na hasira, na ninakuomba kuwa na msimamo sahihi kwenye hali ya utajiri na umasikini, na ninakuomba neema zisizomalizika, na ninakuomba kitulizo cha jicho kisichokatika, na ninakuomba kuridhia baada ya kupita hukumu, na ninakuomba maisha ya utulivu baada ya kifo, na ninakuomba ladha ya kutazama uso wako, na shauku ya kukutana na Wewe, bila ya madhara yenye kudhuru, wala majaribu yenye kupoteza. Ewe Mwenyezi Mungu, tupambe kwa pambo la imani, na utufanye kuwa viongozi wa walioongolewa." [121] Ameipokea An-Nasai kwa nambari 1305, na Ahmad 4/264, na Albaani alisema kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahih An-Nasai" 1/280 na 1/281.
108. "Ewe Mwenyezi Mungu, niruzuku kukupenda, na kupenda yule ambaye kumpenda kutaninufaisha kwako. Ewe Mwenyezi Mungu, fanya katika kile ulichoniruzuku miongoni mwa ninachopenda kuwa ni nguvu kwangu kwa kile unachokipenda. Ewe Mwenyezi Mungu, fanya katika kile ulichonikunjia miongoni mwa vile ninavyovipenda kuwa chenye kunipa muda wa kufanya kile unachokipenda." [122] Ameipokea At-Tirmidhi kwa nambari 3491 na akasema kwamba ni Hadithi nzuri (Hasan), na Sheikh Abdul-Qaadir Al-Arnaut alisema: "Nayo ni kama alivyosema." Angalia uhakiki wake kwenye "Jaamii Al-Usuul", 4/341.
109. "Ewe Mwenyezi Mungu, nitakase kutokana na madhambi na makosa. Ewe Mwenyezi Mungu, nitakase kutokana na madhambi kama jinsi inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na uchafu. Ewe Mwenyezi Mungu, nisafishe kwa theluji na kwa maji, na kwa barafu." [123] Ameipokea Hadithi hii Muslim kwa nambari 476, na An-Nasai kwa nambari 400.
110. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na ubahili, na uoga, na umri mbaya, na majaribu ya kifua, na adhabu za kaburi." [124] Ameipokea An-Nasai kwa nambari 5469 na matamshi ya hadithi yake ni: "Alikuwa Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akijikinga kutokana na mambo matano: Kutokana na ubahili, na uoga, na umri mbaya, na majaribu ya kifua, na adhabu za kaburi." Vile vile, ameipokea Abu Daud kwa nambari 1539, na Al-Arnaut akasema kuwa ni hadithi nzuri katika kubainisha kwake upokezi wa Hadithi za kitabu "Jaami'ul-Usuul" 4/363.
111. "Ewe Mwenye Mungu, Mola Mlezi wa Jibril, na Mikail, na Israfiil, ninajikinga kwako kutokana na joto la Moto, na kutokana na adhabu ya kaburi." [125] Ameipokea An-Nasai kwa nambari 1344, na Ahmad 6/61, na Al-Baihaqi katika "Ad-Daawaat" kwa nambari 109, na Albaani akasema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih An-Nasai" 3/1121, na katika "Silsilatul-Ahadithi As-Swahiihah" kwa nambari 1544.
112. "Ewe Mwenyezi Mungu, nijaze uongofu wangu, na unikinge kutokana na shari ya nafsi yangu." [126] Ameipokea At-Tirmidhiy na matamshi ya hadithi hii ni yake 5/519 kwa nambari 3483, na ameipokea Ahmad 33/197 kwa nambari 19992, na Al-Haakim 1/510 kwa mfano wake vile vile, na akasema kwamba ni hadithi sahihi, na Adh-Dhahabii akakubaliana naye. Walisema wahakiki wa mtiririko wa mapokezi ya "Al-Musnad" kuhusu hadithi ya Ahmad 33/197: "Mtiririko wa wapokezi wake ni sahihi kwa masharti ya Bukhari na Muslim". Na ama matamshi ya hadithi ya At-Tirmidhiy, hayo ameyadhoofisha Albaaniy katika "Dhaif At-Tirmidhiy" ukurasa wa 379.
113. "Ewe Mwenye Mungu, hakika mimi ninakuomba elimu yenye manufaa, na ninajikinga kwako kutokana na elimu isiyo na manufaa." [127] Ameipokea An-Nasai katika kitabu cha "Al-Kubraa" kwa nambari 7867, na Ibn Majah kwa nambari 3843, Albani alisema kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahihi Sunan Ibn Majah" 2/327, na matamshi ya Hadithi yake ni: "Muombeni Mwenyezi Mungu elimu yenye manufaa na mjikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na elimu isiyokuwa na manufaa."
114. "Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mbingu (saba) na Mola Mlezi wa ardhi, na Mola Mlezi wa Kiti cha Enzi kitukufu, Mola wetu Mlezi na Mola Mlezi wa kila kitu, Mwenye kupasua mbegu na kokwa, na Mwenye kuteremsha Taurati na Injili na Qur'ani, ninajikinga kwako kutokana na shari ya kila kitu ulichokishika kwa nywele za utosi. Ewe Mwenyezi Mungu, Wewe ndiye wa Mwanzo hakuna kitu kabla yako, na Wewe ndiye wa Mwisho hakuna kitu baada yako, na Wewe ni wa Wazi hakuna kitu juu yako, na Wewe ni wa Ndani hakuna kitu chini yako, tulipie madeni na ututosheleze kutokana na ufakiri." [128] Ameipokea Muslim kwa nambari 2713, kutoka kwa Abu Huraira - radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
115. "Ewe Mwenyezi Mungu, unganisha baina ya nyoyo zetu, na tengeneza mambo ya baina yetu, na tuongoze njia ya amani, na tuokoe kutoka kwenye giza kwenda kwenye mwangaza, na tukinge kutokana na uchafu unaoonekana na usioonekana, na utubariki katika usikivu wetu, na kuona kwetu, na mioyo yetu, na wake zetu, na vizazi vyetu, na tusamehe, hakika wewe ni Msamehevu, Mrehemevu, na tufanye tuwe ni wenye kushukuru neema zako, wenye kukusifu kwa neema hizo, wenye kuzipokea, na tutimizie neema hizo." [129] Ameipokea Hadithi hii Abu Daud kwa nambari 969, na Al-Haakim, na matamshi ya hadithi hii ni yake 1/265, na amesema: "Ni hadithi sahihi kwa masharti ya Muslim." Na Adh-Dhahabi alikubaliana naye katika hilo 26/1, na Albaani akasema kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahih Al-Adab Almufrad" kwa nambari 630.
116. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba kukuomba kwa heri, na dua ya heri, na kufaulu kwa heri, na matendo ya heri, na malipo ya heri, na maisha ya heri, na kifo cha heri, na niimarishe, na ifanye mizani yangu kuwa nzito, na nihakikishie imani yangu, na unyanyue daraja zangu, na unikubalie swala zangu, na unisamehe makosa yangu, na ninakuomba daraja za juu Peponi. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba ufunguzi wa heri, na mwisho wake, na mkusanyiko wake, na mwanzo wake, na uwazi wake, na undani wake, na daraja za juu Peponi amiin. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba heri zenye kuja, na heri za ninayofanya, na heri ninazotenda, na heri za ndani, na heri za nje, na daraja za juu Peponi, amiin. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba unyanyue utajo wangu, na uniondolee makosa yangu, na ulifanye vizuri jambo langu, na uusafishe moyo wangu, na uihifadhi tupu yangu, na utie mwangaza moyoni mwangu, na unisamehe dhambi zangu, na ninakuomba daraja za juu Peponi, amiin. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba utie baraka ndani ya nafsi yangu, na ndani ya masikio yangu, na ndani ya macho yangu, na ndani ya roho yangu, na ndani ya maumbile yangu, na ndani ya tabia yangu, na kwa watu wangu, na ndani ya uhai wangu, na ndani ya kifo changu, na ndani ya matendo yangu, nikubalie mema yangu, na ninakuomba daraja za juu Peponi, amiin"[130]. Ameipokea Hadithi hii Al-Haakim kutoka kwa Ummu Salama hali ya kuwa imenyanyuliwa mpaka kwa Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, 1/520, na akasema kwamba ni hadithi sahihi, na Adh-Dhahabi akakubaliana naye 1/520, na vile vile Al-Baihaqi katika kitabu "Ad-Dawaat" kwa nambari 225, na At-Twabarani katika kitabu "Al-Kabiir" 23/326, kwa nambari 717.
117. "Ewe Mwenyezi Mungu, niepushe na tabia mbovu, na matamanio mabaya, na matendo machafu, na maradhi yenye kuambukiza." [131] Ameipokea Al-Haakim 1/523 na amesema: "Ni sahihi kwa sharti la Muslim." Na Adh-Dhahabi akakubaliana naye 1/532. Na vile vile ameipokea At-Twabarani katika "Al-Mu'ujam Al-Kabiir" 19/19 kwa nambari 36, na Albaani akasema kwamba ni hadithi sahihi katika "Dhwilaal Al-Jannah" kwa nambari 13.
118. "Ewe Mwenyezi Mungu, nifanye niridhike kwa kile unachoniruzuku, na unibariki ndani yake, na unipe kilicho heri badala ya kila kilichopotea." [132] Ameipokea Al-Haakim 1/532 na akasema ni hadithi sahihi, na Adh-dhahabi akakubaliana naye 1/510, kutoka kwa Ibn Abas - radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, na vile vile ameipokea Al-Baihaqi katika kitabu "Al-Aadaab" kwa nambari 1084, na katika "Ad-Daawaat Al-Kabiir" 211, Al-Haafidh Ibn Hajar akasema kwamba ni hadithi nzuri (Hasan) katika "Al-Futuuhaat Ar-Rabaaniyya" 4/383.
119. "Ewe Mwenyezi Mungu, nifanyie hesabu nyepesi (juu ya matendo)." [133] Ameipokea Ahmad 6/48, na Al-Haakim 1/255, na akasema: "Ni sahihi kwa sharti la Muslim", na Adh-dhahabi akakubaliana naye 1/255. Amesema Aisha - radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, "Pindi alipoondoka, nikasema: 'Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, ni ipi hesabu iliyo nyepesi?' Akasema: "Ni Mwenyezi Mungu atazame ndani ya kitabu cha mja kisha amsamehe. Na hakika atakayehojiwa hesabu (ya matendo) siku hiyo ewe Aisha, basi ataangamia. Na kila kinachomsibu Muumini, Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka humfutia makosa kwa hilo hata mwiba unaomdunga." Mwanachuoni Albaani alisema kuhusu hadithi hii katika "Mishkaat Al-Maswaabiih": Mtiririko wa mapokezi yake ni mzuri."
120. "Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie katika kukutaja, na kukushukuru, na kukufanyia ibada kwa uzuri." [134] Ameipokea Ahmad 2/299, na Al-Haakim 1/499, na akasema kwamba ni hadithi sahihi, na Adh-dhahabi akakubaliana naye. Na hadithi hii ni kama walivyosema, na vile vile ipo kwa Abuu Daud kwa nambari 1524, na An-Nasaai katika kitabu "Al-Kubraa" kwa nambari 9973, na Albaani alisema kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahih Al-Adab Al-Mufrad" kwa nambari 534.
121. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba imani isiyorudi nyuma, na kuwa karibu na Mtume Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ndani ya Pepo za juu zenye kubakia milele." [135] Ameipokea Ibn Hibaan "Mawaarid" ukurasa wa 604, kwa nambari 2436 kutoka kwa Ibn Masud - radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - mapokezi yake yakiishia kwake. Na ameipokea Ahmad katika mapokezi mengine 1/386, 400, na Nasaai katika kitabu "A'amalul-yaumi wallailah" kwa nambari 869 na Albaani akasema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Asilsilati Al-Sahiihah" kwa nambari 2301.
122. "Ewe Mwenyezi Mungu, nikinge kutokana na shari za nafsi yangu, na nipe maazimio juu ya uongofu wa jambo langu. Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe makosa niliyoyafanya kwa siri, na niliyoyafanya kwa wazi, na niliyoyakosea, na niliyoyakusudia, na niliyoyatambua, na nisiyoyatambua."[136] Ameipokea An-Nasai katika kitabu "Al-Kubraa" 6/246 kwa nambari 10830, na Al-Haakim 1/510 na akasema ni hadithi sahihi, na Adh-dhahabi akakubaliana naye. Vile vile ameipokea Ahmad 4/444, na pia iko katika "Al-Musnad Al-Muhaqqaq", 33/197, kwa nambari 19992. Alisema Al-Hafidh katika kitabu "Al-Iswaabah": Mtiririko wa mapokezi yake ni sahihi." Na Albaani alisema kwamba ni hadithi sahihi katika kitabu "Takhriij riyadhi As-Swaalihiin" alipokuwa anaielezea Hadithi nambari 1495.
123. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutokana na maadui zangu kufurahia misiba yangu." [137] Ameipokea An-Nasai kwa nambari 5475, na Ahmad 2/173, na Albaani akasema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih An-Nasai" 3/1113.
124. "Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe, na uniongoze, na uniruzuku, na unipe salama. Ninajikinga kwako kutokana na ufinyu wa kisimamo siku ya Kiyama." [138] Ameipokea An-Nasai kwa nambari 1617, na Ibn Majah kwa nambari 1356, na Albani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih Sunan An-Nasai" 1/356, na katika "Sahihi Ibn Majah", 1/226.
125. "Ewe Mwenyezi Mungu, nistareheshe kwa usikivu wangu, na kuona kwangu, na yafanye macho yangu na masikio yangu ni vyenye kubakia pamoja nami, na ninusuru dhidi ya atakayenidhulumu, na nifanyie kisasi dhidi yake." [139] Ameipokea At-Tirmidhiy kwa nambari 3681, na Bukhari katika "Al-Adab Al-Mufrad" kwa nambari 650 na Al-Hakim 1/523, na akasema kwamba ni hadithi sahihi na Adh-dhahabi akakubaliana naye. Na Albaani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih At-Tirmidhiy" 3/188.
126. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba maisha yaliyo bora, na kifo kizuri, na marejeo ya Akhera yasiyo na hizaya wala kufedhehesha." [140] Ameipokea hadithi hii Al-Haakimu, 1/154, na kwenye kitabu cha "Zawaaidu Musnadi Al-Bazzaar" 2/442, kwa nambari 2177, na vile vile ameipokea At-Tabaraani katika "Ad-dua'a", kwa nambari 1435, na akasema Al-Haithami katika kitabu "Majmau' Azzawaaidi", 10/179: "Mtiririko wa mapokezi ya At-Twabaraani ni mzuri."
127. "Ewe Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni zako. Ewe Mwenyezi Mungu, hakuna wa kukunja ulichokikunjua, wala hakuna wa kukunjua ulichokikunja, wala hakuna wa kumuongoa uliyempoteza, wala hakuna wa kumpoteza uliyemuongoa, wala hakuna wa kutoa ulichokizuia, wala hakuna wa kuzuia ulichokitoa, na wala hakuna wa kumuweka karibu uliyemuweka mbali, na wala hakuna wa kumuweka mbali uliyemuweka karibu. Ewe Mwenyezi Mungu, tukunjulie baraka zako, na rehema zako, na fadhila zako, na riziki zako. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba neema zenye kubakia ambazo hazibadiliki wala haziondoki. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba neema siku za umasikini, na amani siku za hofu. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na shari ya ulichotupa na shari ya ulichotuzuia. Ewe Mwenyezi Mungu, tufanye kuipenda imani na uipambe kwenye mioyo yetu, na utufanye kuchukia ukafiri, kuvuka mipaka na uasi, na utufanye miongoni mwa walioongoka. Ewe Mwenyezi Mungu, tufishe tukiwa ni Waislamu, na tupe uhai tukiwa ni Waislamu, na tukutanishe na waja wema bila ya kupata hizaya wala kujaribiwa. Ewe Mwenyezi Mungu, wapige vita makafiri wanaowapinga Mitume wako, na wanaozuia njia yako, na weka juu yao maangamivu yako ya adhabu zako. Ewe Mwenyezi Mungu, wapige vita makafiri waliopewa Kitabu, Wewe ndiye Mungu wa kweli, [amiin]." [141] Ameipokea Ahmad kwa matamshi ya hadithi hii, 3/424 na 24/246, kwa nambari 15492, na yaliyo kwenye mabano ni upokezi wa Al-Haakim 1/507, 3/23-24. Na ameipokea Bukhari katika kitabu "Al-Adab Al-Mufrad" kwa nambari 699, na Albaani akasema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Takhriji fiqh As-Siirah" ukurasa 284, na katika "Sahih Al-Adab Al-Mufrad" cha Bukhari, kwa nambari 538, ukurasa 259.
128. "Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe, na unirehemu, na uniongoe, na unipe salama, na uniruzuku." [142] Ameipokea Muslim kwa nambari 2696, na kwa nambari 2697, na katika upokezi wa Muslim: "Hakika maneno hayo yanakukusanyia dunia yako na Akhera yako" na katika Sunan Abi Daud kwa nambari 850: Alisema: "Pindi alipoondoka bedui huyo, akasema Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, "Hakika ameijaza heri mikono yake."
"....na niunge na uninyanyue." [143] Tazama: Sunan Ibn Majah, kwa nambari 898, na Sunan At-Tirmidhi, kwa nambari 284, na Sahih Ibn Majah 1/148, na Sahih At-Tirmidhi 1/90.
129. "Ewe Mwenyezi Mungu, tuzidishie wala usitupunguzie, na ututukuze na wala usitudhalilishe, na utupe na wala usitunyime, na utupendelee na wala usipendelee wengine kuliko sisi, na uturidhishe na uturidhie." [144] Ameipokea At-Tirmidhi 5/326 kwa nambari 3173, na Al-Haakim 2/98, na amesema Abdul Qaadir Al-Arnautu kwamba ni Hadithi sahihi na nzuri (Hassan) katika uhakiki wake kwenye kitabu "Jaamii Al-Usuul" 11/282 kwa nambari 8847.
130. "Ewe Mwenyezi Mungu, ulifanya vizuri maumbile yangu, basi ifanye tabia yangu kuwa nzuri." [145] Ameipokea Ahmad 6/68/6 na 155, na 1/403 na Ibn Hibaan (2423-Mawaarid) na At-Twayaalisi 374, na Musnad Abi Ya'alaa kwa nambari 5075, na amesema Albani kwamba ni Hadithi sahihi katika "Irwaai Al-Ghaliil" 1/115, kwa nambari 74.
131. "Ewe Mwenyezi Mungu, niimarishe na unifanye kuwa muongofu aliyeongolewa."[146] Hii imeashiriwa na maombi ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, akimuombea Jariri - radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Angalia: Bukhari kwa nambari 6333, na vile vile kwa nambari 3020, 3036, na nyinginezo.
132. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba kuwa imara katika mambo, na kuwa na azimio juu ya uongofu, na ninakuomba mambo yenye kuleta rehema zako, na matendo yatakayotilia nguvu kupata msamaha wako, na ninakuomba kushukuru neema zako, na kukuabudu kwa uzuri, na ninakuomba moyo uliosalimika, na ulimi unaosema kweli, na ninakuomba heri unazozijua, na ninajikinga kwako kutokana na shari unazozijua, na ninakutaka msamaha kwa unayoyajua. Hakika Wewe ndiye Mjuzi zaidi wa mambo yaliyofichikana." [96] Ameipokea Ahmad 28/338, kwa nambari 17114, na 28/356, kwa nambari 17133, na Tirmidhi kwa nambari 3407, na At-Tabarani katika kitabu "Al-Muujamu Al-Kabiir" kwa matamshi ya Hadithi hii kwa nambari 7135, na kwa nambari 7157, na 7175, na kwa nambari 7176, na 7177, na 7178, na 7179, na 7180. Na ameipokea Ibn Hibaan katika sahihi yake 3/215 kwa nambari 935, na 5/310, kwa nambari 1974, na Sha'iib Al-Arnautu alisema ni Hadithi nzuri (Hasan) katika "Sahih Ibn Hibaan", 5/312. Nao wahakiki wa "Musnad" walisema kwamba ni Hadithi nzuri (Hasan) kwa njia zake za upokezi, 28/338, na ameitaja Albaani katika "Silsilati Al-Ahaadithi Al-Sahihih" katika juzuu ya saba, kwa nambari 3228, na katika "Mawaarid Adh-Dhamaan" kwa nambari 2416, na 2418, na amesema: "Ni Hadithi sahihi kwa sababu ya upokezi mwingine."
133. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba Pepo ya Firdausi (ambayo) ndiyo Pepo ya juu zaidi." [97] Haya yamechukuliwa kutokana na kauli ya Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -"... Kwa hivyo mnapomuomba Mwenyezi Mungu, basi muombeni Pepo ya Firdausi. Kwani hakika Pepo hiyo ndiyo Pepo ya kati na kati, na ndiyo Pepo ya juu zaidi, na juu yake ndiko kuna Kiti cha Enzi cha Mwenyezi Mungu, nako ndiko itokapo mito ya Pepo." Ameipokea Bukhari kwa nambari 2790, na nambari 7423.
134. "Ewe Mwenyezi Mungu, ifanye upya imani ndani ya moyo wangu." [149] Haya yamechukuliwa kutoka kwenye Hadithi ya Abdullahi Ibn Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao - kwamba alisema: Amesema Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -: "Hakika imani inazeeka ndani ya moyo wa mmoja wenu kama jinsi nguo inavyozeeka. Basi muombeni Mwenyezi Mungu azifanye upya imani ndani ya mioyo yenu." Ameipokea Al-Hakim 1/4, na akasema kwamba ni Hadithi sahihi na Adh-dhahabi akakubaliana naye. Na amesema Al-Haithami katika "Majma'i Az-Zawaaid" 1/52: "Ameipokea At-Tabaraani katika kitabu Al-Kabiir, na mtiririko wa mapokezi yake ni mzuri." Na Albaani alisema kwamba ni Hadithi nzuri katika "Silsilati Al-Ahaadithi As-Sahiiha", 4/113, kwa nambari 1585.
135. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na swala isiyokuwa na manufaa." [150] Abu Daud kwa nambari 1549, na akasema Albaani kwamba ni Hadithi sahihi katika Sahihi Sunan Abi Daud 1/424.
136. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na jirani mbaya, na mke atakayenitoa mvi kabla ya uzee, na kutokana na mtoto atakayekuwa bwana juu yangu, na kutokana na mali zitakazokuwa ni adhabu juu yangu, na kutokana na rafiki mwandani mwenye vitimbi, jicho lake likiniona na moyo wake ukinichunguza. Akiona jema, analifunika. Na akiona ovu, analitangaza." [151] Ameipokea At-Tabaraani katika kitabu cha "Ad-Duaa", 3/1425 kwa nambari 1339, na akasema Albaani katika "Silsilat Al-Ahaadith As-Sahiiha", 7/377 kwa nambari 3137: "Nilisema: Na mtiririko huu wa upokezi ni mzuri, wapokezi wake wote ni wale wale wapokezi wa kitabu cha "At-Tahdhib..."
137. "Ewe Mwenyezi Mungu, usinipe hizaya siku ya Kiyama." [152] Ameipokea Ahmad katika "Musnad" 29/596, kwa nambari 18056, na wamesema wanaohakiki Musnad: "Mtiririko wa mapokezi yake ni sahihi". Na ameipokea At-Twabaraani katika "Al-Mu'ujam Al-Kabiir", 3/20, kwa nambari 2524 kwa matamshi haya: "Ewe Mwenyezi Mungu usinifedheheshe siku ya Kiyama, na wala usinifedheheshe siku yenye balaa."
138. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba salama Duniani na Akhera." [153] Ameipokea Ibn Maajah kwa nambari 3851, na amesema Albaani kwamba ni Hadithi sahihi katika Sahih Ibn Majah 3/259, na katika "Silsilat Al-Ahaadithi As-Sahiiha kwa nambari 1138.
139. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na elimu isiyofaa, na matendo yasiyopandishwa, na moyo usio na hofu, na kauli isiyosikika" [154] Ameipokea Ibn Hibaan kwa nambari 2440 "Mawaarid" na amesema Albani kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih Mawaarid Adh-Dhwamaan", 2/454, kwa nambari 2066.
140. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na msongo wa mawazo na huzuni, na kushindwa na uvivu, na ubahili na uoga, na uzito wa madeni, na kushindwa na watu." [155] Ameipokea Bukhari kwa nambari 6363. Alisema Anas, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Nilikuwa nikimtumikia Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kila mara anaposhuka mahali safarini, nilikuwa nikimsikia akisema mara nyingi: "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako..."
141. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na adhabu ya Moto, na ninajikinga kwako kutoka na adhabu za kaburi, na ninajikinga kwako kutokana na majaribu yenye kuonekana na yasiyoonekana, na ninajikinga kwako kutokana na majaribu ya Masihi Dajjal" [156] Ameipokea Muslim kwa nambari 2867, na ndani yake kuna: "Jilindeni kwa Mwenyezi Mungu kutokana na adhabu za Moto...", ["Jilindeni kwa Mwenyezi Mungu kutokana na adhabu za kaburi..."] mpaka mwisho wake.
142. "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba kufa kwa ajili ya dini katika njia yako." [157] (158) Ameipokea Muslim kwa nambari 1909, na yaliyo kwenye mabano yanatokana na kauli yake Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: "Atakayemuomba Mwenyezi Mungu kufa kwa ajili ya dini kwa ukweli, basi Mwenyezi Mungu atamfikisha daraja za waliokufa kwa ajili ya dini, hata kama atafia juu ya kitanda chake."
143. "Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe. Ewe Mwenyezi Mungu, nifanye Siku ya Kiyama niwe juu ya wengi miongoni mwa viumbe wako katika watu. Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe makosa yangu, na Siku ya Kiyama uniingize mahali patukufu pa kuingia." [158] Ameipokea Bukhari kwa nambari 4323, na Muslim kwa nambari 2498, nayo imechukuliwa kutoka kwenye maombi ya Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alipomuombea 'Ubeid Abi 'Amir, na kutokana na maombi yake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alipomuombea Abuu Burdah, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao.
144. "Ewe Mwenyezi Mungu, niongoe miongoni mwa uliowaongoa, na unipe salama miongoni mwa waliopewa salama, na unisimamie miongoni mwa uliowasimamia, na unibariki katika kile ulichonipa, na unikinge kutokana na shari ulizozipitisha, kwani hatodhalilika uliyemuweka karibu, umetukuka Mola wetu Mlezi na umetakasika." [159] Ameipokea Ahmad katika "Musnad" 3/249 kwa nambari 1723, na wamesema wahakiki wa "Musnad" 3/249: "Mtiririko wa mapokezi yake ni sahihi." Na upokezi huu ni wa moja kwa moja bila kuifungamanisha na swala ya witri kama jinsi ilivyokuja katika mapokezi mengine. Katika upokezi huu, alisema Anas, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, "Alikuwa Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akitufundisha maombi haya..."
145. "Mola wangu Mlezi, nisamehe makosa yangu siku ya Malipo." [160] Ameipokea Muslim kwa nambari 214. Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, aliambiwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika Ibn Jud'aan alikuwa katika zama za ujinga akiunganisha udugu, na akiwalisha masikini. Je, hayo yatamnufaisha? Akasema: "Hayatamsaidia. Hakika yeye hakusema hata siku moja Mola wangu Mlezi nisamehe makosa yangu Siku ya Malipo."
146. "Ninaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu Mkuu, ambaye hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Yeye, aliye Hai, Mwenye kusimamia mambo yote milele, na ninatubia kwake." Ameipokea At-Tirmidhi kwa nambari 3577, na Albani akasema kwamba ni hadithi sahihi katika Sahih At-Tirmidhi 3/469: "Atakayeyasema maneno haya, Mwenyezi Mungu atamsamehe hata kama alikimbia kutoka katika safu za vita vya kidini."
147. "Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe makosa yangu, na niondoshee chuki ndani ya moyo wangu, na unikinge kutokana na majaribu yenye kupotosha." [162] Haya yamechukuliwa kutoka katika maombi ya Mtume -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alipomuombea Aisha - radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu, msamehe makosa yake, na muondoshee chuki ndani ya moyo wake, na mkinge kutokana na majaribu yenye kupotosha." Ameipokea Ibn Asaakir kwa mapokezi yake katika "Al-Arbauna fii manaaqib ummahaat Al-Muuminina" ukurasa wa 85 kutoka kwa Aisha, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na alisema: "Hadithi hii ni sahihi nzuri (Sahiihun Hasan), kutokana na hadithi ya Baqiyah Ibn Al-Waliid." Na ameipokea Ibn As-Suniyyi kwa mfano wake katika 'A'amalu Al-Yaumi wallailah, kwa nambari 457, na katika nakala nyingine ya Ibn Suniyyi alisema: "Na unikinge kutokana na Shetani" badala ya "kutokana na majaribu yenye kupotosha." Angalia upokezi wake kwa Albaani katika kitabu "Adh-Dhaifu" kwa nambari 4207. Hadithi hii inatiliwa nguvu na hadithi zingine kutoka kwa Ummu Salamah - radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na inapatikana kwa Ahmad kwa nambari 26576, 44/2 kwa mfano wake, na matamshi yake ni: "Sema: 'Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa Nabii Muhammad, nisamehe makosa yangu, na uniondoshee chuki ndani ya moyo wangu, na unikinge kutokana na majaribu yenye kupotosha kwa muda wote utakaotuweka hai." Al-Haithami alisema kwamba ni Hadithi nzuri katika "Majmau' Az-Zawaaid" 10/27. Vile vile, ipo kwa At-Twabaraani katika "Al-Muujam Al-Kabiir" 23/388 kwa nambari 785 bila ya matamshi yake: "Kwa muda wote utakaotuweka hai." Na hadithi hii ina ushahidi kutokana na Hadithi ya Ummu Haanii -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwamba alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nifundishe maombi nitakayokuwa nikiomba, akasema: "Sema: 'Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe makosa yangu...'" Hadithi hii ameipokea Al-Kharaaitwii katika kitabu "Al-i'itilaal Al-Quluub" kwa nambari 52, na katika "Masaawi'u Al-Akhlaaq" kwa nambari 323.
148. "Ewe Mwenyezi Mungu, nibakishe hai kwenye mwenendo wa Nabii wako - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na unifishe nikiwa kwenye mila yake, na unikinge kutokana na majaribu yenye kupotosha." [163] Ameipokea Al-Baihaq katika Al-Kubraa, 5/95 kutokana na maombi ya Ibn Omari ikiwa ni maombi yaliyosimamia kwake, na amenukuu hayo Ibn Al-Mulaqqin katika kitabu "Al-Badri Al-Muniir" 6/309, na amesema hali ya kunukuu kutoka katika kitabu "Adh- Dhwiyaai": "Mapokezi yake ni mazuri" na amesema Ibn Masud - radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Asiseme mmoja wenu: Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na majaribu, kwani hakuna yeyote isipokuwa anakuwa amefungamana na majaribu. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu anasema: "Hakika ya mali zenu na watoto wenu ni majaribu." (Surah Taghabun:15) Basi yeyote atakayejikinga, basi ajikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na majaribu yenye kupotosha. Ameipokea Ibn Jarir, katika Tafsiri yake,13/475 kwa namabri 15912, na ameitaja Ibn Batwaal katika ufafanuzi wake wa Sahihi Al-Bukhari, 4/13.
149. "Ewe Mwenyezi Mungu, shusha rehema juu ya Muhammad na wafuasi wake Muhammad kama ulivyoshusha rehema juu ya Ibrahim na wafuasi wa Ibrahim. Hakika Wewe ni Msifiwa, Mtukufu. Na shusha baraka juu ya Muhammad na wafuasi wa Muhammad kama ulivyoshusha baraka juu ya Ibrahim na wafuasi wa Ibrahim. Hakika Wewe ewe ni Msifiwa, Mtukufu." Ameipokea Bukhari kwa nambari 3370, na yaliyo baina ya mabano yanayotokana na Hadithi ya Abuu Huraira - radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - yanapatikana kwa Muslim kwa nambari 405.
Na kila sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe wote, kama inavyoendana na utukufu wake, na ukubwa wa utawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu, teremsha rehema na amani juu ya Nabii wetu Muhammad na juu ya watu wake, na Maswahaba zake, na waliomfuata kwa wema mpaka siku ya Malipo.
Tiba kwa kufanya Ruqya
Kutoka katika Qur'ani na Sunna
cha Mhitaji kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu,
Dkt. Sa'id bin Ali bin Wahf Al-Qahtwaani
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu
Utangulizi: Umuhimu wa kutibu kwa Qur'ani na Sunna
Hakika sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, tunamsifu, tunamtaka msaada, tunamuomba msamaha, na tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na uovu wa nafsi zetu, na ubaya wa matendo yetu. Yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, basi hakuna wa kumpoteza. Na yule ambaye amempoteza, basi hakuna wa kumuongoa. Na ninashuhudia kuwa hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Yeye peke yake asiye na mshirika, na ninashuhudia kuwa Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake, rehema na amani nyingi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na juu ya watu wake, na Maswahaba wake, na wote wanaomfuata kwa wema hadi siku ya Malipo. Ama baada ya hayo:
Hapana shaka kutibu kwa kutumia Qur'ani Tukufu, na yale yaliyothibiti kutoka kwa Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ya kufanya ruqya ni katika tiba yenye manufaa, na uponyaji kamili. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Sema: Hii Qur'ani ni uongofu na ponya kwa wenye kuamini." [1] Surat Fusswilat, aya ya 44. Na amesema Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka: "Na tunateremsha katika Qur'ani yale ambayo ni uponyaji na rehema kwa Waumini. Wala hayawazidishii madhalimu isipokuwa hasara." Surat Al-Israa, aya ya 82. Neno "min (katika)" kwenye aya hii linafafanua kategoria ya jumla. Kwani, Qur'ani yote ni ponya, kama ilivyo katika aya iliyotangulia [3]. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi watu! Yamekwisha wajia mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na ponya ya yale yaliyo katika vifua, na uongofu, na rehema kwa Waumini." Surah Yunus, aya: 57.
Hivyo basi, Qur'ani ndiyo tiba kamili ya maradhi ya moyo, mwili, na maradhi ya dunia na akhera. Lakini si kila mtu anastahiki wala kuwezeshwa kupata uponyaji katika Qur'ani. Hata hivyo, ikiwa mgonjwa atajitibu vizuri kwayo na akatumia kutibu ugonjwa wake kwa ukweli, imani, kukubali kikamilifu, itikadi thabiti, na kutimiza masharti yake, basi ugonjwa huo hautaweza kuyapinga hayo kamwe. Vipi magonjwa yanaweza kupingana na maneno ya Mola Mlezi wa ardhi na mbingu, ambayo lau yangeshuka juu ya milima, basi yangeupasua, au juu ya ardhi, basi yangeichana vipande vipande. Kwa hivyo, hakuna ugonjwa wa moyo au mwili isipokuwa kuna njia inayoashiria tiba yake na sababu yake katika Qur'ani, na vile vile humo kuna njia ya kujilinda kutokana nao kwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amempa ufahamu wa Kitabu chake. Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaja katika Qur'ani magonjwa ya moyo na mwili, na tiba ya moyo na mwili: Tazama: "Al-Jawaab Al-Kaafii liman sa-ala 'an Addawaai Ashshaafii", cha Ibn Al-Qayyim, ukurasa wa 20.
Ama maradhi ya moyo, hayo yana aina mbili: Maradhi ya kuwa na utata na shaka, na maradhi ya matamanio na upotofu. Mwenyezi Mungu aliyetakasika ameyataja maradhi ya moyo kwa kina, na akataja sababu zake na tiba yake. [5] Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Je, kwani hayakuwatosha ya kwamba tumekuteremshia Kitabu hiki wanachosomewa? Hakika katika hayo, zipo rehema na mawaidha kwa watu wanaoamini." [6] Surat Al-Ankabut, aya ya 51. Amesema mwanachuoni Ibnil-Qayyim, Mwenyezi Mungu amrehemu: "Yeyote ambaye hataponywa na Qur'ani, basi Mwenyezi Mungu hatomponya. Na asiyetoshelezwa nayo, basi Mwenyezi Mungu hatomtosheleza." [3]. Zaad al-Ma’aad cha Ibnil-Qayyim, 4/6, na 4/352. Zaad al-Ma'aad, 4/352.
Ama kuhusu maradhi ya mwili, Qur'ani imetuongoza kwenye misingi ya tiba yake, misingi ya jumla na kanuni zake. Hayo ni kwa sababu kanuni zote za utabibu zimo ndani ya Qur'ani Tukufu, nazo ni tatu: Kuhifadhi afya, kujiepusha na vitu vyenye madhara, kuondoa vitu vibovu na vinavyodhuru na kutumia haya kama ushahidi kwa watu wa aina zote hizi. [8] "Zaad al-Ma’aad", 4/352, na 4/6.
Kama mja atajitibu vizuri kwa Qur'ani, basi ataona matokeo ya ajabu ya hilo katika kupona haraka.
Imaam Ibnil-Qayyim, Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu, alisema: "Niliugua wakati mmoja huko Makka, na sikuweza kupata daktari wala dawa. Basi nikawa ninajitibu kwa Al-Fatiha, na ninaona kwamba ilikuwa na athari ya ajabu. Nilikuwa nikichukua maji ya Zamzam na kuyasomea Al-Fatiha mara kadhaa, kisha ninayanywa na kupona kikamilifu kutokana na maradhi hayo. Kisha nikaanza kutegemea hayo kwa maradhi mengi, na ninanufaika kwayo sana. Basi nikawa ninamuelezea hivyo yeyote aliyekuwa akilalamika kwamba ana maumivu, na wengi wao walikuwa wakipona haraka." [9] Tazama: "Zaad al-Ma’aad", 4/178, na "Al-Jawaab al-Kaafii", ukurasa wa 21.
Vile vile, kutibu kwa ruqya ya Mtume iliyothibiti ni miongoni mwa dawa zenye manufaa zaidi, na dua, ikiwa haina vikwazo, ni miongoni mwa njia zenye manufaa zaidi katika kuepusha madhara na kufikia kile kinachotakikana, hasa kwa kuirudiarudia, na ni adui wa balaa, huwa zinaizuia, kuitibu na kuizuia kutokea au huipunguza inapotokea; kwa kauli ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: “Dua inanufaisha katika yale ambayo yametokea na yale ambayo hayajatokea. Kwa hivyo, enyi waja wa Mwenyezi Mungu, shikamaneni na dua.” [11] Na kwa kauli ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, “Hakuna kinachoweza kuzuia mipango ya Mwenyezi Mungu isipokuwa dua, na hakuna kinachoweza kuongeza umri wa kuishi isipokuwa wema.” [12] Lakini hapa kuna jambo ambalo linapaswa kutiliwa maanani: kwamba aya mbalimbali, nyiradi, dua, na kujikinga kwa Mwenyezi Mungu kwa njia mbalimbali ambazo hutumika kwa ajili ya uponyaji na kwa ajili ya ruqya, hizo zinamanufaa na uponyaji, lakini zinahitaji kukubalika na nguvu ya mwenye kuziomba na athari yake. Hivyo basi, pindi uponyaji unapokosa kupatikana, basi ni kwa sababu ya udhaifu wa athari ya mwenye kuziomba au kutokubaliwa anayeombewa, au kwa sababu ya kizuizi chenye nguvu kilicho ndani yake kinachozuia dawa kumuathiri. Kwa maana, kutibu kwa ruqya huwa kwa mambo mawili: Tazama: "Al-Jawab Al-Kafi", ukurasa wa 22-25. At-Tirmidhi, namba 3548, Al-Haakim, 1/670, na Ahmad, namba 22044, na Al-Albaani alisema kwamba ni hadithi nzuri (Hasan). Tazama "Sahih al-Jami’i", 3/151, namba 3403. Al-Hakim, 1/670, na At-Tirmidhi, namba 2139, na Al-Albaani alisema kwamba ni Hadithi nzuri (Hasan) katika: Mlolongo wa Hadithi Sahihi, 1/76, namba 154.
Jambo la kwanza: Kutoka upande wa mgonjwa, nalo ni yeye mwenyewe kuwa na nguvu, kuelekea kwake kwa ukweli kwa Mwenyezi Mungu, imani yake thabiti kwamba Qur'ani ni ponya na ni rehema kwa Waumini, na kutafuta kimbilio kwa njia sahihi ambayo moyo na ulimi vimeafikiana ndani yake. Kwani, hii ni aina ya vita, na shujaa hawezi kupata ushindi dhidi ya adui yake isipokuwa kwa mambo mawili:
Kwamba silaha yenyewe iwe sahihi na nzuri, na kwamba kishikio chake kiwe na nguvu. Kwani, pindi moja kati ya hayo litakosekana, basi silaha hiyo haitakuwa na manufaa. Basi itakuwaje ikiwa vitu hivi viwili vyote vitakosekana: Wakati moyo umeharibika na hauna upwekeshaji wa Mwenyezi Mungu, kumtegemea Mwenyezi Mungu, uchaMungu, kumuelekea Mwenyezi Mungu na wala hana silaha.
Jambo la pili: Linahusiana na yule anayetibiwa kwa Qur'ani na Sunna. Yeye pia anapaswa kuwa na mambo haya mawili [13]; Ndiyo maana Ibnut-Tiin, Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu, alisema: "Kufanya ruqya kwa dua za kujikinga kwa Mwenyezi Mungu na majina mengineyo ya Mwenyezi Mungu ni dawa ya kiroho. Ikisomwa na watu wema miongoni mwa viumbe, uponyaji utatokea, Mwenyezi Mungu akipenda." [14]. Tazama: "Zad al-Ma’aad" 4/68, na "Al-Jawab al-Kaafi" uk.21. "Fat-h Al-Baari", cha Ibn Hajar, 10/196.
Wanachuoni wamekubaliana kwamba ruqya inaruhusiwa pale yanapokutana masharti matatu:
Sharti la kwanza: Iwe kwa maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kwa majina na sifa zake, au kwa maneno ya Mtume wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
Sharti la pili: Ni lazima iwe kwa lugha ya Kiarabu, au kwa lugha nyingineyo ambayo maana yake inajulikana.
Sharti la tatu: Ni lazima iaminike kwamba ruqya haina athari ndani yake yenyewe tu. Bali, ni kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu [15], na ruqya ni sababu moja tu kati ya visababu. Tazama "Fat-hul-Baari", 10/195, na Fatwa za sheikh Ibn Baaz, 2/384.
Basi kwa sababu ya umuhimu huu mkubwa, nimefupisha sehemu ya ruqya kutoka katika kitabu changu: "Dhikri, dua na tiba kwa kufanya ruqya kutoka katika Qur'ani na Sunna", na nimeiongezea sehemu hiyo faida zenye manufaa, Mwenyezi Mungu Mtukufu akipenda. Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa majina yake mazuri na sifa zake za juu zaidi aifanye kazi hii iwe kwa ajili ya uso wake mtukufu, na aninufaishe kwayo na amnufaishe kwayo kila atakayeisoma, au kuichapisha, au atayesaidia katika kusambaa kwake, na awanufaishe kwayo Waislamu wote. Hakika Yeye, aliyetakasika, ndiye Msimamiaji wa hayo na ndiye Muweza wa kufanya hivyo. Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie Mtume wetu Muhammad, na aali zake, na Maswahaba wake, na wote wanaowafuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Mhitaji kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu
Dkt. Sa'id bin Ali bin Wahf Al-Qahtani
Kimeandikwa tarehe 18/6/1414 Hijria
1. Matibabu ya uchawi
Matibabu ya kimungu kwa uchawi yamegawanywa katika sehemu mbili:
Sehemu ya kwanza: Yanayotumika kulijinda kwayo dhidi ya uchawi kabla haujatokea:
1- Kutekeleza wajibu zote, kuacha haramu zote na kutubia mabaya yote.
2- Kusoma Qur'ani Tukufu kwa wingi, kiasi kwamba anakuwa na kiasi maalumu anachosoma kila siku.
3- Kujilinda kwa dua mbalimbali, kujikinga kwa Mwenyezi Mungu, kufanya nyiradi zinazoruhusiwa kisheria, ikiwa ni pamoja na: “Bismillahi lladhi laa yadhurru ma'as mihii shay-un fil ardhwi walaa fiis samaai wahuwas samii'ul 'aliim" (Kwa jina la Mwenyezi Mungu, ambaye hakuna chochote kinachoweza kudhuru pamoja na jina lake duniani wala mbinguni, naye ni Mwenye kusikia, ajuaye zaidi), mara tatu asubuhi na jioni [16], na kusoma Ayatul-Kursi baada ya kila swala, na wakati wa kulala, na asubuhi na jioni, na vile vile kusoma: [17] "Sema Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee." Na suratul-Falaq na suratun-Naas (Mu’awwidhatain) mara tatu tatu asubuhi na jioni, na kabla ya kulala, na kusema: “Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu peke yake, hana mshirika, ufalme ni wake, na sifa njema ni zake, na Yeye ni Muweza wa kila kitu.” mara mia kila siku.[18] Kudumu kufanya nyiradi za asubuhi na jioni, na baada ya swala, na nyiradi za kabla ya kulala na kuamka, na nyiradi za kuingia na kutoka nyumbani, na nyiradi za kupanda kipando, na nyiradi za kuingia na kutoka msikitini, na nyiradi za kuingia na kutoka chooni, na nyiradi anazosema mwenye kumuona mtu aliyepewa majaribu, na nyiradi nyinginezo. Nimetaja mengi ya mambo haya katika Hisnul-Muslim, kwa mujibu wa hali mbalimbali, matukio, mahali na nyakati. Hakuna shaka kwamba kudumisha hili ni moja ya sababu zinazozuia kupatwa na uchawi, kijicho na majini, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, pia ni katika tiba kubwa zaidi baada ya kupatwa na balaa hizi na nyinginezo [19]. At-Tirmidhi, nambari 3388, Abu Daud, nambari 5088, na Ibn Majah, nambari 3869. Al-Albaani alisema kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahih Ibn Majah", 2/332. Ameipokea Al-Haakim na akasema kwamba ni hadithi sahihi, na Adh-Dhahabi akakubaliana naye, 1/562, na Al-Albani alisema kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahih At-Targhiib wa At-Tarhiib", 1/273, namba 658. Bukhari, 4/95, namba 3293, na Muslim, 4/2071, namba 2691. Tazama: "Zaad al-Ma’aad", 4/126, na "Majmu’u Fatawa al-‘Allama Ibn Baaz", 3/277, na tazama sababu kumi zinazoondoa uovu wa mwenye husuda na mchawi katika sehemu ya tatu ya kutibu kijicho, katika kitabu hiki.
4- Kula tende saba za 'Ajwa asubuhi kabla ya kula chochote, ikiwezekana. Kwa sababu Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alisema: "Mwenye kula tende saba za 'Ajwa asubuhi, hatadhurika siku hiyo kwa sumu wala uchawi." [20] Ni katika hali kamili zaidi kwamba ziwe ni katika tende za Madina, kutoka baina ya sehemu zake mbili tambarare zenye mawe meusi, kama ilivyo katika riwaya ya Muslim. Na sheikh wetu, mwanachuoni Abdul-Aziz ibn 'Abdillah ibn Baaz, Mwenyezi Mungu amrehemu, ana maoni kwamba tende zote za Madina zina sifa hii. Kwa sababu Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alisema: "Yeyote atakayekula tende saba kutoka kati ya sehemu zake mbili tambarare zenye mawe meusi [21] asubuhi..." Hadi mwisho wa hadithi. [22] Bukhari na vile vile katika "Al-Fat-h", 10/247, namba 5445, na Muslim, 3/1618, namba 2047. Labataihaa: Ni sehemu mbili za Madina zenye lava na mawe meusi makavu kana kwamba yaliunguzwa kwa moto. Tazama "Faidh al-qadiir", cha Al-Munaawii, 2/514. Muslim 3/1618, namba 2047.
Vile vile, anaona (mwanachuoni Abdul-Aziz ibn 'Abdillah ibn Baaz), Mwenyezi Mungu amrehemu, kwamba hayo yanatarajiwa pia kwa mwenye kula tende saba hata kama si za kutoka Madina.
Sehemu ya pili: Kutibu uchawi baada ya kutokea, na hilo lina aina kadhaa:
Aina ya kwanza: Kuutoa na kuubatilisha ikiwa mahali pake panajulikana kwa njia zinazoruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu. Na hilo ni miongoni mwa njia bora zaidi za kumtibu mtu aliyerogwa. [23] Tazama: "Zaad al-Ma’aad", 4/124, na Bukhari na vile vile katika "Al-Fat-h", 10/132, namba 5765, na Muslim, 4/1917, namba 2189, na "Majmu’u Fatawaa Ibn Baaz", 3/228.
Aina ya pili: Kufanya ruqya ya kisheria, ikijumuisha yafuatayo [24]: Tazama: "Fat-hul-Haqq al-Mubin fi 'ilaajis-swar'i wassihri wala-'ayn", ukurasa 138.
Kwanza: "Ayaponde majani saba ya mkunazi wa kijani kibichi kwa jiwe au kitu mfano wake, kisha (ayaweke kwenye chombo) na ayamiminie maji ya kumtosha kuoga, kisha asomee ndani yake:
"A'udhu billahi minash Shaitwanir rajiim" (Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa). "Mwenyezi Mungu - hapana mungu isipokuwa Yeye, Aliye hai, Msimamizi wa mambo yote milele. Hashikwi na kusinzia wala kulala. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo duniani. Ni nani huyo awezaye kufanya uombezi mbele yake isipokuwa kwa idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao, na yaliyo nyuma yao, wala wao hawajui vyema chochote katika elimu yake isipokuwa kwa kile akitakacho. Kursi yake imeenea mbingu na dunia, na wala haelemewi na kuvilinda vyote viwili. Na Yeye ndiye aliye juu zaidi, Mkuu." [25] Suratul-Baqarah, aya ya 255.
"Nasi tukamfunulia Musa kumwambia: Itupe fimbo yako, na tazama, ikawa inavimeza vyote vile walivyovizulia uongo. "Basi haki ikathibiti na yakabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda". 119. Kwa hivyo wakashindwa huko, na wakageuka kuwa wadogo. 120. Na wachawi wakatupwa chini wakisujudu 121. Wakasema: Tumemuamini Mola Mlezi wa walimwengu. 122. Mola Mlezi wa Musa na Haarun." [26] Suratul-A'raf, aya ya 117-122.
"Na Firauni akasema: Nileteeni kila mchawi ajuaye zaidi! "80. Basi walipokuja wachawi hao, Musa akawaambia: Vitupeni mnavyovitupa! 81. Basi walipotupa, Musa akasema; Mliyoleta ndiyo uchawi. Hakika Mwenyezi Mungu ataubatilisha. Hakika Mwenyezi Mungu hayatengenezi matendo ya waharibifu." 82. Na Mwenyezi Mungu huihakikisha haki kwa maneno yake, hata wakichukia wahalifu." [27] Surat Yunus, aya ya 79-82.
"Wakasema: Ewe Musa! Ima utupe wewe, au tuwe sisi ndio wa kwanza wa kutupa? "66. Akasema: Bali tupeni nyinyi! Tahamaki! Kamba zao na fimbo zao zikaonekana mbele yake, kwa uchawi wao, kuwa zinakwenda mbio. 67. Basi Musa akaingia hofu katika nafsi yake. 68. Tukasema: Usihofu! Hakika wewe ndiye utakayeshinda. 69. Na kitupe kilicho katika mkono wako wa kulia; kitavimeza walivyoviunda. Hakika walivyounda ni hila za mchawi tu, na mchawi hafanikiwi popote afikapo. 70. Basi wachawi hao wakaangushwa chini wakasujudu. Wakasema: Tumemuamini Mola Mlezi wa Harun na Musa!" [28] Surat Taha, aya ya 65-70.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu "Sema: 'Enyi makafiri.' 2. Siabudu mnachokiabudu; 3.Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. 4.Wala sitaabudu mnachoabudu. 5. Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. 6. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu."
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu "Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. 2. Mwenyezi Mungu ndiye Mkusudiwa. 3. Hakuzaa wala hakuzaliwa. 4. Na hakuna anayelingana naye hata mmoja."
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu 1. "Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko. 2. Kutokana na shari ya alivyoviumba. 3. Na kutokana na shari ya giza la usiku liingiapo. 4. Na kutokana na shari ya wanaopuliza mafundoni. 5. Na kutokana na shari ya hasidi anapohusudu."
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. 1. "Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa watu. 2. Mfalme wa watu. 3. Mungu wa watu. 4. Kutokana na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas (mwingi wa kurudi nyuma). 5. Anayetia wasiwasi katika vifua vya watu. 6. Kutokana na majini na watu."
Baada ya kusomea ndani ya maji kile kilichotajwa, atakunywa kwayo mara tatu na ataoga kwa yaliyosalia, na kwa hayo ugonjwa utaondoka, Mwenyezi Mungu akipenda. Ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo mara mbili au zaidi, basi hakuna ubaya mpaka ugonjwa huo uishe. Tiba hii imejaribiwa mara nyingi, na Mwenyezi Mungu akanufaisha kwayo, nayo ni nzuri kwa mume ambaye amezuiliwa kumuingilia mke wake. [29] Tazama: "Fataawa za Ibn Baaz", 3/279, "Fat-hul-Majid", ukurasa wa 346, na "As-Swaarim al-Battaar fiit-Taswaddii lis-sahara wal-ashraar", cha Wahiid Abdus-Salam, ukurasa wa 109-117. Humo kuna ruqya ndefu na yenye manufaa Mwenyezi Mungu Mtukufu akipenda, na vile vile "Muswannaf Abdirrazzaq", 11/13, na "Fat-hul-Baarii", cha Ibn Hajar, 10/233.
Pili: Itasomwa Surat Al-Fatihah, Ayatul-Kursi, aya mbili za mwisho za Surat Al-Baqarah, Surat Al-Ikhlas, Suratul-Falaq na Suratun-Naas mara tatu au zaidi, huku ukipuliza na kupangusa eneo la maumivu kwa mkono wa kulia. [30] Muslim, 4/1728, namba 2202.
Tatu: Kujikinga kwa Mwenyezi Mungu, na kufanya ruqya, na dua zinazojumuisha mambo mengi: Tazama: Bukhari pamoja na vile vile "Al-Fat-h", 9/62, nambari 5016, na Muslim, 4/1723, nambari 2192, na Bukhari na vile vile Al-Fat-h, 10/208.
1- "Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi wa Kiti kikuu cha Enzi, akuponye." (mara saba) [31] Abu Daud, 3/187, namba 3106, na At-Tirmidhi, 2/410, namba 2083, na Al-Albaani alisema kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahih Al-Jami’i", 5/180, na 322 na katika "Sahih Sunan Abi Daud", 2/276.
2- Mgonjwa ataweka mkono wake kwenye sehemu ya mwili wake inayomuuma na aseme: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu” mara tatu, kisha aseme: “Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu na uwezo wake kutokana na shari ya ninayoyapata na kuyaogopa.” (mara saba) [32] Muslim 4/1728, namba 2709.
3- “Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa watu, niondolee balaa na uponye. Wewe ndiye Mponyaji. Hakuna uponyaji isipokuwa uponyaji wako. Uponyaji ambao hauachi ugonjwa wowote nyuma.” [33] Bukhari na vile vile "Al-Fat-h" 10/206, namba 5745, na Muslim, 4/1724, namba 2194.
4- “Ninajikinga kwa maneno makamilifu ya Mwenyezi Mungu kutokana na kila shetani na wadudu wenye sumu, na kutokana na kila jicho baya.” [34] Bukhari na vile vile "Al-Fat-h" 6/408, namba 3371.
5- “Ninajikinga kwa maneno makamilifu ya Mwenyezi Mungu kutokana na shari ya vile alivyoviumba.” [35]
6- “Ninajikinga kwa maneno makamilifu ya Mwenyezi Mungu kutokana na ghadhabu yake, na adhabu yake, na shari ya waja wake, na minong’ono na wasiwasi za mashetani, na kwamba wasinikaribie.” [36] Abu Daud, namba 3893, na At-Tirmidhi, namba 3528, na Al-Albaani alisema kwamba ni hadithi nzuri katika Sahih At-Tirmidhi, 3/171.
7- “Ninajikinga kwa maneno makamilifu ya Mwenyezi Mungu, ambayo mwema wala muovu hawezi kuyavuka, kutokana na uovu wa alichokiumba, kukianzisha na kukieneza, na kutokana na uovu wa kile kinachoteremka kutoka mbinguni, na kutokana na uovu wa kile kinachopanda ndani yake, na kutokana na uovu wa alichokieneza katika ardhi, na kutokana na uovu wa yale yanayotoka humo, na kutokana na uovu wa majaribu ya usiku na mchana, na kutokana na uovu wa kijacho usiku, isipokuwa kijacho usiku kwa uzuri, Ewe Mwingi wa rehema.” [37] Musnad Ahmad, 3/119, namba 15461, yenye mnyororo sahihi wa wapokezi, na Ibn as-Sunni, nambari 637. Tazama pia: "Majma’ az-Zawa’id", 10/127, na Al-Albani alisema kwamba ni hadithi sahihi katika "Silsilat al-Ahadith Asswahiiha" 7/196.
8- “Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mbingu saba, na Mola Mlezi wa Ardhi, na Mola Mlezi wa Kiti cha Enzi kikuu, Mola wetu Mlezi na Mola Mlezi wa kila kitu, Mwenye kupasua mbegu na kokwa, Mwenye kuiteremsha Taurati, Injili na Qur'ani, ninajikinga kwako kutokana na uovu wa kila kitu unachokishikilia kwa nywele za utosini. Wewe ndiye wa Kwanza, na hakuna chochote kabla yako. Na Wewe ndiye wa Mwisho, na hakuna chochote baada yako. Na Wewe ndiye wa Dhahiri na hakuna chochote juu yako. Na Wewe ndiye wa Siri na hakuna chochote chini yako...” [38] Muslim, 4/2084, namba 2713.
9- “Kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakufanyia ruqya kutokana na kila jambo linalokudhuru, na kutokana na uovu wa kila nafsi au jicho lenye husuda. Mwenyezi Mungu akuponye, kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakufanyia ruqya." Muslim kutoka kwa Abu Said, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, 4/1718, namba 2186.
10- “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, akupe afueni, na akuponye kutokana na kila maradhi, na kutokana na shari ya kila mwenye husuda anapohusudu, na kutokana na shari ya kila mwenye kijicho.” [40] Muslim kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, 4/1718, namba 2185.
11- “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, ninakufanyia ruqya kutokana na kila jambo linalokudhuru, kutokana na husuda ya mwenye kijicho, na kutokana na kila chenye jicho baya. Mwenyezi Mungu akuponye.” [41] Sunan Ibn Majah, namba 3527, kutoka kwa 'Ubada ibn as-Samit, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, na Al-Albani amesema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih Ibn Majah", 2/268.
Dua hizi za kujikinga kwa Mwenyezi Mungu, na dua mbalimbali na ruqya hutumika kutibu uchawi, kijicho, kumilikiwa na majini na magonjwa yote. Kwani ni ruqya inayojumuisha sana na yenye manufaa, Mwenyezi Mungu akipenda.
Aina ya tatu: Kutoa uchawi kwa kutoa damu chafu katika sehemu au kiungo ambacho athari za uchawi huo zimeonekana, ikiwa hilo linawezekana. Lakini ikiwa hilo haliwezekani, basi yale yaliyotajwa hapo awali miongoni mwa matibabu yanatosha, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mtukufu. [42] Tazama: "Zaad al-Ma’aad", 4/125. Na kuna aina mbalimbali za matibabu ya uchawi baada ya kutokea kwake ambazo zinakubalika ikiwa zitajaribiwa na kuthibitika kuwa ni zenye manufaa. Tazama: "Muswannaf Ibn Abi Shaiba", 7/386-387, Fat-hul Baari, 10/233-234, "Muswannaf Abdir-Razzaq", 11/13, "As-Swaarim al-Battaar", uk. 194-200, na Uchawi, uhalisia wake na hukumu yake, uk. 64-66.
Aina ya nne: Dawa za asili. Zipo dawa za asili zenye manufaa, ambazo zimeashiriwa na Qur'ani Tukufu na Sunna safi ikiwa mtu atazitumia kwa yakini, ukweli, na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, pamoja na kuamini kuwa manufaa hayo yanatoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akipenda. Vile vile kuna dawa zinazoundwa na miti shamba na mfano wake. Dawa hizo zinatokana na uzoefu, kwa hivyo hakuna ubaya kunufaika kwazo kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, maadamu si haramu.[43] Tazama: "Fat-hul-Haqq al-Mubin fi ’ilaaj asswar’i, wassihr wal-'ayn", ukurasa139. Tazama yaliyotajwa hapo awali katika aina ya pili ya matibabu ya uchawi katika kitabu hiki.
Na miongoni mwa matibabu ya asili yenye manufaa, Mwenyezi Mungu akipenda, ni Asali [44], Habbati Saudaa [45], maji ya Zamzam [46], na maji ya mvua; kutokana na maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyobarikiwa." [47] Surat Qaf, aya ya 9. [36] Tazama: "Fat-hul-Haqq al-Mubin", ukurasa 140. Matibabu kwa asali yatatajwa baadaye katika kitabu hiki. [37] Tazama: "Fat-hul-Haqq al-Mubin", ukurasa 141. Matibabu kwa Habbati Saudaa yametajwa katika kitabu hiki. [38] Tazama: "Fat-hul-Haqq al-Mubiin", ukurasa 144. Matibabu kwa maji ya Zamzam yatatajwa baadaye katika kitabu hiki.
Na mafuta ya zaituni; kwa sababu ya maneno ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: "Kuleni mafuta (ya zaituni) na jipakeni kwayo. Kwa kuwa huo ni katika miti iliyobarikiwa.” [39] Na vile vile, imethibiti kutokana na uhalisia wa majaribio, na matumizi, na usomaji kwamba hayo ndiyo mafuta bora zaidi [40]. Na katika dawa asilia ni kuoga, kujisafisha na kupaka manukato [41]. Ahmad katika "Al-Musnad", 3/497, nambari 16055, At-Tirmidhi, namba 1851, Ibn Majah, namba 3319, na Al-Albani alisema kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahih At-Tirmidhi", 2/166. Tazama: "Fat-hul-Haqq al-Mubin fi ’ilaaj asswar’i, wassihr wal-'ayn", ukurasa142. Tazama: Rejeleo lililotangulia, ukurasa145.
2- Matibabu ya kijicho
Matibabu ya kijicho yana aina mbalimbali:
Sehemu ya kwanza: Kabla ya kupatwa, nayo ina aina nyingi:
1- Kujikinga na kuwalinda wale ambao wanaohofiwa kupatwa nacho kwa nyiradi, na dua, na mambo ya kujikinga kwayo kwa Mwenyezi Mungu, kama ilivyo katika sehemu ya kwanza ya kutibu uchawi [51]. Tazama yale yaliyotajwa hapo awali katika kitabu hiki kuhusu kutibu uchawi.
2- Mwenye kuhofu au kuogopa kuathiri kwa kijicho chake – akiona kitu anachokipenda nafsini mwake, au katika mali yake, au kwa mtoto wake, au kwa ndugu yake, au katika kitu chochote kile – basi aombe dua kwa kusema: “Atakalo Mwenyezi Mungu, hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, Ewe Mwenyezi Mungu mpe baraka." Kwa sababu Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alisema: "Mmoja wenu akiona kitu anachokipenda kwa nduguye, basi amuombee baraka." [52] Muwatta-a Malik, 2/938, Ibn Majah, 2/1160, namba 3509, Ahmad, 4/447, namba 15700, na Al-Albani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih Ibn Majah", 2/265, "Zaad Al-Ma’aad", 4/170, na "Asswaaarim al-bataar fi attaswadi lissahrat wal-ashraar", cha sheikh Wahiid Abdis-Salam, ukurasa wa 229-252.
3- Kuficha mambo mazuri mbali na mtu ambaye anahofiwa kuathiriwa na kijicho.[53] Tazama: "Sharh as-Sunna", cha Al-Baghawii, 13/116, na "Zaad al-Ma’aad", 4/173.
Sehemu ya pili: Baada ya kupatwa na kijicho, na hilo lina aina mbalimbali:
1- Iwapo atajulikana aliyesababisha kijicho hicho, basi ataamrishwa kutawadha, kisha aliyepatwa na kijicho chake ataoga kwa maji yake ya udhu. [54] Tazama: "Sunan Abi Daud", 4/9, namba 5056, na Al-Albani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Silsilat Al-Ahadith As-Sahihah", 6/61, na Zaad Al-Ma’aad, 4/163. Tazama pia: Al-Wiqaya wal-‘ilaaj minal kitaab was-sunnah", cha Muhammad bin Shaayi'i, ukurasa 144-147.
2- Kusoma haya kwa wingi: "Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee." Na suratul-Falaq na suratun-Naas, suratul-Fatiha, Ayatul-Kursii, Aya za mwisho za Suratul-Baqarah, na dua zinazoruhusiwa kisheria kuzisoma katika ruqya, pamoja na kupuliza na kupangusa sehemu ya maumivu kwa mkono wa kulia, kama ilivyo katika aina ya pili ya matibabu ya uchawi, sehemu ya (jim), kuanzia namba 1-11.[55] Tazama: Aina ya pili ya matibabu ya uchawi, kutoka katika kitabu hiki.
3- Atasomea ndani ya maji huku akipuliza, kisha mgonjwa atakunywa maji hayo, na ajimiminie yaliyobakia [56], au asomee kwenye mafuta ya zaituni na ajipake [57]. Na ikiwa kisomo kitafanywa katika maji ya Zamzam, basi hilo ndilo kamilifu zaidi ikiwezekana [58], au maji ya mvua. [59] Sunan Abi Daud, 4/10, namba 3885. Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, alimfanyia hivyo Thabit ibn Qays. Al-Albaani alisema kwamba ni Hadithi dhaifu katika Da’if Abi Daud, nambari 836. "Musnad Ahmad", 3/497, namba 16055, na Al-Albaani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Silsilat Al-Ahadith Al-Sahihah", 1/108, nambari 379. Tazama yaliyotajwa hapo awali katika aina ya nne ya matibabu ya uchawi, katika kitabu hiki. Tazama: Aina ya pili ya matibabu ya uchawi, katika kitabu hiki.
4- Hakuna ubaya mgonjwa kuandikiwa Aya za Qur'ani, kisha zimiminiwe maji kisha ayanywe [60]. Aya zenyewe ni kama vile Al-Fatiha, Ayatul-Kursi, na Aya mbili za mwisho za Surat Al-Baqarah. "Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee." Na Suratul-Falaq, Suratun-Naas na dua za ruqya, kama ilivyokuja katika aina ya pili ya matibabu ya uchawi, aya (b) na (j), kutoka namba 1-11. [61] Tazama: "Zaad al-Ma’aad, cha Ibn al-Qayyim", 4/170, na "Fataawa Ibn Taymiyyah", 19/64. Tazama yaliyotajwa hapo awali katika aina ya nne ya matibabu ya uchawi, katika kitabu hiki.
Sehemu ya tatu: Kufanya visababu ambavyo huepusha kijicho, ambazo ni kama ifuatavyo:
1- Kujikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake.
2- Kumcha Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka, na kutunza maamrisho na makatazo yake. “Mlinde Mwenyezi Mungu naye atakulinda.” [62] At-Tirmidhi, namba 2516, na Al-Albaani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih At-Tirmidhi", 2/309.
3- Kumfanyia subira mwenye husuda, na kumsamehe. Asipigane naye, wala asilalamike kutokana naye, wala asifikirie kumdhuru.
4- Kumtegemea Mwenyezi Mungu, kwani anayemtegemea Mwenyezi Mungu, basi Yeye humtosheleza.
5- Kutomuogopa mwenye husuda, wala asiujaze moyo wake na mawazo juu yake, na hii ni miongoni mwa dawa zenye manufaa zaidi.
6- Kumuelekea Mwenyezi Mungu aliyetakasika, kwa kumsafishia ibada na kutaka radhi zake.
7- Kutubia dhambi; kwa sababu hizo huwapa mamlaka maadui wa mtu: "Na misiba inayokupateni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu. Naye anasamehe mengi." [63] Surat Ash-Shuraa, Aya ya 30.
8- Sadaka na wema kiasi inavyowezekana. Kwani haya yana athari ya ajabu katika kuepusha balaa, kijicho na uovu wa mwenye husuda.
9- Kuzima moto wa mwenye husuda, mchokozi, na mwenye kuleta madhara kwa kuwafanyia wema. Kila wanavyokuleteeni madhara, maovu, uchokozi na husuda, ndivyo mnavyofaa kuwatendea wema, na kuwapa nasaha na kuwaonea huruma. Haya hawezeshwi kuyafikia isipokuwa mwenye fungu kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
10- Kuitakasa tauhidi na kumpwekesha Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima, ambaye hakuna kinachoweza kudhuru wala kunufaisha isipokuwa kwa idhini yake aliyetakasika. Na hayo ndiyo yanayoyazunguka yote hayo, na juu yake vinazungukia visababu hivi. Kwani Tauhidi ndiyo ngome kuu ya Mwenyezi Mungu, ambayo anayeingia humo, anakuwa miongoni mwa watakaopata amani.
Hizi ni sababu kumi za kuepusha uovu wa mwenye husuda, kijicho na mchawi. [64] Tazama: "Badai’ Al-Fawa’id", cha Ibn Al-Qayyim, 2/238-245.
3- Matibabu ya mwanadamu kuingiwa na jini
Matibabu ya mwanadamu kuingiwa na jini yana aina mbili:
Sehemu ya Kwanza: Kabla ya kuingiwa:
Katika njia za kuzuia hilo ni kushikamana na faradhi zote na mambo ya wajibu, kujiepusha na mambo yote yaliyoharamishwa, kutubia madhambi yote, na kutafuta ulinzi kwa nyiradi, dua mbalimbali na kujikinga kwa Mwenyezi Mungu kwa njia zilizowekwa katika sheria.
Sehemu ya Pili: Matibabu ya baada ya kuingiwa na jini:
Haya yanakuwa kwa Muislamu kusoma Qur'ani, unafaa moyo wake uingiliane na ulimi wake, na amsomee ruqya mtu aliyeingiwa na jini. Na ruqya kubwa sana huwa kwa kusoma Alfatiha [65], Ayatul-Kursi, na Aya mbili za mwisho za Surat Al-Baqarah, na "Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee." na "Sema: "Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko." na "Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa watu." Atazisoma pamoja na kumpulizia aliyeingiliwa na jini, na kurudia hayo mara tatu au zaidi, na Aya nyinginezo za Qur'ani; kwa sababu Qur'ani nzima ina uponyaji kwa yale yaliyomo ndani ya nyoyo, na uongofu na rehema kwa Waumini [66]. Vile vile asome dua za ruqya kama ilivyo katika aina ya pili ya tiba ya uchawi, sehemu ya (b) na (c) [67]. Kuna mambo mawili muhimu katika tiba hii: Tazama: Sunan Abi Daud, 4/13-14, namba 3896, na Ahmad, 5/210, namba 21835, na Al-Albaani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Silsilat Al-Ahadith Al-Sahihah", namba 2028. Tazama: "Al-Fat-h Ar-Rabbani", "Tartiib Musnad Al-Imam Ahmad", 17/183.
La kwanza ni kutoka upande wa aliyeingiliwa na jini, kupitia kwa nguvu ya nafsi yake, ukweli wa kuelekea kwake kwa Mwenyezi Mungu, na kutafuta kimbilio sahihi ambako moyo na ulimi vimeafikiana juu yake.
Jambo la pili ni kutoka kwa anayetoa tiba kwamba yeye vile vile awe hivyo. Kwa maana silaha inategemea anayeshambulia kwayo. [68] Tazama: Ruqya yenye maelezo ya kina na yenye manufaa katika "As-Swaarim Al-Battaar", ukurasa 109-117, cha Sheikh Wahiid Abdus-Salam. Vile vile tazama: "Zaad Al-Ma’aad", 4/66-69, na "Iidhwaahal-haqq fii dukhulil-jinni bil-insiyyi warradd 'alaa man ankara dhaalik", cha mwanachuoni Abdulaziz bin Abdillah bin Baaz, ukurasa 14, na "Fataawa Ibn Taimiyyah", 19/9-65, na 24/276 "Al-Wiqaayatu wal-'ilaaj minal-kitaabi was-sunna, cha Muhammad bin Shaay'i", ukurasa 66-69. Na tazama: "Kaifiyyatu tward al-jinn minal-bait, wal-wiqaayatu wal-'ilaaj", cha Muhammad bin Shaay’i, uk. 59, na "Aalamul-jinn wash-shayaatwiin", cha Al-Ashqar, uk. 130.
Ikiwa adhana itaadhiniwa kwenye sikio la aliyeingiwa na jini, basi hilo pia ni zuri; kwa sababu Shetani hukimbia hilo. [69] Tazama: "Fat-hul-Haqq al-Mubin fi ilaaj As-Swar’i wassihr wal-'ayn", ukurasa 112, na Bukhari, namba 574.
4- Matibabu ya magonjwa ya kisaikolojia:
Tazama katika suala hili: Sababu za kupanuka kwa kifua katika "Zaad al-Ma’aad", 2/23-28, na kitabu "Al-Wasaail al-mufiida lilhayaatis sa'iida", cha mwanachuoni Abdur-Rahman ibn Naaswir Assa’di, Mwenyezi Mungu amrehemu.
Tiba kubwa zaidi ya magonjwa ya kisaikolojia [70] na dhiki ya kifua, kwa ufupi, ni yafuatayo:
1- Uongofu na kumpwekesha Mwenyezi Mungu, kama vile upotofu na ushirikina ni miongoni mwa sababu kubwa za dhiki ya kifua.
2- Nuru ya imani ya ukweli ambayo Mwenyezi Mungu huitupa ndani ya moyo wa mja, pamoja na matendo mema.
3- Elimu yenye manufaa. Kiasi mja anavyozidi kuwa na elimu pana, ndivyo moyo wake unavyozidi kufunguka na kupanuka.
4- Kutubia, na kurejea kwa Mwenyezi Mungu aliyetakasika, na kumpenda kwa moyo wote, na kuelekea kwake na kufurahia kumuabudu.
5- Kumtaja Mwenyezi Mungu kila mara katika kila hali na kila mahali, kwani kumtaja kuna athari ya ajabu katika kufungua kifua, kufariji moyo, na kuondoa wasiwasi na huzuni.
6- Kuwatendea viumbe wema kwa aina zote, na kuwanufaisha kiasi inavyowezekana. Kwa maana mtu mkarimu, afanyaye wema ndiye mtu mwenye moyo uliofunguka zaidi ya watu wote, na ndiye mwenye nafsi nzuri zaidi, na mwenye moyo wenye furaha zaidi.
7- Ujasiri, kwani mtu shujaa ana kifua kilichofunguka na moyo mpana.
8- Kuondoa uchafu wa moyo [71] miongoni mwa sifa mbaya zinazosababisha dhiki na adhabu, kama vile husuda, chuki, uadui, kuzozana na dhuluma. Ilithibiti kwamba Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, aliulizwa kuhusu mtu bora zaidi. Akasema: "Kila mwenye moyo safi na ulimi wa ukweli." Wakasema: Tunamjua mwenye ulimi wa ukweli, lakini ni nani aliye na moyo safi? Akasema: “Ni mcha Mungu, safi, hana dhambi ndani yake wala dhuluma, wala chuki wala husuda.” [72] Neno 'daghal' linamaanisha kasoro ya kitu inayokiharibu. Imepokelewa na Ibn Majah, namba 4216, na Al-Albaani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih Ibn Majah", 2/411.
9- Kujiepusha kupita kiasi katika kuangalia, kuzungumza, kusikiliza, kuchanganyika na watu, kula na kulala. Kwani kuacha hayo ni sababu mojawapo ya kufunguliwa kifua, na moyo kuwa na furaha na kuondolewa wasiwasi wake na huzuni wake.
10- Kujishughulisha na matendo au elimu yenye manufaa. Kwa sababu hayo huufanya moyo kusahau kile kinachoupa wasiwasi.
11- Kujishughulisha na matendo ya siku ya leo, na kujiepusha na kujali mambo ya wakati ujao na kuhuzunikia yaliyopita. Hivyo basi, mja anafaa kujitahidi kufanya yanayomnufaisha katika dini na dunia hii, na amuombe Mola wake Mlezi kufaulu kufikia lengo lake, na atafute msaada wake katika hilo. Kwa sababu hayo huliwaza na kuondoa wasiwasi na huzuni.
12- Kumtazama yule aliye chini yako, na kutotazama aliye juu yako, katika kuwa salama na mambo yanayofuatana nayo, na katika riziki mambo yanayofuatana nayo.
13- Kusahau magumu yaliyopita ambayo hawezi kuyabadilisha, wala asifikirie juu yake kabisa.
14- Mja anapokifikwa na msiba, basi ni lazima ajitahidi kuupunguza kwa kutathmini matokeo mabaya zaidi ya hali hiyo na kuizuia kwa kiasi cha uwezo wake.
15- Nguvu ya moyo, na kutosumbuka kwake na kuathirika juu ya mambo yasiyo na uhakika ambayo huletwa na mawazo mabaya, na kutokasirika, na kutotarajia kutoweka kwa mambo anayopenda, na kutokea kwa mambo mabaya. Bali, anapaswa kumuachia Mwenyezi Mungu Mtukufu mambo yake, huku akifanya visababu vyenye manufaa na kumuomba Mwenyezi Mungu msamaha na usalama.
16- Moyo kumtegemea Mwenyezi Mungu, kumkabidhi mambo, kuwa na dhana nzuri juu ya Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka. Kwani, anayemtegemea Mwenyezi Mungu, haathiriwi na mambo yasiyo ya uhakika. Abu Daud, 4/324, namba 5090, na Ahmad, 5/42, namba 0430, na Al-Albaani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih Al-Jami’i", nambari 3388, na akasema kwamba ni hadithi nzuri (Hassan) katika "Sahih Sunan Abi Daud", 3/251.
17- Mwenye akili nzuri anajua kuwa maisha yake sahihi ni maisha ya furaha na utulivu, na kwamba ni mafupi sana, kwa hivyo hafai kuyafupisha kwa wasiwasi na kuendelea kujiingiza katika huzuni. Kwa sababu hayo ni kinyume na maisha yenye afya nzuri.
18- Likimtokea jambo baya, basi alinganishe kati ya neema nyinginezo alizo nazo, ziwe ni za kidini au za kidunia, na ubaya uliompata. Anapofanya ulinganisho huo, itambainikia wazi kwamba yuko katika neema nyingi sana. Na vile vile, na alinganishe kati ya madhara anayohofu kumtokea na kati ya uwezekano mwingi ulioko wa kusalia salama, hapo asiache uwezekano dhaifu ushinde uwezekano mwingi wa nguvu wa kuwa salama. Na kwa kufanya hivyo, utaondoka wasiwasi wake na hofu yake.
19- Ajue kwamba madhara ya watu hayawezi kumdhuru, hasa kwa maneno mabaya. Bali yanawadhuru wao wenyewe. Kwa hivyo, asiyachukulie kwa uzito wala asiyafikirie; ili yasije yakamdhuru.
20- Aelekeze mawazo yake kwenye yale yatakayomfaa katika dini na dunia hii.
21- Mja asitake kushukuriwa kwa wema aliowafanyia wengine, isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ajue kuwa hayo alimfanyia Mwenyezi Mungu, kwa hivyo asijali shukrani ya yule ambaye alimfanya wema. "Hakika sisi tunakulisheni kwa ajili ya wajihi (radhi) za Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani." [73] Sura Al-Insan, Aya ya 9.
22- Kuyaweka mambo yenye manufaa mbele ya macho yake, kufanya juhudi ili kuyafikia, na kutotazama mambo yenye madhara, wala asiishughulishe akili yake wala mawazo yake na hayo.
23- Kufanya na kumaliza matendo ya sasa, na kuweka muda katika katika siku zijazo ili aweze kufanya matendo yajayo kwa nguvu ya fikira na vitendo.
24- Kuchagua matendo yenye manufaa zaidi na elimu zenye manufaa, muhimu zaidi kisha muhimu zaidi, hasa yale anayotamani sana miongoni mwake, na atafute msaada wa Mwenyezi Mungu katika hilo, kisha atafute ushauri. Pindi yanapopatikana masilahi, na akaazimia, basi na amtegemee Mwenyezi Mungu Mtukufu.
25- Kuzungumza kuhusu neema za Mwenyezi Mungu zilizo dhahiri na zilizofichikana. Kwani, kuzijua na kuzizungumzia, Mwenyezi Mungu huondoa kwa hayo wasiwasi na huzuni, na kumhimiza mja kushukuru.
26- Kumtendea wema mke, jamaa, mfanyakazi mwenzako, na kila mtu ambaye una uhusiano naye - unapopata kosa kwao - kwa kutambua sifa zao nzuri na kuzilinganisha na kosa lao. Unapofanya hivyo, urafiki utadumu na kifua kitafunguka. Na ndiyo maana Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alisema: "Mwanamume Muumini asimchukie mwanamke Muumini. Iwapo atachukia tabia moja kwake, ataridhika na nyingine."[74] Muslim, 2/1091, namba 1469.
27- Dua ya kuboresha mambo yote, na kubwa zaidi katika hizo ni: "Ewe Mwenyezi Mungu, nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo ngome ya mambo yangu, na nitengenezee dunia yangu ambayo ninaishi ndani yake, na nitengenezee Akhera yangu ambayo ndiyo marejeo yangu, na ufanye uhai kuwa ziada katika kila kheri, na kifanye kifo kuwa ni nafuu kutokana na kila shari." [75] Na vile vile: "Ewe Mwenyezi Mungu, ninatarajia rehema zako. Basi usiniache nijisimamie mwenyewe kwa kiasi cha kupepesa jicho, na nitengenezee mambo yangu yote. Hapana mungu ila Wewe." [76] Muslim, 4/2087, namba 2720. Abu Daud, 4/324, namba 5092, na Ahmad, 5/42, namba 20430, na Al-Albaani alisema kwamba ni Hadithi nzuri (Hasan) katika "Irwa’ Al-Ghaliil", 3/357, na Al-Arna’ut katika uhakiki wake wa "Al-Musnad", 34/75.
28- Kufanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu; kwa sababu ya kauli ya Mtume, rehema na amani za Mweneyzi Mungu zimshukie, “Fanyeni jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwani jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa milango ya Pepo, ambayo kwayo Mwenyezi Mungu huokoa kutokana na wasiwasi na huzuni.” [77] Ahmad, 5/314, 316, 319, 326, 330, yenye namba 21624, 22680, 22732, na Al-Hakim, na akasema kwamba ni Hadithi sahihi, na Adh-Dhahabi akakubaliana naye, 2/75, na Al-Albaani pia alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Silsilat Al-Ahaadith Assahiiha", 2/274.
Sababu na njia hizi ni tiba yenye manufaa kwa magonjwa ya kisaikolojia, na ni miongoni mwa tiba kubwa zaidi ya wasiwasi wa kisaikolojia kwa wale wanaozitafakari na kuzifanyia kazi kwa ukweli na ikhlasi. Baadhi ya wanazuoni walitibu kwazo hali na magonjwa mengi ya kisaikolojia, na Mwenyezi Mungu akanufaisha sana kwazo. [78] Tazama: "Muqaddimat al-wasaail al-mufiida", toleo la tano, ukurasa wa 6.
5- Tiba ya vidonda na majeraha
Kila mtu alipokuwa akilalamika kuhusu maumivu fulani, au ikiwa alikuwa na vidonda au majeraha, Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikuwa akifanya hivi kwa kidole chake - Sufian akiweka kidole chake cha shahada juu ya ardhi -, kisha anakiinua na kusema: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mchanga wa ardhi yetu, kwa mate ya baadhi yetu, wagonjwa wetu wanaponywa kwayo, kwa idhini ya Mola wetu Mlezi." [79] Bukhari na vile vile "Al-Fat-h" 10/206, namba 5750, na Muslim, 4/1721, namba 2191.
Neno hili hutamkwa hivi "Assukht" na pia hutamkwa hivi "Assakhat", nalo linamaanisha kinyume cha kuridhia, yaani kughadhibika. Tazama: "As-Swihaah", mzizi wa neno “Sakhitwa”, na "Al-Misbaah Al-Muniir", mzizi wa neno “sakhitwa”.
Maana ya hadithi hii ni kwamba atachukua baadhi ya mate yake kwenye kidole chake cha shahada, kisha ayaweke juu ya udongo, na baadhi yake yasalie juu yake, kisha apanguse kwa udongo huo juu ya sehemu iliyojeruhiwa au mahali penye ugonjwa, na kusema maneno haya huku akipangusa.[80] Tazama: Ufafanuzi wa An-Nawawi wa Sahih Muslim, 14/184, na "Fat-hul-Baari" cha Ibn Hajar, 10/208, na utazame maelezo ya kina ya hadithi hii katika "Zaad Al-Ma’aad", 4/186-187. Maana ya mja hapa ni mtu Muislamu.
6- Tiba ya msiba
"Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika Kitabu kabla hatujauumba. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi. 23. Ili msihuzunike kwa kilichokupoteeni, wala msijitape kwa alichokupeni. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila anayejivuna akajifahirisha." [81] Sura Al-Hadid, aya ya 22-23.
2- "Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, huuongoa moyo wake. Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi kila kitu." Sura At-Taghabun, Aya ya 11.
3- "Hakuna mja ambaye atafikwa na msiba na akasema: “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi kwake tutarejea. Ewe Mwenyezi Mungu, nilipe katika msiba wangu huu na unibadilishie kilicho bora zaidi", isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atamlipa katika msiba wake huo na atambadilishia kilicho bora zaidi." [83] Muslim, 2/633, namba 918.
4- "Anapofariki mtoto wa mja, Mwenyezi Mungu Mtukufu huwaambia Malaika wake: "Je, mmemchukua mtoto wa mja wangu?" Nao wanasema: "Ndiyo." Kisha anasema: "Je, mmechukua matunda ya moyo wake?" Wanasema: "Ndiyo." Kisha anasema: "Alisema nini mja wangu?" Wanasema: "Alikusifu na kutarajia malipo." [84] Anasema: "Mjengeeni mja wangu nyumba katika Pepo, na muiite nyumba ya kumsifu Mwenyezi Mungu." [85] Yaani alisema: Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake tutarejea. At-Tirmidhi, namba 1021, na Al-Albani alisema kwamba ni hadithi nzuri (Hasan) katika Sahih At-Tirmidhi, 1/298.
5- "Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Mja wangu Muumini hana malipo kutoka kwangu ikiwa nitamtoa mteule wake katika watu wa dunia na akatarajia malipo kutoka kwangu isipokuwa Pepo.” [86] Bukhari na vile vile "Al-Fat-h" 11/242, namba 6424.
6- Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alimwambia mwanamume mmoja ambaye mtoto wake wa kiume alifariki dunia: “Je, hupendi kwamba ufike kwenye mlango wowote miongoni mwa milango ya Peponi isipokuwa utamkuta anakungojea?” [87] Ahmad, nambari 15595, na An-Nasa’i, 4/23, katika Mazishi, mlango wa amri ya kutarajia malipo na kuwa na subira unapotokea msiba, nambari 1870, na mlolongo wake wa upokeaji ni sahihi kwa mujibu wa masharti ya hadithi sahihi, na Ibn Hibban alisema kwamba ni hadithi sahihi 8/209, na Al-Albaani alisema kwamba ni hadithi sahihi katika "Sahihi At-Targhib wat-Tarhiib", namba 2007. Tazama pia: "Fat-hul-Baari", 11/243.
7- "Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Nikimpa mtihani mja wangu kwa vipenzi vyake viwili, naye akasubiri [akitaraji malipo ya Mwenyezi Mungu], basi nitamfidia kwa Pepo badala yake." Akimaanisha macho yake. [88] Bukhari na vile vile "Al-Fat-h" 10/116, namba 5653, na kilicho baina ya mabano ni kutoka katika "Sunan At-Tirmidhi", namba 2400. Tazama: "Sahih At-Tirmidhi", 2/286.
8- “Hapana Muislamu anayefikwa na madhara kama vile maradhi au kitu chochote kile, isipokuwa Mwenyezi Mungu humuondolea kwayo madhambi yake, kama vile mti unavyodondosha majani yake.” [89] Bukhari na vile vile "Al-Fat-h" 10/120, namba 5648, na Muslim, 4/1991, namba 2571.
9- “Hakuna Muislamu anayechomwa na mwiba au kitu kikubwa zaidi kuliko hivyo, isipokuwa anaandikiwa kwa hilo daraja moja, na anafutiwa kwa hilo makosa yake.” [90] Muslim, 4/1991, namba 2572.
10- “Hakuna kinachompata Muumini kama vile maumivu yasiyoisha [91], wala uchovu [92], wala maradhi, wala huzuni, hata wasiwasi unaompata [93], isipokuwa anafutiwa kwa hayo baadhi ya dhambi zake.” [94] Wasb: Ni maumivu yasiyoisha, kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na watapata adhabu ya kudumu", yaani isiyoisha. Tazama maelezo ya An-Nawawi, 16/130. Annaswab ni uchovu. Neno hili lilitamkwa hivi "Yahummuhuu" na pia lilitamkwa hivi "Yahammuhuu" na matamshi yote mawili ni sahihi. Nalo linamaanisha kupatwa na wasiwasi. Tazama: Ufafanuzi wa An-Nawawi kuhusu Sahih Muslim, 16/130 Muslim, 4/1993, namba 2573.
11- “Hakika ukubwa wa malipo ni kulingana na ukubwa wa balaa. Na hakika Mwenyezi Mungu akiwapenda watu, basi huwapa mtihani. Kwa hivyo, atakayeridhia, basi atapata radhi za Mwenyezi Mungu. Na atakayekasirika, basi atapata hasira za Mwenyezi Mungu.” [95] [96] At-Tirmidhi, namba 2698, na Ibn Majah, namba 4023, na Sheikh Al-Albaani alisema kwamba ni hadithi nzuri (Hasan) katika Sahih At-Tirmidhi, 2/286.
12- “...Msiba haumuachi mja [97] isipokuwa unamwacha akitembea juu ya ardhi huku hana dhambi yoyote.” [98] At-Tirmidhi, nambari 2396, na Ibn Majah, nambari 4031, na Al-Albaani alisema kwamba ni hadithi nzuri (Hasan) katika Sahih At-Tirmidhi, 2/286.
7- Tiba ya wasiwasi na huzuni
1- Mja hatapatwa na wasiwasi wala huzuni, na akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mja wako, mtoto wa mja wako, mtoto wa kijakazi wako. Nywele zangu za utosi zipo mkononi mwako. Hukumu zako kwangu ni zenye kupita, na maamuzi yako kwangu ni ya uadilifu. Ninakuomba kupitia kila jina lako, ulilojiita kwalo mwenyewe, au uliloteremsha ndani ya Kitabu chako, au ulimfundisha yeyote katika viumbe wako, au ulilificha ndani ya elimu ya ghaibu iliyo kwako, uifanye Qur'ani ndiyo kitulizo cha moyo wangu, na mwangaza wa kifua changu, na kiondoshaji cha huzuni yangu, na kimalizaji cha msongo wa mawazo yangu;" isipokuwa Mwenyezi Mungu humuondolea huzuni yake na wasiwasi wake, na anambadilishia faraja mahali pake." [99] Ahmad, 1/391, namba 3712, na Al-Albaani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih At-Targhiib wa At-Tarhiib", nambari 182.
2- “Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na wasiwasi na huzuni, kutoweza na uvivu, ubakhili na woga, mzigo wa deni na kuzidiwa nguvu na watu.” [100] Bukhari, 7/158, namba 2893. Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikuwa akisema dua hii kwa wingi. Tazama: Bukhari na vile vile "Al-Fat-h", 11/173.
8- Tiba ya dhiki
1- “Hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu, Mkubwa, Mvumilivu. Hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa Kiti kikuu cha Enzi. Hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mbingu, na Mola Mlezi wa ardhi, na Mola Mlezi wa Kiti cha Enzi kitukufu". [101] Bukhari, 7/154, namba 6346, na Muslim, 4/2092, namba 2730.
2-
“Ewe Mwenyezi Mungu, ninataraji rehema zako, basi usiniache kujisimamia kwa kiasi cha kupepesa jicho, na unitengenezee mambo yangu yote, hakuna mungu ila Wewe.” [102]
3- “Hakuna mungu ila Wewe, umetakasika. Hakika mimi nilikuwa katika madhalimu."[103] At-Tirmidhi, 5/529, namba 3505, na Al-Hakim, na akasema kwamba ni hadithi sahihi, na Adh-Dhahabi akakubaliana naye, 1/505, na Al-Albaani akasema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih At-Tirmidhi", 3/168.
4- "Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi. Simshirikishi na chochote." [104] Abu Daud, 2/87, namba 1525, na Al-Albaani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih Ibn Majah", 2/335, na "Sahih At-Tirmidhi", 4/196.
9- Mgonjwa kujitibu mwenyewe
“Weka mkono wako kwenye sehemu ya mwili wako ulio na maumivu na useme: 'Kwa jina la Mwenyezi Mungu' mara tatu, na sema mara saba: 'Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu na uweza wake kutokana na shari ya ninayoyapata na ninayoyaogopa." [105] Muslim, 4/1728, namba 2202.
10- Kumtibu mgonjwa wakati wa kumtembelea
“Hakuna mja Muislamu anayemtembelea mgonjwa ambaye muda wake wa kifo haujafika na kusema mara saba: “Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi wa Kiti cha Enzi kitukufu, akuponye;" isipokuwa ataponywa.” [106] At-Tirmidhi, nambari 2083, na Abu Daud, nambari 3893, na Al-Albani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih At-Tirmidhi", 2/210, na "Sahih Al-Jami’i", 5/180.
11- Tiba ya wasiwasi na hofu usingizini
“Ninajikinga kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyo kamili kutokana na ghadhabu yake, na adhabu yake, na shari ya waja wake, na minong’ono ya mashetani, na wasinikaribie.” [107] Abu Daud, 4/12, namba 3893, na Al-Albani alisema kwamba ni Hadithi nzuri (Hasan) katika "Sahih At-Tirmidhi", 3/171.
12- Tiba ya homa
Amesema Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: “Homa inatokana na joto la Jahannam. Kwa hivyo ipozeni kwa maji.” [108] Bukhari na vile vile "Al-Fat-h" 10/174, namba 3264, na Muslim, 4/1733, namba 2210.
13- Tiba ya kuumwa na mdudu
1- Inasomwa Al-Fatiha pamoja na kukusanya mate na kuyapuliza kwenye mahali alipoumwa. [109] Bukhari pamoja na "Al-Fat-h", 10/208, Kitabu cha Tiba, mlango wa Ruqya ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
2- Patapanguswa mahali hapo kwa maji na chumvi huku ukisoma: "Sema: Enyi makafiri." Na suratul Falaq na suratun-Naas. [110] At-Twabarani katika "Al-Mu’jam Al-Saghir", 2/830, na Al-Haithami alisema kwamba mlolongo wa upokezaji wake ni mzuri katika "Majma’ Al-Zawaa-id", 5/111, na vile vile Al-Albani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Silsilat Al-Ahadith Al-Sahiiha", nambari 548.
14- Tiba ya hasira
Hasira inaweza kutibiwa kwa njia mbili:
Njia ya kwanza: Kinga
Hilo huwa kwa kuepuka visababishi vya hasira, na miongoni mwake ni kiburi, kujiona, majigambo, pupa isiyofaa, mzaha usiofaa, kutoyapa mambo uzito na mengineyo.
Njia ya pili: Tiba wakati hasira inapotokea
Njia hizo zinakusanyika katika aina nne:
Kujikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani, aliyelaaniwa.
Kushika Udhuu
Kubadilisha hali aliyonayo mwenye hasira, kwa kukaa, au kulala chini, au kuondoka, au kuacha kuzungumza, au kitu kinginecho.
Kukumbuka yale yaliyotajwa kuhusu malipo ya kuzuia hasira, na yale yaliyotajwa kuhusu matokeo ya hasira, kama vile kuachwa bila kusaidiwa. [111] Tazama maelezo haya pamoja na ushahidi wake sahihi katika: Aafaatullisaan, uku. 110-112, na "Alhikmatu fii ad-da'awati ilallahi", ukurasa 64-66 cha mwandishi huyu huyu.
15- Kujitibu kwa Habbati Saudaa
Amesema Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: "Katika Habbati Saudaa (mbegu nyeusi) kuna ponya kutokana na kila ugonjwa isipokuwa kifo." Ibn Shihab alisema: “As-Saam" maana yake ni kifo, na mbegu nyeusi maana yake ni 'Ash-shuuniiz'.” [112] Na Habbati Saudaa ina manufaa mengi, na kauli yake: "ponya kutokana na kila maradhi" ni kama kauli yake Mtukufu: "Inaangamiza kila kitu kwa amri ya Mola wake Mlezi." [113] Surat Al-Ahqaf, aya ya 25. Yaani, kila kitu kinachoweza kuharibiwa na mfano wake. [100] [99] Bukhari na vile vile Al-Fath, 10/143, nambari 5688, na Muslim kwa nambari 1735, nambari 2215. Tazama: "Zad al-Ma’aad", 4/297, na Tiba kutoka katika Kitabu na Sunna, cha mwanachuoni "Muwaffaq ad-Din Abdul-Latwif al-Baghdadi", ukurasa 88.
16- Kujitibu kwa Asali
1- Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kumtaja nyuki: "Katika matumbo yao kinatoka kinywaji chenye rangi mbalimbali; ndani yake kuna ponya kwa watu. Hakika katika haya ipo Ishara kwa kaumu wanaotafakari." [115] Sura An-Nahl, aya ya 69.
2- Amesema Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie:
"Uponyaji upo katika mambo matatu: Kufanya chale kwa kikombe (kupiga chuku), kinywaji cha Asali, au kuchoma kwa moto, lakini ninaukataza umma wangu kujitibu kupitia kuchoma kwa moto." [116] Bukhari na vile vile Al-Fat-h, 10/137, namba 5681. Tazama Faida za Asali katika: "Zaad Al-Ma’aad", 4/50-62, na "Tiba kutoka katika Kitabu na Sunna", cha mwanachuoni Muwaffaq Ad-Din Abdullatif Al-Baghdadi, uk. 129-136.
17- Kujitibu kwa maji ya Zamzam
1- Amesema Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie kuhusu maji ya Zamzam: “Hakika, hayo yamebarikiwa, na hakika ni chakula kizuri mno, [na ponya nzuri sana ya magonjwa].” [117]. Muslim, 4/1922, namba 2473, na kilicho baina ya mabano kiko kwa "Al-Bazzar", 2/86, na Al-Baihaqi katika "As-Sunan Al-Kubra", 5/147, na At-Tabarani katika "Al-Mu’jam Al-Awsat", 3/247, na mlolongo wa upokeaji wake ni sahihi. Tazama: "Majma’a Az-Zawaaid", 3/286.
2- Na Hadithi ya Jabir kutoka kwa Mtume: “Maji ya Zamzam ni kwa kile yanayonywewa kwa ajili yake.” [118] Ibn Majah, 3062, na wengineo, na Al-Albaani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih Ibn Majah", 2/183, na "Irwa’ al-Ghaliil", 4/320.
3- Ilithibiti kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwamba: “Alikuwa akibeba maji ya Zamzam [katika vyombo] [119] na viriba vya maji, na alikuwa akiwamiminia wagonjwa na kuwanywesha.” [120] Amesema Ibnul-Qayyim, Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu: "Mimi na wengine tumepitia mambo ya ajabu katika uponyaji kwa maji ya Zamzam, na nilitafuta kuponywa kwayo kutokana na magonjwa kadhaa na nikapona [121] kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. [122] Al-idaawa: Ni chombo cha kujisafishia. Tazama: "Mukhtar as-Swihaah", 1/11. At-Tirmidhi, 1/180, namba 963, na Al-Baihaqi, 5/202, na Al-Albaani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih At-Tirmidhi", 1/284, na "Silsilah Al-Ahadith Al-Sahihah", 2/572, nambari 883, na "Zaad Al-Ma'aad" 4/392. Na watu wasiokuwa watu wa Hijaz husema: “Fabari-itu." Yaani, kisha nikapona. Tazama: "An-Nihaya fi Ghariib al-Hadith", 1/111. Zaad al-Ma’aad, 4/393, na 178.
18- Tiba ya magonjwa ya moyo
Mioyo ina aina tatu:
1- Moyo ulio salama: Ni moyo ambao hataokoka yeyote siku ya Kiyaama isipokuwa atakayemjia Mwenyezi Mungu na moyo huu. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: 88. "Siku ambayo mali wala watoto havitomfaa mtu. 89. Isipokuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi." [123] Surat Ash-Shu'araa, aya ya 88-89.
Na Moyo ulio salama ni ule ambao umeepukana na kila matamanio yanayopingana na maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu, na kutokana na kila shaka inayopingana na habari zake, hivyo basi ukawa umesalimka kutokana na kuabudu kitu chochote kisichokuwa Yeye, na ukasalimika kutokana na kutafuta hukumu kwa asiyekuwa Mtume wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
Kwa ufupi, moyo mzuri na wenye afya njema ni ule usio na uhusiano wowote wa kitu chochote na mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu. Badala yake, utumwa wake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu: katika mapenzi, upendo, uaminifu, toba, unyenyekevu, hofu, tumaini na amali yake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee. Na ikiwa utachukia, unachukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na ikiwa utatoa, unatoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na ikiwa utanyima, unanyima kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Fikira zake zote ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, upendo wake wote ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, makusudio yake ni kwa ajili yake, mwili wake ni kwa ajili yake, na matendo yake ni kwa ajili yake, usingizi wake ni kwake, kukesha kwake ni kwake, na mazungumzo yake, na kuzungumza juu yake, ni jambo la kutamanika zaidi kwake kuliko mazungumzo yoyote, na mawazo yake yanazunguka katika yale yanayompendeza Yeye na yale anayoyapenda. [124] Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu moyo kama huu. Tazama: "Ighaathat al-Lahfan min Maswaa-id al-Shaitan" cha Ibnul-Qayyim, Mwenyezi Mungu amrehemu, 1/7, na 73.
2- Moyo uliokufa: Ni kinyume cha wa mwanzo, na ni ule usiomjua Mola wake, wala haumuabudu kwa amri yake, wala haumpendi wala haumridhishi. Bali unasimama na matamanio yake na raha zake, hata ikiwa ndani yake kuna hasira na ghadhabu ya Mola wake Mlezi. Anaabudu badala ya Mwenyezi Mungu: kwa mapenzi, hofu, matumaini, kuridhika, hasira, na unyonge. Anapochukia, anachukia kwa ajili ya matamanio yake, na anapotoa, anatoa kwa ajili ya matamanio, na anaponyima, ananyima kwa ajili ya matamanio yake. Hamu ni kiongozi wake na Tamaa ni imamu wake, ujinga ni dereva wake, na uzembe ni gari lake. [125] Tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na moyo huu. Tazama: Ighaathatu llahfaani Min Maswaa-idish- Shaitwani, 1/9.
3- Moyo mgonjwa: Ni moyo unaoishi lakini umeathiriwa na ugonjwa. Unapata nguvu kutoka katika viini viwili, kila kimoja kikitawala kwa nyakati tofauti. Moyo huo unajielekeza kuelekea kile kinachoutawala zaidi. Ndani yake kuna upendo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na imani kwake, na kumkusudia Mwenyezi Mungu pekee, na kumtegemea Yeye, ambavyo ni viini vya uhai wake. Hata hivyo, pia kuna upendo kwa matamanio, hamu ya kuyapata, wivu, kiburi, kujipenda, upendo wa kuinuka, uharibifu duniani kupitia uongozi, unafiki, kujionyesha, tamaa, na uchoyo, ambavyo ni viini vya uharibifu na kuangamia kwake. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atulinde dhidi ya moyo kama huu. Tazama: Ighathat al-lahfan, 1/9.
Qur'ani Tukufu ina tiba ya magonjwa yote ya moyo.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi watu! Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uponyaji wa yaliyomo nyoyoni, na uongofu na rehema kwa Waumini.." [127] Surat Yunus, aya ya 57. Na akasema Mwenyezi Mungu: "Na tunateremsha katika Qur'ani yale ambayo ni uponyaji na rehema kwa Waumini. Wala hayawazidishii madhalimu isipokuwa hasara." Surah Al-Isra, aya: 82.
Na magonjwa ya moyo yana aina mbili:
Aina ambayo mmiliki wake hahisi maumivu mara moja, ambao ni ugonjwa wa ujinga, mashaka na wahaka. Hii ni aina chungu zaidi kati ya aina hizi mbili, lakini kutokana na uharibifu wa moyo, moyo hauhisiwi hilo.
Na aina nyingine: Ni ugonjwa mchungu zaidi katika zama hizi: Kama vile wasiwasi, huzuni, simanzi, na hasira. Ugonjwa huu unaweza kutibika bila dawa za asili, kwa kuondoa visababishi vyake na mambo mengine. Tazama: "Ighaathat al-Lahfan", 1/44.
Tiba ya moyo hufanywa kupitia mambo manne:
Jambo la kwanza: kwa Qur'ani Tukufu; kwani ni tiba ya mashaka katika nyoyo, na inawaondolea shirki, uchafu wa ukafiri, maradhi ya shaka, na matamanio, na ni uongofu kwa anayeijua haki na akaifanyia kazi, na ni rehema kwa malipo ya haraka (Duniani) na yaliyoahirishwa (Akhera) ambayo Waumini huyapata kutoka kwayo, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hivi yule aliyekuwa maiti na tukamhuisha na tukamjalia kuwa na nuru ambayo kwayo anatembea kati ya watu, ni kama mfano wa mtu ambaye mfano wake yuko gizani?, hivyo ndivyo hupendezewa makafiri yale waliyokuwa wakiyafanya." [130] Surah Al-An'aam, aya: 122.
Jambo la pili: Moyo unahitaji vitu vitatu:
1- Kinachodumisha nguvu zake, nacho ni kwa imani, matendo mema, na kufanya matendo ya utiifu ya kila siku.
2- Kujiepusha na mambo yenye kudhuru, kwa kujiepusha na madhambi na kila aina ya makosa.
3- Kuondoa vitu vyote vyenye madhara, kwa kutubu na kuomba msamaha.
Jambo la tatu: Kutibu ugonjwa wa moyo unaosababishwa na kutawaliwa na Nafsi:
Huu una tiba mbili: Kuiwajibisha na kuipinga. Kuna aina mbili za uwajibikaji:
Aina ya kwanza: Kabla ya kitendo, na ina viwango vinne:
1- Je, kazi hii inawezekana kwake?
2- Je kufanya kitendo hiki ni bora kwake kuliko kukiacha?
3- Je, kitendo hiki kinafanywa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu?
4- Je, kitendo hiki kinavisaidizi, na kuna wasaidizi wanaomsaidia na kumpa msaada endapo kitendo hicho kinahitaji wasaidizi? Ikiwa jibu litapatikana, anapaswa kuendelea, na vinginevyo basi kamwe asifanye.
Aina ya pili: Baada ya kitendo, na hii ina aina tatu:
1- Kujihesabia mwenyewe kwa yale matendo ya ibada ambayo amekosa kutimiza haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa kutoyatekeleza kwa njia inayotakiwa na miongoni mwa haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu ni pamoja na: Kutakasa nia, na Nasaha, kumfuata Mtume, na kushuhudia ushuhuda wa wema, na kukiri neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yake katika hilo, na kukiri mapungufu baada ya hayo yote.
2- Kujihesabu kwa kila kitendo ambacho kukiacha kwa ingekuwa bora kwake kuliko kukifanya.
3- Kujihesabu kwa kitendo kinachoruhusiwa au cha kawaida ambacho hakukifanya, na ikiwa mtu amemkusudia nacho Mwenyezi Mungu na Akhera, katika hali hiyo mtu atakuwa mshindi, au aliyekusudia ulimwengu, katika hali hiyo atakuwa ni mwenye hasara.
Jumla ya hayo ni kwamba kwanza ajihesabu katika wajibu wa faradhi, kisha akamilishe ikiwa kuna upungufu, kisha ajihesabu kwa yale yaliyoharamishwa, ikiwa anajua kwamba amefanya jambo moja kati ya hayo, basi afidie kwa kutubia na kuomba msamaha, kisha kwa yale yaliyofanywa na viungo vyake, kisha kwa kughafilika kwake. [131] Tazama: "Ighaathat al-Lahfan", 1/136.
Jambo la nne: Kutibu ugonjwa wa moyo uliotokana na kutawaliwa na Shetani juu yake:
Shetani ni adui wa wanadamu, na njia ya kumkimbia ni kupitia yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyaweka ikiwemo kutafuta hifadhi, pamoja na kutaka kujikinga na shari ya nafsi na shari ya Shetani. "Sema: Ewe Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa ghaibu na yenye kushuhudiwa, Mola Mlezi wa kila kitu na Mmiliki wake, nashuhudia ya kwamba hapana mungu ila Wewe. Najikinga Kwako na shari ya nafsi yangu, shari ya Shetani na ushirikina wake, na nisifanye maovu juu ya nafsi yangu au kuyaleta juu ya Muislamu. Sema unapoamka, na jioni inapoingia, na wakati wa kulala". [132] At-Tirmidhi, nambari 3392, na Abu Daud, nambari 5058, na Al-Albaani alisema kwamba ni Hadithi sahihi katika "Sahih At-Tirmidhi", 3/142.
Na kuomba hifadhi kwa Mwenyezi Mungu, na kutegemea kwake, na kumsafishia Yeye ibada, kunazuia mamlaka ya Shetani [133]. Tazama: "Ighaathat al-Lahfan", 1/145-162.
Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie mja wake na Mtume wake Muhammad, na aali zake na Maswahaba zake wote, na wote wanaowafuata kwa wema mpaka siku ya Malipo.
Related books
All books
UCHAMBUZI NA UFAFANUZI WA MASUALA MENGI YA HIJA, UMRA NA ZIARA KWA MUJIBU WA MUONGOZO WA QUR'ANI NA SUNNA54 lughaUCHAMBUZI NA UFAFANUZI WA MASUALA MENGI YA HIJA, UMRA NA ZIARA KWA MUJIBU WA MUONGOZO WA QUR'ANI NA SUNNA
Kitabu kinafafanua hukumu za Hija, Umra na Ziara kwa mujibu wa Qur'ani na Sunna, na kinaeleza mambo ya wajibu katika Hija na Umra. Vile vile kinaeleza mambo yaliyokatazwa wakati wa Ihramu na adabu za kuutembelea Msikiti wa Mtume, huku kikihadharisha dhidi ya uzushi (Bid'aa) katika ibada hizi.
Hisnu Al-Muslim Kutoka Katika Nyiradi Za Kitabu Na Sunna57 lughaHisnu Al-Muslim Kutoka Katika Nyiradi Za Kitabu Na Sunna
Kitabu kinakusanya Adhkari kutoka katika Kitabu na Sunna ili iwe rahisi kuzikariri katika nyakati na hali mbalimbali, na kinajumuisha Dua (maombi) za kuamka, kutawadha, swala, safari, na mengineyo, jambo ambalo linamsaidia Muislamu kuikinga nafsi yake ili awe katika hifadhi ya Mwenyezi Mungu na uangalizi wake.
(Kitabu cha Adabu za kwenda katika Swala)11 lugha(Kitabu cha Adabu za kwenda katika Swala)
Mtunzi: Sheikh Al- islaam na alama miongoni mwa alama, kiongozi aliyerudisha upya elimu ya dini, Sheikh Muhammad bin Abdulwahhab Allah Mtukufu amrehemu. Wamefanya kazi ya kusahihisha na kulinganisha Nakala iliyoandikwa kwa mkono katika Maktaba ya Saudia kwa namba 269/86 na nakala nyingine nyingi zimechapishwa na masheikh wafuatao: Abdul karim bin Muhammad Al-laahim. Naasir bin Abdillahi Al- Twariim, Suud bin Muhammad Al- bashar. Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu: (Mlango wa adabu za kwenda katika Swala) Ni Sunna kutoka kuiendea swala hali ya kuwa umejitwaharisha…
NJIA ZENYE FAIDA KWA MAISHA YENYE FURAHA85 lughaNJIA ZENYE FAIDA KWA MAISHA YENYE FURAHA
Kitabu "Njia zenye Faida kwa Maisha yenye Furaha" cha Sheikh, mwanachuoni Abdur-Rahman bin Naasir As-Sa'adiy – Mwenyezi Mungu amrehemu – kinashughulikia sababu zinazopelekea furaha ya kweli kutoka katika mtazamo wa kiimani wa kina, na kinamwongoza msomaji kufikia utulivu wa moyo kupitia imani na matendo mema, kumtaja Mwenyezi Mungu, kuridhika, kutafakari neema zake, kufanya ihsani, kutegemea Mwenyezi Mungu, kuwa na subira, na kuyapima mambo ipasavyo; kwa mtindo mzuri unaoweka mbele yako ramani ya maisha yenye utulivu, yenye uwiano, na yenye furaha licha ya misukosuko ya maisha.