المنتقى من المتجر الرابح في ثواب العمل الصالح - المعتمد
كتاب جامع لجملة من أحاديث النبي -صلى الله عليه وسلم- الصحيحية في ثواب الأعمال الصالحة كطلب العلم والطهارة والصلاة، وصلاة التطوع، والجمعة والجنائز، والصدقات والصوم والحج والجهاد، وقراءة القرآن، وذكر الرحمن وغيرها.
This PDF is generated automatically from the book's text; its layout may differ from the printed edition.
YALIYO CHAGULIWA KUTOKA KATIKA SOKO LENYE FAIDA KATIKA THAWABU ZA MATENDO MEMA.
Thawabu za elimu na wanachuoni.
Kutoka kwa Muawiya -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
Imepokelewa na Bukhari (71) na Muslim (103)
Na kutoka kwa Abuu huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-
Imepokelewa na Muslim 2699.
MALIPO YA KUIFUNDISHA ELIMU.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
Imepokelewa na Muslim 1631.
Na kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Muslim 2674.
Kutoka kwa Abii Masuudi Al Answari alisema: Amesema Mtume rehema na Amani zimfikie:
Imepokelewa na Muslim 1893.
THAWABU ZA KUSHIKA UDHU KIKAMILIFU.
kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Muslim 244.
Na kutoka kwa Uthman bin Afani -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-
Imepokelewa na Muslim 229.
THAWABU ZA KUTAWADHA KIKAMILIFU KATIKA KIPINDI CHA BARIDI NA MAUMIVU YA MWILI.
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
Imepokelewa na Muslim 251.
THAWABU ZA KUPIGA MSWAKI.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu-Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Imepokelewa na Nasaai 1/10 na akaitolea maelezo Bukhari katika sahihi zake 4/158
THAWABU ZA KUTUNZA UDHU.
Kutoka kwa Thawbaan -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Allah- Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake:
"Kuweni na imani na msimamo wa dini na hamta weza kuyadhibiti mambo yote, na mjue kuwa swala ndio tendo bora kuliko yote, na hakuna atakaye hifadhi udhu ila ni Muumini"
Ameipokea Ahmad (22378)
THAWABU ZA KUTOA SHAHADA MBILI BAADA YA UDHU.
kutoka kwa Omar Bin Khatwab radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Muslim 234.
THAWABU ZA KUSALI BAADA YA UDHU.
kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema kumwambia Bilali wakati wa swala ya Alfajiri:
'Bilal Akasema: Sijafanya ibada kubwa isipokuwa sijawahi kutawadha usiku au mchana isipokuwa ninaswali kwa udhu huo idadi ya rakaa alizo nijaalia Allah niziswali'
Imepokelewa na Bukhari (1149) na Muslim (2458)
Na kutoka kwa Uqbah bin Aamir-Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-
Imepokelewa na Muslim 234.
Na kutoka kwa Othmaan -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Yeyote atakaye tawadha mfano wa udhu wangu huu, kisha akasali rakaa mbili, na asiizungumzishe ndani ya nafsi yake atasamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake".
Imepokelewa na Bukhari (164) na Muslim (103)
MALIPO YA MUADHINI.
Kutoka kwa Bin Abii Swa'aswa'h Al'answar: kuwa Aba Said Al'khudry Allah amridhie alisema kumwambia:
"Hakika mimi ninakuona unapenda Kondoo na kuishi Kijijini, utakapo kuwa upo kwenye Kondoo wako na Kijijini kwako Basi watolee watu Adhana kwa Ajili ya Sala na kisha unyanyue Sauti yako kwa Wito kwa Hakika ilivyo: Hato sikia ukomo wa Sauti ya Mtoa Adhana Jini wala Mtu wala kitu chochote isipokuwa kitamtolea ushahidi siku ya Kiyama"
Amesema Abu Said: Nimesikia kauli hii kutoka kwa Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake.
Ameipokea Bukhari (3296).
Na kutoka kwa Twalha Bin Yahya, kutoka kwa Baba yake Mdogo Amesema:
"Nilikuwa kwa Mua'wiyah Bin Abii Sufyaan, Akamjia Mtoa Adhana akimuita kwenda Kusali kisha akasema Mua'wiyah:
Nilimsikia Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake akisema: "Watoa Adhana watakuwa na Shingo ndefu siku ya Kiyama"
Imepokelewa na Muslim 387.
Kutoka kwa Anas Bin Malik Amesema:
"Alikuwa Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake akianza vita inapo chomoza Alfajiri. Na alikuwa anaposikia Adhana anajizuia (ana akhirisha vita) na kama hakusikia anauvaa mji kwa vita, kisha akamsikia Mtu akisema: 'Allahu Akbar Allahu Akbaru', Akasema Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake:"Huyu yuko katika uislamu" kisha akasema: Ash-hadu An laa ilaha ila llahu, Ash-hadu An laa ilaha ila llahu', kisha akasema Mtume Sala na Amani ziwe juu yake"umetoka Moto" (Yaani: Umesalimika na moto wa Mwenyezi Mungu kwa maneno yako hayo), wakatazama, ghafla wakamuona ni mchunga Mbuzi.
Imepokelewa na Muslim 382.
MALIPO YA ANAYE MFUATISHA MUADHINI.
Kutoka kwa Omar Bin Khatwab Allah amridhie amesema: Amesema Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake:
Imepokelewa na Muslim 385.
MALIPO YA DHIKIRI NA DUA YA KISHERIA BAADA YA ADHANA.
kutoka kwa Abdillah bin Amri Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba amemsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake anasema:
Imepokelewa na Muslim 384.
Na kutoka kwa Jaabir Bin Abdillah kuwa Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake amesema:
Ameipokea Bukhari (614).
Na kutoka kwa Sa'd Bin Abi Waqaas Allah amridhie kutoka kwa Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake amesema:
Imepokelewa na Muslim 386.
MALIPO YA SALA.
Kutoka kwa Ma'adan Bin Abi Twalha Alya'mary amesema:
Akasema Ma'dan: kisha nikamkuta Aba Dardai nikamuuliza akasema mfano wa yale aliyo nieleza Thauban.
Imepokelewa na Muslim 387.
Kutoka kwa Rabii'ah Bin Ka'b Al'aslamy amesema:
Nilikuwa ninalala pamoja na Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake kisha nikamletea chombo cha kutawadhia na mahitajio yake akasema kuniambia: "Omba" Nikasema: Ninakuomba ukaribu na wewe Peponi', akasema: "Unajingine kinyume na hilo?" nikasema ni hilo tu" Akasema: "Nisaidie mimi juu ya Nafsi yako kwa wingi wa kusujudu".
Imepokelewa na Muslim 489.
MALIPO YA SWALA ZA FARADHI NA KUDUMU NAZO.
kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Mwaonaje kama Mto ungelikuwa mbele ya Mlango wa mmoja wenu anakoga kila siku mara tano, hivi kungebakia chochote kutokana na uchafu wa mwili wake? Wakasema: hakubaki chochote kutokana na uchafu wa mwili wake, Basi mfano huo ndio mfano wa Sala Tano, Allah anafuta kwa Hizo Sala Tano Makosa'.
Imepokelewa na Bukhari (528) na Muslim (103)
Kutoka kwa Amr Bin Sa'd Bin A'swi amesema:
Nilikuwa kwa Othmani kisha akaomba chombo cha kutawadhia kisha akasema nimemsikia Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake anasema:
Imepokelewa na Muslim 227.
MALIPO YA SALA YA ALFAJIRI NA LASIRI KWA PAMOJA.
kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Wanapishana kwenu Malaika wakati wa usiku, na Malaika wakati wa mchana, na wanakusanyika katika swala ya alfajiri na swala ya Alaasiri, kisha wanapanda kwake wale waliolala kwenu, basi huwauliza hali yakuwa anajua: 'Mmewaachaje waja wangu? Husema: Tumewaacha wakiwa wanaswali, na tulifika wakiwa wanaswali".
Imepokelewa na Bukhari (555) na Muslim (103)
Na kutoka kwa Jariir Bin Abdillah amesema:
Imepokelewa na Bukhari (554) na Muslim (103)
kutoka kwa Ammar Bin Ruaibah Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
Anakusudia Alfajir na Asri.
Imepokelewa na Muslim 634.
Na kutoka kwa Abi Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Bukhari (574) na Muslim (103)
Maana ya baridi mbili: Ni Sala ya Lasiri na Sala ya Alfajiri.
MALIPO YA SALA YA LASIRI.
Kutoka kwa Abi Basrah Radhi za Allah ziwe juu yake alisema:
Alitusalisha Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake Sehemu inayo itwa Mukhamas, kisha Akasema: "Sala hii ilihudhurishwa kwa wale walio kuwa kabla yenu wakaipoteza, Basi atakaye ihifadhi atakuwa na malipo yake mara mbili"
Imepokelewa na Muslim 830.
MALIPO YA SALA YA ALFAJIRI.
Kutoka kwa Jundub -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
Imepokelewa na Muslim 657.
MALIPO YA SWALA YA ISHAA NA ALFAJIRI KATIKA JAMAA.
kutoka kwa Othmani Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
"Atakaye Sali Isha kwa jamaa kana kwamba amesimama nusu ya Usiku,na atakaye Sali Alfajiri kwa Jamaa kana kwamba amesali usiku mzima"
Imepokelewa na Muslim 656.
MALIPO YA SWALA KATIKA WAKATI WAKE.
Kutoka kwa Ibnu Masoud- Radhi za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Bukhari (527) na Muslim (103)
Ubora wa kuitikia Amiini ndani ya Sala
kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Atakapo sema Imamu: Ghayril Maghbuubi Alayhim wala Dhwaalliin) Basi semeni Amiini, Basi, itakaye afikiana kauli yake na kauli ya Malaika atasamehewa yale yaliyo tangulia katika Madhambi yake"
Imepokelewa na Bukhari (782) na Muslim (103)
Na kutoka kwa Abi Musa Al'ash'ary Allah Amridhie amesema: Hakika Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake alitutolea Hotuba akatubainishia sunna zetu na akatufundisha Sala zetu, kisha akasema: "Mtakapo Sali Basi nyoosheni Safu zenu, kisha awaongoze mmoja wenu, atakapo piga takbira na nyie pigeni Takbira, na atakapo sema: Ghayril Mghbuub Alayhim wala dhwaaliin) basi semeni :(Amiini), Allah atakujibuni"
Imepokelewa na Muslim 404.
Ubora wa kusema (Rabbana lakal hamdu) baada ya kutoka kwenye Rukuu.
kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Atakapo sema Imamu: Ghayril Maghbuubi Alayhim wala dhwaalliin) Basi semeni Amiini, Kwani, yule itakaye afikiana kauli yake na kauli ya Malaika atasamehewa yale yaliyo tangulia katika Madhambi yake"
Imepokelewa na Bukhari (796) na Muslim (103)
Kutoka kwa Abi Musa Al'ash'ary Radhi za Allah ziwe juu yake alisema:
Hakika Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake alitutolea Hotuba akatubainishia Sunna zetu na akatufundisha Sala zetu kisha akasema: "Mtakapo taka kusali Basi nyoosheni Safu zenu, kisha awasalishe mmoja wenu, na atakapo sema: (Samia llahu liman Hamidahu) Basi semeni: (Allahumma Rabbana lakal Hamdu) Allah anakusikieni"
Imepokelewa na Muslim 404.
Ubora wa kusema (Rabbana walakal hamdu hamdan kathiira...) baada ya kuinuka kutoka kwenye Rukuu.
Kutoka kwa Rifaah Bin Raafii Azarqy amesema:
Siku moja tulikuwa tukisali nyuma ya Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake pindi alipo nyanyua Kichwa chake kutoka kwenye Rukuu akasema: (Samia llahu liman Hamidah). Akasema mtu nyuma yake: (Rabbanaa walakal Hamdu Hamdan kathiiran Twayyiban Mubaarakan fiih), alipo maliza Mtume kusali, akasema: "Nani aliye sema maneno hayo" Akasema: "mimi", Akasema: "Nimewaona Malaika thelethani na zaidi wakipupia maneno hayo ni yupi wa mwanzo atayaandika".
Ameipokea Bukhari (799).
MALIPO YA SALA YA PAMOJA.
kutoka kwa bin Omar -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-
"Swala ya pamoja ni bora kuliko swala ya mtu mmoja kwa daraja ishirini na saba".
Imepokelewa na Bukhari (645) na Muslim (103)
Na kutoka kwa Abuu huraira-Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-
Imepokelewa na Bukhari (647) na Muslim (103)
MALIPO YA KUSALI KATIKA SAFU YA KWANZA.
Kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Bukhari (615) na Muslim (103)
Na Wito ndio Adhana.
Na kuchagua ni Kupiga kura.
Na kutoka kwa Abuu huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-:
Imepokelewa na Muslim 440.
MALIPO YA SALA NDANI YA MISIKITI MITUKUFU, WA MAKKA NA MADINA.
kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Bukhari (1190) na Muslim (103)
MALIPO YA ATAKAYE JENGA MSIKITI KWA KUTARAJI UJIRA KWA ALLAH MTUKUFU.
kutoka kwa Othmani Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
"Atakaye jenga Msikiti akitafuta Radhi za Allah aliye takasika na kutukuka, Allah atamjengea nyumba ndani ya Pepo"
Imepokelewa na Bukhari (450) na Muslim (103)
MALIPO YA KUTEMBEA KWENDA MSIKITINI KWA AJILI YA SALA.
Na kutoka kwa Abuu Musa -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Watu wenye malipo makubwa katika Sala ni wale wanaotoka mbali kisha wanaotoka mbali zaidi kwa kutembea kwa miguu, na mwenye kusubiri Sala Mpaka aisali pamoja na Imamu ana malipo makubwa kuliko yule anaye Sali kisha akalala".
Imepokelewa na Bukhari (651) na Muslim (103)
"Na katika Sahihi Al-Bukhari pia kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Atakaye kwenda asubuhi msikitini au mchana, Mwenyezi Mungu humuandalia nyumba peponi kila anapotoka asubuhi au jioni"
Imepokelewa na Bukhari (662) na Muslim (103)
Kutoka kwa Ubayi Bin Ka'ab Radhi za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Muslim 663.
Na kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah- Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Zilikuwa nyumba zetu ziko mbali na Msikiti, tukataka kuziuza ili tuwe karibu na Msikiti, Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake akatukataza akasema: "Hakika mnapata nyinyi kwa kila hatua Daraja".
Imepokelewa na Muslim 664.
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-
"Atakaye Shika Udhu nyumbani kwake, kisha akaenda kwenye nyumba miongoni mwa Nyumba za Allah kwa ajili ya kutekeleza Sala ya lazima miongoni mwa Sala alizo lazimisha Allah, itakuwa moja ya hatua zake ikifuta makosa, na Nyingine ikimpandisha Daraja".
Imepokelewa na Muslim 666.
MALIPO YA MWENYE KUFUNGAMANA MOYO WAKE NA MSIKITI.
kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
Imepokelewa na Bukhari (1423) na Muslim (103)
MALIPO YA ATAKAYE KAA MSIKITINI AKISUBIRI SWALA.
kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Hata achakuwa Mja akiwa ndani ya Sala kwa Muda ambao atakuwa katika pahala pa kusalia kwake akisubiri Sala, Na wakisema Malaika: "Ewe Mwenyezi Mungu msamehe, Ewe Mwenyezi Mungu mhurumie, mpaka atakapo maliza Kusali au atokwe na Udhu".
Imepokelewa na Bukhari (176) na Muslim (103)
MALIPO YA SALA YA HIYARI (SUNNA) NYUMBANI.
Na kutoka kwa Jaabir bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-
"Atakapo maliza Mmoja wenu Kusali Msikitini kwake Basi Aipe nyumba yake sehemu ya Sala Zake, Hakika Allah huweka kheri ndani ya nyumba yake kutokana na Sala zake".
Imepokelewa na Muslim 387.
MALIPO YA KUDUMU NA SALA ZA SUNNA ZINAZO ENDANA NA SWALA ZA FARADHI.
kutoka kwa Umu Habiba Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
"Hakuna Mja Muislamu atasali kwa ajili ya Allah kila siku Rakaa kumi na mbili za kujitolea zisizo kuwa za Lazima, isipokuwa Allah atamjengea Nyumba Peponi, Au isipokuwa atajengewa Nyumba Peponi"
Amesema Ummu Habiba: "Sikuacha kuzisali Rakaa hizo baada ya hapo".
Na amesema Amru: "Sikuacha kuzisali Rakaa hizo baada ya hapo".
Na amesema Nu'maan Mfano wa hayo.
Amepokea Muslimu (728)
MALIPO YA RAKAA MBILI ZA ALFAJIRI.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu-Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema:
"Rakaa mbili za Alfajiri (kabla ya sala ya Faradhi) ni Bora kuliko Dunia na vilivyomo ndani yake".
Na katika mapokezi mengine: "Rakaa hizo mbili zapendeza kwangu mimi kuliko Dunia na vilivyomo"
Imepokelewa na Muslim 725.
MALIPO YA SALA YA WITIRI MWISHO WA USIKU.
Na kutoka kwa Jaabir -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Atakaye hofia kuwa hatosimama usiku basi aswali witiri mwanzo wake, na atakaye tamani kusimama mwisho wa usiku basi aswali mwisho wa usiku, kwani swala za mwisho wa usiku hushuhudiwa, na hilo ni bora"
Imepokelewa na Muslim 755.
MALIPO YA ATAKAYE SIMAMA USIKU NA AKAWAAMSHA WATU WAKE KWA AJILI YA HILO.
Na kutoka kwa Abi Said Alkhudriy na Abi Huraira-Radhi za Allah ziwe juu yao- Wamesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Yetote atakaye amka Usiku na akamuamsha Mke wake, kisha wasali Rakaa mbili kwa pamoja, huandikwa miongoni mwa wanaume wenye kumtaja Allah kwa Wingi, na wanawake wenye kumtaja Allah kwa wingi".
Ameipokea Abuu Daud (1451)
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-
"Allah humhurumia mtu anaye Simama Usiku, kisha akasali, na akamuamsha Mke wake, kisha akasali, kama Mke atakataa kuamka akammwagia maji Usoni mwake, Na Allah humhurumia Mwanamke anaye simama Usiku, kisha akasali, na akamuamsha Mume wake, kisha akasali, kama atakataa akammwagia maji Usoni mwake"
Kaipokea Ahmad na Abuu daud Tirmidhi.
MALIPO YA SALA YA DHUHA.
Na kutoka kwa Abi Dharri Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Kila kiungo cha Mmoja wenu huwa na Sadaka, kila anapo sema (Sub-haana llah) ni Sadaka, na anaposema (Al-hamdulillah) ni Sadaka, na kila anaposema (Laa ilaaha illa llahu) ni Sadaka, na anaposema (Allahu akbaru) ni sadaka, na kuamrisha wema ni Sadaka, na kukataza uovu ni Sadaka, na yote hayo yanatoshelezwa na Rakaa mbili za Dhuha"
Imepokelewa na Muslim 720.
MALIPO YA SWALA YA IJUMAA.
kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Sala tano, na Sala ya Ijumaa Mpaka Ijumaa, ni kifuta madhambi yanayo fanyika baina ya hizo Ijumaa mbili, ikiwa hato fanya madhambi makubwa"
Imepokelewa na Muslim 233.
MALIPO YA KUOGA NA KUTUMIA MANUKATO NA KUNYAMAZA KWA AJILI YA HOTUBA.
Na kutoka kwa Salmani Alfaaris -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Atakaye Koga siku ya Ijumaa, Na akajitwaharisha kwa kiasi awezacho katika twahara, kisha akapakaa mafuta au manukato, kisha akaenda( msikitini) na hakutenganisha baina ya Watu wawili, kisha akasali Sala ya Suna, kisha anapotoka Imamu akanyamaza (kwa ajili ya kuhutubu), Anasamehewa madhambi yaliyopo baina yake na baina ya Ijumaa nyingine".
Ameipokea Bukhari (910).
Na kutoka kwa Abi Huraira Allah amridhie kutoka kwa Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake amesema:
"Atakaye koga, kisha akaiendea Sala ya Ijumaa, kisha akasali alicho wezeshwa, kisha akanyamaza mpaka hatibu amalize Hotuba yake, kisha akasali pamoja na Imamu wake, anasamehewa madhambi yaliyoko baina yake na baina ya Ijumaa nyingine, Na ziada ya siku tatu"
Imepokelewa na Muslim 857.
Malipo ya kwenda Mapema kwa ajili ya Sala ya Ijumaa.
kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Bukhari (881) na Muslim (103)
Na kutoka kwa Abuu huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-
"Inapokuwa siku ya Ijumaa, huwa katika kila mlango miongoni mwa milango ya Msikitini Malaika wakiandika mmoja baada ya mwingine, anapo kaa Imamu Malaika hukunja Vitabu vyao, Na wanakuja kusikiliza Ukumbusho, Na mfano wa yule anaye toka mapema ni kama mfano wa anaye toa Sadaka ya Ngamia, Kisha kama yule anaye toa Sadaka ya Ng'ombe, Kisha kama yule anaye toa Sadaka ya Kondoo, Kisha kama yule anaye toa Sadaka ya Kuku, Kisha kama yule anaye toa Sadaka Yai, Kisha anapo toka Imamu wanafunga Vitabu Vyao, Na wanasikiliza Ukumbusho".
Imepokelewa na Bukhari (929) na Muslim (103)
Malipo ya Kuutafuta muda wa Kujibiwa maombi Siku ya Ijumaa.
Na kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Hakika katika siku ya Ijumaa kuna saa ambayo Muislamu haito mpata akimuomba Allah Kheri ndani ya saa hiyo isipokuwa atampatia Ombi lake".
Akasema: Nao ni wakati Mfinyu.
Ameipokea Bukhari (935) Na Muslimu (852) na tamko ni la Muslimu
MALIPO YA LITAKAYE KUWA NENO LAKE LA MWISHO NI (LAA ILAAHA ILLA LLAAH)
Na kutoka kwa Mua'dhi -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Mwenye kuwa mwisho wa maneno yake ni laa ilaaha ila LLah ataingia Peponi".
Ameipokea Abu Daud (1451)
MALIPO YA ATAKAYE SINDIKIZA JENEZA.
kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Atakaye sindikiza Jeneza la Muislamu kwa Imani na kutarajia malipo, Na akawa yupo nalo mpaka likasaliwa na kumalizika kuzikwa kwakwe, Hakika atarudi akiwa na malipo ya sawa na qiratu mbili, kila Qiratu moja ni sawa na Mlima wa Uhudi ,Na atakaye Msalia kisha akarudi kabla ya kuzika, Basi atarudi na malipo ya Qiratu moja"
Imepokelewa na Bukhari (47) na Muslim (103)
Malipo ya atakaye Saliwa na Waislamu Mia Moja Au Arobaini.
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
"Hakuna Maiti yeyote Itasaliwa na watu miongoni mwa Waislamu wanao fikia Mia Moja,Wote wakimuombea msamaha, isipokuwa watakubaliwa kwa msamaha huo"
Imepokelewa na Muslim 947.
Na kutoka kwa Kuraibu kutoka kwa Abdillah Bin Abbas Radhi za Allah ziwe juu yao kuwa yeye alifiwa na Mtoto wake sehemu za Kadiid au Asfan Akasema: Ewe Kuraibu, Angalia kiasi cha watu walio kusanyika kwa ajili yake, akasema: Nikatoka,wakati huo watu wamejikusanya kwa ajili yake, nikamueleza, akasema: "Unasema wapo Arobaini? Akasema: Ndio, akasema: "Mtoeni,Hakika mimi nimemsikia Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake akisema: "Hakuna Mtu yeyote Muislamu atakufa, kisha wakasimama katika Jeneza lake Watu Arobaini, wasio mshirikisha Allah na chochote isipokuwa Allah atawakubalia msamaha wao kwa Maiti huyo"
Imeipokelewa na Muslim 387.
Malipo ya atakaye sema Innaa lilaah Wainnaa Ilaihi Raajiuni.
kutoka kwa Ummu Salamah Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
Akasema: Pindi alipo Fariki Abu Salama, nikasema: Ni yupi Muislamu Bora kuliko Abu Salama? Nyumba ya kwanza kuhamia ilikuwa ni ya Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe Juu yake, kisha mimi nimeisema Nyumba hiyo, kisha Allah akanipa Badala Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake.
Imeipokelewa na Muslim 387.
Malipo kwa atakaye kufa kwa Ugonjwa wa Tauni (Ugongwa wa mlipuko).
kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
"Ugonjwa wa Tauni ni Shahada kwa kila Muislamu"
Imeipokelewa na Bukhari (2830) na Muslim (103)
Kutoka kwa Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: "Nilimuuliza Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake kunako Ugonjwa wa Tauni, akaniambia kuwa Ugonjwa huo ni Adhabu Allah anaituma kwa anaye mtaka, Na hakika Allah ameujalia ni Rehema kwa Waumini wa Kiislamu, na hakuna yeyote atapatwa na Ugonjwa wa Tauni, kisha akafa kwenye Mji wake akiwa ni mwenye Subira mwenye kutarajia Malipo, anatambua kuwa halimpati isipokuwa lile lililo andikiwa na Allah, isipokuwa anakuwa na mfano wa malipo ya Shahidi"
Ameipokea Bukhari (3474).
Malipo ya Mtu atakaye fiwa na watoto wawili au Watatu ambao hawajabalehe.
Kutoka kwa Anas -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Hakuna mtu yeyote miongoni mwa waislamu akafiwa na watoto Watatu ambao hawafikia utu uzima, isipokuwa Allah atamuingiza Peponi kwa Fadhila ya Huruma yake kwa watoto hao".
Ameipokea Bukhari (3296).
Kutoka kwa Abuu Said Radhi za Allah ziwe juu yake: Yakuwa Wanawake walisema kumwambia Mtume Sala na Amani ziwe juu yake: Tupangie nasi siku (uwe watupa Mawaidha) Basi akawatolea Mawaidha, Akasema: "Mwanamke yeyote atakaye fiwa na Watoto watatu, watakuwa ni kizuizi cha Moto" akasema Mwanamke mmoja: Na Wawili? Akasema Mtume: "Na wawili".
Imepokelewa na Bukhari (1249) na Muslim (103)
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe Juu yake kutoka kwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake Amesema:
"Hatofiwa yeyote miongoni mwa Waislamu na watoto Watatu kisha iwe ni sababu ya kuingia motoni, isipokuwa huwa kama mfano wa kafara ya kiapo"
Imepokelewa na Bukhari (1251) na Muslim (103)
Malipo ya atakaye fiwa na Kipenzi chake miongoni mwa watu wa Duniani kisha akatarajia Malipo.
kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hana mja wangu muumini toka kwangu malipo yoyote pindi ninapomchukua kipenzi chake katika familia yake duniani kisha akasubiri isipokuwa atapata pepo"
Ameipokea Bukhari (6424).
Na Swafiy: Ni kipenzi anaye pendeka kama, Mtoto na Ndugu wa Kiume na kila anaye pendwa na Mtu.
MALIPO YA SADAKA.
Kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Muslim 387.
Kutoka kwa Anas bin Malik -Radhi za Allah ziwe juu yake alisema:
Alikuwa Abu Twalha Al'answari ni miongoni mwa watu wenye mali nyingi za Mitende, Na ilikuwa Mali inayo mpendeza zaidi ni ile iliyopo katika sehemu ya Bairuhai, Na ilikuwa inaulekea Msikiti, Na alikuwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake akiingia humo na akinywa maji yaliyo mazuri ndani yake.
Amesema Anas: Pindi ilipo teremka Aya hii "Hamto ufikia wema mpaka mtoe mnavyo vipenda" Alisimama Abu Twalha kwenda kwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake akasema: Ewe Mtume wa Allah, Hakika Allah Mtukufu anasema "Hamto ufikia wema mpaka mtoe mnavyo vipenda" Na hakika mali zangu inayo pendeka kwangu ni ile iliyopo Bairuhai, Na hakika nimeitoa Sadaka kwa ajili ya Allah, Na ninatarajia wema wake, na badala yake mbele ya Allah, Basi iweke ewe Mtume wa Allah mali hiyo mahala popote atakapo kuonyesha Allah.
Akasema Mtume wa Allah Sala na Amani ziwe juu yake: "Eeeh Uzuri ulioje, Mali hiyo yenye Faida, Mali hiyo yenye Faida, Na hakika nimesikia ulicho sema, Na hakika Mimi naonelea Mali hii iwe kwa Ndugu wa karibu" Akasema Abuu Twalha: "Nitafanya hivyo ewe Mtume wa Allah", Abuu Twalha akaigawanya kwa ndugu zake wa Karibu na watoto wa Baba zake wadogo.
Ameipokea Bukhari (1461) Na Muslimu (998)
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-
"Atakaye toa sadaka kiasi cha tende kutoka katika chumo zuri (halali), na wala hakubali Mwenyezi Mungu isipokuwa kizuri, basi hakika Mwenyezi Mungu huikubali na huipokea kwa mkono wake wa kulia, kisha anailea kwa ajili ya mfanyaji wake kama anavyolea mmoja wenu ndama wake, mpaka iwe mfano wa jabali".
Imepokelewa na Bukhari (7430) na Muslim (103)
Malipo ya Mtumishi wa Sadaka na Mtunza Hazina wanapo kuwa Waaminifu.
Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema:
"Hakika Mtunza Hazina Muislamu Muaminifu, ambaye anatekeleza-Na huenda alisema mwenye kutoa- Yale aliyo Amrishwa yakiwa kamilifu, kwa moyo mkunjufu, kisha akayatoa kwa ambaye ameamrishwa ampatiye na mmoja wa watoa Sadaka".
Imepokelewa na Bukhari (1438) na Muslim (1023).
Malipo ya Sadaka ya Masikini.
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Dirhamu moja imezishinda Dirhamu Laki moja" Wakasema ewe Mtume wa Allah inakuaje?
Akasema: "Ni Mtu mwenye Dirhamu mbili akachukua moja kisha akaitoa Sadaka, Na kuna Mtu mwenye mali nyingi akachukua katika bidhaa za mali zake ambazo ni Dirhamu laki moja akaitolea Sadaka"
Amepokea Ahmad (8929) Na Annasai (2527)
Na kutoka kwa Abu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Ewe Mtume wa Allah, Ni sadaka ipi iliyo bora? Akasema: "Ni sadaka ya masikini kadiri ya uwezo wake, Na anza kutoa kwa waliochini ya uangalizi wako".
Kaipokea Ahmad (8707) na Abuu daud (1677).
MALIPO YA SADAKA INAYOTOLEWA KWA SIRI.
kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
Imepokelewa na Bukhari (1423) na Muslim (103)
Malipo ya mtu aliye ruzukiwa kujizuilia na kuomba akatosheka na akasubiri na akajihifadhi na hakumuomba yeyote, akiwa na imani na Allah na akitegemea kwake.
kutoka kwa Abdallah bin Amri Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema:
Imepokelewa na Muslim 1054.
Kutoka kwa Abu Said Al-khudriy Radhi za Allah ziwe juu yake: Kuna watu miongoni mwa Answari walimuomba Mtume wa Allah Sala na amani ziwe Juu yake, akawapa, kisha wakamuomba, akawapa, kisha wakamuomba, akawapa mpaka kikamalizika kile alicho kuwa nacho, kisha akasema: "Hakuna chochote nitakacho kuwanacho nikakizuia kuto wapeni, Na atakaye jizuilia kuto omba basi Allah atamsitiri (kwa hilo), Na mwenye kuridhika Allah atamtosheleza, Na atakaye vuta subira Allah Atampa Subira, Na hakuna yeyote aliye pewa kipawa bora na kipana kama Subira"
Imepokelewa na Bukhari (1469) na Muslim (103)
Malipo ya atakaye lisha chakula kwa kutafuta Radhi za Allah Mtukufu.
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Hakika Allah Mtukufu atasema siku ya kiyama: "Ewe mwanadamu niliugua na hukunitembelea", Atasema: "Ewe Mola wangu vipi nikutembelee na wewe ndiye Mola wa viumbe?".
Atasema: "Hivi hukutambua mja wangu fulani aliugua na hukumtembelea, hivi hukutambua kuwa wewe ungemtembelea ungenikuta kwake?,
Ewe mwanadamu nilihitaji unilishe na hukunilisha", Atasema: "Ewe Mola wangu vipi nikulishe na wewe ni Mola wa viumbe?"
Atasema: "Hivi hukutambua kuwa mja wangu fulani alihitajia chakula kutoka kwako na hukumlishiza?, Hivi hukutambua kama ungemlishiza ungelipata hilo kwangu?,
Ewe mwanadamu nilihitaji unipe maji, na hukunipatia maji", Atasema: "Ewe Mola wangu vipi nikupe maji na wewe ni Mola wa viumbe?"
Atasema: "Alikuhitajia maji mja wangu fulani na hukumpatia Maji, Hivi hukutambua kama ungempatia maji ungeli yakuta maji hayo kwangu".
Imepokelewa na Muslim: 2569.
Malipo ya atakaye mnywesha mtu maji au mnyama.
Na kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema kuwa:
"Kuna mtu alimuona mbwa akila udongo kwa sababu ya kiu, akachukua kiatu chake, akawa akimchotea mbwa yule vibaba vya maji mpaka akakata kiu, Allah akamshukuru mtu yule, kisha akamuingiza Peponi".
Ameipokea Bukhari (173).
Na kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Hakika mwanamke malaya siku moja aliona mbwa wakati wa joto kali akizunguka kisimani ulimi wake ukiwa umetoka nje kwa sababu ya kiu, akamvulia kiatu chake, akamnywesha, akasamehewa kwa sababu ya kitendo hicho".
Imepokelewa na Muslim 2245.
Malipo ya atakaye panda mmea au akapandikiza chochote.
Kutoka kwa Anas bin Malik Allah amridhie amesema: Amesema Mtume wa Allah Sala na amani ziwe juu yake:
"Hakuna Muislamu yeyote atakaye panda mbegu, au akapanda mmea, kisha wakala katika na mmea ule ndege au binadamu au mnyama, isipokuwa itakuwa ni sadaka kwakwe".
Imepokelewa na Bukhari (2320) na Muslim (103)
Na kutoka kwa Jaabir -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Hakuna muislamu atapandikiza mbebu yoyote isipokuwa itakuwa kila kinacho liwa kutokana na mmea ule ni sadaka, Na kitakacho ibiwa kwake ni sadaka, Na kitakacho liwa na mnyama kutokana na mmea wake basi kwake ni sadaka, Na alicho kula ndege kwake ni sadaka, Na hakuna yeyote atapunguza isipokuwa kwakwe ni sadaka"
Imepokelewa na Muslim 1552.
Malipo ya kutoa katika sehemu za kheri.
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume -Sala na amani ziwe juu yake- Amesema:
Imepokelewa na Bukhari (1442) na Muslim (103)
Na kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Bukhari (5352) na Muslim (103)
Malipo ya atakaye mfanyia wepesi mwenye Uzito au akamsaidia au akamtatulia tatizo lake.
Na kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Kulikuwa na mfanya biashara akiwadai watu, akimuona ana hali ngumu, huwaambia vijana wake: Msameheni, huenda Allah akatusamehe nasi, basi Allah akamsamehe".
Imepokelewa na Bukhari (2078) na Muslim (103)
Na kutoka kwa Abdillah bin Qatadah: Yakuwa Abu Qatadah alimtafuta mdeni wake, akajificha kisha akampata, akasema: Hakika mimi nina hali ngumu, akasema: "Unamuapa Allah?" Akasema: Namuapia Allah, Akasema: Hakika mimi nimemsikia Mtume wa Allah Sala na amani ziwe juu yake akisema: "Atakaye furahishwa Allah amkinge na shida za siku ya Kiyama, Basi na amsamehe mwenye hali ngumu, au amuondolee deni".
Imepokelewa na Muslim 1563.
Na kutoka kwa Abuu huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake -
Imepokelewa na Muslim 2699.
Kutoka kwa Abul yasiir Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
"Atakaye mfanyia subira mwenye hali ngumu au akamfutia deni lake, Allah atamkinga kwenye kivuli chake".
Imepokelewa na Muslim 3006.
Malipo ya Funga.
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Amesema Allah aliye takasika na kutukuka": "Kila matendo ya mwanadamu ni yake isipokuwa funga, Hakika hiyo ni yangu na mimi ndio mwenye kuilipa, anaacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili yangu", Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammadi ipo mikononi mwake, Hakika harufu ya mdomo wa mfungaji inapendeza mbele ya Allah siku ya kiyama kuliko harufu ya Miski, Na mfungaji anafuraha mbili anazozifurahia; Anapo fungua anafurahi kwa kufungua kwake, na anapo kutana na Mola wake anafurahi kwa swaumu yake".
Imepokelewa na Bukhari (1904) na Muslim (103)
Na kutoka kwa Sahli Radhi za Allah ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Bukhari (1896) na Muslim (103)
Malipo ya Atakaye funga Ramadhani kwa Imani na kutarajia Malipo.
Na kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Bukhari (37) na Muslim (759)
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-
"Inapoingia Ramadhani hufunguliwa milango ya Pepo na hufungwa milango ya moto, na mashetani hufungwa minyororo".
Ameipokea Bukhari (3277) Na Muslimu (1079) na tamko ni la Muslimu.
Malipo ya Atakaye simama Ramadhani kwa Imani na kutarajia malipo.
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Atakaye simama Ramadhani kwa imani na kwa kutaraji malipo, atasamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake".
Imepokelewa na Bukhari (37) na Muslim (103)
Malipo ya Atakaye simama usiku wa cheo kwa Imani na kutarajia malipo.
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake:
Imepokelewa na Bukhari (1901) na Muslim760)
Malipo ya kula daku.
Kutoka kwa Anas bin Malik Allah amridhie amesema: Amesema Mtume wa Allah Sala na amani ziwe juu yake:
Imepokelewa na Bukhari (1923) na Muslim (1095)
Malipo ya kuharakisha kufungua.
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Bukhari (1957) na Muslim (1057).
Malipo ya atakaye funga Ramadhani kisha akafuatisha siku sita za Shawwal.
Kutoka kwa Abuu Ayub Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Atakaye funga Ramadhani kisha akafuatisha siku sita za Shawal atakuwa kama aliye funga Mwaka mzima".
Imepokelewa na Muslim 1164.
Malipo ya Atakaye funga siku ya Arafah.
Kutoka kwa Abu Katadah Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliulizwa Mtume Sala na amani ziwe juu yake kunako funga ya Arafa? Akasema: "Inafuta madhambi ya Mwaka ulio pita na uliopo".
Imepokelewa na Muslim 1162.
Malipo ya Atakaye funga siku ya Ashuraa.
Kutoka kwa Abu Katadah Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliulizwa Mtume -Sala na amani ziwe juu yake- kunako funga ya Ashuraa? Akasema: "Inafuta madhambi ya Mwaka ulio pita".
Imepokelewa na Muslim 1162.
Malipo ya funga ya mwezi wa Allah Mtukufu wa Muharram.
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Funga bora baada ya Ramadhani ni mwezi wa Allah Mtukufu wa Muharram".
Imepokelewa na Muslim 1163.
Malipo ya funga ya mwezi wa Shabani.
Kutoka kwa Osama bin Zaid Radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Allah, sijakuona ukifunga katika mwezi miongoni mwa miezi zaidi kuliko unavyo funga mwezi wa Shabani?.
Akasema:"Huo ni mwezi watu wengi wameghafilika ndani yake, uko baina ya Rajabu na Ramadhani, nao ni mwezi ndani yake matendo hupandishwa kwa Mola wa viumbe, Basi napenda matendo yangu yapandishwe na mimi nikiwa nimefunga".
Kaipokea Nasaai (2357).
Malipo ya atakaye funga siku tatu kila mwezi.
kutoka kwa Abdillah bin Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-
"Funga siku tatu kila mwezi, huko ndiko kufunga mwaka mzima, au ni kama kufunga mwaka mzima".
Imepokelewa na Bukhari (3419) na Muslim115959)
Na katika riwaya nyingine ya Bukhari na Muslim:
"Hakika yakutosha ufunge siku tatu kila mwezi, hakika kwa kila Jema moja ni mema kumi mfano wake, na huko ndiko kufunga mwaka mzima".
Imepokelewa na Bukhari (6134) na Muslim(1159)
Na kutoka kwa Abu Katadah -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-
"Kufunga siku tatu kila mwezi, na kufunga Ramadhani mpaka Ramadhani nyingine, ni kufunga mwaka mzima"
Imepokelewa na Muslim 1162.
Malipo ya funga ya siku ya Juma tatu.
Kutoka kwa Abu Katadah Al-Answari Radhi za Allah ziwe juu yake Yakuwa Mtume wa Allah Sala na amani ziwe juu yake Aliulizwa kunako funga ya siku ya Juma tatu? Akasema: "Ndio siku niliyo zaliwa, na ndiyo siku niliyo pewa Utume au niliyo teremshiwa ufunuo".
Imepokelewa na Muslim 1162.
Malipo ya kufunga siku moja na kufungua siku moja.
Kutoka kwa Abdillah bin Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume wa Mwenyezi Mungu-Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-
"Funga inayo pendeza kwa Allah ni funga ya Nabii Daudi, alikuwa akifunga siku moja na anafungua siku moja".
Imepokelewa na Bukhari (3420) na Muslim (1159)
Malipo ya Hijjah na Umra.
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
"Mwenye kuhiji na akawa hakusema maneno machafu wala kutenda matendo machafu, anarudi kama alivyo zaliwa na mama yake (akiwa hana dhambi).
Imepokelewa na Bukhari (1521) na Muslim (1350)
Kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Kwenda Umra mpaka Umra nyingine ni kusamehewa kwa madhambi yanayo fanyika baina ya Umra hizo mbili, na Hija yenye kukubalika haina malipo isipokuwa ni Pepo".
Imepokelewa na Bukhari (1773) na Muslim (1349).
Malipo ya Umra ndani ya Mwezi wa Ramadhani.
Kutoka kwa bin Abbas Radhi za Allah ziwe juu yao kuwa Mtume Sala na amani ziwe juu yake, Alisema kumwambia mwanamke miongoni mwa Answari, anaitwa Mama Sinan: "Kitu gani kilikuzuia kuto hiji pamoja na sisi?" Akasema: "Wanyama wawili wanao mwagilizia walikuwa kwa baba fulani- Mume wake- alihiji yeye na kijana wake kwa kutumia mnyama mmoja kati yao, na alikuwa mnyama mwingine kijana wetu akimtumia kumwagilizia. Akasema: Kufanya ibada ya Umra ndani ya mwezi wa Ramadhani ni sawa kulipa Hija au kuhiji pamoja na mimi".
Imepokelewa na Bukhari (1782) na Muslim (1256).
Malipo ya matendo ndani ya siku kumi za Dhul Hija.
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu-Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema:
"Hakuna matendo bora zaidi kuliko yanayo fanyika ndani ya siku hizi, (za Dhul Hija)" Wakasema: Hata Jihad? akasema: "Hata Jihad, isipokuwa mtu aliye toka akihatarisha nafsi yake na mali zake, kisha asirudi na chochote".
Ameipokea Bukhari (969).
Malipo ya kuishi mji wa Madinah.
Kutoka kwa Saa'd Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Madina ndio bora kwao laiti wangelijua, hatou acha yeyote hali ya kuuhitajia Mji wa Madina isipokuwa Allah atambadilishia ndani ya mji wa Madina kilicho bora zaidi kuliko alicho kiomba, na hata thibiti yeyote kwa kushikilia bendera ya Mji wa Madina na hakupigania kwa Ajili ya Mji wa Madina Isipokuwa nitakuwa muombezi wake au shahidi wake siku ya Kiyama".
Imepokelewa na Muslim 1363.
Malipo ya kujifunza Qur'ani na Kuisoma.
Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
Ameipokea Bukhari (5020) na Muslim (797).
Na kutoka kwa Abuu huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-.
Imepokelewa na Muslim 802.
Na kutoka kwa Ukbah bin Amiri Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Alikuja Mtume wa Allah Sala na amani ziwe juu yake na sisi tukiwa ndani ya Msikiti kisha akasema: "Yupi miomgoni mwenu anapenda atoke nyakati za asubuhi kila siku aende Jangwani au Aqiiq (Soko), alete kutoka huko Ngamia wawili walio nona bila ya tatizo, wala kukata udugu?" Tukasema: Ewe Mtume wa Allah sisi tunapenda hivyo, akasema: "Bora aende mmoja wenu Msikitini ajifunze, au asome Aya mbili kutoka katika kitabu cha Allah Mtukufu, ni bora kwake yeye kuliko Ngamia wawili, na Aya tatu ni bora kwake kuliko Ngamia watatu, na Aya nne ni bora kwake kuliko Ngamia wanne, na idadi nyingineyo ni bora kuliko Ngamia"
Imepokelewa na Muslim 803.
Na kutoka kwa Othmani Radhi za Allah ziwe juu yake -Kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Ameipokea Bukhari (5027).
Na katika mapokezi yake pia:
"Mbora wenu ni yule aliyejifunza Qur'ani na akaifundisha".
Na kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-
Ameipokea Bukhari (4937) na Muslimu (798) na tamko ni la Muslim.
Na kutoka kwa Abuu Umama Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
"Isomeni Qur'ani, kwani itakuja kuwaombea watu wake (wenye kuisoma) siku ya Kiyama"
Imepokelewa na Muslim 804.
Na kutoka kwa Aamir bin Waathib kuwa Nafii Bin Abdil Harithi alikutana na Omar- sehemu iitwayo -Asfaan, na Omar alikuwa amemuweka kuwa Gavana wa Makka, Akasema: Nani umemuacha kuwa Gavana wa watu wa Makka? Akasema: Bin Abza, Akasema Ibn Abza ndio nani? Akasema: Ni muachwa huru miongoni mwa waachwa huru wetu, Akasema: Umewatawalishia muachwa huru?Akasema: Hakika yeye ni msomaji wa kitabu cha Allah, na hakika yeye ni mjuzi wa elimu ya Mirathi, Akasema Omar: Kwa hakika amesema Mtume wenu Sala na amani ziwe juu yake: "Hakika Allah anawainua watu kwa hiki kitabu, na wengine anawaporomosha".
Imepokelewa na Muslim 817.
Na katika Sahihi Bukhari pia kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Muslim 2699.
Malipo ya kusoma Suratul-faatiha.
Na kutoka kwa bin Abbas- Radhi za Allah ziwe juu yao amesema:
Imepokelewa na Muslim 806.
Malipo ya kusoma Suratul-baqarah.
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Muslim 780.
Na kutoka kwa Abuu Umamah Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika alimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
"Isomeni Suratul-baqarah, hakika kuichukua ni baraka na kuiacha ni majuto na wala wachawi hawaiwezi".
Akasema Muawiyah: Ilinifikia kuwa neno (Al-batwalah): Maana yake ni mchawi.
Imepokelewa na Muslim 804.
Malipo ya kusoma Ayatul Kursiy.
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake alisema:
Mtume wa Allah -sala na amani ziwe juu yake- alinipa jukumu la kuhifadhi zaka za Mwezi wa Ramadhani, mara akanijia mwenye kunijia, akawa anamwaga chakula, nikamkamata, nikasema: Nakupeleka kukushitaki kwa Mtume wa Allah Sala na amani ziwe juu yake, kisha akaelezea mazungumzo, akasema: Utakapo taka kulala soma Ayatul kursiy, haitaacha kuwa ni hifadhi pamoja nawe kutoka kwa Allah, na hato kukaribia shetani mpaka uamke, Mtume akasema sala na amani ziwe juu yake: "Kakwambia kweli naye ni muongo, huyo ni shetani".
Ameipokea Bukhari (3275).
Malipo ya Kusoma Aya za mwisho katika suratul-baqarah.
Na kutoka kwa Abuu Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Aya mbili kutoka mwishoni mwa Suratul-baqarah atakaye zisoma kila usiku zitamtosheleza"
Imepokelewa na Bukhari (5009) na Muslim (1350)
Malipo ya kusoma Suratul-baqarah na Al-Imran.
Kutoka kwa Abuu Umamah Al-bahily Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake anasema:
Imepokelewa na Muslim 804.
Na kutoka kwa Nawwasi bin Samaan -Radhi za Allah ziwe juu yake-Amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake akisema
"Italetwa Qur'ani na watu wake siku ya Kiyama wale ambao walikuwa wakiifanyia kazi, itatangulia Suratul-baqarah na Al-imran" kisha Mtume wa Allah Sala na amani ziwe juu yake akazipigia mifano mitatu sikupata kuisahau baada ya hapo akasema: "Utadhania sura hizo mbili ni kama mawingu mawili au vivuli viwili vyeusi baina yake kuna mashariki, au ni kama mbawa mbili za ndege mwenye kuzitandaza, zikimuombea mwenye kuzisoma".
Imepokelewa na Muslim 805.
Malipo ya kusoma Suratul Kahf.
Kutoka kwa Baraa bin Azib, Amesema: Alikuwa mtu akisoma Suratul Kahf, na Pembezoni mwake kuna Farasi aliye fungwa na kamba mbili, akifunikwa na Mawingu, yakawa yanamsogelea na yakazidi kumsogelea, na Farasi wake akawa anamkimbia, alipoamka alimjia Mtume wa Allah Sala na amani ziwe juu yake akamueleza jambo lile, kisha Mtume akasema: "Ni utulivu ulio teremshwa na Qur'ani".
Imepokelewa na Bukhari (5011) na Muslim (795).
Malipo ya kuhifadhi Aya kumi za mwanzoni katika Suratul Kahf.
Kutoka kwa Abuu Dardai Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume Sala na amani ziwe juu yake Amesema:
Imepokelewa na Muslim 809.
Malipo ya atakaye soma Suratul Ikhilas (Qul huwa llahu Ahad).
Na kutoka kwa Abuu Dardai Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Je anashindwa mmoja wenu kusoma usiku mmoja theluthi ya Qurani?" Wakasema: Ataweza vipi kusoma theluthi ya Qur'ani?Akasema: "Qul huwa llahu Ahad inalingana na theluthi ya Qur'ani"
Imepokelewa na Muslim 811.
Malipo ya kumtaja Allah Mtukufu.
wakasema maswahaba ni kina nani hao mufariduna ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni wale wenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi wanaume na wanawake"
Imepokelewa na Muslim 2676.
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
Anasema Allah: "Mimi niko pamoja na dhana ya mja wangu kwangu, Na mimi nipo naye anapo nitaja, atakapo nitaja kwenye nafsi yake nitamtaja kwenye nafsi yangu, atakapo nitaja kwenye mkusanyiko nitamtaja kwenye mkusanyiko bora kuliko wao, na akijiweka karibu yangu kwa kiasi cha shibri moja nitakuwa karibu yake kwa kiasi cha dhiraa moja, akijiweka karibu yangu kwa kiasi cha dhiraa moja nitakuwa karibu yake kiasi cha baa moja, na akinijia kwa kutembea nitamuendea kwa kukimbia".
Imepokelewa na Bukhari (7405) na Muslim (2675)
Malipo ya vikao vya dhikri (Kumtaja Mwenyezi Mungu).
Kutoka kwa Muawiyah Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume wa Allah Sala na amani ziwe juu yake alitoka kwenda katika kikao cha sahaba wake akasema: "Kipi kilicho wakalisha?" Wakasema: Tumekaa tukimtaja Allah na tukimsifu kwa yale aliyo tuongoza kwenye uislamu na kwa yale aliyo tuneemesha juu yetu", Akasema: "Ninamuapa Allah, je hakuna lililo wakalisha isipokuwa hilo?", Wakasema: Tunamuapa Allah hakuna kilicho tukalisha isipokuwa hicho", Akasema "Hakika mimi sijawaapiza kwa kuwatuhumu, lakini amenijia Jibrili akanieleza kuwa Allah Mtukufu anajifaharisha kwenu nyinyi mbele ya Malaika".
Imepokelewa na Muslim 2701.
Kutoka kwa Abuu Huraira na Abuu Said Al-khudury Radhi za Allah ziwe juu yao, Ya kwamba wao walishuhudia kwa Mtume Sala na amani ziwe juu yake kuwa yeye amesema: "Hawatakaa watu wakimtaja Allah Mtukufu isipokuwa watafunikwa na Malaika, na itawaenea rehema, na utateremka utulivu juu yao, na Allah atawataja kwa wale walioko kwake (Malaika)"
Imepokelewa na Muslim 2700.
Malipo ya neno la Tauhidi (Laa ilaha iIla llahu).
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Allah, ni nani atakayepata furaha ya kupata utetezi wako kuliko watu wote siku ya Kiyama?Akasema: "Hakika nilijua kuwa hakuna yeyote wa mwanzo kuniuliza hadithi hii zaidi yako, kwa kile ninacho kiona kwa pupa yako juu ya hadithi, atakaye pata furaha zaidi kwa utetezi wangu siku ya Kiyama ni yule atakaye sema: (Laa ilaha illa llahu-Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu-) kwa usafi wa nia kutoka nafsini mwake".
Ameipokea Bukhari (6570).
Malipo ya kusema (Laa ilaha illa llahu wah'dahu laa shirika lahu, lahulmulku walahul-hamdu wahuwa alaa kulli shain qadiir) kila siku mara mia moja (100).
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Ameipokea Bukhari (5020) na Muslim (2691)
Malipo ya kusema (Sub-haana llahi wabihamdihi) kwa siku mara mia moja
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Atakaye sema: Sub-haana llaahi wabihamdihi- Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake- kwa siku mara mia moja, atasamehewa makosa yake hata kama yatakuwa mfano wa povu la bahari".
Imepokelewa na Bukhari (6405) na Muslim (2692)
Malipo ya kusema (Sub-hana llahi wabihamdihi, Sub-haana llahil-'adhwimi).
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Bukhari (6406) na Muslim (2694)
Malipo ya kusema (Sub-haana llahi, wal-hamdu lillahi).
Kutoka kwa Abuu Maliki Al-Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
Imepokelewa na Muslim 223.
Malipo ya kusema: (Sub-haana llaah, wal hamdulillaah, wa laa ilaaha illa llaahu wallaahu Akbaru,- Ametakasika Mwenyezi Mungu na kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu na hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu Mkubwa).
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
Imepokelewa na Muslim 2695.
Na kutoka kwa Samura bin Jundub -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-:
Imepokelewa na Muslim 2137.
Malipo ya Tasbihi.
Kutoka kwa Sa'd Radhi za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Muslim (2698).
Malipo ya kusema: (Sub-haana llahi Wabihamdihi, Adada khalqihi, Waridhwaa nafsihi, Wazinata Arshihi, Wamidaada kalimaatihi).
Imepokelewa na Muslim 2726.
Malipo ya kusema: (Laa haula wala Quwwata illaa Billahi) Hakuna hila za kuacha madhambi wala nguvu za kufanya ibada ila ni kwa nguvu za Mwenyezi Mungu.
Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Je nisikujulishe kunako hazina miongoni mwa hazina za peponi?" Nikasema: Nifahamishe, akasema: "Laa haulaa walaa quwwata illaa billahi".
Imepokelewa na Bukhari (7386) na Muslim (2704)
Ubora wa bwana wa isitighfari (yaani dua kubwa ya kuomba msamaha).
Kutoka kwa Shadaad bin Ausi Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Atakaye sema maneno hayo mwanzoni mwa mchana hali ya kuwa na yakini nayo, kisha akafa siku yake hiyo kabla hajafikiwa na jioni, basi atakuwa miongoni mwa watu wa peponi, na atakaye sema mwanzoni mwa usiku wake na hali ya kuwa na yakini nayo, kisha akafa kabla ya asubuhi basi atakuwa miongoni mwa watu wa Peponi".
Ameipokea Bukhari (6306).
Malipo ya kusema: (Audhu bikalimaati llahi tammati min shari maa khalaqa) Ninajikinga kwa maneno ya Allah yaliyo timia kutokana na shari ya alivyo viumba.
Kutoka kwa Khaulah bint Hakim Asulamiyah Radhi za Allah ziwe juu yake amesema; Nimemsikia Mtume wa Allah sala na amani ziwe juu yake anasema: "Atakaye fika Sehemu kisha akasema: (Audhu bikalimaati llahit taammaati min sharri maa Khalaqa) hakita mdhuru kitu, mpaka atakapo ondoka sehemu yake ile".
Amepokea Muslimu (7208).
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake alisema:
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume sala na amani ziwe juu yake kisha akasema: Ewe Mtume wa Allah niliyo yapata kutokana na maumivu ya Nge aliye ning'ata usiku wa kuamkia leo. Akasema: "Bora ungesema wakati wa jioni: (Audhu bikalimaati llahit taammaati min shari maa Khalaqa, kisinge kudhuru kitu)
Imepokelewa na Muslim 2709.
Malipo ya yale yanayo semwa kabla ya kulala.
Kutoka kwa Baraa bin Aazib -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Utakapo taka kulala shika udhu kama udhu unapo taka kusali, kisha lalia ubavu wa kulia, kisha sema: (Allahuma Aslamtu Waj-hi Ilaika, Wafawwadhtu amri ilaika, Waal-jatu dhwahari ilaika, raghabatan warahabatan ilaika, laa maljaa wala manja minka illa ilaika, Allahuma aamantu bikitaabil ladhi anzalta, wanabiyyika lladhi arsalta) kama utakufa katika usiku wako huo, basi utakuwa upo kwenye maumbile, na yafanye hayo maneno ndio maneno yako ya mwisho kuyatamka".
Imepokelewa na Bukhari (247) na Muslim (2710)
Malipo ya yale anayo yafanya yule anaye amka usiku.
Na kutoka kwa Ubada bin Swamit -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema:
"Atakaye amka usiku, kisha akasema: (Laa ilaaha illa llahu wahdahu laa sharika lahu, lahul mulku walahul hamdu wahuwa alaa kulli shaini qadiiri, Al-hamdu lillahi, wasub-haana llahi, walaa ilaaha illa llahu, wallahu Akbaru, walaa haula walaa quwwata illaa billahi), kisha akasema:( Allahummagh-firilii), au akaomba, atajibiwa, na kama atashika udhu kisha akasali itakubaliwa sala yake".
Ameipokea Bukhari (1154).
Neno: Taarra: kwa kuiwekea shada raa; maana yake: ameamka.
Malipo ya Adh-kari zinazo semwa baada ya sala ya faradhi.
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake: kuwa mafakiri miongoni mwa Muhajirina walimuendea Mtume wa Allah sala na amani ziwe juu yake wakasema: wametangulia matajiri kwa daraja za juu, na neema za kudumu. Akasema: "Kwa lipi?" Wakasema: Wanasali kama tunavyo sali, wanafunga kama tunavyo funga, wanatoa sadaka na sisi hatutoi sadaka, wanaacha huru watumwa na sisi hatuachi huru, kisha akasema Mtume sana na amani ziwe juu yake: "Je nisikufundisheni kitu ili muyapate yale yalio kupiteni na muwashinde walio baada yenu, na hato kuwa yeyote ni bora zaidi yenu isipokuwa atakaye fanya mfano wa yale mnayo yafanya?" Wakasema tufundishe ewe Mtume wa Allah, akasema: "Mtasema Sub-haana llahu, Allahu Akbaru, Wal-hamdu lillahi, baada ya kila sala mara thelathini na tatu".
Amesema Abuu Swalehe: Wakarudi Mafakiri miongoni mwa Muhajirina kwa Mtume wa Allah Sala na amani ziwe juu yake, wakasema: Wamewasikia ndugu zetu wenye mali kile tunacho fanya, wakafanya mfao wake. Akasema Mtume wa Allah Sala na amani ziwe juu yake: "Hizo ni Fadhila za Allah humpa amtakaye".
Imepokelewa na Bukhari (843) na Muslim (595).
Kutoka kwa Ka'b bin Ujrah Radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Muslim 596.
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Muslim 597.
Malipo ya Kuomba (Dua).
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Hakika Mwenyezi Mungu -Mtukufu-anasema: mimi niko katika dhana ya mja wangu kwangu, na mimi niko pamoja naye pindi anaponiomba".
Imepokelewa na Muslim 2675.
Malipo ya atakaye muombea ndugu yake pasi na uwepo wake.
Kutoka kwa Abuu Dardai -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Hakuna mja muislamu atamuombea ndugu yake bila ya uwepo wake, isipokuwa Malaika husema; na wewe upate mfano wake".
Imepokelewa na Muslim 2732.
Malipo ya kutaka msamaha (Istighfari).
Kutoka kwa Abuu Dhari Radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume sala na amani ziwe juu yake kwa yale anayo pokea kutoka kwa Allah Mtukufu kuwa yeye amesema:
Imepokelewa na Muslim 2577.
Malipo ya kumtakia rehema Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake:
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Mwenye kunitakia rehema mara moja, basi Allah humtakia rehema mtu huyo mara kumi".
Imepokelewa na Muslim 408.
Malipo ya kuwatendea wema wazazi wawili:
Kutoka kwa bin Masoud Radhi za Allah ziwe juu yake. Mtu mmoja Alimuuliza Mtume sala na amani ziwe juu yake; Ni yapi matendo yaliyo bora? Akasema: "Kusali kwa wakati wake,na kuwafanyia wema wazazi wawili".
Ameipokea Bukhari (7534) na Muslim (140)
Na Abdillahi bin Amru bin Al A'swi -Radhi za Allah ziwe juu yao amesema:
Mtu mmoja alimuendea Mtume sala na amani ziwe juu yake akasema; "Nina kupa kiapo cha utiifu kwa kuhama na kupigana Jihadi, ninatafuta malipo kutoka kwa Allah". Akasema: "Je mmoja kati ya wazazi wako wapo hai?" Akasema: "Ndio, bali wote wapo hai", Akasema: "Je unataka malipo kutoka kwa Allah?" Akasema: "Ndio", Akasema: "Rudi kwa wazazi wako ukaishi nao vizuri".
Imepokelewa na Muslim 2549.
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema:
Imepokelewa na Muslim 2551.
Malipo ya kuunga udugu.
Kutoka kwa Anasi bin Malik Radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema:
Imepokelewa na Bukhari (5986) na Muslim (2557)
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema:
"Hakika Allah aliumba viumbe, mpaka alipo maliza kuviumba, udugu ukasema: "Hii ni sehemu ya mwenye kujikinga kwako (Allah) kutokana na kuukata (Udugu)", Akasema: "Ndio, je unaridhia nimuunge anaye kuunga, na nimkate anaye kukata?" Udugu ukasema: "Ndio ewe Mola wangu", Akasema Allah: "Nimefanya hivyo kwa ajili yako", Akasema Mtume sala na amani ziwe juu yake: "Basi someni mkitaka (kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu): (Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na muwatupe jamaa zenu)".
Imepokelewa na Bukhari (5987) na Muslim (2554).
Imepokelewa na Muslim 2558.
Neno: Al-mallu Kwa kuiwekea Shadda lam: Maana yake ni majivu ya Moto.
Malipo ya kutoa matumizi kwa mke na familia.
Kutoka kwa Abuu Masoud Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Bukhari (55) na Muslim(1002)
Na kutoka kwa mama Salama Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Allah, Je mimi ninamalipo ninapotoa matumizi kwa watoto wa Abuu Salama, na pia ni wanangu? Akasema: "Wape matumizi, utakuwa na malipo kwa kile ulicho kitoa kwa wao".
Imepokelewa na Bukhari (1467) na Muslim (1001)
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-.
Imepokelewa na Muslim 995.
Na kutoka kwa Sa'd Bin Abi Waqaas Allah amridhie kutoka kwa Mtume wa Allah Sala na amani ziwe juu yake amesema:
"Hakika wewe hutatoa matumizi ukitafuta radhi za Allah isipokuwa utapewa malipo yake, hata kile unacho kiweka ndani ya mdomo wa mke wako".
Imepokelewa na Bukhari (56) na Muslim (1628).
Malipo ya mwenye kuwa na mabinti wawili au dada wawili akawafanyia subira na akawatendea wema.
Kutoka kwa mama Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alisema:
Alinijia mwanamke akiwa na mabinti zake wawili, akiwa na haja, akaniomba na hakupata kwangu chochote isipokuwa tende moja, nikampatia, akaichukua kisha akaigawa baina ya mabinti zake wawili, na yeye hakula chochote katika tende ile, kisha akasimama akatoka na watoto wake, kisha Mtume akaingia nikamueleza kisa cha mwanamke yule, kisha akasema Mtume sala na amani ziwe juu yake: "Atakaye pewa mtihani wa chochote kutoka kwa watoto wa kike, akawatendea wema, watakuwa ni kinga ya moto kwake yeye"
Amepokea Bukhari (1418) na Muslim (2629)
Na kutoka kwa mama Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Muslim 2630.
Na kutoka kwa Anasi bin Malik Allah amridhie amesema: Amesema Mtume wa Allah Sala na amani ziwe juu yake:
Imepokelewa na Muslim 2631.
Malipo ya kufanya haraka kuwasaidia masikini na wajane.
Kutoka kwa Abuu Hurairah -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
Ameipokea Bukhari (5353) na Muslim (2982).
Malipo ya kuwalea mayatima.
Kutoka kwa Sahal -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Mimi na mwenye kuwalea mayatima tukakuwa Pepo kama hivi" Na akaashiria kwa kidole chake cha shahada na cha kati, akaviachanisha baina yake kidogo.
Ameipokea Bukhari (5304).
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Mwenye kuwalea mayatima wa karibu yake au wasiokuwa wa karibu yake, mimi na yeye peponi tutakuwa hivi" Akaashiria kwa kidole cha shahada na cha kati.
Imepokelewa na Muslim 2983.
Kauli yake: "Wa karibu yake au wasiokuwa wa karibu yake" anakusudia: Sawa sawa awe ni yatima wa karibu yake, au awe sio wa karibu yake hakuna ukaribu baina yake na yeye.
Malipo ya atakaye mtembelea ndugu yake wa udugu kwa Ajili ya Allah Mtukufu.
Kutoka kwa Abuu Hurairah Radhi za Allah ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mtu mmoja alimtembelea ndugu yake kijiji kingine, Allah akamsubirishia Malaika katika njia yake anayo pita, alipo mfikia, akasema: "Wapi unakwenda?" Akasema: "Nakwenda kwa ndugu yangu katika kijiji hiki", Akasema: "Je, una chochote kwakwe unachotarajia katika neema?" Akasema: "Hapana, isipokuwa ninampenda kwa ajili ya Allah", Akasema: "Mimi ni mjumbe wa Allah kwako, basi Allah kakupenda kama jinsi ulivyo mpenda".
Imepokelewa na Muslim 2567.
Malipo ya atakaye tatua shida za ndugu zake waislamu.
Kutoka kwa Abdillah bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema:
"Muislamu ndugu yake ni muislamu, asimdhulumu na wala asimsaliti, na atakaye kuwa katika shida ya ndugu yake, basi Mwenyezi Mungu naye atakuwa katika shida yake, na atakaye tatua kwa muislamu matatizo, basi naye Mwenyezi Mungu atamtatulia tatizo katika matatizo ya siku ya Kiyama, na atakaye msitiri muislamu, Mwenyezi Mungu naye atamsitiri siku ya kiyama".
Imepokelewa na Bukhari (2442) na Muslim (2580).
Na kutoka kwa Abuu Qatada -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
Imepokelewa na Muslim 1563.
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-:
Imepokelewa na Muslim 2699.
Malipo ya atakaye mtembelea mgonjwa.
Kutoka kwa Thauban -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Atakaye mtembelea mgonjwa hato acha kuwa ndani ya njia inayo mpeleka peponi" Pakasemwa: Ewe Mtume wa Allah nini maana ya njia inayo mpeleka peponi? Akasema: "Kitendo chake".
Imepokelewa na Muslim (2568).
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu atasema siku ya kiyama: "Ewe mwanadamu niliugua wala hukunitembelea!" Atasema: "Ewe Mola, nitakutembelea vipi na wewe ndiye Mola mlezi wa walimwengu?!" Atasema: "Hivi hukujua kuwa mja wangu fulani aliugua na hukumtembelea?!, Hivi hukujua kuwa laiti ungelimtembelea ungenikuta kwake! Ewe mwanadamu nilikulisha na hukunilisha!" Atasema: "Nitakulisha vipi hali yakuwa wewe ni Mola mlezi wa walimwengu?!" Atasema: "Hivi hukujua kuwa mja wangu fulani alikuomba chakula na hukumlisha!, Hivi kwani hukujua kuwa laiti ungelimlisha ungelikuta hilo kwangu!, Ewe mwanadamu nilikuomba maji na hukunipa!" Atasema: "Ewe Mola, nitakunywesha vipi hali yakuwa wewe ndiye Mola mlezi wa walimwengu?!" Atasema: "Alikuomba maji mja wangu fulani wala hukumpa!" Hivi hukujua kuwa laiti ungempa maji ungelikuta hilo kwangu".
Imepokelewa na Muslim 2569.
Malipo ya kusema ukweli.
Kutoka kwa Hakim bin Hizam Allah amridhie, amesema: Amesema Mtume wa Allah -Sala na amani ziwe juu yake-:
"Wenye kuuziana wana hiyari kwa muda ambao watakuwa hawaja achana, kama watakuwa wakweli na wakaweka wazi (wanacho uziana) watabarikiwa katika biashara yao, na kama wataficha na wakasema uongo wataondoshewa baraka ya biashara yao".
Imepokelewa na Bukhari (2079) na Muslim (1532).
Na kutoka kwa Abdallah bin Masoud- Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
Amepokea Bukhari (6094) na Muslim (2607)
Malipo ya kusamehe na Kujishusha.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Muslim (2588).
Malipo ya upole katika mambo yote.
Na imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Imepokelewa na Muslim 2593.
Na katika riwaya yake pia: (2594) "Hakika upole hauwi katika kitu isipokuwa utakipendezesha, na wala hauondolewi katika kitu isipokuwa utakiharibu".
Malipo ya atakaye sitiri aibu ya ndugu yake muislamu.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Muslim 2590.
Malipo ya kusuluhisha baina ya watu.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Kila kiungo kwa watu kina sadaka, kila siku inayochomozewa jua: Ukafanya uadilifu kati ya watu wawili ni sadaka, na ukimsaidia mtu katika mnyama wake ukambeba kumpandisha au ukamnyanyulia mzigo wake ni sadaka, na neno zuri ni sadaka, na kwa kila hatua unayokwenda kuelekea msikitini ni sadaka, na ukiondoa maudhi njiani ni sadaka".
Ameipokea Bukhari na Muslim.
Maneno yake: "kuweka sawa baina ya watu Wawili": Maana yake: Kusuluhisha baina yao kwa uadilifu.
Malipo ya atakaye zuia kuondoka kwa heshima ya Muislamu bila ya yeye kuwepo.
Kutoka kwa Abuu Dardai -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Kaipokea Tirmidhiy na akasema: Hadithi ni Hasan.
Malipo ya kupendana kwa ajili ya Allah Mtukufu.
Akasema Anas: Hatukupata kufurahi kwa chochote kama jinsi tulivyo furahi kwa kauli ya Mtume sala na amani ziwe juu yake- kwamba: "Wewe utakuwa pamoja na unaye mpenda".
Imepokelewa na Bukhari (3688) na Muslim (2639).
Na kutoka kwa Abdillahi bin Mas'ud -Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume sala na amani ziwe juu yake akasema: Ewe Mtume wa Allah, wasemaje kwa mtu atakaye wapenda watu na hakuwahi kukutana nao? Akasema Mtume sala na amani ziwe juu yake: "Kila mtu atakuwa na ampendaye (siku ya Kiyama)".
Imepokelewa na Bukhari (6169) na Muslim (2640)
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hakika Allah atasema siku ya Kiyama: "Wapo wapi wenye kupendana kwa utukufu wangu?, Leo hii ninawakinga kwenye kivuli changu siku hii hakuna kivuli isipokuwa kivuli changu".
Imepokelewa na Muslim (2566).
Malipo ya kusubiri juu ya matatizo hata kama yatakuwa kidogo.
Kutoka kwa Abuu Said Al-khuduriy -Radhi za Allah ziwe juu yake-Hakika Mtume wa Allah Sala na amani ziwe juu yake Amesema: "Atakaye vuta subira Allah atamsubirisha (atamtia nguvu), na hakupewa yeyote kipawa bora na kipana zaidi kuliko subira".
Imepokelewa na Bukhari (1469) na Muslim (1053)
Kutoka kwa Abuu Maliki Al-Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
"Subira ni mwangaza".
Imepokelewa na Muslim 223.
Kutoka kwa Atwaa bin Abi Rabaha amesema: Alisema kuniambia mimi bin Abbas: "Je, nisikuonyeshe mwanamke wa Peponi?" Nikasema: Nionyeshe, akasema: "Ni huyu mwanamke mweusi alikuja kwa Mtume sala na amani ziwe juu yake, akasema: "Hakika mimi ninaanguka kifafa na zinafunuka nguo zangu, niombee kwa Allah", akasema: "Ukitaka kuwa na subira na utakuwa na Pepo, na ukitaka nitamuomba Allah akuponyeshe" Akasema: "Nitasubiri", akasema: "Hakika mimi zinafunuka nguo zangu niombee kwa Allah zisifunuke", Mtume akamuombea. Ameipokea Bukhari (5652) na Muslim (2576).
Na kutoka kwa Abuu Said na Abuu Hurairah Radhi za Allah ziwe juu yao, kutoka kwa Mtume sala na amani ziwe juu yake amesema: "Hakuna kimpatacho muumini miongoni mwa tabu na maumivu na msongo wa mawazo na huzuni na kukosa amani, hata mwiba unao mchoma, isipokuwa Allah anamfutia makosa yake" Ameipokea Bukhari na Muslim na tamko ni lake, Amesema: "Hakuna kimpatacho muumini miongoni mwa tabu na maumivu na ugonjwa na huzuni hata msongo wa mawazo unao mpata isipokuwa husamehewa katika makosa yake".
Neno: "Annaswabu" Maana yake ni tabu, na "Al-wasabu" Maana yake: ni maradhi.
Kutoka kwa Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Allah sala na amani ziwe juu yake: "Hakuna matatizo yoyote yanayo mpata muislamu isipokuwa Allah humsamehe kwa matatizo hayo, hata mwiba unao mchoma" Ameipokea Bukhari na Muslim.
Na katika riwaya ya Muslim: "Muumini hachomwi na mwiba au zaidi yake, isipokuwa Allah huondosha kwa mwiba huo makosa yake".
Na katika mapokezi mengine: "Isipokuwa Allah humpandisha kwa mwiba huo daraja, na humfutia kwa kuchomwa kwake huko makosa yake".
Na katika mapokezi mengine ya Muslim, amesema: Waliingia vijana wa kikuraishi kwa Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake akiwa Mina na wao wakiwa wanacheka, akasema: "Kipi kina kuchekesheni?" Wakasema: "Fulani aliporomoka juu ya paa la nyumba ikakaribia shingo yake au jicho lake kung'oka kwa ajili ya Allah" Akasema: "Msimcheke, hakika mimi nimemsikia Mtume wa Allah -Sala na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakuna muislamu atakaye chomwa na mwiba au zaidi yake isipokuwa Allah atamuandikia kwa mwiba huo daraja, na atafutiwa kwa mwiba huo makosa yake".
Na kutoka kwa Abuu Masoud Radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume sala na amani ziwe juu yake amesema: "Hakuna muislamu atapatwa na maudhi yatokanayo na maradhi na zaidi ya maradhi, isipokuwa Allah atamporomoshea kwa maradhi hayo makosa yake, kama ambavyo mti unaporomosha majani yake" Ameipokea Bukhari na Muslim.
Malipo ya kuugua homa.
Kutoka kwa Jabir bin Abdillahi -Radhi za Allah ziwe juu yao- Hakika Mtume wa Allah -Sala na amani ziwe juu yake- siku moja aliingia kwa mama Saibu au mama Musayib akasema: "Una nini ewe mama Musayibu unahangaika huku na kule?" Akasema: "Nina homa, Allah asiipe baraka ndani yake", Akasema: "Usiitukane homa, hakika homa inaondosha makosa ya wanadamu, kama jinsi kipulizo cha mfua vyuma kinavyo ondosha uchafu wa chuma".
Imepokelewa na Muslim 2575.
Na kutoka kwa Abdillah Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimuendea Mtume -Sala na amani ziwe juu yake- akiwa kwenye maradhi yake, naye akiwa anaugulia maumivu makali mno, nikasema: Hakika wewe unaugulia maumivu makali, nikasema; Hali hiyo ni kwakuwa wewe una malipo mara mbili? Akasema: "Ni kweli, hakuna Muislamu atapatwa na udhia isipokuwa Allah atamfutia kwa udhia huo makosa yake, kama jinsi mti unavyo dondosha majani yake".
Imepokelewa na Bukhari (5647) na Muslim (2571)
Malipo ya atakaye kosa jicho kisha akasubiri.
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake-Amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake akisema:
"Hakika Allah amesema: Ninapo mpa mja wangu mtihani kwa vipenzi vyake viwili (Macho) kisha akafanya subira, nitampa Pepo badala ya macho hayo mawili".
Anakusudia: Macho yake mawili.
Ameipokea Bukhari (5653).
Malipo ya kuondosha udhia njiani.
Na kutoka kwa Abuu Dharri -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Nilionyeshwa matendo ya umma wangu mema yake na maovu yake, nikakuta katika matendo mazuri ya umma wangu ni udhia unaoondoshwa njiani, na nikakuta katika matendo mabaya ya umma wangu ni kohozi linalotemwa msikitini, kisha lisifukiwe".
Imepokelewa na Muslim 553.
Na katika sahihi Bukhari pia kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Bukhari (652) na Muslim (1914)
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-"
"Mtu mmoja alilipita tawi la mti likiwa limeelekea barabarani, akasema: Ninamuapa Allah nitalikwepesha tawi hili kwa ajili ya waislamu lisiwaudhi, kisha akaingizwa Peponi".
Imepokelewa na Muslim 1914.
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema:
"Hakika nilimuona mtu akigeuka geuka Peponi, kwa ajili ya mti alio ukata ukiwa njiani ukiwaudhi watu".
Imepokelewa na Muslim 1914.
Malipo ya atakaye ua nyoka au mjusi kafiri (Mjusi wa majumbani mwenye rangi ya maziwa).
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Atakaye muua mjusi kafiri kwa pigo la mwanzo ataandikiwa mema mia moja (100), na kwa pigo la pili si kama la mwanzo, na la tatu si kama la pili".
Imepokelewa na Muslim 2240.
Malipo ya mfanyabiashara mkweli mwaminifu.
Na kutoka kwa Hakim bin Hizam -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume -Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Wenye kuuziana wana hiyari kwa muda ambao watakuwa hawajaachana, kama watakuwa wakweli na wakaweka wazi watabarikiwa katika kuuziana kwao, na kama wataficha na wakasema ungo wataondoshewa baraka ya kuuziana kwao".
Imepokelewa na Bukhari (2110) na Muslim (1532).
Malipo ya upole katika kuuza na kununua.
Na kutoka kwa Jaabir bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-
Ameipokea Bukhari (2076).
Malipo ya mwenye kuhifadhi tupu yake kwa kumuogopa Allah Mtukufu.
Kutoka kwa Sahal bin Saad Allah amridhie amesema: Amesema Mtume wa Allah -Sala na amani ziwe juu yake-:
Ameipokea Bukhari (6474).
Makusudio ya yaliyo baina ya ndevu zake: "Ni ulimi, na yaliyo baina ya miguu yake: " Ni tupu.
Malipo ya kutubia.
Kutoka kwa Anas bin Malik Allah amridhie amesema: Amesema Mtume wa Allah -Sala na amani ziwe juu yake-:
"Mwenyezi Mungu anapata furaha kubwa kwa toba ya mja wake wakati anapotubia kwake, [furaha kubwa] kuliko furaha ya mmoja wenu aliyekuwa katika kipando chake katika ardhi ya jangwa kikamtoroka huku kikiwa kimebeba chakula chake na maji yake, akakitafuta mpaka akakikatia tamaa, akaenda chini ya mti akajiegemeza katika kivuli chake huku akiwa kakikatia tamaa kipando chake, wakati akiwa katika hali hiyo mara ghafla anakiona kimesimama mbele yake, basi akashika kamba yake na akasema kwa furaha kubwa: Ewe Mwenyezi Mungu hakika wewe ni mja wangu na mimi ni mola wako, kakosea kutokana na furaha kubwa".
Imepokelewa na Muslim 2747.
Malipo ya matendo mema wakati zama zinapoharibika.
Kutoka kwa Ma'qal bin Yasari -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Muslim (2948).
Neno: "Alharaji:" kwa Kuiwekea Sakna Raa, Maana yake ni kuhitilafiana pamoja na fitna.
Malipo ya mafukara na wanyonge waliotenzwa nguvu.
Kutoka kwa Imrani bin Huswein -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Nilichungulia Peponi nikawaona walio wengi ndani yake ni mafukara, na nikachungulia motoni nikawaona walio wengi ndani yake ni wanawake".
Ameipokea Bukhari (3241) na ameipokea Muslim (2737) kutoka kwa bin Abbas Radhi za Allah ziwe juu yao.
Na kutoka kwa Osama Radhi za Allah ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Nilisimama katika mlango wa Pepo, wengi walio ingia ni masikini, na wenye mali wakiwa wamezuiliwa (hawajapewa idhini ya kuingia Peponi) isipokuwa watu wa motoni wamekwisha pewa amri ya kuingia motoni, na nilisimama katika mlango wa moto wengi walio ingia ni wanawake".
Imepokelewa na Bukhari (5196) na Muslim (2736)
Na kutoka kwa Thauban Radhi za Allah ziwe juu yake alisema:
Nilikuwa nimesimama mbele ya Mtume -Sala na amani ziwe juu yake- kisha akamjia msomi miongoni mwa wasomi wa Kiyahudi akasema: "Nimekuja kukuuliza", Akasema Mtume kumwambia: "Je jambo nitakalo kueleza litakuwa na manufaa na wewe?" Akasema: "Ninakusikiliza kwa masikio yangu", kisha Mtume akawa akichoma chini kwa kijiti alicho kuwa nacho, kisha akasema: "Uliza" Yahudi akasema: "Watu watakuwa wapi siku ambayo itabadilishwa Ardhi tofauti na Aridhi hii na Mbingu tofauti na Mbingu hii?"
Kisha akasema Mtume wa Allah -Sala na amani ziwe juu yake-: "Watakuwa kwenye giza kabla ya kuvuka daraja (Swiratu)" Akasema: "Nani wa mwanzo kuvuka daraja?" Akasema: "Ni mafukara wa Muhajirina (Walio hamia Madina kutoka Makka)".
Imepokelewa na Muslim 315.
Kutoka kwa Abuu Abdul Rahmani Alhabliy amesema: Walikuja watu watatu kwa Abdillahi bin Amri bin Aswi, na mimi nikiwa naye, wakasema: Ewe baba Muhammad hakika sisi tunamuapia Allah hatuwezi chochote, si matumizi ya kawaida, wala kipando, wala mali. Akasema kuwaambia: "Ikiwa mtataka kurudi baadae tuwape kile alicho tuwezesha Allah (njooni tutawapatia), na ikiwa mtataka tulipeleke jambo lenu kwa kiongozi tutalipeka, na mkitaka kuweni na subira, hakika mimi nilimsikia Mtume -Sala na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika mafukara wa Muhajirina watawatangulia matajiri siku ya Kiyama kuingia Peponi kwa kipindi cha miaka arobaini" Wakasema: Basi, hakika tutasubiri, hatutaomba chochote.
Imepokelewa na Muslim 2979.
Neno: "Aljadu": Kwa kuiwekea Fat-ha jimu, maana yake ni hadhi na utajiri.
Malipo ya kuwa na dhana njema kwa Allah.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Anasema Allah Mtukufu: Mimi niko na dhana ya mja wangu anavyo nidhania mimi".
Imepokelewa na Bukhari (7405) na Muslim (2675).
Malipo ya kutoa salamu.
Imepokelewa na Muslim (93).
Na kutoka kwa Abdillah bin Salam -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akisema: "Enyi watu, toleaneni salamu na muunge udugu, na mlishe chakula, na msali usiku na watu wakiwa wamelala, mtaingia peponi kwa amani".
Kaipokea Tirmidhiy (2485) na akasema: Hadithi ni Hasan na ni sahihi".
Malipo ya kuwatolea salamu watu wa nyumbani.
Kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliniambia Mtume wa Allah -Sala na amani ziwe juu yake-: "Ewe kijana wangu, utakapo ingia kwa watu wako, watolee salamu, itakuwa ni baraka kwako na kwa watu wa nyumbani kwako".
Malipo ya wenye huruma.
Kutoka kwa Osama bin Zaidi Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Si vinginevyo, Allah huwahurumia katika waja wake wale wenye huruma".
Imepokelewa na Bukhari (1284) na Muslim (1284)
Malipo ya kuomba dua katika wakati wa Kujibiwa.
Kutoka kwa Jabiri Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
"Hakika usiku kuna wakati ambao, hakuna mtu muislamu ataupata wakati huo akimuomba Allah kheri miongoni mwa mambo ya kidunia na akhera, isipokuwa atampatia, na wakati huo hupatikana kila usiku".
Imepokelewa na Muslim 757.
Malipo ya kulingania kwa Allah.
Kutoka kwa Sahal bin Saad Allah amridhie amesema: Amesema Mtume wa Allah -Sala na amani ziwe juu yake-:
Imepokelewa na Bukhari (3009) na Muslim (2406)
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
Imepokelewa na Muslim 2674.
Kutoka kwa Jariri bin Abdillahi -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
"Atakaye anzisha ndani ya Uislamu njia nzuri, ikafanyiwa kazi baada yake ataandikiwa mfano wa malipo ya aliye fanyia kazi, na wala hakipungui chochote kwenye malipo yao, na atakaye anzisha ndani ya Uislamu njia mbaya, ikafanyiwa kazi baada yake, ataandikiwa madhambi mfano wa madhambi ya aliye fanyia kazi, na wala hawapunguziwi chochote kwenye madhambi yao".
Imepokelewa na Muslim (1017).
Malipo ya kufikisha hadithi za Mtume -Sala na amani za Allah ziwe juu yake:
Kutoka kwa bin Mas'udi Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
Kaipokea Tirmidhiy na akasema: Hadithi ni Hasan na ni sahihi".
Kutoka kwa Anas bin Maliki Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Hakika Mwenyezi Mungu huridhika kwa mja anapokula chochote, akamshukuru juu ya hicho, au akanywa chochote akamshukuru juu ya hicho".
Imepokelewa na Muslim (2734).
Related books
All books- NAMNA YA SWALA YA MTUME, REHEMA NA AMANI ZIWE JUU YAKE75 lugha
NAMNA YA SWALA YA MTUME, REHEMA NA AMANI ZIWE JUU YAKE
Mheshimiwa, Sheikh, Abdulaziz bin Baaz - Mwenyezi Mungu amrehemu - ameeleza ndani ya kitabu cha "Namna ya Swala ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake", kwa ufupi namna ya swala ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, kwa mbinu rahisi na njia nzuri kabisa, huku akitegemea ushahidi wa kimaandiko yaliyo sahihi; ili kiwe muongozo kwa Muislamu katika swala yake. Alibainisha ndani yake nguzo za swala na sunna zake na namna yake, kuanzia wudhu mpaka kutoa salamu ya kumaliza swala, akikusanya ndani yake kati ya ushahidi na upambanuzi, akilingania watu kumuiga kikamilifu Mtume, rehema na amani ziwe…
- NJIA ZENYE FAIDA KWA MAISHA YENYE FURAHA55 lugha
NJIA ZENYE FAIDA KWA MAISHA YENYE FURAHA
Kitabu "Njia zenye Faida kwa Maisha yenye Furaha" cha Sheikh, mwanachuoni Abdur-Rahman bin Naasir As-Sa'adiy – Mwenyezi Mungu amrehemu – kinashughulikia sababu zinazopelekea furaha ya kweli kutoka katika mtazamo wa kiimani wa kina, na kinamwongoza msomaji kufikia utulivu wa moyo kupitia imani na matendo mema, kumtaja Mwenyezi Mungu, kuridhika, kutafakari neema zake, kufanya ihsani, kutegemea Mwenyezi Mungu, kuwa na subira, na kuyapima mambo ipasavyo; kwa mtindo mzuri unaoweka mbele yako ramani ya maisha yenye utulivu, yenye uwiano, na yenye furaha licha ya misukosuko ya maisha.
- adhkaari ambazo husemwa Asubuhi na Jioni.57 lugha
adhkaari ambazo husemwa Asubuhi na Jioni.
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu Mwenyezi Mungu hakuna mola isipokuwa Yeye,(na) ndiye Mwenye uhai wa maisha, Msimamia kila jambo, Kusinzia hakumshiki wala kulala. Ni Vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, Na nani huyo awezaye kuombea mbele Yake (Mungu) bila idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, hawalijui lolote katika elimu Yake (Mwenyezi Mungu) isipokuwa kwa alipendalo (Mwenyezi Mungu).Kiti chake cha Enzi kimeenea mbingu na na ardhi, wala kuvilinda hivyo hakumshindi, na Yeye (peke yake) ndiye aliye juu na ndiye aliye Mkuu" Ayatul…
- Mtume wa Uislamu, Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake65 lugha
Mtume wa Uislamu, Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake
Kitabu "Mtume wa Uislamuz Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake" kinaweka wazi maisha ya Nabii Muhammad kuanzia kwenye nasaba yake na kuoa kwake kulikobarikiwa mpaka kuanza kuteremka kwa ufunuo na kuanza kwa utume wake ambao ndio wa mwisho, na kinabainisha alama za unabii wake na alama za ukweli wake, na kinaweka wazi sheria aliyokuja nayo na nafasi yake katika kuhifadhi haki za mwanadamu na heshima yake, kama ambavyo kinaweka wazi misimamo ya mahasimu wake na kutoa kwao ushahidi wa kumuunga mkono, pamoja na kutia mwangaza juu ya tabia zake nzuri ambazo sheria imeziweka kuwa ni kiigizo kwa…