صفة الوضوء والصلاة (مرئي)

صفة الوضوء والصلاة (مرئي)

PROJ-187

Language: lang_sw
Prepared by:
Version: 1.0
Translations 42
Akan Amharic Assamese Bengali +38
Attachments 7
PDF
Audio
Video
+3

vipi ninatawadha?

M

Sauti

1

Sauti ya adhana

2

{Enyi mlioamini pindi mtakaposimama kutaka kusali, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka katika viwiko na futeni vichwa vyenu (na muoshe) miguu yenu mpaka katika fundo mbili}

[Suratul Maidah: 6]

3

Hakuna swala bila udhu, wala hakuna udhu bila nia, na wala hakuna nia bila utakasifu wa nia (ikhlaswi),mahala pake ni moyoni, si ulimi.

4

Bismillaah (kwa jina la Mwenyezi Mungu)

Ni sheria kusema Bismillaahi mwanzoni mwa udhu. kwa neno hilo ndio tunaanza udhu wetu. kisha tunatumia mswaki kusafisha kinywa kama itawezekana

5

Tunaosha viganja viwili mara tatu, tunaanzia katika ncha za vidole mpaka katika maungio ya kiganja.

6

Tunaosha viganja viwili mpaka maungio ya kiganja cha mkono mara tatu mfululizo

7

Na inakuwa kwa kuanza na kiganja cha kulia, tunakiosha mara tatu, kitafuatiwa na kiganja cha kushoto mara tatu.

8

kama inavyofaa kuosha kiganja cha kulia kisha cha kushoto kisha cha kulia kisha cha kushoto. na kuendelea.

9

Pamoja na kuhakikisha kuingiza maji kati ya vidole vyetu.

10

kisha tunahamia katika kusukutua na kupandisha maji puani.

11

Kusukutua kunakuwa kwa kuweka maji mdomoni, na kuyatikisa ndani yake, kisha kuyabana na kuyatema.

12

Ama kupandisha maji puani kunakuwa kwa kuvuta maji puani kupitia pumzi, kisha kuyatoa kwa mkono wa kushoto kwa kuyapenga

13

Na ni katika sunna kuzidisha zaidi katika vitendo hivyo viwili tutakapokuwa hatuna swaumu au kuhofia madhara.

14

Na kusukutua na kupandisha maji puani kuna njia mbili:

15

Kuunganisha; na inakuwa kwa kuchukua mchoto mmoja wa maji, tunasukutua nusu yake, kisha tunapandisha puani nusu yake nyingine

Tunatikisa maji mdomoni kisha tunayatema, kisha tunayapenga maji yale tuliyoyapandisha puani kwa mkono wetu wa kushoto.

Tunafanya hivyo mara tatu, kwa michoto mitatu ya maji.

16

Ama kutenganisha inakuwa kwa kutenga maji kwaajili ya kusukutua mchoto wake maalumu, na kupandisha maji puani mchoto mwingine, tunachukua mchoto wa maji na tunauweka wote mdomoni, kisha tunayatikisa, kisha tunayatema, kisha tunachukua mchoto wa pili na tunaupandisha puani, kisha tunapenga kwa mkono wa kushoto.

17

Kinachofuata kusukutua na kupandisha maji puani: ni kuosha uso.

18

Na ukomo wa uso kiurefu ni: kuanzia katika maoteo ya nywele za kichwa yanayofahamika mpaka mwisho wa kidevu, na kiupana ni kati ya masikio mawili

19

Pamoja na ulazima wa kuosha nywele zote katika uso, kama nywele za ndevu nyepesi, na masharubu, na sharafa (nywele za mashavuni) na nyusi, na zilizoko karibu na kidevu (nazo ni nywele zinazoota chini ya mdomo wa chini).

20

Na katika kuosha uso kuna njia mbili:

21

Ya kwanza: tunachukua maji kwa mikono miwili yote, kisha tunaosha uso kwa maji hayo kuanzia katika maoteo ya nywele za kichwa zinazofahamika mpaka kinapoishia kidevu, na kuanzia katika sikio la kulia mpaka katika sikio la kushoto, na ikiwa ndevu ni nyingi ni sunna kuingiza maji chini ya kidevu na tunaziachanisha ndevu.

Tutalifanya hilo mara tatu na ndio ukamilifu, au mara mbili, au mara moja ambayo ndio wajibu.

22

Ya pili: Tunachukua maji kwa mkono wa kulia tu, kisha tunayaweka usoni, na tunaosha uso kwa mikono yote miwili kwa pamoja kama ilivyo katika namna iliyotangulia. tunafanya hivyo mara tatu.

23

Kufuata mpangilio katika viungo vya udhu vya wajibu, na kufuatanisha kati yake ni wajibu vilevile, kiasi ambacho tusitangulize kiungo sehemu ya kiungo kingine, na wala tusichelewe kuhama kutoka kiungo kwenda katika kiungo kinachofuatia.

24

Baada ya kumaliza kuosha uso, tunahamia katika kuosha mikono miwili.

25

Na kikomo cha mikono miwili ambacho ni cha wajibu kukiosha: Ni kuanzia katika ncha za vidole mpaka katika viwiko, pamoja na kuviosha viwiko viwili.

26

Tunaanza kuosha mkono wa kulia kuanzia katika ncha za vidole vya kiganja, na tunavichambua vidole kwa kuvishikamanisha kati ya viganja viwili, kisha tunayafikisha maji katika viwiko

27

Kisha tunahamia katika mkono wa kushoto na tunauosha pia kuanzia katika vidole vya kiganja pamoja na kuvichambua mpaka katika kiwiko

28

Tunahamia katika kupaka kichwa. Tunalowanisha mikono miwili kwa maji mapya, kisha tutaweka mikono miwili hii iliyolowana mwanzo wa kichwa na tunakwenda nayo mpaka kisogoni, kisha tunairudisha mpaka sehemu tulipoanzia. Na hakuna tofauti katika kiwango cha kichwa kati ya mtu mwenye kipara na mwenye nywele.

29

Kisha tunapaka masikio mawili kwa maji yaliyobakia, yale tuliyofutia kichwa, tunafanya hivyo mara moja.

30

Na namna ya kupaka masikio mawili ni kuingiza kidole cha shahada katika tundu za masikio mawili tunayafuta, na tunafuta kwa kidole gumba juu ya masikio mawili, hapo tanakuwa tayari tumeyafuta masikio ndani na nje.

31

Kisha tunahamia katika kuosha miguu miwili, na kiwango cha miguu miwili cha wajibu kukiosha ni: kuanzia katika ncha za vidole vya mguu mpaka katika fundo mbili, hivyo kuosha mwisho wa miguu miwili ni wajibu.

32

Tunaanza na mguu wa kulia, na tunaachanisha kati ya vidole vya mguu. Na tutazingatia kuosha nyuma ya miguu, na juu ya visigino viwili.

33

Tutaosha mguu wa kushoto kama tulivyoosha mguu wa kulia, wala tusisahau kuachanisha vidole vyake, na kuhakikisha kuosha mwisho kikamilifu na maji kufika katika fundo mbili.

34

Nina shuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika, na nina shuhudia kuwa Muhammad ni mja wake na nimtume wake.

35

Ni sunna baada ya kumaliza kutawadha kumtaja Mwenyezi Mungu na kuomba dua, na ni sunna kwa mtu kuzidisha akasema:-

36

Allaahummaj'alniy minat tawwaabiina waj'alniy minal mutatwahhiriina (Ewe Mola wangu nijaalie mimi kuwa miongoni mwa wenye kutubia, na unijaalie kuwa miongoni mwa wenye kujitwaharisha).

37

Au:

Sub-haanakallaahumma (Umetakasika ewe Mwenyezi Mungu) wabihamdika (Na sifa njema ni zako) Ash-hadu an laa ilaaha illaa anta (ninashuhudia kuwa hapana Mola ila wewe), Astaghfiruka wa atuubu ilaika (ninakuomba msamaha na ninatubia kwako).

M

Kilichoandikwa katika kioo (Screen)

1

Ni vipi ninatawadha?

2

{Enyi mlioamini pindi mtakaposimama kutaka kusali, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka katika vifundo na pakeni maji vichwa vyenu (na muoshe) miguu yenu mpaka katika fundo mbili}

[Suratul Maidah: Aya ya 6]

3

kuosha viganja viwili

4

Kusukutua na kupandisha maji puani

5

Kuunganisha

6

Kutenganisha

7

Kuosha uso

8

Ya kwanza

9

Ya pili

10

Ni kunuia na kusema Bismillaah

11

kuosha viganja viwili

12

Kusukutua

13

Kupandisha maji puani

14

Kuosha uso

15

Kuosha mikono miwili pamoja na fundo mbili.

16

Kupaka maji juu ya kichwa na kufuta masikio mawili

17

Kuosha miguu miwili pamoja na fundo mbili

18

Kuosha mikono miwili

19

Kufuta kichwa

20

Mwanzao wa kichwa = Ni pale linapojikunjia paji la uso na mwanzo wa maoteo ya nywele yaliyozoeleka.

21

Mwisho wa kichwa = Ni mwisho wa maoteo ya nywele katika kisogo

22

Kupaka masikio mawili

23

Kuosha miguu miwili

24

Amesema Mtume rehema zamwenyezi munguzie juu yake amani:

"Ole wao (wasiofikisha maji katika) visigino (watakua na adhabu ya) moto, enezeni maji ya udhu".

Imepokelewa na Abuu Daud

25

"Nina shuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika, na nina shuhudia kuwa Muhamad ni mja wake na nimtume wake".

Imepokelewa na Imamu Muslim

26

"Allaahummaj'alniy minat tawwaabiina waj'alniy minal mutatwahhiriina (Ewe Mola wangu nifanye mimi kuwa miongoni mwa wenye kutubia, na unifanya kuwa miongoni mwa wenye kujitwaharisha)".

Kaipokea Imamu Tirmidhiy

27

Sub-haanakallaahumma (Umetakasika ewe Mwenyezi Mungu) wabihamdika (Na sifa njema ni zako) Ash-hadu an laa ilaaha illaa anta (ninashuhudia kuwa hapana Mola ila wewe), Astaghfiruka wa atuubu ilaika (ninakuomba msamaha na ninatubia kwako).

Kaipokea Imamu Nasaai katika (Mlango wa: kazi za usiku na mchana).

Nina swali vipi?

Swala ni kuanzia katika takbira (yaani neno Allaahu Akkbar) mpaka salamu.

m

Sauti

1

sauti ya kukimu swala.

2

Sauti ya kukimu inaendelea.

Kuileta nia ndio kitu cha kwanza anachokifanya mwenye kuswali, na mahala pake ni moyoni

3

Tunaelekea kibla, na utakapokuwa imamu au peke yako basi weka mbele yako sitra (kizuizi).

4

Mwenyezi Mungu ni mkubwa (Allahu Akbar)

Tamko la kuanza swala (Takbiratul ihramu) na kwa tamko hili tunaingia ndani ya swala, na ni lazima kulitamka kwa ulimi.

5

Na wakati wa tamko hili (takbira) tunanyanyua mikono yetu mpaka usawa wa mabega mawili, na tunaelekea kwa matumbo ya vidole vyetu usawa wa kibla.

Au:

Tunainyanyua usawa wa masikio kwa njia hiyo hiyo.

6

Tutaweka mikono miwili baada ya takbira juu ya kifua, au chini ya kifua juu ya kitovu, au chini ya kitovu, yote hiyo iko sawa.

Mkono wetu wa kulia tutauweka juu ya kiganja cha mkono wa kushoto

Au tutashika kwa kiganja cha kulia juu ya kiganja cha mkono wa kushoto

Au tutashika kwa mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto

7

Allaahuma baaid bainiy wabaina khatwaayaaya (Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali kati yangu na kati ya makosa yangu) kamaa baa'atta bainal mashriqi wal maghribi (kama ulivyoweka mbali kati ya mashariki na magharibi, Allaahu naqqiniy min khatwaayaaya (Ewe Mwenyezi Mungu nisafishe kutokana na makosa yangu) kamaa yunaqqath-thaubul abyadh minaddanasi (kama inavyosafishwa nguo nyeupe kutokana na uchafu) Allaahummaghsilniy min khatwaayaaya bith-thalji wal maai wal baradi (Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi kutokana na madhambi kwa barafu na maji na baridi".

Tutaomba kwa dua ya ufunguzi wa swala baada ya takbira ya kuanza swala na kabla ya kusoma, na zimenukulia dua zingine za kufungulia swala, na katika sunna ni kubadili badili aina kati ya dua hizo.

8

Ninajikinga kwa Allah kutokana na shetani aliye laaniwa

Kinachofuata baada ya dua ya ufunguzi ni kuomba kinga, yaani kusema neno lililotangulia hapo juu, kisha kusoma suratul faaiha.

9

kwa unyenyekevu na utulivu, tunasoma aya moja moja.

10

(Aamin) Ewe mwenyezi mungu tukubakie dua.

Kulisema neno hilo ni sunna kwa mwenye kuswali sawa sawa awe imamu au maamuma au peke yake, nalo siyo aya katika suratul faatiha, bali ni dua inamaanisha: Ewe Mwenyezi Mungu pokea dua.

11

Tutasoma baada ya suratul faatiha kile kitakachokuwa chepesi katika Qur'ani, ima iwe ni sura kamili, au sehemu yake, na baada ya kumaliza kusoma tutanyamaza kidogo kabla hatujahamia katika rukuu.

12

(Allaahu Akbar) Mwenyezi Mungu ni mkubwa.

Tutatoa takbira ya kuhama kutoka katika kisimamo kwenda katika rukuu.

Na hii ndiyo sehemu ya pili katika swala ambayo alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake akinyanyua mikono yake; hivyo ni sunna tunyanyue mikono yetu usawa wa mabega mawili au masikio mawili.

13

Tutaweka viganja viwili juu ya magoti mawili, na tutaviachanisha viganja vyetu na tutavituliza katika rukuu kana kwamba tunayakamata magoti.

Tutatulizana katika rukuu yetu, na tutaiweka mbali mikono na mbavu, na wala hatutouchomoza upande mmoja wa shavu ukazidi upande wetu mwingine.

14

Mgongo ulingane usipinde kama upinde, na kichwa kilingane na mgongo, tusikinyanyue, na wala tusikipindishe.

15

"Sub-haana Rabbiyal a'laa" Utakasifu ni wa Mola wangu aliye wa juu

Tutairudia tasbihi (yaani neno hilo) mara tatu, nayo ndiyo ukamilifu wa chini kabisa, na tasbihi moja inafaa, na tutazidisha kama tukitaka, na tunaweza kuleta aina zingine zilizofundishwa.

16

Nyiradi (dhikiri) zinazosemwa katika rukuu ni nyingi.

17

Sami'allaahu liman hamidah (Amesmsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi).

Tutalisema wakati tunatoka katika rukuu, na katika hali ambayo tutakuwa tukiswali wenyewe au mtu akawa ni imamu.

18

Na tutanyanyua mikono yetu usawa wa mabega mawili au masikio mawili, na hii ndiyo sehemu ya tatu ambayo tunanyanyua ndani yake mikono.

19

Kisha tutalingana wima huku tukisema:

"Rabbanaa walakal hamdu" Mola wetu na sifa ni zako.

20

Na tutakua na hiyari baada ya kutoka katika rukuu ya kuachia mikono yetu au kuifunga.

21

Na ni sunna kurefusha kisimamo baada ya kutoka katika rukuu, na kutulizana hapo.

22

(Allaahu Akbar) Mwenyezi Mungu ni mkubwa

Kisha tutaporomoka katika ardhi huku tukitoa takbira ya kuhama kutoka katika kisimamo kwenda katika sijida.

Na tunatanguliza mikono miwili kabla ya magoti mawili, au magoti mawili kabla ya mikono miwili, vyovyote itakavyokuwa vyepesi kwetu.

23

Na inatupasa tusujudu juu ya mifupa saba; kama alivyotufundisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:

Paji la uso pamoja na pua, na viganja viwili, na miguu miwili, na magoti mawili.

24

Tutaweka ncha za vidole vya miguu miwili vikielekea upande wa kibla, na tutaisimamisha miguu miwili.

Na tutatenganisha kati ya mapaja mawili na tutalinyanyua tumbo lisiyaguse hayo.

Tutafanya miundi ya mikono miwili kuwa imenyanyuliwa juu kutoka katika ardhi ikiwa mbali na mbavu, madamu tu hatuswali jamaa na tukahofia kuwaudhi walioko pembezoni mwetu.

Na tutafanya viganja viwili kuwa usawa wa mabega mawili, au usawa wa masikio mawili.

25

"Sub-haana Rabbiyal 'alaa" Utakasifu ni wa Mola wangu aliye wa juu

Tutairudia tasbihi (yaani neno hilo) mara tatu, nayo ndiyo ukamilifu wa chini kabisa, na tasbihi moja inafaa, na tutazidisha kama tukitaka, na tunaweza kuleta aina zingine zilizofundishwa, na tutaomba tunachokipenda katika kheri za dunia na Akhera.

26

Amesema Mtume wa Allah Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Mahala anapokuwa karibu zaidi mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu, zidisheni dua".

27

(Allaahu Akbar) Mwenyezi Mungu ni mkubwa

Huku tukitoa takbira tunanyanyua na vichwa vyetu kutoka katika sijida.

Tutautandika mguu wetu wa kushoto na tutaukalia tukiwa na utulivu, na tutausimamisha mguu wa kulia, na tutavielekeza vidole vyake upande wa kibla.

Au:

Tutasimamisha miguu yote miwili na tutakaa juu ya visigino viwili.

Tutanyoosha miundi ya mikono yetu; wa kulia juu ya paja la kulia, na wa kushoto juu ya paja la kushoto, kwenye magoti au juu ya magoti.

28

(Rabigh-firlii) Mola wangu nisamehe mimi.

Tutaomba kwa dua hiyo kati ya sijida mbili, kiasi kwamba tutakaa tukiwa na utulivu.

29

(Allaahu Akbaru) Mwenyezi Mungu ni mkubwa.

Tutaporomoka huku tukitoa takbira kwenda katika sijida ya pili, nayo ni sawa na sijida ya kwanza katika namna yake, na yale yanayosemwa hapo.

30

(Allaahu Akbaru) Mwenyezi Mungu ni mkubwa.

Tutaleta rakaa ya pili, kwa sifa ambayo tuliitekeleza rakaa ya kwanza.

Kuweka mikono miwili, kusoma suratul faatiha, na aya moja au nyingi ndani ya Qur'ani.

Kisha tunarukuu.

Mwenyezi Mungu ni mkubwa

Na tunasimama:

Sami'allaahu liman hamidah (Amesmsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi).

Kisha tunakwenda kwaajili ya kusujudu.

Mwenyezi Mungu ni mkubwa

Tunasujudu sijida mbili kisha tunakaa kwaajili ya tashahudi (tahiyatu).

Mwenyezi Mungu ni mkubwa

"Allaahu Akbaru" Mwenyezi Mungu ni mkubwa

"Allaahu Akbaru" Mwenyezi Mungu ni mkubwa

31

Baada ya kumaliza rakaa ya pili inakuwa ni kikao kwaajili tahiyatu, tunakaa tukiwa tumekalia mguu

32

Kikao cha kukalia mguu kinakuwa katika tashahudi (tahiyatu) za swala za rakaa mbili mbili; kama sub-hi na ijumaa na iddi mbili, kama inavyokuwa katika tahiyatu ya kwanza katika swala za rakaa tatu na rakaa nne, na katika kikao kati ya sijida mbili.

33

Na wala hakuna tatizo kwa asiyeweza kukalia mguu kwasababu ya ukubwa wa mwili wake, au kwasababu ya maumivu katika mguu wake au kinginecho akae kwa namna atakayoiweza.

34

Katika tahiyatu tunaweka mkono wa kulia juu ya paja la kulia pamoja na kukunja vidole vyote isipokuwa kidole cha shahada tutaashiria kwa hicho.

35

Au tutengeneze duara kwa kidole gumba na kidole cha kati, na tuashirie kwa kidole cha shahada.

36

Ama mkono wa kushoto, ima tuukunjue juu ya paja la kushoto, au tuukunje juu ya goti.

Na inapendeza katika tahiyatu iwe kutazama kwetu ni katika kidole cha shahada cha mkono wa kulia.

37

"Attahiyyaatu lillaahi, wasswalawaatu wattwayyibaatu, assalaamu a'laika ayyuhan nabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu a'lainaa wa a'laa ibaadillaahi sswaalihiin, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu" Tafsiri yake: Maamkizi (Amani) ni ya Mwenyezi Mungu, na swala na vile vilivyo vizuri, amani iwe juu yako ewe nabii na rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake, amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu, nashuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni mjumbe wake.

Tunasoma tashahudi ya kwanza pekee itakapokuwa swala ni ya rakaa tatu au nne.

Ama itakapokuwa swala ni ya rakaa mbili kama swala ya sub-hi, au ijumaa au iddi mbili, tutaikamilisha tashahudi, kwa kusoma swala (dua) ya nabii ibrahim.

"Allaahumma swalli 'alaa Muhammad wa a'laa aali Muhammad, kamaa swallaita 'alaa Ibraahiima wa 'alaa aali Ibrahiima, Innaka hamiidun majiid, Allaahumma baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa baarakta 'alaa Ibraahiima wa 'alaa aali Ibrahiima, Innaka hamiidun majiid" Tafsiri yake: Ewe Allah teremsha rehma juu ya Muhamad na ali zake (familia yake) Muhamad kama ulivyo teremsha juu ya Ibrahim na watu wa Ibrahim hakika wewe ni mwenye sifa tukufu, na teremsha baraka juu ya Muhamad na watu wa Muhamad kama ulivyo teremsha baraka juu ya Ibrahim na watu wa Ibrahim hakika wewe ni mwenye sifa tukufu.

38

(Assalaamu 'alaikum warahmatullaah) Amani iwe juu yenu na rehema za Mwenyezi Mungu

(Assalaamu 'alaikum warahmatullaah) Amani iwe juu yenu na rehema za Mwenyezi Mungu

Ataleta salamu baada ya kumaliza tashahudi na kusoma dua zilizofundishwa katika sunna za Mtume. Lakini hii ni katika swala za rakaa mbili.

39

Tutasikia kwa chini neno: Allaahu Akbaru.

Ama itakapokuwa swala ni ya rakaa tatu kama maghribi, au nne kama adhuhuri au laasiri au ishaa.

40

Kwani sisi tutasimama baada ya tashahudi ya kwanza kuswali rakaa moja tutakapokuwa tunaswali magharibi au rakaa mbili tutakapokuwa tunaswali adhuhuri au Alaasiri au ishaa, tutasoma ndani yake suratul faatiha, pamoja na kufanya maelekezo yote yaliyotangulia katika kurukuu na kusujudu na kukaa.

41

"Allaahu Akbaru" Mwenyezi Mungu ni mkubwa

42

Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akikaa mkao wa kulaza mguu katika tashahudi ya mwisho katika swala zote zenye tashahudi mbili.

43

Kinakuwa kikao cha kulaza mguu katika tashahudi ya mwisho pekee katika swala zenye rakaa tatu au nne, na kina namna zaidi ya moja.

44

Kuutandika mguu wa kushoto, na kuusimamisha wa kulia, na kuitoa yote upande wa kulia na kuweka makalio mawili katika ardhi.

Au:

Kuitandika miguu yote miwili, na kuitoa upande wa kulia.

Au:

Atandike mguu wa kulia, na aingize mguu wa kushoto kati ya paja na muundi wa kulia.

45

Na katika kikao cha tashahudi ya mwisho, tunasoma tashahudi, kisha tutaifuatisha na swala ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-.

46

Kabla ya salamu, na baada ya kumaliza tashahudi, tutaomba kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na mambo manne: Kutokana na adhabu ya jahanamu, na kutokana na adhabu ya kaburi, na kutokana na fitina ya uhai na kifo, na kutokana na shari ya fitina ya masihi dajali.

Na tutaomba tunayoyataka katika kheri za dunia na akhera.

47

(Assalaamu 'alaikum warahmatullaah) Amani iwe juu yenu na rehema za Mwenyezi Mungu

(Assalaamu 'alaikum warahmatullaah) Amani iwe juu yenu na rehema za Mwenyezi Mungu

Haiwezi kumalizika swala wala kujiondoa ndani yake ila kwa salamu.

48

Kwa kutoa salamu tunakuwa tumemaliza swala yetu,

Astaghfirullaah- Namuomba Allah msamaha,Astaghfirullaah- Namuomba Allah msamaha,Astaghfirullaah- Namuomba Allah msamaha.

49

Na ni katika sunna kwa mwenye kuswali atakapotoa salamu amuombe Allah msamaha mara tatu, kisha amtaje Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa dua zilizo thibiti kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake.

27

Kilichoandikwa katika kioo (Screen)

1

Sawa sawa uwe imamu au peke yako

2

Takbira ya kufungua swala (Takbiratul ihramu)

3

Tutanyanyua mikono miwili usawa wa mabega mawili.

4

Au tunainyanyua usawa wa masikio kwa njia hiyo hiyo.

5

Tunaweka mikono miwili juu ya kifua

6

Au juu ya kitovu

7

Au chini ya kitovu

8

Mkono wetu wa kulia tutauweka juu ya kiganja cha mkono wa kushoto

9

Au tutashika kwa mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto

10

Dua ya ufunguzi wa swala

11

Allaahumma baaid bainiy wabaina khatwaayaaya (Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali kati yangu na kati ya makosa yangu) kamaa baa'atta bainal mashriqi wal maghribi (kama ulivyoweka mbali kati ya mashariki na magharibi, Allaahu naqqiniy min khatwaayaaya (Ewe Mwenyezi Mungu nisafishe kutokana na makosa yangu) kamaa yunaqqath-thaubul abyadh minaddanasi (kama inavyosafishwa nguo nyeupe kutokana na uchafu) Allaahummaghsilniy min khatwaayaaya bith-thalji wal maai wal baradi (Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi kutokana na madhambi kwa barafu na maji na baridi".

12

Na ni katika sunna kusoma aina tofauti tofauti

13

Kujikinga

14

Ninajikinga kwa Allah kutokana na shetani alie laaniwa

15

Suratul faatiha

16

(Al-hamdulillaahi Rabbil aalamiin. Arrahmaanir Rahiim. Maaliki Yumiddiin. Iyyaakana'budu wa iyyaaka nastaiin. Ihdinasswiraatwal mustaqiim. Swiraatwalladhiina an 'amta a'laihim, Ghairil maghdhwuubi a'laihim waladh dhwaaliin) Tafsiri yake: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu bwana wa walimwengu. Mwingi wa rehema mwenye kurehemu. Mmiliki wa siku ya malipo. Wewe tu tunakuabudu na ni wewe tu tunakuomba msaada. Tuongoze njia iliyonyooka, njia ya wale uliowaneemesha, siyo ya wale waliokasirikiwa, wala ya wale waliopotea.

17

Ewe mola wetu tukubalie dua

18

Hiyo ni dua ikiwa na maana ya: Ewe Mola wetu kubali (pokea)

19

Tutasoma kiasi tunachokiweza katika Qur'ani

20

Rukuu

21

Mwenyezi Mungu ni mkubwa

22

Mgongo ulingane sawa usijipinde

23

"Sub-haana Rabbiyal a'laa" Utakasifu ni wa Mola wangu aliye wa juu

24

Miongoni mwa Adhkari (dua) za rukuu zilizothibiti ni

25

Subbuuhun, Qudduusun, Rabbul Malaaikati Warruuh. Yaani: Sifa za hali ya juu, na utukufu wa hali ya juu, ni wa Mola wa Malaika na roho (Jibrili).

26

Sub-haanaka Rabbanaa wabihamdika, Allaahumma ghfirli. Yaani: Umetakasika Mola wetu, na sifa njema ni zako, Ewe Mola wangu nisamehe.

27

Sami'allaahu liman hamidah (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi).

28

Rabbanaa walakal hamdu, Hamdan kathiira twayyiban mubaarakan fiihi. Yaani: Mola wetu na sifa njema ni zako, shukran nyingi nzuri zenye baraka ndani yake.

29

Tunaiachia mikono yetu

30

Au tunaifunga

31

Sijida

32

Paji la uso pamoja na pua

33

Viganja viwili

34

Magoti mawili

35

Na miguu miwili

36

"Sub-haana Rabbiyal a'laa" Yaani: Utakasifu ni wa Mola wangu aliye wa juu

37

"Mahala anapokuwa karibu zaidi mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu, zidisheni dua".

38

Mkao wa kukalia mguu

39

Mkao wa kusimamisha vidole na kunyoosha muundi

40

"Rabbighfirli" Mola wangu nisamehe (mara tatu)

41

Allaahummaghfirli, warhamni, wajburni, wahdini, warzuqni. Yaani: Ewe Mola wangu nisamehe, na unihurumie, na unipe nguvu, na uniongoze, na uniruzuku.

42

Sub-hi

43

Ijumaa

44

Iddi mbili

45

Adhuhuri

46

Asri

47

Maghribi

48

Ishai

49

"Attahiyyaatu lillaahi, wasswalawaatu wattwayyibaatu, assalaamu a'laika ayyuhan nabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu a'lainaa wa a'laa ibaadillaahi sswaalihiin, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu" Tafsiri yake: Maamkizi (Amani) ni ya Mwenyezi Mungu, na swala na vile vilivyo vizuri, amani iwe juu yako ewe nabii na rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake, amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu, nashuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni mjumbe wake.

50

"Allaahumma swalli 'alaa Muhammad wa a'laa aali Muhammad, kamaa swallaita 'alaa Ibraahiima wa 'alaa aali Ibrahiima, Innaka hamiidun majiid, Allaahumma baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa baarakta 'alaa Ibraahiima wa 'alaa aali Ibrahiima, Innaka hamiidun majiid" Tafsiri yake: Ewe Allah teremsha rehma juu ya Muhamad na ali zake (familia yake) Muhamad kama ulivyo teremsha juu ya Ibrahim na watu wa Ibrahim hakika wewe ni mwenye sifa tukufu, na teremsha baraka juu ya Muhamad na watu wa Muhamad kama ulivyo teremsha baraka juu ya Ibrahim na watu wa Ibrahim hakika wewe ni mwenye sifa tukufu.

51

Adhuhuri, Laasiri, Magharibi, Ishaa

52

Sub-hi, Ijumaa, na idd mbili.

53

"Allaahumma swalli 'alaa Muhammad wa a'laa aali Muhammad, kamaa swallaita 'alaa Ibraahiima wa 'alaa aali Ibrahiima, Innaka hamiidun majiid, Allaahumma baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa baarakta 'alaa Ibraahiima wa 'alaa aali Ibrahiima, Innaka hamiidun majiid" Tafsiri yake: Ewe Allah shusha rehma juu ya Muhamad na ali zake (familia yake) Muhamad kama ulivyo shusha juu ya Ibrahim na watu wa Ibrahim hakika wewe ni mwenye sifa tukufu, na shusha baraka juu ya Muhamad na watu wa Muhamad kama ulivyo shusha baraka juu ya Ibrahim na watu wa Ibrahim hakika wewe ni mwenye sifa tukufu.

54

(Assalaamu 'alaikum warahmatullaah) Amani iwe juu yenu na rehema za Mwenyezi Mungu

55

"Na anapokaa katika rakaa ya mwisho, anatanguliza mguu wake wa kushoto, na mwingine anaukunja, na anakalia makalio yake". Imepokelewa na Al-Bukhaariy

56

Mkao wa kukalia mguu

57

"Allaahumma inni a'udhubika min adhaabi jahannama, wa min adhaabil qabri, wamin fitnatil mahyaa wal mamaati, wamin sharri fitnatil masiihiddajjaali" Ewe Mola wangu hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na adhabu za jahanamu, na fitina za uhai na za kifo, na kutokana na fitina za masihi dajali. Kaipokea Muslim.

58

"Ewe Mola wangu hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu dhulma nyingi, na wala hakuna anayesamehe madhambi ila wewe, nisamehe mimi msamaha unaotoka kwako, na unihurumie kwani hakika wewe ni mwingi wa kutoa msamaha na ni mpole" Kaipokea Bukhariy.

59

Astagh-firullaah (Namuomba Mwenyezi Mungu msamaha) mara tatu

60

kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Hakika ya kwanza atakayohesabiwa kwayo mja siku ya kiyama katika matendo yake ni swala yake, ikiwa itatengemaa, basi atakuwa kafaulu na kasalimika, na ikiharibika atakuwa kaharibikiwa na kapata hasara". Imepokelewa na Abuu Daud na Tirmidhiy na Nasaai.