Namna ya kufanya Umrah, maelezo kwa vitendo na kwa ufupi Unafanya vipi Umra? Kipande cha video cha mafunzo kilichorahisishwa. Kipande cha video kinachoeleza ibada za Umrah kwa mpangilio kuanzia Ihramu hadi Tahalluli (kumaliza Umrah), kwa mtindo mwepesi na ulio wazi. Tazama kipande hiki cha video na jifunze namna ya kutekeleza Umrah yako kwa urahisi na usahihi. Namna ya kufanya Umrah Ni wajibu kwa mwenye kutaka kufanya Umrah ahirimie kutokea katika kituo kilichowekwa kwake. Vituo vya kuhirimia: Ni sehemu alizoziainisha Mtume, rehema na amani ziwe juu yake Ili ahirimie hapo mwenye kutaka…
Namna ya kufanya Umrah, maelezo kwa vitendo na kwa ufupiUnafanya vipi Umra? Kipande cha video cha mafunzo kilichorahisishwa.Kipande cha video kinachoeleza ibada za Umrah kwa mpangilio kuanzia Ihramu hadi Tahalluli (kumaliza Umrah), kwa mtindo mwepesi na ulio wazi. Tazama kipande hiki cha video na jifunze namna ya kutekeleza Umrah yako kwa urahisi na usahihi.Namna ya kufanya Umrah
Ni wajibu kwa mwenye kutaka kufanya Umrah ahirimie kutokea katika kituo kilichowekwa kwake.
Vituo vya kuhirimia: Ni sehemu alizoziainisha Mtume, rehema na amani ziwe juu yakeIli ahirimie hapo mwenye kutaka kufanya Hija au Umrah.
Kwa hivyo, yeyote anayepita katika mojawapo ya hizo akikusudia Hija au Umrah, ni wajibu kwake kuhirimia hapo, wala haijuzu kuzipita bila kuhirimia.
Na yeyote aliye karibu na Makka kuliko vituo hivi, kama vile wakazi wa Jeddah:Basi kituo chake ni mahali anapoishi; atahirimia papo hapo Hija na Umrah.
Na ama watu wa Makka, watahirimia Hija kutokea majumbani mwao hapo Makka.Na ama kwa Umrah, basi watatoka nje ya eneo takatifu, kisha wahirimie huko, kama vile Tan'iim na mfano wake.
Na yeyote atakayekuwa ndani ya ndege, yeye atahirimia atakapofika usawa wa kituo chake (Miqat).Hivyo basi, anafaa kujiandaa na kuvaa nguo za ihram kabla ya kufika usawa wa kituo chake (Miqat).Atakapofikia usawa wake, basi papo hapo atahirimia.Pia anaweza kuchukua hadhari akafanya Talbiya kabla ya kufika usawa wa Miqat kwa kuhofia asijepita mahali pa kuhirimia kwa sababu ya kasi kubwa ya ndege.Wala haruhusiwi kuchelewesha mpaka atue uwanjani.
Namna ya kuhirimia na hukumu zake
Atakayetaka kuhirimia, basi:
1. Inapendekezwa kwake kuoga.
2. Na inapendekezwa kwa wanaume kutumia manukato,na iwe mwilini na kwenye ndevu, si katika nguo za ihramu.
3. Na ni wajibu kuvaa nguo za Ihram, ambazo kwa mwanamume, ni kikoi na shuka.Na Sunnah ni kwamba ziwe nyeupe na safi, au ziwe mpya.
Na mwanamke atahirimia katika nguo yoyote anayotaka, bila ya kuonyesha mapambo yake,lakini atajiepusha kuvaa nikabu na glovu,na afunike uso wake na mikono yake kwa kitu kingine.
4. Na kuhirimia, ni nia ya kuingia katika ibada, basi atasema:"Nimekuitikia ewe Mwenyezi Mungu kwa kufanya Umrah"Labbayka Allaahumma 'UmratanNa ikiwa anafanya Umra kwa niaba ya mtu mwingine, atasema:"Nimekuitikia ewe Mwenyezi Mungu kwa kufanya Umra kwa niaba ya fulani."Labbayka Allaahumma 'Umratan 'an fulaanin.
5. Na iwapo mtu anayetaka kuhirimia anahofia kizuizi kitakachoweza kumzuia kukamilisha ibada yake,basi inafaa kwake aweke sharti anapoingia katika Ihram, kwa kusema:"Nimekuitikia ewe Mwenyezi Mungu kwa kufanya Umrah, na ikiwa nitazuiliwa na kizuizi, basi mahali pangu pa kutoka katika Ihramu ni pale utakaponizuilia."Labbayka Allaahumma 'Umratan, wa in habasanii haabisun, famahil-lii haythu habastaniiBasi pindi atakapoweka sharti na akapatwa na cha kumzuia kukamilisha ibada yake, basi atatoka katika ihramu na wala hakutakuwa na chochote juu yake.
6. Kisha atakithirisha kufanya Talbiyah:"Nimekuitikia ewe Mwenyezi Mungu nimekuitikia, nimekuitikia huna mshirika nimekuitikia. Hakika sifa njema na neema na ufalme ni vyako, huna mshirika."Labbayka Allaahumma labbayk. Labbayka laa shariika laka labbayk. Innal-hamda wan-ni'mata laka wal-mulk, laa shariika lak.Mwanaume atanyanyua sauti yake katika hilo,na vilevile mwanamke, maadamu hayuko mbele ya wanaume wasio maharimu wake.
7. Mtu aliyehirimia analazimika kuepuka makatazo ya ihramu mpaka atakapotoka katika ihramu yake.
Makatazo ya Ihramu ni sehemu tatu:
Kwanza: Mambo yaliyoharamishwa kwa wanaume na wanawake:
Kunyoa nywele au kuzipunguza au kuzing'oa kutoka sehemu yoyote ile ya mwili.
Kukata kucha zote au baadhi yake kwenye miguu au mikono.
Kujipaka manukato mwilini au katika nguo za ihramu.
Kuua viwindwa vya mwituni, au kuwawinda hata kama hatawauwa.
Kuposa au kumposea mtu mwingine.
Kufunga ndoa.
Kumpapasa mwanamke katika sehemu zisizokuwa tupu, kama vile kumbusu na kumgusa kwa matamanio.
Kujamiiana kwenye uke.
Pili: Mambo yaliyoharamishwa kwa wanaume:
Kufunika kichwa kwa kitu kinachoshikamana nacho, kama vile kofia, kilemba, na kuweka shuka juu ya kichwa, au kitu kingine chochote kinachokusudiwa kufunika.
Kuvaa mavazi ya kawaida yaliyoshonwa ili kuvaliwa kwenye mwili mzima, kwa njia ya kawaida, kama vile: Nguo iliyoshonwa, suruali, na shati.
Tatu: Mambo yaliyoharamishwa kwa wanawake:
Kuvaa nikabu, au barakoa, au pazia linalofanana na nikabu, na ni lazima kwake kufunika uso wake mbele ya wanaume wasio maharimu wake kwa kitu kinginecho.
Kuvaa glovu mikononi mwake, na itamlazimu kufunika mikono yake mbele ya wanaume wasio maharimu wake.
Mwenye kufanya Umrah ataanza Umrah yake kwa kuzunguka Al-Kaaba (tawafu).
Na ni sharti kwa mwenye kuzunguka Al-Kaaba awe na twahara.
Mtu aliyehirimia atakapoingia kwenye Msikiti Mtukufu, ni sunna kwake autangulize mguu wake wa kulia,na atasema dua ya kuingia msikitini, nayo ni:"Ewe Mola, nifungulie milango ya rehema zako.""Allaahumma iftah lii abwaaba rahmatika."
Atakapoiona Al-Ka'aba, atakata Talbiyah.
Anapotaka kuanza Tawafu, ni sunna kwake kufanya idhtwibaa,kwa kuweka katikati ya shuka lake ndani ya kwapa lake la kulia, na ncha zake kwenye bega lake la kushoto.Atakapomaliza tawafu, atalirudisha shuka lake na kufunika mabega yake, kwa sababu Idhtwibaa hufanywa katika tawafu peke yake.
Tawafu huanzia kwenye Jiwe Jeusi.
Basi inapendekezwa aliguse Jiwe Jeusi kwa mkono wake wa kulia na kulibusu.Na ikiwa haitawezekana kulibusu, ataligusa kwa mkono wake, kisha aubusu mkono wake.Na ikiwa haitakuwa rahisi kwake, ataligusa kwa kitu alicho nacho kama vile fimbo au mfano wa hivyo na kukibusu.Na ikiwa hataweza kufanya hivyo, basi atalielekea Jiwe hilo na aliashirie kwa mkono wake lakini asiubusu.Na ni bora asisongamane akawaudhi watu na kuudhiwa nao.
Na inapendekezwa aseme atakapoligusa Jiwe hilo au kuliashiria:"Mwenyezi Mungu ni Mkuwa.""Allaahu Akbar."
Kisha atakwenda upande wa kulia na aiweke Al-Ka'aba upande wake wa kushoto.Atakapofika kwenye Kona ya Yemeni, ataigusa bila kuibusu.Na isipowezekana, asilete msongamano, wala asiliashirie.
"Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na akhera tupe mema, na utukinge kutokana na adhabu ya Moto.""Rabbanaa aatinaa fid-dunyaa hasanatan, wa fil aakhirati hasanatan, waqinaa 'adhaaban-naar."
Atasema baina ya Kona ya Yemen na Jiwe Jeusi:
Kila mara atakapolipita lile Jiwe Jeusi, ataliashiria kwa mkono wake na kusema:"Mwenyezi Mungu ni Mkubwa.""Allaahu Akbar."
Na mizunguko yake iliyosalia, atasema chochote anachopenda miongoni mwa dhikri, dua na kusoma Qur’ani.
Sunna ni kwenda kwa kasi katika mizunguko mitatu ya kwanza tu, ikiwa ni wepesi kwake,kwa kwenda mwendo wa haraka kwa hatua za karibu karibu.Na ama mizunguko minne iliyosalia, hiyo haina kuharakisha.
Akimaliza tawafu, inapendeza aswali rakaa mbili nyuma ya Maqam Ibrahim ikiwa itakuwa rahisi.Vinginevyo, ataswalia mahala popote pa Msikitini Mkuu.Atasoma katika rakaa ya kwanza baada ya Al-Fatiha:"Sema: Enyi makafiri!"Na katika rakaa ya pili, baada ya Al-Fatihah, atasoma:"Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa Pekee."
Kisha inapendekezwa kwamba aelekee Kibla, yaani Al-Ka'aba, na aseme:Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee asiye na mshirika, ufalme ni wake na sifa njema ni zake, naye juu ya kila kitu ni Muweza.Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee, alitimiza ahadi yake, na akamnusuru mja wake, na akayashinda makundi ya maadui peke yake.Laa ilaaha illallaahu wahdahuu laa shariika lahuu, lahul-mulku wa lahul-hamdu, wa huwa 'alaa kulli shay-in qadiir.Laa ilaaha illallaahu wahdahuu, anjaza wa'dahuu, wa naswara 'abdahuu, wa hazamal ahzaaba wahdahuu.Atayarudia haya mara tatu, na ataomba dua baina ya hayo.
Kisha atashuka kutoka kwenye Swafa kwenda Marwa kwa kutembea kwa miguu.Atakapofika kwenye alama ya kijani, wanaume pekee watatembea haraka.Na atakapoifikia alama ya pili ya kijani, atatembea.
Atakapofika Marwa, anaruhusiwa kufanya yale aliyoyafanya kwenye Swafa.Kama vile takbira, dua, kusoma Qur'ani na kuelekea Al-Kaaba.
Kisha atashuka kutoka kwenye Marwa kwenda Swafa kwa kutembea kwa miguu.Atakapofika kwenye alama ya kijani, atatembea haraka.Atakapofika kwenye alama ya kijani ya pili, atatembea.
Ataendelea hivi hadi amalize mizunguko saba.Kutoka Swafa hadi Marwa ni mzunguko mmoja,na kurudi kutoka Marwa hadi Swafa ni mzunguko mwingine.Ataanza na Swafa na kumalizia Marwa.
Na atasema katika sa'yi yake chochote anachopenda miongoni mwa dhikri, dua na kusoma Qur'ani.
Namna ya kunyoa na kupunguza nywele:
Mwenye kufanya Umra atakapomaliza tawafu na sa’yi, itamlazimu mwanaume anyoe nywele za kichwa chake au azipunguze,na la wajibu ni kunyoa au kupunguza kichwa chote.
Na mwanamke atapunguza kwenye ncha za nywele zake kiasi cha ncha ya kidole.
Na kufikia hapa, Umrah inakuwa imekamilika.
Hukumu za Mawaaqiit (Vituo vya kuhirimia)
MadinaDhul-HulaifaDhaat 'IrqAl-Juhfa
YalamlamQarnul-ManaazilMawaaqiit (Vituo vya kuhirimia)
MakkaMiqaat (Kituo cha kuhirimia)Kuhirimia kwa aliye karibu na MakkaMahali pake
Ihramu ya watu wa MakkaKwa HijaKutokea kwenye nyumba zaoKwa UmrahTan'iim.
Kuhirimia kwa anayekuja kwa ndegeKabla ya kufika usawa wa Miqat (Kituo cha kuhirimia)Anavaa nguo za ihramAnapokuwa usawa wa MiqatAnanuia kuhirimiaAnaanza TalbiyahHaifai kuchelewesha kuhirimia mpaka uwanja wa ndege
Namna ya kuhirimia na hukumu zake
Kuoga
Kutumia manukato
Kwa wanaume na si wanawakeKiwiliwiliNdevu.Mavazi
Kuvaa nguo za Ihram.Shuka na kikoiWa kiumeVyeupe viwiliWa kikeNguo yoyote anayotakaAsiyeonyesha uremboNikabuGlovu
Kuhirimia Umrah:
MaradhiTukio
Kuweka sharti kwenye nia
Anatoka katika Ihramu na wala hana chochote juu yake
Namna ya Talbiya:
Epuka makatazo ya Ihramu
mpaka atakapotoka katika ihramu yakeMakatazo ya IhramuNi haramu kwa wanaume na wanawakeKuposa au kumposea mtu mwingineKufunga ndoaNi haramu kwa wanaumeWa kiumeNi haramu kwa wanawake
Namna ya kuzunguka Al-kaabaNi sharti kwa tawafu mtu awe na twahara
Dua ya kuingia msikitini
Mguu wa kulia.
Kuvaa lubegaKuvaa lubega ni kwa tawafu pekeeTawafu huanzia kwenye Jiwe Jeusi
Kona ya Yemeni
Anachosema baina ya Kona mbili za Yemen
DhikiriDuaKusoma Qur'aniUhalali wa kuongeza mwendoKatika raundi tatu za mwanzo
Kuswali nyuma ya Maqam IbrahimIkiwezekana
"Na pafanyeni Maqam Ibrahim mahali pa kuswalia."
Namna ya kufanya sa'yi
MarwaSwafaa
Mara tatuAnakimbiaAnatembeaAlama ya kijaniTakbiraKuelekea Al-KaabaMizunguko sabaKutoka Safa kwenda Marwa ni mzunguko mmojaMzunguko mmojaNamna ya kunyoa na kupunguza nywele
Wajibu wa kunyoa na kupunguza nywele kwa mwanaumeKuenea kichwa kizimaWajibu wa kupunguza nywele kwa mwanamkeWa kike
MUHTASARI WA NAMNA YA KUFANYA UMRAH NA HUKUMU ZAKE
65 lugha
MUHTASARI WA NAMNA YA KUFANYA UMRAH NA HUKUMU ZAKE
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, na rehema na amani ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad, na watu wake na Maswahaba zake wote. Ama baada ya hayo: Hii ni makala fupi juu ya namna ya kufanya Umra, hukumu zake na adabu zake. Tumejitahidi kubainisha ndani yake mengi katika yale anayohitaji mtu anayefanya ‘Umra. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aifanye iwe kwa ajili ya uso wake mtukufu, na kwamba anufaishe kwayo Waislamu wote.
Kijitabu "Namna ya kufanya Umrah" cha Sheikh, Abdulaziz bin Baaz, Mwenyezi Mungu amrehemu, kinaeleza ibada za Umrah kwa mtindo ulio wazi na unaoeleweka kwa urahisi; ili kitumike kama mwongozo wa kivitendo katika kusaidia Waislamu kutekeleza ibada zao za Hija au Umra kwa unyenyekevu na urahisi, kikiambatana na dua na nyiradi zilizopokelewa kutoka kwa Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, katika kila hatua.
UCHAMBUZI NA UFAFANUZI WA MASUALA MENGI YA HIJA, UMRA NA
ZIARA KWA MUJIBU WA MUONGOZO WA QUR'ANI NA SUNNA
54 lugha
UCHAMBUZI NA UFAFANUZI WA MASUALA MENGI YA HIJA, UMRA NA
ZIARA KWA MUJIBU WA MUONGOZO WA QUR'ANI NA SUNNA
Kitabu kinafafanua hukumu za Hija, Umra na Ziara kwa mujibu wa Qur'ani na Sunna, na kinaeleza mambo ya wajibu katika Hija na Umra. Vile vile kinaeleza mambo yaliyokatazwa wakati wa Ihramu na adabu za kuutembelea Msikiti wa Mtume, huku kikihadharisha dhidi ya uzushi (Bid'aa) katika ibada hizi.
MAKOSA YANAYOFANYIKA KATIKA HIJA, UMRAH NA KUTEMBELEA MSIKITI WA MTUME
39 lugha
MAKOSA YANAYOFANYIKA KATIKA HIJA, UMRAH NA KUTEMBELEA MSIKITI WA MTUME
Makosa na ukiukaji unaohusiana na Umra Kwanza: Ukiukaji wa watu na makosa yao katika Ihram 1. Kuacha kufanya ihlaal, kwa kutoinua juu sauti yake mwanzoni mwa kuhirimia ibada aliyokusudia sawa iwe Hija au Umra. Na Sunna: Ni kunyanyua sauti katika hilo.