عربي - Arabic English Qafár af - Afar Afrikaans - Afrikanns Akan Shqip - Albanian አማርኛ - Amharic Հայերեն - Armenian অসমীয়া - Assamese Azərbaycanca - Azerbaijani Bamanankan - Bambara Bassa Bemba বাংলা - Bengali Bosanski - Bosnian Български - Bulgarian မြန်မာဘာသာ - Burmese Bisaya - Cebuano Cham Нохчий - Chechen chiCheŵa - Chewa 中文 - Chinese Адыгэбзэ - Circassian Hrvatski - Croatian Česky - Czech Dagbani Dansk - Danish فارسی دری - Dari Dendi ދިވެހި ބަސް - Dhivehi Nederlands - Dutch إستوني - Estonian Suomi - Finnish Français - French Fulfulde - Fula ქართული - Georgian Deutsch - German Ελληνικά - Greek ગુજરાતી - Gujrati Kreyòl ayisyen - Haitian Creole Hausa हिन्दी - Hindi Magyar - Hungarian Igbo Indonesia - Indonesian Italiano - Italian 日本語 - Japanese Jóola - Jola ಕನ್ನಡ - Kannada Қазақша - Kazakh ភាសាខ្មែរ - Khmer Kikuyu Ikinyarwanda - Kinyarwanda Ikirundi - Kirundi 한국어 - Korean كوردی سۆرانی - kurdish كوردي kurmancî - Kurmanji Kyrgyz ລາວ - Lao latviešu - Latvian Lingala lietuvių - Lithuanian Luganda Македонски - Macedonian Maguindanaon Malagasy - Malagasy Bahasa Melayu - Malay മലയാളം - Malayalam Mandinka मराठी - Marathi Mõõré - Moore नेपाली - Nepali أنكو - NKo Norwegian ଓଡ଼ିଆ - Odia oromoo - Oromo پښتو - Pashto فارسی - Persian Polski - Polish Portuguese ਪੰਜਾਬੀ - Punjabi Română - Romanian Русский - Russian Српски - Serbian Shona සිංහල - Sinhala Slovenščina - Slovenian Soomaaliga - Somali Soninke Sesotho - Sotho Español - Spanish Kiswahili - Swahili Svenska - Swedish Tagalog Тоҷикӣ - Tajik தமிழ் - Tamil తెలుగు - Telugu ไทย - Thai ትግረኛ - Tigrinya Türkçe - Turkish Ukrainian اردو - Urdu ئۇيغۇرچە - Uyghur Ўзбек - Uzbek Việt Nam - Vietnamese Wolof Yao Yorùbá - Yoruba Zarma زولو - Zulu
839 Hadithi
Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii
Chuja matokeo
Kadi 839
Daraja la hadithi
Imesimuliwa katika
Onyesha vyanzo vilivyobaki
Msimulizi
Onyesha wasimulizi wote (234)
"Laiti nyinyi mgetegemea kwa Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni kama anavyowaruzuku ndege, wanatoka asubuhi wakiwa na njaa, wanarudi jioni wakiwa wameshiba".
Sahihi Imepokelewa na Imam Ahmad, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ibn Hibban katika Sahih yake na Haakim
"Wema ni tabia njema, na dhambi ni lile lililokukereketa katika nafsi yako na ukawa hukupendezwa watu walione".
Sahihi Hadithi ya kwanza ameipokea Muslim, na hadithi ya pili ameipokea Ahmad na Ad-Darimi.
Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimtuma kwenda Yemen, akamuuliza kuhusu vinywaji fulani vinavyotengenezwa huko, akasema: Ni vipi hivyo?, akasema: "Ni Bit'u na Mizru" akaulizwa Abuu Buraida: Bit'u ni nini? Akasema: Ni mvinyo wa Asali, na Mizru: Ni mvinyo wa ngano, akasema: "Kila kilevi ni haramu" Ameitoa Bukhari.
Sahihi Imepokelewa na Bukhari na Muslim
"Ulimi wako usiache kuwa mbichi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu".
Sahihi Imepokelewa na Ahmad, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ibn Hibban
"Mambo manne yatakayekuwa kwake basi atakuwa mnafiki, ana akiwa na jambo moja miongoni mwa hayo basi atakuwa na tabia ya unafiki mpaka aiache: Yule anayesimulia akasema uongo, na akiahidi hatimizi, na akigombana hupita mipaka, na akiingia makubaliano hufanya hiyana".
Sahihi Imepokelewa na Bukhari na Muslim
"Watatokea katika zama za mwisho watu wenye umri mdogo (vijana), wenye mawazo ya kipumbavu, watazungumza maneno mazuri kuliko maneno ya viumbe wote, (lakini) wanatoka katika Uislamu kama unavyotoka mshale katika upinde, imani yao haitovuka koromeo zao, mahali popote mtakapokutana nao basi wauweni, kwani kuwaua kwao kuna malipo siku ya Kiyama kwa atakayewaua".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Mwenyezi Mungu alipoumba Pepo na Moto alimtuma Malaika Jibril -Amani iwe juu yake- aende peponi Akamwambia: Iangalie hiyo pepo na yale niliyo waandalia humo watu wa peponi, basi Jibrili akaiangalia Pepo kisha akarudi, akasema: Naapa kwa utukufu Wako ewe Mwenyezi Mungu hatozisikia mtu yeyote habari za pepo kisha asiingie humo, kisha akamuamrisha kuizungushia Pepo hiyo mambo yenye kuchukiza, kisha akamwambia nenda tena ukaiangalie na uangalie yale niyowaandalia
watu wake humo peponi. Basi akaiangalia ghafla akaiona imezungushwa vyenye kuchukiza, akasema: Naapa kwa utukufu Wako kwa hakika ninahofia kuwa hatoingia mtu yeyote. Akasema kumwambia Jibrili nenda na uuangalie Moto na yale niliyo waandalia humo watu wa Motoni. Basi akauangalia Moto na akauona Moto ulivyopambwa, basi akarudi na akasema: Naapa kwa utukufu Wako hatoingia yeyote humo, basi akaamrisha ukazungushwa mambo yenye kutamanisha, basi akamwambia: Rudi na uuangalie tena. Basi akauangalia akaukuta umepambwa na kuzungushwa yenye kutamanisha, basi akarudi na akasema: Naapa kwa utukufu wako kwa hakika nahofia yakuwa hatosalimika mtu yeyote isipokuwa ataingia Motoni."
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai
"Atakayemtatulia muumini tatizo moja katika matatizo ya dunia, Mwenyezi Mungu atamtatulia yeye tatizo katika matatizo ya siku ya Kiyama, na atakayemfanyia wepesi mwenye ugumu (katika jambo lake) Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi duniani na Akhera, na atakayemsitiri muislamu Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na Akhera, na Mwenyezi Mungu humsaidia mja pale mja anapokuwa katika kumsaidia ndugu yake, na atakayeshika njia akitafuta ndani yake elimu, Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi kupitia njia hiyo njia ya kuingia peponi, na hawajawahi kukusanyika watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu wakisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu na wakisomeshana baina yao, isipokuwa huwashukia utulivu na huwagubika rehema na Malaika huwafunika, na Mwenyezi Mungu huwataja (vizuri) kwa wale walioko kwake (Malaika), na yeyote ambaye matendo yake yatamchelewesha kuingia peponi basi ukoo wake hautompeleka mbio (kuingia)".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim