Kitabu cha Kuzuru Pango la Hiraa, kinazungumzia mahali hapa ambapo ndipo mahali pa mwanzo wa Ujumbe wa Utume na mahali pa mwanzo pa kuteremkia aya za mwanzo za Qur'ani tukufu, na kinatanabahisha kuwa ibada zilizofanywa kuwa katika sheria huwa kule Makka katika Msikiti Mtukufu pekee na maeneo matakatifu yaliyotengwa kwa ajili ya Hija, na kinapinga kila uzushi wa kutaka kuokolewa na kutaka baraka kutoka katika maeneo au vitu visivyokuwa vya kisheria, kama vile Pango la Hiraa. Vile vile, kinatahadharisha dhidi ya kwenda kinyume na sunna ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, na kinawaita watu…
Lugha: lang_sw
Imeandaliwa na: Kamati ya Kielimu ya Jumuia ya Kuhudumia Maudhui za Kiislamu kwa Lugha Mbalimbali.
Kamati ya Kielimu ya Jumuia ya Kuhudumia Maudhui za Kiislamu kwa Lugha Mbalimbali.
Pango la Hiraa liko katika kilele cha mlima Nuru kaskazini mashariki mwa mji mtukufu wa Makkah. Unakaridiriwa urefu wa mlima kuwa mita mia sita na thelathini na nne (634).
Pango hili ni finyu sana ambalo halichukui zaidi ya watu watatu kwa kukaa.
Alikuwa Mtume Mtukufu Muhammadi, rehema na amani ziwe juu yake, akijitenga hapo kabla ya utume kwa siku kadhaa, na hasa hasa katika mwezi wa Ramadhani kwa ajili ya kutafakari na kuzingatia mamlaka ya Mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini akiwa mbali na watu, na alifanywa kupenda kujitenga.
Na sehemu hii inakuwa ya kipekee kwa mambo mengi, ya muhimu zaidi ni:
Ni kuwa pako mbali na kelele za watu na kero zao. Mlima huo ni mgumu sana kuupanda, njia zake zina vikwazo vigumu na uko mbali na Al-Ka'ba kwa takribani kilomita mbili. Zamani, kulikuwa na kiuwazi kidogo upande wa magharibi wa pango ambako Al-Ka'ba tukufu ilikuwa ikionekania. Hili lilipafanya mahali hapa kuwa ni sehemu nzuri ya kutafakari na kuchukua mazingatio.
Na katika sehemu hii yenye kutisha na juu ya kilele cha mlima huo mgumu ulianza utume wa Nabii mtukufu rehema na amani ziwe juu yake na zikateremka kwake aya za mwanzo kabisa za Qur'ani:"Soma, kwa Jina la Mola wako Mlezi aliyeumba."[Al-'Alaq: 1]
Kisha akarejea kwa Khadija, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akiwa na hofu na mfadhaiko kutokana na msukosuko wa kile alichokiona, huku akisema:"Nifunikeni, nifunikeni" [1].Rehema na amani kwa wingi ziwe juu yake mpaka siku ya malipo.
Kaka yangu Muislamu, dada yangu Muislamu mwenye kutembelea pango la Hiraa,[1] Imekusanywa na Bukhari: Kitabu cha tafsiri, nambari 4642, na Muslim, mlango wa kuanza kwa Ufunuo juu ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, nambari 160.
Bila shaka kusoma na kujua kwa Muislamu historia ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, ni jambo lenye umuhimu wake ili tujifananishe naye kama kiigizo kwetu katika hali zake zote na mambo yake yote. Lakini jambo ambalo si katika dini wala sheria tukufu haikuelekeza hivyo bali limekuja katazo juu yake, ni kile wanachoweza kukifanya baadhi ya wanaokuja kuzuru -Mwenyezi Mungu awaongoze- katika mambo yanayokwenda kinyume na yale aliyokuja nayo Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, katika muongozo na maelekezo, kama wale wanaojipangusa katika mawe au wale wanaoyabusu na kuyalamba au mengineyo katika matendo maovu.
Je, Mtume rehema na amani ziwe juu yake alifanya chochote katika hayo, au aliamrisha, au baada yake walifanya Maswahaba zake watukufu radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao!? Laa hashaa mara elfu, na lenye madhambi makubwa zaidi kuliko yote hayo ni wale wanaotaka kuokolewa na asiyekuwa Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka. Katika usia wa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, akimuusia Abdullahi bin Abbasi, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, alisema:"Ewe kijana, mhifadhi Mwenyezi Mungu, atakuhifadhi. Mhifadhi Mwenyezi Mungu, utamkuta mbele yako. Unapoomba, basi muombe Mwenyezi Mungu. Na unapotaka msaada, basi taka msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu..." [2]
Kama ambavyo baadhi ya watu hukusudia kwenda katika pango la Hiraa wakati wa ziara yake ya Hija au Umra au kwa kinginecho, na anahimili matatizo na anapanda mahali pagumu na anajitaabisha katika matendo ambayo anadhani kuwa yanamuweka karibu na Mwenyezi Mungu, na hali si hivyo. Bali mfano wa mtu kama huyu anajitaabisha kwa jambo ambalo halimuweki karibu wala si katika kumtii Mwenyezi Mungu, bali ameingia katika mambo aliyoyakataza Mwenyezi Mungu.
Na baadhi yao - tunaomba Mwenyezi Mungu awaongoze - wanafanya baadhi ya matendo yanayokwenda kinyume na ujumbe wa Tauhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) aliokuja nao Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, au anafanya baadhi ya uzushi ulioanzishwa unaochafua ukamilifu wa imani.
Na alikuwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, akifanya ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu katika pango la Hiraa kabla ya wahyi haujamteremkia kutoka mbinguni, na baada ya kufuatana kwa wahyi hakuwahi kwenda huko tena, si kwa ajili ya dua wala swala wala kwa ajili ya kinginecho.
Na aliishi Makka takribani miaka kumi na tatu (13) na haikuwahi kuthibiti kuwa aliwahi kwenda Hiraa wala mahali pengine katika maeneo ambayo baadhi ya watu wanadhani kuwa kuyatembelea ni sunna na ni kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.
Bila shaka mahali pekee huko Makka ambapo ni sheria kupatembelea kwa ajili ya ibada na kuomba dua ni Msikiti Mtukufu pekee.
Na ama maeneo matakatifu anayoenda hujaji kama vile Arafa, Mina na Muzdalifa, si katika sheria kuyatemebelea isipokuwa katika siku za Hija zinazofahamika kwa kila Muislamu, na hii haiwi isipokuwa katika siku maalumu, kwa kuendana na yale aliyoyaweka Mwenyezi Mungu katika sheria, hakuna kuzitanguliza wala kuzichelewesha. Bali utatembelewa Msikiti Mtukufu pekee, na wala hakuna ukomo wa wakati wake, kama ilivyokuja kwa njia sahihi katika hadithi:"Enyi wana wa Abdi Manafi, msimzuie yeyote atakayetufu katika nyumba hii na akaswali saa yoyote atakayotaka, iwe usiku au mchana".Wameipokea watu wa vitabu vya sunani [4].
Ndugu yangu mheshimiwa Muislamu, ikiwa maeneo matatu matukufu ya ibada Arafa, Mina, Muzdalifa na Jamaraat, aliyoyaweka Mwenyezi Mungu Mtukufu katika sheria kwa watu kuanzia zama za Ibrahim, amani iwe juu yake, na inasemekana: Kuanzia zama za Adam, yana wakati maalumu na hali maalumu, inakubalika vipi watu kubuni maeneo ya kutembelea kwa ajili ya ibada na kujikurubisha, na wakaweka wakati wake kuwa huru muda wowote kwa atakayetaka katika kila zama, kama vile pango la Hiraa na kwingineko?[4] Ameipokea Tirmidhi: Milango ya Hija, mlango wa yaliyokuja katika swala baada ya Lasiri, na baada ya Al-fajiri kwa anayetufu, kwa nambari 868, na Nasaai: Kitabu cha Nyakati, mlango wa kuhalalisha swala katika saa zote huko Makka, nambari 585.
Na baada ya kuhama kwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, alikwenda Makka kwa mara kadhaa, na hakuwahi kwenda katika pango la Hiraa milele, na lau kama ingekuwa ni katika sheria na ni katika kujikurubisha, basi angelitembelea, na yeye ndiye angelikuwa mtu anayefaa zaidi kutembelea pango la Hiraa; kwa sababu yeye alikuwa akifanya ibada hapo kabla ya utume, na katika pango hilo anakumbukumbu kubwa ambayo haijawahi kutokea kwa yeyote kabla yake wala baada yake.
Na kinachofahamika ni kuwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, alifanya Umra yake ya nne pamoja na Hija ya kuaga, na wakahiji pamoja naye jopo kubwa la Waislamu, hakuna aliyekwenda kinyume na Hija pamoja naye isipokuwa yule aliyemtaka Mwenyezi Mungu.Na yeye katika hayo yote, si yeye wala yeyote katika Maswahaba zake, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, hakuna aliyepanda katika pango la Hiraa wala kulitembelea, wala sehemu yoyote katika maeneo ya Makka, na hapakuwa na ibada yoyote huko isipokuwa katika Msikiti Mtukufu na baina ya Swafa na Marwa na Mina na Muzdalifa na Arafa kisha baada yake mahalifa wake waongofu na wengineo miongoni mwa wale waliotangulia mwanzo, na hawakuwa wakitembea pango la Hiraa na mfano wake kwa ajili ya kuswali ndani yake na kufanya dua au kutaka baraka hapo.
Na lau kama hili lingekuwa ni katika sheria na katika sunna anayolipa thawabu Mwenyezi Mungu juu yake; basi Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, angelijua zaidi hilo kuliko watu wengine na angelipendelea zaidi kuliko waliokuja baada yao. Ikiwa hawakufanya lolote katika hayo; basi itajulikana kuwa hilo ni uzushi ulioanzishwa uliokatazwa kisheria na katika dini, atakayeasi baada ya hapo na akaifanya kuwa ni ibada na kujikurubisha na ni utiifu, basi atakuwa kafuata njia isiyokuwa njia yao, na atakuwa ameyafanya sheria mambo ambayo Mwenyezi Mungu hakuyaidhinisha. Amesema Mtukufu:"Hakika nyinyi mnacho kiigizo chema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anayemtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamtaja Mwenyezi Mungu sana."[Al-Ahzab: 21].
UCHAMBUZI NA UFAFANUZI WA MASUALA MENGI YA HIJA, UMRA NA
ZIARA KWA MUJIBU WA MUONGOZO WA QUR'ANI NA SUNNA
43 lugha
UCHAMBUZI NA UFAFANUZI WA MASUALA MENGI YA HIJA, UMRA NA
ZIARA KWA MUJIBU WA MUONGOZO WA QUR'ANI NA SUNNA
Kitabu kinafafanua hukumu za Hija, Umra na Ziara kwa mujibu wa Qur'ani na Sunna, na kinaeleza mambo ya wajibu katika Hija na Umra. Vile vile kinaeleza mambo yaliyokatazwa wakati wa Ihramu na adabu za kuutembelea Msikiti wa Mtume, huku kikihadharisha dhidi ya uzushi (Bid'aa) katika ibada hizi.
MAKOSA YANAYOFANYIKA KATIKA HIJA, UMRAH NA KUTEMBELEA MSIKITI WA MTUME
36 lugha
MAKOSA YANAYOFANYIKA KATIKA HIJA, UMRAH NA KUTEMBELEA MSIKITI WA MTUME
Makosa na ukiukaji unaohusiana na Umra Kwanza: Ukiukaji wa watu na makosa yao katika Ihram 1. Kuacha kufanya ihlaal, kwa kutoinua juu sauti yake mwanzoni mwa kuhirimia ibada aliyokusudia sawa iwe Hija au Umra. Na Sunna: Ni kunyanyua sauti katika hilo.
FATWA ZA HIJA, UMRA NA KUTEMBELEA MSIKITI WA MTUME
22 lugha
FATWA ZA HIJA, UMRA NA KUTEMBELEA MSIKITI WA MTUME
Ambayo yalichaguliwa kutoka katika Mkusanyiko wa Fatwa za Kamati ya Kudumu ya Fatwa katika Ufalme wa Saudi Arabia, huku maswali yakiwa yamefupishwa ili kuendana na kila hali. Kwanza: Majibu (Fatwa) ya kiujumla Swali: Je, inaruhusiwa kwa baba yangu kufanya Umra kwa pesa alizokopa benki? Jibu: Ni lazima kwa anayetaka kuhiji au kufanya Umra kwa niaba yake au kwa niaba ya mtu mwingine achague pesa nzuri kwa ajili ya matumizi katika Hija yake na Umra. Kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mzuri na hakubali isipokuwa yaliyo mazuri tu.
Uislamu ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu Muumba wa dunia na Mwenye kuiendesha dunia, na kujifungamanisha kwake kwa mapenzi na kumtukuza, na msingi wa Uislamu ni kumuamini Mwenyezi Mungu, na kuwa Yeye Mwenyezi Mungu ni Muumbaji, na kila kisichokuwa Mwenyezi Mungu kimeumbwa, na kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anastahiki kuabudiwa peke yake asiye na mshirika, hakuna wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, majina mazuri yote ni yake na sifa za juu zote ni zake, na ni Mwenye ukamilifu wa moja kwa moja bila ya upungufu, hakuzaa wala hakuzaliwa wala hakuna wa kulinganishwa naye wala kufananishwa naye,…