كتاب التوحيد
كتاب التوحيد أحد أهم الكتب في العقيدة الإسلامية، حيث يركز على مفهوم التوحيد وأهميته في الإسلام. يعرض الشيخ في هذا الكتاب أركان التوحيد الثلاثة: توحيد الربوبية، وتوحيد الألوهية، وتوحيد الأسماء والصفات. ويعزز أهمية التوحيد في عبادة الله وحده ونبذ الشرك بجميع صوره وأشكاله. يتميز الكتاب بأسلوبه الواضح والمباشر، مع استشهادات من القرآن الكريم والسنة النبوية لتوضيح المفاهيم. يعد مرجعًا أساسيًا لكل مسلم يسعى لفهم التوحيد بشكل صحيح وتطبيقه في حياته.
Kitabu cha Tauheed {upwekeshaji}
Ambayo ndiyo haki ya ALLAH juu ya waja
Utunzi wa Shekh wa kiislam.
MUHAMMAD IBN ABDUL WAHAAB ATTAMIIMY.
1206H
Kimetiliwa umuhimu na.
Abdul Azizi bin Daakhil Al Mutweyry
Kwa jina la mwenyezi mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu.
Kila sifa njema ni zake ALLAH na sifa za ALLAH ziwe juu MTUME MUHAMMAD na jamaa zake na swahaba wake.
Kitabu cha Tauheed {upwekeshaji}.
Na kauli ya ALLAH Mtukufu: "Na sikuumba majini na binadamu isipokuwa waniabudu mimi Peke Yangu". [Surah Adh-Dhariyat: 56].
Na kauli yake ALLAH: Na hakika tulituma katika kila zama mtume -akiwaambia watu wake- muabuduni ALLAH na mjiepushe na miungu inayo abudiwa kinyume na ALLAH. [Surah An-Nahli: 36].
Na kauli yake ALLAH: Na ameamrisha MOLA wako msimuabudu isipokuwa yeye-ALLAH-na wazazi wawili wafanyiwe wema ima akafikia kwako mmoja wao na utu uzima au wote wawili basi usiseme kuwaambia wao neno la kuwakemea na wala usiwafokee na waambie maneno mazuri na wafunike kwa mbawa za unyenyekevu kutokana huruma na sema MOLA wangu wahurumie kama jinsi walivyo nilie nikiwa mtoto. [Surah Al-israa: 23-24].
Na kauli yake ALLAH: Na Muabuduni ALLAH na msimshirikishe na kitu chochote. [Surah An-Nisaai: 36].
Na kauli yake ALLAH: Sema ewe MUHAMMAD:Njooni niwasomee mambo ambayo aliyo haramisha MOLA wenu Msimshirikishe pamoja nae na kitu chochote na kwa wazazi wawili muwafanyie wema na msiue watoto wenu kutokana na umasikini sisi ndio tunao kupeni riziki nyinyi na wao na wala msikurubie mambo machafu yanayo onekana miongoni mwa hayo mambo machafu na yaliyo jificha na msiue nafsi ambazo ALLAH amekataza zisiuwawe isipokuwa kwa njia ya haki hayo tuliyo kupeni wosia hakika mtapata mazingatio. Na wala msikaribie mali za mayatima isipokuwa kwa zile ambazo ni nzuri mpaka afikie utu uzima na pimeni ujazo na mizani kwa uwadilifu na nafsi haijalazimishwa isipokuwa imefanyiwa wepesi na mtakapo sema fanyeni uwadilifu na hata kama atakuwa ni jamaa wa karibu na kwa ahadi za ALLAH zitekelezeni hayo mliyo pewa wosia ili mpate kukumbuka. Na kwa hakika hii ndio njia yangu iliyo nyooka basi msifuate viji njia njia ikasa sababu ya kuwatenganisha kunako njia ALLAH hayo mliyo pewa wosia ili mpate kumuogopa ALLAH. [Surah A-An'am: 151-153].
Na amesema Ibn Mas'udi: Atakayetaka kutazama katika wosia wa Muhammadi sala na Amani ziwe juu yake ambao ndani yake kuna hitimisho lake basi na asome kauli yake ALLAH Mtukufu: Sema ewe MUHAMMAD njooni niwasomee mambo ambayo aliyo haramisha MOLA wenu juu yenu ni kuto mshirikisha na kitu chochote. Mpaka katika kauli yake ALLAH: Na hakika hii ndio njia yangu iliyo nyooka{UISLAMU}.
Na kutoka kwa Muadhi bin Jabali -Radhi za ALLAH ziwe juu yake- Amesema: "Nilikuwa nimepanda nyuma ya Mtume -sala na Amani ziwe juu yake- juu ya punda, akasema kuniambia: Ewe Muadhi, hivi unajua ni ipi haki za ALLAH juu ya waja, na ni ipi haki za waja juu ya ALLAH? Nikasema: Allah na Mtume wake ndiyo wajuzi, akasema: Haki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja ni kumuabudu yeye na wala wasimshirikishe na chochote, na haki ya waja juu ya ALLAH ni kuto kumuadhibu yule asiyemshirikisha yeye na chochote. Nikasema ewe mjumbe wa ALLAH hivi niwaeleze watu habari hizi njema? Akasema: Hapana usiwaeleze watabweteka. Wameitoa hadithi hii maimamu wawili katika sahihi zao (kitabu: sahihi Bukhari na Muslim}.
Hapa kuna mambo ya msingi:
La kwanza: Hekma ya kuumbwa majini na watu.
La pili: Nikuwa ibada ndiyo upwekeshaji; kwa sababu ogomvi mkubwa uko hapo.
La tatu: Nikuwa ambaye hatolifanya hilo atakuwa hajamuabudu ALLAH, Hivyo ndani yake kuna maana ya kauli yake-mtume-: na wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu.
La nne: Hekma ya kutuma Mitume.
La tano: Nikuwa ujumbe umeukusudia umma mzima.
La sita: Nikuwa dini ya Manabii ni moja.
La saba: Jambo kubwa: Nikuwa ibada ya ALLAH haiwezi kupatikana isipokuwa kwa kukufuru twaghuti (chochote chenye kuabudiwa kinyume ALLAH) hapa kuna maana ya kauli yake ALLAH: Basi yeyote atakaye ipinga miungu inayo abudiwa kinyume na ALLAH na akamuamini ALLAH} Mpaka mwisho wa Aya.
La nane: Twaghuti ni kila kinacho abudiwa kinyume na Allah.
La tisa: Ukubwa wa swala la hizi haya tatu zilizowazi katika Surah An'am kwa wema waliotangulia, Na ndani yake kuna mambo kumi: La kwanza kabisa ni katazo la ushirikina.
La kumi: Aya za wazi katika suratul Israa, na ndani yake kuna mambo kumi na nane; Ameyaanza mambo hayo ALLAH kwa kauli yake: Usijalie pamoja na ALLAH mungu mungine itakuwani sababu ya kukaa hali ya kuwa ni mwenye kusemwa vibayamwenye kufedheheka. Na akahitimisha kwa kauli yake ALLAH: Na usijalie pamoja na ALLAH mungu mungine ikawa nisababu ya ukaja kutiwa ndani ya moto wa Jahanamu hali ya kuwa mi mwenye kulaumiwa mwenye kuwekwa mbali. Na akatutahadharisha ALLAH juu ya ukubwa wa mambo haya kwa kauli yake: Hayo tuliyo kueleza ni miongoni mwa mambo aliyo kufunulia MOLA wako kutokana na hekma.
La kumi na moja: Aya ya surah-An-Nnisaa huitwa kuwa ni aya ya haki kumi alizozianza ALLAH mtukufu kwa kauli yake: Na Muabuduni ALLAH na msimshirikishe na chochote}.
La kumi na mbili: Kuchukua tahadhari juu ya wosia wa Mtume -sala na Amani ziwe juu yake- wakati wa kufa kwake.
La kumi na tatu: Ni kujua haki ya ALLAH mtukufu juu yetu.
La kumi na nne: Kujua haki ya waja juu ya ALLAH pale watakapotekeleza haki zake.
La kumi na tano: Nikuwa maswala haya hawayajui maswahaba wengi.
La kumi na sita: Ruhusa ya kuficha elimu kwa maslahi
La kumi na saba: Inapendeza muislamu kuwa na bishara kwa yale yanayomfurahisha.
La kumi na nane: Hofu ya kubweteka katika upana wa rehma za ALLAH.
La kumi na tisa: Kauli ya muulizwaji katika yale asiyoyajua:Ni kusema ALLAH na Mtume wake ndio wajuzi.
La Ishirini: Kufaa kuwapendelea baadhi ya watu kwa kuwapa elimu pasina kuwapa wengine.
La Ishirini na moja: Unyenyekevu wake -sala na Amani ziwe juu yake- kwa kupanda kwake punda tena kwa kupakizana.
La Ishirini na mbili: Kufaa kupakizana juu ya mnyama.
La Ishirini na tatu: Ubora wa Muadhi bin Jabali.
La Ishirini na nne: Ukubwa wa mambo haya.
MLANGO WA KUBAINISHA UBORA WA TAUHEED{KUPWEKESHA ALLAHAAAA] NA YALE INAYOYAFUTA KATIKA MADHAMBI.
Na kauli yaALLAH Mtukufu: wale ambao walio amini na hawakuchanganya imani yao na ushirikina hao ndio wenye amani na wao ndio walio ongoka. [Al An'am: 82].
Na kutoka kwa Ubada bin Swaamit -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema mtume wa ALLAH -SALA na AMANI ziwe juu yake: "Atakaye kubali ya kwamba hapana MOLA apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa ni ALLAH aliye wa pekee asiye na mshirika na hakika MUHAMMAD ni mtume wake,, na kuwa ISSAH ni mja wa ALLAH na ni mtume wake na neno la kuumbwa kwake ISSAH ALLAH aliliweka kwa MARIAM na kwa kupitia malaika JIBREEL atokae kwake,na pepo ni kweli,na moto ni kweli,ALLAH atamuingiza peponi kwa kiasi atakacho kuwa nacho kutokana na matendo. wameipokea masheikh wawili (Bukhari na Muslim), na pia wana hadithi nyingine katika hadithi ya Utban. Hakika ALLAH amemuharamishia moto yeyote atakayesema 'Laa ilaaha illa llaahu" Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa ALLAH akitafuta kwa neno hilo radhi za ALLAH.
Na kutoka kwa AbI Saidi Al khudriy Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake amesema: Alisema Musa, Ewe Mola wangu nifundishe mimi jambo ambalo nitakutaja na nitakuomba kwalo, Akasema: sema ewe Musa: Laa ilaaha illa llaahu, Akasema: Ewe Mola wangu waja wako wote wanalisema hili, Akasema: Ewe Musa lau mbingu saba na vyote vilivyomo kasoro mimi na ardhi zote saba zikawa katika upande wa mizani, na Laa ilaaha illa llaahu ikawa upande wa pili wa mizani, Laa ilaaha illa llaahu itavizidi vyoye. Kaipokea ibin Hibban na Hakim na akaisahihisha.
Na kwa imamu Tirmidhiy -Na hadithi kaifanya kuwa Hasan- Kutoka kwa Anas: Nilimsikia Mtume -Sala na Amani ziwe juu yake- anasema: Amesema ALLAH Mtukufu: "Ewe mtoto wa ADAMU Hakika wewe lau ungenijia na ujazo wa Ardhi makosa, kisha ukakutana na mimi hali yakuwa huja nishirikishia mimi na chochote, basi ningekujia na msamaha ujazo wake.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Upana wa fadhila za ALLAH.
La pili: wingi wa malipo ya kumpwekesha ALLAH mbele ya ALLAH.
La tatu: Pamoja na hivyo ni kufuta kwake madhambi pia.
La nne: Tafsiri ya aya ambazo ziko katika suratul An'am.
La tano: kuyazingatia mambo matano ambayo yako katika hadithi ya Ubadah.
La sita: Nikuwa utakapoyakusanya kati ya hayo na yaliyoko katika hadithi ya Utban na yale yaliyoko baada yake utaona wazi maana ya kauli ya (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa ni ALLAH) na utaona wazi kosa la waliohadaika.
La saba: Tahadhari katika sharti ambazo ziko katika hadithi ya Itban.
La nane: kuwa hata Manabii wanahitaji kukumbushwa juu ya fadhila za Laa ilaaha illah llaah.
La tisa: Kukumbushwa juu ya-laa ilaah illa ALLAH- kuvishinda kwake viumbe vyote, pamoja nakuwa watu wengi wanaolisema wana daraja duni.
La kumi: Dalili juu ya kuwa mbingu ziko saba kama zilivyo mbingu.
La kumi na moja: Nikuwa mbingu hizo na Ardhi zina wakazi.
La kumi na mbili: Kuthibitisha sifa za Allah, tofauti na madhehebu ya ashairah.
La kumi na tatu: Nikuwa utakapofahamu hadithi ya Anasi utafahamu kuwa kauli yake katika hadithi ya Itban:hakika ALLAH amemuharamishia moto yeyote atakayesema:Laa ilaa illa llaah-Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa ALLAH-akitaraji kwa hilo(uso)radhi za ALLAH"Maana yake ni kuacha ushirikina na si kutamka tu kwa ulimi.
La kumi na nne: Zingatia kukusanywa kati ya kuwa ISSAH na MUHAMMAD ni waja wa Mwenyezi Mungu na Mitume wake.
La kumi na tano: Kutambua kutengwa kwake ISSAH kwakuwa kwake ni neno la ALLAH.
La kumi na sita: Kufahamu kuwa ni roho toka kwake.
La kumi na saba: Kutambua ubora wa kuamini pepo na moto.
La kumi na nane: Ni kufahamu kauli ya mtume: "Kulingana na yale atakayokuwa nayo katika matendo".
La kumi na tisa: kufahamu kuwa Mizani ina pande mbili.
La Ishirini Kufahamu kutajwa kwa uso.
MLANGO ATAKAYE IHAKIKISHA TAUHEED ATAINGIA PEPONI BILA YA HESABU:
Na kauli ya ALLAH Mtukufu: Hakika Ibrāhīm alikuwa kiongozi hali ya kuwa ni mnyenyekevu kwa ajili ya ALLAH hali ya kuwa ni mpwekeshaji na hakuwa ni miongoni mwa washirikina. [An Nahli:120]
Na amesema Allah Mtukufu: Na wale ambao wao kwa MOLA wao si wenye kumshirikisha. [Al Mu'minuun:59]
Na kutoka kwa Huswain bin Abdil Rahman Amesema: Nilikuwa kwa Saidi bin Jubairi, Akasema: Ni nani kati yenu aliyeiona nyota iliyodondoka usiku wa jana? nikasema: mimi, kisha nikasema: ama mimi sikuwa katika swala lakini niling'atwa, Akasema: nini ulifanya? Nikasema: Nilijifanyia kisomo: Akasema ni kipi kilichokupelekea kufanya hivyo? Nikasema: ni hadithi alituhadithia Sha'biy, Akasema: aliwahadithia nini? Nikasema: Alituhadithia kutoka kwa Buraida bin Huswaibi yakuwa yeye alisema: "Hakuna kufanya kisomo (Ruqya) isipokuwa kwa ajili ya kijicho au homa (maumivu), Akasema: Amefanya vizuri aliyeishia pale aliposikia; lakini sisi alituhadithia bin Abbasi kutoka kwa Mtume -Sala na Amani ziwe juu yake yakuwa yeye Amesema: Zilihudhurishwa kwangu umma, nikamuona Nabii akiwa pamoja na kundi na Nabii akiwa na mtu mmoja au wawili, na Nabii akiwa hana mtu mmoja, ghafla likanyanyuliwa giza nene, nikadhania kuwa hao ni umma wangu, nikaambiwa huyo ni Musa na watu wake, nikatazama tena basi ghafla tena nikaona giza nene zaidi, nikaambiwa huu ndiyo umma wako, wakiwa pamoja nao watu elfu sabini wakiingia peponi bila ya hesabu wala adhabu. Kisha akanyanyuka akaingia nyumbani kwake, watu wakazungumza mengi kuhusu watu hao, wakasema baadhi yao: Huenda ni wale walioishi karibu na Mjumbe wa ALLAH -Sala na Amani ziwe juu yake-, na wakasema baadhi yao: Huenda ni wale waliozaliwa katika uislamu na wakawa hawakumshirikisha ALLAH na kitu chochote, na wakataja mambo mengi, akawatokea Mtume -Sala na Amani ziwe juu yake- wakamueleza, Akasema: Ni wale wasiotafuta wa kuwafanyia visomo, na wala hawajitibu kwa moto, na wala hawaamini mikosi, na kwa Mola wao ndiko wanakotegemea. Akasimama Ukasha bin Mihswan akasema: Ewe Mjumbe wa ALLAH muombe Allah anifanye kuwa miongoni mwao, Akasema: "Wewe ni miongoni mwao", kisha akasimama mtu mwingine, akasema: muombe Allah anifanye kuwa miongoni mwao, Akasema: "Amekutangulia kwa hilo Ukasha".
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Kujua daraja za watu katika TAUHEED.
La pili Ni nini maana ya kuihakikisha TAUHEED?
La tatu: ALLAH kumsifia Ibrahim kwa kuwa hakuwa miongoni mwa washirikina.
La nne: Kuwasifia kwake mawalii watukufu kwa kusalimika kwao na ushirikina.
La tano: Nikuwa kuacha kufanyiwa kisomo na kujitibu kwa moto ni katika kuihakikisha TAUHEED.
La sita: Nikuwa linalokusanya mambo hayo yote ni kumtegemea ALLAH.
La saba: Upana wa elimu ya maswahaba kwa kufahamu kwao ya kuwa hawakulipata hilo isipokuwa kwa matendo.
La nane: Pupa yao juu ya mambo ya kheri.
La tisa: Ubora wa umma huu kwa idadi kubwa ya watu na kwa wingi wa matendo na kwa namna.
La kumi: Ubora wa wanafunzi wa Musa.
La kumi na moja: Kuhudhurishwa umma zote kwake Amani iwe juu yake.
La kumi na mbili: Nikuwa kila umma utafufuliwa peke yake pamoja na Nabii wake.
La kumi na tatu: Uchache wa waliowakubali Mitume.
La kumi na nne: Nikuwa ambaye hakukubaliwa na mtu hata mmoja basi atakuja peke yake.
La kumi na tano: Matunda ya elimu hii nikutodanganyika na wingi na kutokuubeza uchache.
La kumi na sita: Ruhusa ya kufanya kisomo (Ruqya) kwa sababu ya kijicho au homa (maumivu).
La kumi na saba: Kina au undani wa elimu ya wema waliotangulia kwa kauli yake: (Amefanya vizuri aliyeishia aliposikia, lakini kadhaa wa kadhaa) ikaonekana kuwa hadithi ya kwanza haipingani na ya pili.
La kumi na nane: Kuwa mbali wema waliotangulia na swala la kumsifu mtu kwa mambo ambayo hana.
La kumi na tisa: Kauli yake: "Wewe ni miongoni mwao" Hii ni alama miongoni mwa alama za Utume.
La Ishirini Ubora wa Ukasha.
La Ishirini na moja: Kutumia vifaa vya kuonyeshea.
La Ishirini na mbili: Uzuri wa tabia yake -Sala na Amani ziwe juu yake-.
Mlango wa kuhofia ushirikina.
Na kauli ya ALLAH Mtukufu: "Hakika ALLAH hafuti Madhambi ya kushirikishwa naye, na anafuta madhambi kinyume na ushirikina kwa anayemtaka. [Al- nisaa :48]
Na alisema Al Khalili (Ibrahim) Amani iwe juu yake: "Na uniepushe mimi na wanangu tusije kuabudu masanamu". [Ibrahim: 35]
Na katika hadithi: "Ninaloliogopea zaidi kwenu nyinyi ni shirki ndogo", Akaulizwa kuhusu hilo, Akasema: ni "Riyaa" (kujionyesha).
Na kutoka kwa bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Atakayekufa naye akiomba kinyume na ALLAH mshirika, ataingia motoni" Imepokelewa na Al-Bukhaariy Na kwa Imamu Muslim kutoka kwa Jaabir bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Atakayekutana na ALLAH hali yakuwa hamshirikishi na chochote ataingia peponi, na atakaye kutananaye hali yakuwa anamshirikisha na chochote ataingia motoni".
Hapa kuna mambo mawili:
La kwanza: kuhofia ushirikina
La pili Nikuwa kujionyesha ni katika ushirikina.
La tatu: Nikuwa ni katika shirki ndogo.
La nne: kuwa ni jambo linalo ogopewa zaidi kwa watu wema.
La tano: Ukaribu wa pepo na moto.
La sita: Kukusanywa baina ya ukaribu wake katika hadithi moja.
La saba: Nikuwa atakayekutana naye ALLAH hali yakuwa hamshirikishi na chochote ataingia peponi, na atakayekutana naye hali yakuwa anamshirikisha na chochote ataingia motoni hata kama atakuwa ni mchamungu kuliko watu wote.
La nane: Swala kubwa ni kuomba kwa kipenzi wa ALLAH Ibrahim yeye mwenyewe na kwa watoto wake kinga ya kutoabudu masanamu.
La tisa: Alisema hivyo kwa kuzingatia hali ya watu wengi kwa kauli yake: "Mola wangu hakika wao wamewapoteza watu wengi"
La kumi: Hapa kuna tafsiri ya -Laa ilaaha illa llaah- kama alivyoeleza Bukhariy.
La kumi na moja: Ubora wa atakayesalimika na ushirikina.
Mlango wa kuwaita watu katika kushuhudia kuwa Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa ALLAH.
Na amesema ALLAH Mtukufu: Sema ewe MUHAMMAD hii ndio njia yangu ninayo itia kwa ALLAH juu ya utambuzi mimi na atakaye nifuata na utakasifu wa ALLAH na sikuwa mimi ni miongoni mwa washirikina. [Yusuf: 108].
Kutoka kwa bin Abbasi -Radhi za ALLAH ziwe juu yao- yakwamba Mtume -Sala na Amani ziwe juu yake- alipomtuma Muadhi kwenda Yemen alisema kumwambia: "Hakika wewe unawaendea watu waliopewa kitabu, basi na liwe jambo la mwanzo utakalowaita kwalo ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa ALLAH" na katika upokezi "Mpaka wampwekeshe ALLAH-, ikiwa wao watakuitikia katika hilo, basi wajulishe kuwa ALLAH amewalazimisha juu yao swala tano katika kila usiku na mchana, ikiwa wao watakubali kwa hilo, basi wajulishe kuwa ALLAH amewalazimisha juu yao sadaka, zinachukuliwa kutoka kwa matajiri wao, na kurejeshwa kwa masikini wao, ikiwa wao watakubali kwa hilo, basi tahadhari na mali zao za thamani, na ogopa sana maombi ya mwenye kudhulumiwa, kwani hayo hayana kati yake na ALLAH kizuizi". Wameitoa hadithi hii Maimamu wawili.
Na wamepokea wawili hao kutoka kwa Sahli bin Sa'di: Hakika Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema siku ya vita vya Khaibar: "Nitampa bendera kesho mtu ambaye anampenda Allah na Mtume wake, na anapendwa na Allah na Mtume wake, kupitia yeye Allah ataleta ushindi". Watu wakalala usiku kucha wakinong'ona, ni nani kati yao atakayepewa, palipopambazuka walikwenda mapema kwa Mtume -Sala na Amani ziwe juu yake-, kila mmoja kati yao akitaraji kupewa yeye, Akasema: "Yuko wapi Ally bin Abii Twaalib?".
Wakasema: Anasumbuliwa na macho, akaagiza akaletwa, akamtemea machoni mwake na akamuombea dua, basi akapona, kana kwamba hakuwa na maumivu yoyote, akampatia bendera, Akasema: "Nenda kwa nidhamu mpaka ushuke uwanjani kwao, kisha uwaite katika uislamu, na uwaeleze yaliyoyawajibu juu yao katika haki za ALLAH Mtukufu, Basi Namuapa ALLAH ikiwa atakuongozea ALLAH mtu mmoja hilo ni bora zaidi kwako kuliko Ngamia mwekundu".
(Wakinong'ona) Yaani: wakijadili.
Hapa kuna mambo mawili:
La kwanza: Hakika kuwaita watu kwa ALLAH ni njia ya yule aliyemfuata Mtume Sala na Amani ziwe juu yake.
La pili: Tahadhari juu ya swala kutakasa nia (ikhlaswi), kwa sababu watu wengi hata kama analingania katika haki utakuta analingania kwa ajili ya maslahi ya nafsi yake.
La tatu: kuwa na elimu ni katika mambo ya lazima.
La nne: Katika alama za uzuri wa kumpwekesha ALLAH ni pale inapokuwa ni kumtakasa ALLAH kutokana na matusi.
La tano: Nikuwa katika ubaya wa ushirikina nikuwa; ni matusi kwa ALLAH.
La sita: Nalo ni jambo muhimu sana: kuwatenga mbali waislamu na washirikina; ili wasijekuwa miongoni mwao hata kama hawajafanya ushirikina.
La saba: Nikuwa TAUHEED ndiyo wajibu wa kwanza.
La nane: Ndiyo hutangulizwa kabla ya kila kitu hata swala pia.
La tisa: Nikuwa maana ya (Mpaka wampwekeshe ALLAH) ndiyo maana ya kushuhudia kuwa Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa ni ALLAH.
La kumi: Nikuwa mtu anaweza kuwa ni katika Mayahudi au wakristo, hali yakuwa hajui au anajua lakini hafanyii kazi.
La kumi na moja: Tahadhari juu ya kuwafundisha watu kwa hatua.
La kumi na mbili: Kuanza na lenye umuhimu zaidi kisha linalofuata.
La kumi na tatu: Mgao wa zaka.
La kumi na nne: Msomi anatakiwa Kumuondolea utata mwenye kujifunza.
La kumi na tano: Katazo kuhusu mali za watu za thamani.
La kumi na sita: Kuogopa maombi ya mwenye kudhulumiwa.
La kumi na saba: Tumeelezwa kuwa hayazuiliwi.
La kumi na nane: Katika alama za Tauhidi ni yale yaliyotokea kwa bwana wa Mitume,bwana wa mawalii wema miongoni mwa shida, na njaa, na maradhi.
La kumi na tisa: Kauli yake: "Hakika nitampa bendera" mpaka mwisho, hii ni alama miongoni mwa alama za utume.
La Ishirini Kutema kwake machoni mwake ni alama miongoni mwa alama za utume pia.
La Ishirini na moja: Ubora wa Ally Radhi za Allah ziwe juu yake
La Ishirini na mbili: Ubora wa maswahaba katika kukesha kwao usiku kucha, na kushughulishwa kwao na swala la ufunguzi.
La Ishirini na tatu: Kuamini makadirio ya ALLAH kwa kuipata bendera hiyo mtu ambaye hakuikimbilia na kutopewa wale walioipupia.
La Ishirini na nne: Adabu katika kauli yake: (Tembea kwa nidhamu).
La Ishirini na tano: kuwalingania watu katika uislamu kabla ya vita.
La Ishirini na sita: Nikuwa ni sheria kwa watakaolinganiwa kabla ya hapo kupigwa.
La Ishirini na saba: kulingania kwa hekima kwa kauli yake: (Waeleze yale yaliyowajibu juu yao).
La Ishirini na nane: Kutambua haki za ALLAH katika uislamu.
La Ishirini na tisa Malipo ya mtu ambaye ataongoka mtu mmoja kupitia mikononi mwake.
Thelathini Kuapa wakati wa kutoa majibu.
MLANGO WA TAFSIRI YA TAUHEED NA KUKUBALI HAKUNA APASAYE KUABUDIWA KWA HAKI ISIPOKUWA NI ALLAH.
Na kauli yake ALLAH Mtukufu: "Hao ambao-washirikina wanawaomba miongoni mwa Manabii na watu wema na Malaika -wao wenyewe wanashindana kujiweka karibu na Mola wao-kwa matendo mema wanayoyaweza-wanatarajia rehma zake na wanaogopa adhabu zake hakika adhabu ya Mola wako zamekuwa ni zenye kuchukuliwa tahadhari. [Al Israai: 57].
na kauli yake ALLAH mtukufu: Na pindi aliposema IBRAHIM kumwaambia baba yake na watu wake hakika mimi nimejiweka mbali kutokana na mnayo yaabudu. Isipokuwa yule ambaye aliye niumba hakika yeye ataniongoza. na akalifanya neno hilo ni lenye kubakia baada yake huwenda wao wakarejea. [Azzukhruf: 26-28]
na kauli yake ALLAH: wamewafanya wanazuoni wao ni miungu kinyume na ALLAH pia walimfanya MASIHI ISSAH mwana wa Maryam kuwa ni mungu na hawakuamrishwa isipokuwa wao wamuabudu mungu mmoja hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa ni yeye ametakasika na yote wanayo mshirikisha. [At Tauba: 31].
na kauli yake ALLAH: Na kuna miongoni mwa watu wapo wanao jifanyia kinyume na ALLAH miungu mingine wakiwapenda kama mapenzi ya kumpenda ALLAH na wale ambao walio amini wana mapenzi makubwa ya kupenda ALLAH. [Baqara: 165].
Na katika sahihi (Bukhari) kutoka kwa Mtume -sala na Amani ziwe juu yake- ya kwamba yeye Amesema: Atakaye sema laa ilaha illa ALLAH na akapinga yote yanayo abudiwa kinyume na ALLAH imeharamishwa mali zake na kumwaga damu yake,na hesabu zake zipo juu ya ALLAH MTUKUFU.
Na ufafanuzi wa tafsiri hizi ni milango inayofuata baada yake.
Ndani yake kuna swala kubwa na la muhimu kuliko yote, nalo ni:
Tafsiri ya TAUHEED na tafsiri ya SHAHADA, na akayabainisha mambo haya mawili kwa mambo yaliyo wazi:
Miongoni mwayo ni aya ya suratul Israa, amebainisha ndani yake kuwajibu washirikina wale wanaowaomba watu wema, hapa kuna uwazi kuwa hii ndiyo shirki kubwa.
Na miongoni mwake ni aya ya suratu Baraa (Tauba) Amebainisha ndani yake kuwa Mayahudi na Manaswara wamewafanya wasomi wao na watawa wao kuwa ni miungu kinyume na ALLAH, Na akabainisha kuwa wao hawakuamrishwa isipokuwa ni kumuabudu Mungu mmoja, pamoja nakuwa tafsiri yake ambayo haina shaka ndani yake ni kuwatii wanavyuoni na viongozi wa dini katika yale yasiyomuasi ALLAH, na wala si kuwaomba wao.
Na miongoni mwake ni kauli ya kipenzi Ibrahim Amani iwe juu yake- kuwaambia makafiri: "Hakika mimi niko mbali mno na yale mnayoyaabudu" [26] "Isipokuwa yule aliyeniumba" Akawaondoa wale wenye kumuabudu Mola wake.
Na akaeleza ALLAH Mtukufu kuwa huku kujiweka mbali na huku kuwatawalisha ndiyo tafsiri ya -Laa ilaaha illa llaah- Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa ni ALLAH,Akasema: Na alilifanya neno la kumpwekesha ALLAH (Lā ilāha illā Allāh) ni lenye kusalia baada yak ili wapate kurejea.
Na miongoni mwake ni aya ya suratul Baqara kuhusu makafiri ambao alisema Mwenyezi Mungu kuhusu wao: "Na wao hawatotoka motoni" Ameeleza kuwa wao wanaipenda hiyo miungu kama wanavyompenda ALLAH,Hili limeonyesha kuwa wao wanampenda Mtume mapenzi makubwa, lakini hilo halikuwaingiza katika uislamu, ni vipi atakayeipenda miungu mapenzi makubwa kuliko hata ALLAH?!
Na vipi ambaye hatopenda chochote isipokuwa hii mizimu pekee na akawa hajampenda ALLAH?.
Na miongoni mwake ni kauli ya Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake: "Atakayesema: Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa ALLAH na akayapinga yanayoabudiwa kinyume na ALLAH, ni haramu mali yake, na damu yake, na hesabu yake ni juu ya ALLAH"
na hili ni kutokana na jambo kubwa ambalo linabainisha maana ya{ laa ilaha ilaa ALLAH}hakika neno hilo halikuajalia kutamka neno hilo ni kinga kwa damu na mali ,bali hata kufahamu maana yake pamoja na kulitamka ,bali hata kulikubali,bali hata kuwa kwake haombi isipokuwa ALLAH peke yake asiye na mshirika,bali hata isipo haramishwa mali zake na damu yake mpake ionganishwe na ule ukafiri kwa yale yanayo abudiwa kinyume na ALLAH ,na kama atakuwa na mashaka au akasita haita haramishwa mali zake na damu yake ,ubora ulioje wa neno hilo{laa ilaha ilaa ALLAH}kutokana na mambo ukubwa na utukufu ulioje wa neno hilo!.
Na ni ubainifu mzuri ulioje! Na ni ufafanuzi mzuri ulioje! na ni uzuri ulioje wa hoja za kukata mzozo?!
MLANGO ULIO KUJA KUBAISHA UBAYA WA USHIRIKINA KUVAA BANGILI NA KAMBA NA MFANO WAKE KWA AJILI YA KUONDOA MATATIZO AU KUZUIA.
Na kauli ya ALLAH Mtukufu: Sema ewe MUHAMMAD mwaonaje ambayo mnayo yaomba kinyume na ALLAH kama akinikusudia ALLAH kunipa madhara hivi hiyo miungu yenu ni yemye kuondosha madhara ya ALLAH au akinikusudia allah kunipa rehma hivi hiyo miungu ni yenye kuzuia rehma za ALLAH sema ewe MUHAMMAD anitosha ALLAH juu yake wanategemea wenye kutegemea. [Azzumar: 38]
Kutoka kwa Imrani bin Huswain -Radhi za ALLAH ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Sala na Amani ziwe juu yake- alimuona mtu mmoja mkononi mwake kuna bangili la shaba, Akasema: "Nini hiki?" Akasema: Ni kwa ajili ya ugonjwa: "Livue kwani hilo halikuzidishii isipokuwa maradhi, kwani laiti ungelikufa nalo likiwa kwako usingefaulu milele" Kaipokea imamu Ahmadi kwa isnadi isiyokuwa na tatizo.
Na amepokea pia kutoka kwa Uqba bin Aamiri hadithi Marfu'u: "Atakayetundika (moyo wake) katika hirizi basi ALLAH hatomtimizia, na atakayetundika konokono ALLAH hatomuacha salama". Na katika upokezi: (Atakayetundika hirizi basi atakuwa kafanya ushirikina)
Na imepokelewa kwa bin Abii Hatim kutoka kwa Hudhaifa yakwamba yeye alimuona mtu mkononi mwake kukiwa na kamba kama kinga ya homa, akaikata na akasoma kauli yake: Na si wengi wao ni wenye kumuamini ALLAH isipokuwa ni washirikina. [Yusuf: 106].
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Kutiwa uzito katika kuvaa bangili na kamba na mfano wake kwa mfano kama huo.
La pili: Nikuwa swahaba lau kama angelikufa nalo likiwa kwake basi asingefaulu, hapa kuna ushahidi wa maneno ya swahaba kuwa shirki ndogo ni katika madhambi makubwa.
La tatu: Nikuwa yeye hakupewa udhuru wa ujinga.
La nne: Nikuwa hilo halimnufaishi katika maisha yake, bali linamdhuru kwa kauli yake: (Halikuzidishii isipokuwa maradhi).
La tano: Kukemewa kwa nguvu kwa atakayefanya mfano wa hilo.
La sita: Ni Wazi kuwa Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho.
La saba: Ni wazi kuwa Atakayetundika hirizi basi atakuwa kafanya ushirikina.
La nane: Nikuwa kutundika kamba kwa sababu ya maradhi ni miongoni mwa hilo lililokatazwa.
La tisa: Kusoma Hudhaifa Aya ni dalili kuwa maswahaba wanatoa ushahidi wa aya ambazo ni za shirki kubwa juu ya shirki ndogo, kama alivyoeleza bin Abbas katika aya ya Baqara.
La kumi: Nikuwa kutundika konokono kwasababu ya kijicho ni sehemu katika hilo la ushirikina.
La kumi na moja: Dua mbaya kwa atakayetundika hirizi kuwa ALLAH asimtimizie,na atakayetundika konokono basi ALLAH asimuache salama.
MLANGO ULIO KUJA KUELEZEA RUQYA NA HIRIZI.
Katika sahihi (Bukhari) kutoka kwa Abii Bashiri Al Answariy Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: yakwamba yeye alikuwa pamoja na Mtume Sala na Amani ziwe juu yake katika baadhi ya safari zake, akatuma mjumbe: "Ahakikishe kusibakie katika shingo za Ngamia kengele inayofungwa kwa ajili ya kijicho, au kifungo chocho ila kimekatwa".
kutoka kwa bin Mas'udi Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Hakika ruqya-za kishirikina- na mahirizi na limbwata ni ushirikina." Kaipokea Ahmad na Abuu daud.
Hirizi: Ni kitu kinachotundikwa kwa watoto kwa ajili ya kinga ya kijicho, lakini ikiwa kilichotundikwa kimetokana na Qur'ani waliruhusu baadhi ya wema waliotangulia, na baadhi yao hawakuruhusu, na wamelifanya kuwa ni katika mambo yaliyokatazwa, miongoni mwao ni bin Mas'udi Radhi za ALLAH ziwe juu yake.
Na Ruqya za kishirikina ni zile zinazoitwa maazima, na sheria ikaondoa ruqya katika uharamu kwa muda ambao kutakuwa hakuna ushirikina, kwani hayo aliyaruhusu Mtume Sala na Amani ziwe juu yake kwa atakayepatwa na kijicho au homa.
Limbwata: Ni kitu wanachokitengeneza wakidai kuwa kinamfanya mwanamke apendeke kwa mume wake na mwanaume kwa mke wake.
Na kutoka kwa Abdillah bin Ukaim Hadithi Mrfu'u: "Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho" Ameipokea Ahmad na Attirmidhiy.
Na amepokea Imamu Ahmad kutoka kwa Ruwaifiy Amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume Sala na Amani zimfikie: "Ewe Ruwaifiy huenda maisha yatakuwa marefu kwako, basi waambie watu kuwa yeyote atakayezifunga ndevu zake, au akavaa kamba ya upinde, au akastanji kwa kinyesi cha wanyama au mfupa, basi hakika Muhammadi yuko mbali naye".
Na kutoka kwa Saidi bin Jubairi Amesema: "Atakayekata hirizi kutoka kwa mtu yeyote atakuwa na malipo sawa na kuacha huru mtumwa" kaipokea Wakii.
Na pia Kutoka kwa Ibrahim Amesema: "Walikuwa wakizichukia kombe zote, zilizotokana na Qur'ani na zisizokuwa za Qur'ani".
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya ruqya za kishirikina na mahirizi.
La pili: Tafsiri ya limbwata.
La tatu: Nikuwa mambo haya matatu yote ni katika shirki bila kubagua lolote.
La nne: Nikuwa kufanya kisomo kwa maneno ya haki kwa ajili kuondoa kijicho na homa si katika hayo.
La tano: Nikuwahi hirizi itakayo andikwa kutokana na Qur'ani wametofautiana wanachuoni je linaingia katika hayo au la?
La sita: Nikuwa kutundika kamba za upinde juu ya wanyama kwa sababu ya kijicho ni sehemu katika hilo la ushirikina.
La saba: Ahadi ya adhabu kali kwa atakayetundika kamba kama hizo.
La nane: Ubora wa malipo ya atakayekata hirizi kutoka kwa mtu yeyote.
La tisa: Nikuwa maneno ya Ibrahim hayapingani na maneno yaliyotangulia; kwa sababu makusudio yake ni watu wa Abdallah bin Mas'udi.
MLANGO ULIO KUJA KUELEZEA UBAYA WA YULE ATAKE TAKA BARAKA KWENYE MITI AU MAWE NA MFANO WAKE.
Na amesema ALLAH Mtukufu: Mwaonaje mungu lata na uza. Na mungu manata akiwa ni watatu miongoni mwao. je nyie mnao watoto wa kiume na yeye ALLAH anao wa kike.ametukuka ALLAH kutokuwa na mtoto wala mke. Hicho ni kigawanyo cha kidhalimu. hayakuwa hayo isipokuwa ni majina mmewaita nyinyi na baba zenu mambo ambayo ALLAH hakuteremsha hoja na hawana wanachao kifuata isipokuwa ni dhana na yale yanayo pendwa na nafsi zao na hakika walijiliwa kutika kwa MILA wao uwongofu. [An Najm: 19-23].
Na kutoka kwa Abuu Waaqid Al laithiy Amesema: "Tulitoka pamoja na Mtume Sala na Amani ziwe juu yake kwenda katika vita vya Hunain, na sisi tukiwa ni wageni hatuna muda mrefu tangu kutoka katika ukafiri, na washirikina wakawa wana mti wa mkunazi ambao wanauzunguka kwa ibada na wanatundika hapo silaha zao, Mti huo ukiitwa (Dhaata anwaatwi) Yaani mahali pa kutundikia, Tukaupita mti mwingine wa mkunazi nasi tukasema: Ewe Mjumbe wa ALLAH, tuwekee na sisi mahala pa kutundikia kama wao walivyo na mahala pa kutundikia, akasema Mtume Sala na Amani ziwe juu yake: "Allaahu Akbar hakika huo ni mfumo, Mlichosema namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake kama walivyosema wana wa Israeli kumwambia Musa: "Tuwekee nasi mungu kama ambavyo wao wana mungu akasema: hakika nyinyi ni watu msioelewa" [Al A'raf: 138] Hakika bila shaka mtafuata mfumo wa wale waliokuwa kabla yenu" Kaipokea Tirmidhiy na akaisahihisha.
Hapa kuna mambo mawili:
La kwanza: Tafsiri ya aya za suratun najim.
La pili: Kufahamu uhalisia wa jambo waliloliomba.
La tatu: Nikuwa hawakulifanya.
La nne: Nikuwa lengo lao walikusudia kujiweka karibu na ALLAHkwa hilo kwa dhana zao kuwa analipenda.
La tano: Nikuwa kitendo cha wao kutolijua hilo basi kwa wengine ndio zaidi.
La sita: Nikuwa wana mema na ahadi ya msamaha ambao hauko kwa watu wengine.
La saba: Nikuwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake hakuwapa udhuru bali aliwajibu kwa kusema: "Allaahu Akbar hakika huo ni mfumo, hakika bila shaka mtafuata mfumo wa wale waliokuwa kabla yenu" Jambo hili akalifanya kuwa zito kwa mambo haya matatu.
La nane: jambo kubwa -Nalo ndilo linalokusudiwa- Nikuwa yeye alieleza kuwa ombi lao ni kama ombi la wana wa Israeli waliposema kumwambia Musa: Hebu tufanyie sisi mungu.
La tisa: Nikuwa kulikanusha hili ni katika maana za(Laa ilaaha illa llaah)Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa ALLAH,pamoja na undani wake na kufichikana kwake kwa hao.
La kumi: Nikuwa yeye ameapa juu ya jibu alilolitoa, na yeye hua haapi isipokuwa kwa masilahi.
La kumi na moja: Nikuwa shirki iko kubwa na ndogo; kwa sababu hawakuritadi kwa hilo.
La kumi na mbili: Kauli yao: (Nasi tukiwa wageni tangu kutoka katika ukafiri) hapa pana maanisha kuwa watu wengine hawawezi kushindwa kulijua hilo.
La kumi na tatu: Kumtukuza ALLAH wakati wa mshangao, na hii ni tofauti na mtu anayelichukia hili.
La kumi na nne: Kuziba njia za kupelekea katika ushirikina.
La kumi na tano: Katazo la kujifananisha na watu wajinga.
La kumi na sita: Kukasirika wakati wa kufundisha.
La kumi na saba: Kanuni kuu na ya kiujumla kwa kauli yake: "Hakika huu ni mfumo"
La kumi na nane: Nikuwa hii ni alama katika alama za utume kwakuwa imetokea kama alivyoeleza.
La kumi na tisa: Nikuwa yote aliyowakataza ALLAH Mayahudi na Manaswara ndani ya Qur'ani pia ni makatazo kwetu.
La Ishirini Nikuwa inajulikana kwao kuwa ibada zote msingi wake ni maamrisho, hapa kukawa na tahadhari juu ya maswali ya kaburini, ama swali (Nani Mola wako?) Hili liko wazi, Na ama (Ni nani Nabii wako?) Haya ni katika kueleza kwake habari za mambo ya ghaibu (yaliyofichikana) Na ama (Ni ipi dini yako?) ni katika kauli yao: {Tufanyie sisi mungu} mpaka mwisho.
La Ishirini na moja: Nikuwa utaratibu wa Mayahudi na Maswara ni mbaya ni kama utaratibu wa washirikina.
La Ishirini na mbili: Nikuwa mwenye kuhama kutoka katika kile ambacho moyo wake ulikizoea haaminiki katika moyo wake kukosa chembe ya mazoea yake; kwa kauli yao: Nasi tukiwa wageni tangu kutoka katika ukafiri.
MLANGO ULIO KUJA KUELEZEA UBAYA WA KUCHINJA KWA ASIYE KUWA ALLAH.
Na amesema ALLAH Mtukufu: Sema ewe MUHAMMAD hakika swala zangu na vichinjwa vyangu na uhai wangu na kifo changu vyote ni kwa ajili ya ALLAH MOLA wa viumbe. Asiye kuwa na mshirika na kwa hayo nimeamrishwa na mimi ni wa mwanzo miongoni mwa waislamu. {Suratul An-am 162-163}
na kauli yake Mtume: Basi omba kwa ajili ya mola wako na uchinje. [Al kauthar: 2].
"kutoka kwa Ally bin Abii Twaalib Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake kwa maneno manne: ALLAH amemlaani atakayechinja kwa asiyekuwa ALLAH,ALLAH amemlaani mwenye kuwalaani wazazi wake, ALLAH amemlaani mwenye kumuhami mzushi,ALLAH amemlaani ambaye atakaebadilisha mipaka ya ardhi. Imepokelewa na Imamu Muslim
Na kutoka kwa Twaariq bin Shihabi Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Aliingia peponi mtu mmoja kwa sababu ya nzi na aliingia motoni mtu mmoja kwa sababu ya nzi".
Wakasema: Kwani ilikuwaje ewe mtume wa ALLAH?
Akasema: "Walipita watu wawili katika jamii ya watu waliokuwa na sanamu ambalo halivuki yeyote mpaka ajikurubishe kwa samu hilo kwa chochote.
Wakasema kumwambia mmoja wao: Toa.
Akasema: Hapa sina chochote cha kutoa.
Wakamwambia: Toa walau hata nzi, akatoa nzi wakamfungulia njia, ikawa ni sababu ya kuingia motoni.
Na wakasema kumwambia mwenzie: Toa.
Akasema: Siwezi kutoa kafara kwa yeyote asiyekuwa ALLAH Mtukufu, wakamuua, akaingia peponi" Imepokelewa na Ahmad
Hapa kuna mambo mawili:
La kwanza: Tafsiri ya aya {Hakika swala yangu na kuchinja kwangu}
La pili Tafsiri ya "Basi, mtakasie Mola wako ibada yako yote na uchinje mnyama wako kwa ajili Yake, Peke Yake, pamoja na kutaja jina Lake".
La tatu: Kuanza kwa kumlaani atakayechinja kwa ajili ya asiyekuwa ALLAH.
La nne: Kulaaniwa mwenye kuwalaani wazazi wake wawili, na miongoni mwake ni wewe kumlaani mzazi wa mtu mwingine naye akamlaani mzazi wako.
La tano: kulaaniwa kwa mwenye kumuhami mzushi: naye ni mtu anazusha jambo ambalo ni wajibu ndani ya haki za ALLAH,kisha akategemea kwa atakae msaidia kufanikisha jambo hilo.
La sita: Kulaaniwa mwenye kubadili mipaka ya ardhi: Navyo ni vigingi vinavyotenganisha kati ya haki yako na haki ya jirani yako katika ardhi; ukavibadilisha kwa kuvisogeza mbele au nyuma.
La saba: Tofauti kati ya kumlaani mtu maalumu na kuwalaani watenda maasi ni kwa njia ya ujumla.
La nane: Hiki ni kisa kikubwa nacho ni kisa cha nzi.
La tisa: nikuwa aliingia motoni kwa sababu ya nzi huyo ambaye wala hakukusudia bali alifanya tu ili kujiepusha na shari yao.
La kumi: Kufahamu kiwango cha shirki katika nyoyo za waumini, ni jinsi gani alivyoweza kuvumilia juu ya kifo na hakukubaliana nao katika ombi lao pamoja nakuwa hawakumtaka isipokuwa kufanya matendo ya nje tu.
La kumi na moja: Nikuwa aliyeingia motoni ni muislamu; kwa sababu laiti angelikuwa kafiri basi asingesema: (Aliingia motoni kwa ajili ya nzi)
La kumi na mbili: Kuna ushahidi wa hadithi sahihi: "Pepo iko karibu na mmoja wenu kuliko hata kisigino cha kiatu chake, na moto mfano huo huo".
La kumi na tatu: Ni kujua kuwa moyo ndio unaokusudiwa sana mpaka hata kwa waabudu masanam.
MLANGO ULIO KUJA KUELEZEA HAKUNA KUCHINJA KWA AJILI YA ALLAH KATIKA SEHEMU HUCHINJWA KWA ASIYE KUWA ALLAH.
Na amesema ALLAH Mtukufu Usisimame ndani yake milele hakika msikiti ulio asisiwa kwa kumcha ALLAH toka siku ya mwanzo ndio una haki ya kusimama ndani yake ndani yaka kuna watu wanapenda kusafishwa. [Attauba: 108]
Kutoka kwa Thabit bin Dhahaku Radhi za ALLAH ziwe juu yake Amesema: (Aliweka nadhiri mtu mmoja ya kuchinja Ngamia maeneo ya Buwana, akamuuliza Mtume Sala na Amani ziwe juu yake Akasema: "Je kulikuwa na sanamu lolote hapo katika masanamu ya enzi za ujinga likiabudiwa"
Wakasema: Hapana.
Akasema: "Je kulikuwa na sherehe yoyote miongoni mwa sherehe zao?"
Wakasema: Hapana! Akasema Mtume wa Allah Sala na amani za Allah ziwe juu yake: "Timiza nadhiri yako, kwani hakuna kutimiza nadhiri katika kumuasi ALLAH, na wala hakuna kutimiza katika yale asiyoyamiliki mwanadamu" kaipokea Abuudaudi, na isnadi yake ipo kwa shart zao.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya kauli yake: {Usimame hapo milele}.
La pili Nikuwa maasi yanaweza kuathiri katika ardhi. Na hivyo hivyo utiifu.
La tatu: Kuyarudisha maswala yenye utata katika maswala ya wazi ili utata uondoke.
La nne: Mfundishaji kuuliza maswala anapohitaji kufanya hivyo.
La tano: Nikuwa kutenga eneo kwa ajili ya nadhiri inafaa patakapokuwa hakuna vikwazo.
La sita: Kukatazwa ikiwa kuna sanamu katika masanamu ya zama za ujinga hata kama limekwisha ondoshwa.
La saba: Kukatazwa kukiwa na sikukuu miongoni mwa sikukuu hata kama baada ya kuondolewa.
La nane: Nikuwa haifai kutimiza nadhiri alizoziweka katika maeneo kama hayo; kwani hiyo ni nadhiri ya kumuasi Mwenyezi Mungu.
La tisa: Kutahadhari na kujifananisha na washirikina katika sikukuu zao hata kama mtu hajakusudia kufanya hivyo.
La kumi: Hakuna nadhiri katika maasi
La kumi na moja: Hakuna nadhiri kwa mwanadamu katika yale asiyoyamiliki.
MLANGO ULIO KUJA KUELEZA UBAYA WA USHIRIKINA KUTIA NADHIRI KWA ASIYE KUWA ALLAH.
Na amesema ALLAH Mtukufu: Wanatakeleza nadhiri na wanaogopa siku ambayo shari zake ni zenye kuendelea. [Al In saan:7]
na kauli yake ALLAH: Na mnacho kitoa katika mnavyo vitoa au mkatia nadhiri miongoni mwa nadhiri hakika ALLAH anajua. [Al Baqara]
Na katika sahihi kutoka kwa Aisha -Radhi za ALLAJ ziwe juu yake -kwamba Mtume wa ALLAH-Sala na Amani ziwe juu yake- amesema: "Aliyeweka nadhiri ya kumtii ALLAH basi na afanye, na aliyeweka nadhiri ya kumuasi ALLAH basi na asifanye".
Hapa kuna mambo mawili:
La kwanza: Ulazima wa kutimiza Nadhiri.
La pili Kwakuwa imethibiti kuwa ni ibada basi kuipeleka kwa asiyekuwa ALLAH ni ushirikina.
La tatu: Nikuwa nadhiri ya maasi haitakiwi kuitimiza.
MLANGO ULIO KUJA KUELEZA MIONGONI MWA USHIRIKUNA NI KUTAKA MSAADA KWA ASIYE KUWA ALLAH.
Na amesema ALLAH Mtukufu: Ni kwamba kulikuwako wanamume miongoni mwa watu wakijikinga kwa wanamume kutokana na majini wakawazidishia hofu. [Al jinni: 6]
kutoka kwa Khaula bint Hakim Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake akisema: Atakayeshuka mahala popote kisha akasema: -A'udhu bikalimaati llaahit taammaati min sharri maa khalaqa- (Najilinda kwa maneno ya ALLAH yaliyotimia, kutokana na shari ya vile alivyoviumba), hakitomdhuru chochote mpaka aondoke mahala pake hapo" Imepokelewa na Imamu Muslim
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya za suratul Jinni.
La pili Nikuwa ni katika ushirikina
La tatu: Kutoa ushahidi juu ya hilo kwa hadithi; kwa sababu wanachuoni hutoa ushahidi kwa hilo kuwa maneno ya ALLAH hayakuumbwa, wakasema: kwa sababu kutaka kinga kwa kiumbe ni shirki.
La nne: Ubora wa dua hii pamoja na ufupi wake.
La tano: Nikuwa kitu kikisababisha kupatikana manufaa ya kidunia kama kuzuia shari au kuleta manufaa haimaanishi kuwa si ushirikina.
MLANGO ULIO KUJA KUELEZA MIONGONI MWA SHIRKI NI KUTAKA KUOKOLEWA KWA ASIYE KUWA ALLAH AU KUMUOMBA ASIYE KUWA ALLAH.
Na amesema ALLAH Mtukufu: Na wala usiombe kinyume na ALLAH kitu ambacho hakitakudhuru wala kukunufaisha kama utafanya hivyo wakati huwo utakuwa miongoni mwa watu madhalimu. "Na kama ALLAH atakupatiliza kwa madhara hakuna wa kuondosha kwake yeye isipokuwa ni yeye na kama atakukusudia kheri hakuna wa kurejesha fadhila zake humpata fadhila za ALLAH yule amtakae katika waja wake na yeye ni mfuta mdhambi mrehemevu. [Yunus: 106-107]
na kauli yake: {Basi tafuteni kwa ALLAH riziki na mumuabudu yeye na mumshukuru yeye kwake mtarejeshwa} [Al Ankabut: 17].
na kauli yake: Na hakuna mpotevu zaidi kuliko yule ambaye anaomba kinyume na ALLAH kitu ambacho hakina uwezo wa kumjibia- maombi yake- mpaka siku ya qiyamah. Na pindi watakapo fufuliwa watu walikuwa wao ni maadui zao na walikuwa kwa kuwaabudu wao ni wenye kupinga. [Al Ahqaaf: 5,6]
na kauli yake: Hivi yule ambaye anamjibu yule mwenye matatizo na anaondoa madhara na anakufanyeni ni watawala wa nchi hivi mnajalia pamoja na ALLAH mungu mungine. [An Namli: 62].
Na amepokea Twabaraniy kwa isnadi yake: Yakwamba katika zama za Mtume Sala na Amani ziwe juu yake kulikuwa na mnafiki akiwaudhi waumini, wakasema baadhi yao: simameni tutake msada kupitia kwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake kutokana na mnafiki huyu: "Kwa hakika mimi siombwi msaada hakika anayeombwa msaada ni ALLAH."
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Nikuwa kuiunganisha dua na swala la kuomba msaada ni katika kuunganisha jambo la kiujumla kwa jambo maalumu.
La pili Tafsiri ya kauli yake ALLAH Mtukufu:{Na wala usiombe kinyume na ALLAH yale yasiyokunufaisha wala kukudhuru}.
La tatu: Nikuwa hili ndiyo shirki kubwa.
La nne: Nikuwa kuwarekebisha watu laiti mtu atafanya hivyo kwa kumridhisha asiyekuwa yeye atakuwa ni katika madhalimu.
La tano: Tafsiri ya aya iliyoko baada yake.
La sita: Nikuwa hilo halinufaishi chochote duniani pamoja nakuwa ni ukafiri.
La saba: Tafsiri ya aya ya pili.
La nane: Nikuwa kutafuta riziki hakutakiwi isipokuwa kutoka kwa ALLAH kama ambavyo pepo haiombwi kwa yeyote isipokuwa kwake.
La tisa: Tafsiri ya aya ya nne.
La kumi: Nikuwa hakuna mtu aliyepotea zaidi kuliko aliyemuomba asiyekuwa ALLAH.
La kumi na moja: Nikuwa huyo anayeombwa haelewi na wala hajui chochote kuhusu maombi ya huyo anayemuomba.
La kumi na mbili: Nikuwa maombi hayo ni sababu ya muombwaji kumchukia anayemuomba na ni sababu ya uadui kwake.
La kumi na tatu: Kuitwa maombi hayo kuwa ni kumuabudu anayeombwa.
La kumi na nne: Ni kuzikanusha muombwaji ibada hizo.
La kumi na tano: Nikuwa maombi haya ndiyo sababu ya kuwa kwake ni mpotevu zaidi kuliko watu wote.
La kumi na sita: Tafsiri ya aya ya tano.
La kumi na saba: Jambo la ajabu, nalo ni kukubali hawa waabudu masanamu kuwa hakuna mwenye kumjibu aliyedhikika isipokuwa ALLAH, na ndiyo maana huwa wanamuomba kwa utakasifu mkubwa wakati wa matatizo.
La kumi na nane: Kumuhami Mtume Sala na Amani ziwe juu yake ni kuihami TAUHEED na kuwa na Adabu na ALLAH.
MLANGO ULIO KUJA KUELEZEA KAULI YAKE ALLAH MTUKUFU. Hivi wanafanya ushirika na kitu ambacho hakina uwezo wa kuumba chochote na wao wanaumbwa. Na wala hawana uwezo wa kuwanusuru wao na wala hawawezi kuzinusuru nafsi zao. [Al A'raf: 191,192]
na kauli yake: "Na wale mnaowaomba kinyume na yeye hawamiliki hata ganda la kokwa" Na mkiwaomba{wafu}hawasikii maombi yenu na hata kama wangesikia hawawezi kuwajibu na siku ya qiyamah watapinga maombi yenu na hakuna wa kukuelezea {hayo}mfano wa muelezaji. [Faatir: 13,14].
Na katika (sahihi Bukhari) kutoka kwa Anasi Amesema: "Alijeruhiwa usoni Mtume Sala na Amani ziwe juu yake siku ya vita vya Uhudi, na yakavunjwa meno yake ya mbele, Akasema: "Watafaulu vipi watu ambao wamemjeruhi Nabii wao?". Ikateremka: "Humiliki chochote katika maamuzi" [Al-Imran: 28].
Na pia kutoka kwa bin Omari Radhi za ALLAH ziwe juu yao: (Ya kwamba yeye alimsikia Mtume Sala na Amani ziwe juu yake akisema anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu katika rakaa ya mwisho katika swala ya alfajiri: (Ewe ALLAH mlaani fulani na fulani), Baada yakuwa amesema: (Samiallaahu liman hamidah, Rabbanaa walakal Hamdu) Akateremsha ALLAH: "Humiliki chochote katika maamuzi" [Al-Imran: 28].
Na katika riwaya nyingine: "Alikuwa akimuombea dua mbaya Swafwani bin Umaiyya, na Suhaili bin Amri, na Harith bin Hisham, Ikateremka: "Humiliki chochote katika maamuzi" [Al-Imran: 28].
Na pia kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za ALLAH ziwe juu yake Amesema: "Alisimama Mtume Sala na Amani ziwe juu yake alipoteremshiwa: "Na uwaonye jamaa zako wa karibu" [Ash shu'raa: 214] Akasema: "Enyi jamaa wa kikuraishi (Au alisema neno mfano wa hili) Zinunueni nafsi zenu (zikomboeni); Sitokunufaisheni kwa ALLAH kwa chochote, Ewe Abbasi bin Abdil Muttwalib sitokufaa wewe kwa ALLAH kwa chochote, Ewe Safia -Shangazi yake na Mtume Sala na Amani ziwe juu yake- sitokufaa wewe kwa ALLAH kwa chochote, Na Ewe Fatma bint Muhammadi, Niombe mimi katika mali zangu chochote ukitakacho, sitokufaa wewe kwa ALLAH kwa chochote"
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya mbili:
La pili Kisa cha vita vya Uhudi.
La tatu: Kuomba dua Mtukufu wa Mitume na nyuma yake kukiwa na waheshimiwa Maswahaba (Mawalii) wakiitikia katika swala
La nne: Nikuwa waliokuwa wakiombewa dua mbaya ni makafiri.
La tano: Nikuwa wao walifanya mambo ambayo hawakuwahi kuyafanya makafiri wengine, miongoni mwa hayo: Ni kumjeruhi kwao Nabii wao, na pupa yao ya kutaka kumuua, na miongoni mwa hayo: kuwakata viungo waliokufa pamoja nakuwa ni watoto wa baba zao wadogo.
La sita: ALLAH alimteremshia katika hilo: "Humiliki chochote katika maamuzi"
La saba: Kauli yake: "Au anaweza kuwasamehe au kuwaadhibu" Akawasamehe na wakaingia katika imani.
La nane: Kuomba dua ya kunuti wakati wa matatizo.
La tisa: Kuwataja wanaoombewa dua mbaya ndani ya swala na majina ya baba zao.
La kumi: Kumlaani mtu maalumu katika kunuti.
La kumi na moja: Kisa chake Sala na Amani ziwe juu yake- alipoteremshiwa: "Na watahadharishe, ewe Muhammad, watu wako wa karibu, ukianzia na wale walio karibu na wewe zaidi.
La kumi na mbili: Juhudi zake mtume Sala na Amani ziwe juu yake katika jambo hili kiasi ambacho alilifanya swala ambalo lilifanya akaitwa mwendawazimu, na hivyo hivyo muislamu yeyote akilifanya yatamfika hayo hayo.
La kumi na tatu: Kauli yake kwa ndugu wa karibu na wa mbali: "sitokufaa wewe kwa ALLAH kwa chochote", Mpaka akafikia kusema: ((Ewe Fatma bint Muhammadi, sitokufaa wewe kwa ALLAH kwa chochote)).
Anapoweka wazi hali yakuwa yeye ndiye bwana wa Mitume kuwa yeye hasaidii chochote kwa mtukufu wa wanawake wa ulimwengu, na mtu akiamini kuwa yeye hazungumzi isipokuwa haki, kisha akatazama yaliyojitokeza katika nyoyo za baadhi ya watu leo hii, ataona wazi ni namna gani watu walivyoiacha TAUHEED na dini ilivyopotea.
MLANGO ULIO KUJA KUELEZEA KAULI YAKE ALLAH MTUKUFU{walipo ondoshewa kunako mioyo yao wakasema jambo gani amesema MOLA wenu wakasema ni haki na yeye ni wa juu zaidi mwenye ukubwa.}
Na katika Sahihi Al-Bukhari pia kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: Anapolihukumia ALLAH jambo mbinguni Malaika hupiga mbawa zao kwa kuonyesha unyenyekevu kwa ALLAH Mtukufu katika kauli yake, utadhani ni mnyororo uliyoko juu ya jiwe kubwa, huwachukua hilo mpaka pale mfadhaiko unapoondolewa nyoyoni mwao husema: ni nini amesema Mola wenu? Husema: kasema kweli naye ndiye aliye juu na mkubwa, huyasikia maneno hayo mwizi wa kusikiliza, na wezi wa kusikiliza huwa katika namna hii; wanabebana baadhi yao kwa baadhi, alielezea Sufyani kwa viganja vyake, akavigeuza na akaachanisha kati ya vidole vyake, anasikiliza neno kisha anamtupia aliyeko chini yake, mpaka analifikisha katika ulimi wa mchawi au kuhani, na huenda kikamfikia kimondo kabla hajalitupia, na huenda akalitupia kabla hakijamfikia, anaongeza katika neno hilo uongo mia moja, Basi husemwa: Kwani hakusema fulani siku fulani itakuwa kadhaa wa kadhaa? Basi huaminiwa kwa neno hilo lililosikika kutoka mbinguni".
Na kutoka kwa nawwasi bin Samaan -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema mtume wa Mwenyezi Mungu -Sala na AMANI za ALLAH ziwe juu yake na amani- "Anapotaka ALLAH Mtukufu kuteremsha wahyi wa jambo, huzungumza kwa wahyi, hapo mbingu huanza kutetemeka kwa sababu yake, Au alisema: hupatwa na mtikisiko mkubwa, kwa kumuogopa ALLAH aliyetakasika na kutukuka, wanaposikia hivyo wakazi wa mbinguni hupiga ukelele na kuporomoka wakimsujudia ALLAH, anakuwa wa mwanzo kunyanyua kichwa chake ni Jibrili, basi ALLAH humsemesha katika wahyi wake kile anachotaka kumsemesha, kisha anapita Jibrili kwa Malaika, kila anapopita katika mbingu wanamuuliza Malaika wake: Kasema nini Mola wetu Ewe Jibrili?
Basi anasema: Amesema kweli, na yeye ni Mtukufu na Mkubwa, basi hapo wote husema kama alivyosema Jibrili, basi Jibrili huupeleka wahyi mpaka pale alipoamrishwa na ALLAH Aliyetakasika na Kutukuka"
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Tafsiri ya Aya
La pili Ni hoja zilizomo za kubatilisha ushirikina hasa hasa atakayeshikamana na watu wema, nayo ni aya ambayo inasemekana kuwa: inakata mizizi ya mti wa ushirikina kutoka moyoni.
La tatu: Tafsiri ya kauli yake: "Husema amesema kweli naye ni mkubwa aliye juu".
La nne: Sababu ya kuuliza kwao hivyo.
La tano: Nikuwa Jibrili anawajibu baada ya hapo kwa kauli yake: (Amesema: kadhaa wa kadhaa).
La sita: Kutajwa kuwa wa kwanza kunyanyua kichwa chake ni Jibril.
La saba: Nikuwa huambiwa watu wa mbinguni wote; kwa sababu wao humuuliza.
La nane: Nikuwa kuzimia huwakumba wote walioko mbinguni.
La tisa: Kutetemeka mbingu kwa maneno ya Mwenyezi Mungu.
La kumi: Nikuwa Jibrili ndiye ambaye huupeleka wahyi mpaka pale alipomuamrisha ALLAH.
La kumi na moja: Kutajwa wizi wa mashetani.
La kumi na mbili: Namna ya kupanda baadhi yao juu ya wengine.
La kumi na tatu: Kutumwa kwa vimondo.
La kumi na nne: Nikuwa wakati mwingine humpata kimondo kabla hajalihamisha neno hilo.
Na wakati mwingine hulitia katika sikio la mtu wake wa karibu katika wanaAdamu kabla hakijamfikia kimondo.
La kumi na tano: Ni Kuwa kuhani husema ukweli baadhi ya nyakati.
La kumi na sita: Nikuwa huongopa katika ukweli huo uongo mia moja.
La kumi na saba: Nikuwa hajaaminiwa kwa uongo wake isipokuwa kwa neno lililosikika toka mbinguni
La kumi na nane: Nafsi kuikubali batili: Ni jinsi gani wanavyoshikamana na hilo moja na wala hawayatazami hayo mia moja.
La kumi na tisa: Kuwa kwao wanapokezana baadhi yao kwa baadhi
neno hilo na wanalihifadhi na wanalitumia kama ushahidi.
La Ishirini Kuthibitisha sifa za Allah, tofauti na madhehebu ya ashairah wenye kuharibu sifa.
La Ishirini na moja: Kuwekwa wazi kuwa kule kutetemeka na kuzimia
Ni kwa kumuogopa ALLAH Mtukufu.
La Ishirini na mbili: Nikuwa wao wanaporomoka wakimsujudia ALLAH.
Mlango wa Uombezi:
Na kauli ya ALLAH Mtukufu: Waonye ewe MUHAMMAD wale ambao wanahofu kufufuliwa mbele za MOLA wao hawana wao kinyume na ALLAH mtetezi wala wa kuwaombea huwenda wao wakamuogopa ALLAH. [An A'am: 51].
Na kauli yake: Sema ewe MUHAMMAD uwombezi wote ni wa ALLAH. Az- zumar (44)
Na kauli yake: Hakuna wakuomba mbele za ALLAH isipokuwa kwa idhini yake ALLAH. [Al Baqara: 255].
Na kauli yake: Ni wangapi kutokana na wafalme wa mbinguni haiwatoshelezi uwombezi wao kwa chochote isipokuwa baada ya kutoa idhini ALLAH kwa anaye mtaka. [An najim: 26]
Na kauli yake: Sema ewe MUHAMMAD waombeni ambao mnaodai kinyume na ALLAH wasio miliki mfano wa mdudu chungu katika mbingu wala aridhini na hawana wao ndani ya mbingu ushirika na hawana wao kwake yeye ALLAH mwenye kuwasaidia{22}na haitanufaisha uwombezi mbele ya ALLAH isipokuwa kwa yule atakaepewa idhini. [Sabaa: 22,23]
Amesema Abul Abbas : "Ameyakanusha ALLAH yote yasiyokuwa yeye wanayoshikamana nayo washirikina, akakanusha kuwa na ufalme au sehemu ya ufalme kwa asiyekuwa yeye, au kuwa ni msaidizi wa ALLAH, na ikawa hakujabakia isipokuwa uombezi, basi akabainisha kuwa hata huo uombezi pia haunufaishi isipokuwa kwa yule aliyemuidhinisha Mola, kama alivyosema: "Na wala hawatomuombea isipokuwa yule aliyemridhia" [An biyaa: 28].
Uombezi huu ambao wanaudhania washirikina hautokuwepo siku ya kiyama, kama ilivyoukanusha Qur'ani, na akaeleza Nabii Sala na Amani ziwe juu yake:
"Kuwa yeye atakuja ana atasujudu kwa Mola wake na amsifu -hatoanza na kuombea kwanza- kisha ataambiwa: Nyanyua kichwa chako, na sema usikilizwe, na omba upewe, na tetea ukubaliwe"
Na Abuu Huraira alimuuliza: "Ni nani atakayepata faraja ya utetezi wako? Akasema: "Atakayesema: Laa ilaaha illa llaahu -Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa ALLAH- likiwa limetoka moyoni mwake kwa utakasifu kabisa".
Huo utakuwa ni utetezi wa watu walikuwa watakasifu wa nia katika ibada zao kwa idhini ya ALLAH, na hautokuwa kwa yule aliyemshirikisha ALLAH.
Na kiukweli kabisa nikuwa ALLAH Mtukufu ndiye anayewapa fadhila watu wenye utakasifu (Ikhlaswi), atawasamehe kupitia dua ya yule aliyemuidhinisha kuwatetea ili ampe heshima, na ili apate nafasi nzuri.
Hivyo utetezi ambao imeukanusha Qur'ani ni ule ambao ndani yake kuna ushirikina, na ndiyo maana imethibitisha utetezi kwa idhini yake katika maeneo baadhi, na amebainisha Mtume Saka na Amani ziwe juu yake kuwa hautokuwa isipokuwa kwa watu wenye kumpwekesha ALLAH na utakasifu wa matendo yao (Ikhlaswi). Mwisho wa maneno yake.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya Aya
La pili Namna ya uombezi uliyokatazwa.
La tatu: Namna ya uombezi uliyothibitishwa.
La nne: kumetajwa uombezi mkuu,
Nayo ni nafasi nzuri.
La tano: Namna atakayoifanya Mtume Sala na Amani ziwe juu yake nikuwa yeye hatoanza na kuombea moja kwa moja bali ataanza na kusujudu,
ALLAH Atakapompa idhini basi ataombea watu.
La sita: Ni nani atakayepata furaha ya utetezi huo?
La saba: Nikuwa hautokuwa kwa aliyemshirikisha ALLAH.
La nane: Kumebainishwa uhakika wake.
HUU NI MLANGO ULIO KUJA KUELEZA KAULI YAKE ALLAH MTUKUFU: Hakika wewe MUHAMMAD humuongozi umpendaye na lakini ALLAH anamuongoza amtakaye na yeye ndiye anaye jua walio ongoka. [Suratil Qaswas 56]
Katika kitabu cha (Sahihi Bukhari) imenukuliwa kutoka kwa bin Musayyib, kutoka kwa baba yake amesema: Yalipomfikia mauti Abuu Twaalib, Mtume Sala na Amani ziwe juu yake alimjia na kukiwa kwake yuko Abdallah bin Abii Umaiyya na Abuu Jahli, Akasema kumwambia: "Ewe Ammi yangu, sema: Laa ilaaha illa llaahu -Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa ALLAH, neno ambalo nitakutetelea kwalo mbele ya ALLAH".
Wakasema kumwambia: Hivi unaiacha mila ya Abdil Muttwalib?
Akamrudia Mtume Sala na Amani ziwe juu yake, nao wakarudia, basi likawa neno lake la mwisho alilosema: yeye yuko katika mila ya Abdil Muttwalib, na akakataa kusema: Laa ilaaha illa llaahu.
Akasema Mtume Sala na Amani ziwe juu yake: "Hakika nitakuombea msamaha madamu sijakatazwa kwako".
Akateremsha ALLAH Mtukufu: Hatakikani kwa nabii na wale walio amini kuwatakia msamaha washirikina hata kama walikuwa ni ndugu wa karibu baada ya kubainikiwa wao kuwa wao ni watu wa motoni. [Attauba: 113].
Na akateremsha kuhusu Abuu Twaalib: Hakika wewe MUHAMMAD humuongozi umpendaye lakini ALLAH anamongoza amtakaye. [Suratil Qaswas 56]
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya kauli yake ALLAH: Hakika wewe MUHAMMAD haumuongozi umpendaye na lakini ALLAH anamuongoza amtakaye.
La pili Tafsiri ya kauli yake: "Haifai kwa Mtume na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina".
La tatu: Nalo ni swala kubwa- Tafsiri ya kauli yake: "Sema: Laa ilaaha illa llaahu" Hii ni tofauti na jinsi wanavyodai wale wanaosema kuwa wana elimu.
La nne: Nikuwa Abuu Jahli na wale waliokuwa pamoja naye wanajua makusudio ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake pale anaposema kumwambia mtu: "Sema: Laa ilaaha illa llaah" Mwenyezi Mungu amlipe uovu zaidi mtu ambaye anazidiwa na Abuu Jahli kuelewa asili ya uislamu.
La tano: Juhudi yake Sala na Amani ziwe juu yake, na kutumia kwake nguvu ya ziada katika kutaka ammi yake asilimu.
La sita: Kumjibu anayedai kuwa Abuu twaalib na watangulizi wake walisilimu.
La saba: Kuwa kwake Sala na Amani ziwe juu yake alimuombea msamaha na hakusamehewa, bali alikatazwa hilo.
La nane: Madhara ya marafiki waovu kwa mtu.
La tisa: Madhara ya kuwatukuza waliotangulia na wazee.
La kumi: Shaka wanayoitia watu wa batili katika hilo kwani Abuu Jahli alitumia hilo kama hoja.
La kumi na moja: Panapokusudiwa nikuwa matendo yote huzingatiwa mwisho; kwa sababu laiti angelitamka basi lingemnufaisha.
La kumi na mbili: Kuzingatia ukubwa wa ushawishi huu katika nyoyo za waliopotea; kwa sababu katika kisa hiki hawakumletea mjadala isipokuwa kwa hilo moja tu, pamoja na juhudi zake Sala na Amani ziwe juu yake na kurudia rudia kwake, kwa sababu ya ukubwa wa neno hili la kumpwekesha ALLAH na uwazi wake kwao waliishia kumwambia kauli hiyo moja tu.
MLANGO ULIO KUJA KUELEZA KUWA SABABU YA KUKUFURU WANA WA ADAM NA KUACHA KWAO DINI YAO NI KUVUKA MIPAKA KWA WAJA WEMA.
Na kauli ya ALLAH Mtukufu: Enyi mayahudi na wakristo mzivuke mipaka katika dini yenu na wala msiseme juu ALLAH isipokuwa haki na shani ya jambo ni kuwa ISSAH mtoto MARIAM ni mtume wa ALLAH na neno lake alilitupa kwa MARIAM na roho kutoka kwake. [An Nisaai: 171]
Imepokelewa katika (sahihi Bukhari) kutoka kwa bin Abbasi ALLAH ziwe juu yao katika kauli yake Mtukufu: Na wakasema msiache miungu yenu wala msiache-kumuabudu-wada wala suwaa wala yaghutha na yauqa na nasra. [Nuhu: 23]
Amesema: "haya ni majina ya watu wema miongoni mwa watu wa Nuhu, walipokufa shetani aliwafunulia mawazo watu wao, kuwa tengenezeni picha katika vikao vyao walivyokuwa wakivikaa kisha yasimikeni na yaiteni kwa majina yao, wakafanya hivyo, na hayakuabudiwa kwa wakati huo,mpaka walipokufa hao na elimu ikasahaulika yakaabudiwa masanamu hayo".
Amesema bin Qayyim: "Amesema zaidi ya mmoja katika wema waliotangulia: walipokufa walisimama juu ya makaburi yao, kisha wakachonga sanamu zao, kisha muda baada yakuwa muda umekuwa mwingi wakawaabudu"
Na kutoka kwa Omari Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Msichupe mipaka katika kunisifu kama walivyochupa mipaka manaswara kwa mwana wa Mariam, bila shaka hakika mimi ni mja wake,basi semeni; mja wa Mwenyezi Mungu na mjumbe wake"
Na Amesema: Amesema Mtume wa ALLAH Sala na amani za Allah ziwe juu yake: "Tahadharini na kuchupa mipaka, bila shaka kilichowaangamiza waliokuwa kabla yenu ni kuchupa mipaka"
Na amepokea imamu Muslim kutoka kwa bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Wameangamia wenye kutia mkazo". Alilisema hilo mara tatu.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Nikuwa atakayeuelewa mlango huu na milango miwili baada yake itambainikia ugeni wa uislamu,
Na ataona miongoni mwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na ugeuzaji wake wa nyoyo wa ajabu.
La pili: Kujua shirki ya kwanza kutokea katika ardhi nikuwa ilisababishwa na kuleta hoja za kuwatukuza watu wema.
La tatu: Kufahamu kitu cha kwanza ambacho kilitumika kuibadilisha dini ya Manabii, na ni ipi sababu ya hilo, pamoja na kujua kuwa ALLAH ndiye aliyewatuma.
La nne: Kukubali uzushi pamoja nakuwa sheria na akili ya kawaida inalipinga hilo.
La tano: Nikuwa sababu ya hayo yote ni kuchanganya haki na batili.
Ya kwanza: Ni kuwapenda watu wema.
Na ya pili: Ni kitendo cha baadhi ya watu wenye elimu ambao kusudio lao lilikuwa ni zuri; wakajakudhania wale waliokuja baada yao kuwa walikusudia lengo tofauti na hilo.
La sita: Tafsiri ya aya ambayo iko katika suratu Nuh.
La saba: Umbile la mwanadamu nikuwa siku zote haki hupungua siku hadi siku ndani ya moyo wake na batili huzidi.
La nane: Hapa kuna ushahidi kwa yale yaliyopokelewa kutoka kwa wema waliotangulia kuwa uzushi ni sababu ya ukafiri.
La tisa: Kujua shetani yale ambayo hupelekea kupatikana uzushi hata kama lengo la mfanyaji wake litakuwa zuri.
La kumi: Kujua kanuni muhimu nayo ni katazo la kuchupa mipaka, na kuyajua yanayosababisha uzushi.
La kumi na moja: Madhara ya kukaa juu ya kaburi kwa ajili ya kufanya amali njema.
La kumi na mbili: Kujua katazo la masanamu, na hekima ya kuyaondoa kwake.
La kumi na tatu: Kujua ukubwa wa swala la kisa hiki na ukubwa uhitaji wake, pamoja nakuwa watu wengi hawakijui.
La kumi na nne: Nalo ni -ajabu kweli kweli- kukisoma kwao kisa hiki katika vitabu vya tafsiri na hadithi, na kujua kwao maana ya maneno, nakuwa ALLAH amezunguka baina yao na nyoyo zao (kwa kuwajua vizuri na kuyaona yote wanayoyaficha na wanayoyadhihirisha) mpaka wakaitakidi kuwa kitendo cha watu wa Nuhu ndiyo ibada bora, na wakaitakidi kuwa yale aliyoyakataza ALLAH na Mtume wake ni ukafiri unaohalalisha damu na mali.
La kumi na tano: Kumewekwa wazi kuwa wao hawakukusudia isipokuwa ni kutaka utetezi.
La kumi na sita: Dhana yao kuwa wanachuoni waliotengeneza picha na masanamu hayo walikusudia hivyo
La kumi na saba: Ubainifu mkubwa katika kauli yake: "Msichupe mipaka katika kunisifu kama walivyovuka mipata Manaswara kwa Isa bin Mariam" Basi Amani na salama za ALLAH ziwe juu yake alifikisha ujumbe ufikishaji wa wazi.
La kumi na nane: Nasaha zake kwetu kuwa waliangania wenye kujitia uzito (walijilazimisha kumsifu mpaka wakavuka mipaka na kumuita mungu au mwana wa mungu).
La kumi na tisa: Kumewekwa wazi kuwa hayakuabudiwa masanamu hayo mpaka pale elimu iliposahaulika, hapa ni wazi kuwa kuna umuhimu wa uwepo wa elimu na madhara ya kukosekana kwake.
La Ishirini Kwa sababu ya kukosekana kwa elimu ni kufa wanachuoni.
Mlango uliokuja kumkemea yule atakayemuabudu ALLAH katika kaburi la mtu mwema, sasa ni vipi kama atamuabudu kabisa?!
Imepokelewa katika (kitabu cha sahihi Bukhari) kutoka kwa Aisha Radhi za ALLAH ziwe juu yake, yakwamba Ummu (mama) salama alilielezea kwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake kanisa aliloliona katika Ardhi ya Habash (Ethiopia), na yale yaliyomo ndani yake katika mapicha, Akasema: "Hao ni watu ambao anapokufa kwao mja mwema, au mtu mwema, wanajenga juu ya kaburi lake msikiti, na wanachora hapo mapicha, hao ni viumbe waovu mbele ya ALLAH."
Hawa wamekusanya kati ya fitina mbili: Fitina ya makaburi, na fitina ya masanamu.
Na pia wamepokea kutoka kwake Anasema: (Ilipoteremshwa kwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake akaanza kurusha kanzu yake usoni kwake, inapomfunika anaifunua, akasema naye akiwa katika hali hiyo:- "Amewalaani ALLAH Mayahudi na Manaswara, wameyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa ni misikiti" Anatoa tahadhari juu ya hayo waliyoyafanya, na laiti kama si hivyo basi lingenyanyuliwa kaburi lake, ni kwakuwa alihofia lisije kufanywa ni mahala pa ibada" Wameitoa hadithi hii Maimamu wawili.
Na katika kitabu cha Sahihi Muslim kutoka kwa Jundab bin Abdillahi, Amesema: Nilimsikia Nabii Sala na Amani ziwe juu yake kabla hajafa kwa siku kama tano. naye akisema: "Hakika mimi najiepusha kwa ALLAH kuwa kwangu kati yenu na rafiki wa ndani, kwani ALLAH amenifanya mimi kuwa kipenzi wa ndani kama alivyomfanya Ibrahim kuwa kipenzi wa ndani, na lau kama ningejifanyia kipenzi wa ndani katika umma wangu basi ningemfanya Abuubakari kuwa kipenzi wa ndani,Fahamuni kuwa hakika wale waliyokuwa kabla yenu waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa Misikiti, Tambueni kuwa,msiyafanye makaburi kuwa Misikiti, kwani hakika mimi ninakukatazeni na hilo".
Alilikataa hilo mwisho wa uhai wake- kisha naye akamlaani naye akiwa yuko ndani ya mlolongo wa maneno hayo hayo, kuwa mtu yeyote atakayelifanya, na kusali juu yake ni miongoni mwa hilo, hata kama hautojengwa msikiti. Na ndiyo maana ya kauli yake: (Alihofia lisijekufanywa kuwa Msikiti) Kwani Maswahaba hawakuweza kujenga msikiti pembezoni mwa kaburi lake, na kila sehemu iliyokusudiwa kuswalia hapo basi itakuwa imefanywa kuwa msikiti, bali kila sehemu inayoswaliwa huitwa msikiti, kama alivyosema Sala na Amani ziwe juu yake: "Na nimefanyiwa Ardhi kwangu kuwa ni Msikiti na twahara".
Na imepokelewa na Imam Ahmad kwa isnadi jayyid (nzuri) Kutoka kwa bin Mas'udi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Hadithi Marfu'u: "Hakika katika watu waovu ni wale kitakaowakuta qiyamah wakiwa hai, na wale wanaoyafanya makaburi kuwa ni misikiti." Kaipokea Abuu Hatim na bin Hibban katika sahihi yake pia.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Ni yale aliyoyaeleza Mtume Sala na Amani ziwe juu yake kwa atakayejenga msikiti atakaoabudiwa ALLAH hapo katika kaburi la mtu mwema hata kama nia mfanyaji wake itakuwa nzuri.
La pili: Katazo la masanamu na ubaya wake katika hilo.
La tatu: kuzingatia msisitizo wake Rehema na Amani ziwe juu yake katika hilo ni jinsi gani aliwabainishia hili mwanzo, kisha kabla ya kifo chake kwa siku tano akasema aliyoyasema, kisha alipokuwa katika mazungumzo hakutosheka na yale yaliyotangulia.
La nne: katazo lake la kufanya hilo katika kaburi lake kabla hata halijapatikana kaburi lake.
La tano: Nikuwa hili ni katika taratibu za Mayahudi na Manaswara katika makaburi ya Manabii wao.
La sita: Laana zake kwao juu ya hilo.
La saba: Nikuwa lengo lake Sala na Amani ziwe juu yake ni kututahadharisha sisi kuhusu kaburi lake.
La nane: Sababu ya kutonyanyuliwa kaburi lake.
La tisa: Ni katika maana za kulifanya kuwa msikiti.
La kumi: Ni kuwa ameunganisha pamoja kati ya mwenye kulifanya kaburi kuwa msikiti
na kati ya yule ambaye qiyamah kitasimama kwake, akataja kuwa ni njia ya kupelekea katika ushirikina kabla haujatokea pamoja na mwisho wake.
La kumi na moja: Kulitaja kwake katika hotuba yake kwa siku tano kabla ya kifo chake, hili ni jibu kwa makundi mawili ambayo ndiyo makundi mabaya zaidi katika makundi ya kizushi,
Bali baadhi ya wema waliotangulia wamewatoa hata katika makundi sabini na mbili ambayo yalielezwa na Mtume Sala na Amani ziwe juu yake kuwa yatatokea katika umma wa kiislamu, nao ni Maraafidhwa na Jahamiya, na kwasababu ya hawa Raafidhwa ndiyo ilitokea shirki na ibada za makaburi, na ndiyo wa kwanza kujenga juu yake makaburi.
La kumi na mbili: Ni kile alichotahiniwa nacho Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake katika ukali wa maumivu.
La kumi na tatu: Kile alichokirimiwa kwacho katika mapenzi ya ndani.
La kumi na nne: Kuwekwa wazi kuwa hayo ni zaidi ya mapenzi ya kawaida.
La kumi na tano: kumewekwa wazi kuwa Abuubakari Swiddiq ndiyo swahaba bora.
La kumi na sita: Ishara juu ya utawala wake.
Mlango uliokuja kuwa kuchupa mipaka katika makuburi ya watu wema kunayafanya kuwa ni masanamu yanayoabudiwa kinyume na ALLAH:
Na amepokea Malik katika kitabu (Al Muwattwa'a) Yakwamba Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Ewe Mola wangu usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu lenye kuabudiwa, zimekuwa kali hasira za ALLAH juu ya watu walioyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa Misikiti."
Na imepokelewa kutoka kwa bin Jariir kwa isnadi yake kutoka kwa sufyani kutoka kwa Mansur kutoka kwa Mujaahid: "Mnawaonaje, enyi washirikina, waungu hawa mnaowaabudu: Lāta, 'Uzzā" [An Najim: 19] Amesema: (Alikuwa akiwakorogea uji akafariki, wakakaa kwa ajili ya ibada juu kaburi lake).
Na hivyo ndivyo alivyosema Abul Jauzaa kutoka kwa bin Abbas: (Alikuwa akiwakorogea uji mahujaji).
Na Kutoka kwa bin Abbas- Radhi za Allah ziwe juu yao amesema: "Amewalaani Mtume -Sala na Amani ziwe juu yake- (wanawake) wenye kuzuru makaburi, na wenye kuyafanya kuwa mahala pa ibada (misikiti) na kuweka juu yake taa" Wameipokea waandishi wa vitabu vya sunani.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya masanamu.
La pili Tafsiri ya ibada.
La tatu: Nikuwa yeye Sala na Amani ziwe juu yake hakuomba kinga isipokuwa kwa yale aliyohofia kutokea kwake.
La nne: Kuliunganisha kwake hili la kuyafanya makaburi ya Manabii kuwa Misikiti.
La tano: Kutajwa hasira kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
La sita: Na hili ndiyo la muhimu kuliko yote: Kujua sifa ya ibada ya Lata ambalo ndilo sanamu kubwa.
La saba: Kujua kuwa hilo kumbe ni kaburi la mtu mwema.
La nane: Nakuwa hilo ni jina la mwenye kaburi, na kutajwa maana kuitwa kwa jina hilo.
La tisa: Kuwalaani kwake wanawake wenye kuzuru makaburi.
La kumi: Kumlaani kwake atakayeyawekea taa
Mlango wa yaliyokuja kumhami Mtume Sala na Amani ziwe juu yake upande wa Tauhidi na kumzibia kila njia inayopelekea katika ushirikina:
Na amesema ALLAH Mtukufu: "Hakika amekujieni Mtume atokanae na nafsi zenu yanampa dhiki yale yanayo kusibuni ni mwenye pupa juu yenu kwa waumini ni mpole msamehevu. [Al- taubah 128]
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa ALLAH-ALLAH na Amani za ALLAH ziwe juu yake: "Msizifanye nyumba zenu kuwa makaburi, na wala msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, na mniombee rehema juu yangu, kwani maombi yenu hunifikia mahala popote mtakapokuwa." Kaipokea Abuudaud kwa isnadi hasan, na wapokezi wake ni waaminifu.
Kutoka kwa Ally bin Husein: "Yakwamba yeye aliona mtu mmoja anakuja toka katika kiupenyo kidogo kilikuwa katika kaburi la Mtume -Sala na Amani ziwe juu yake- anaingia na anaomba hapo, akamkataza, na akasema: Hivi nikusimulieni hadithi niliyoisikia toka kwa baba yangu toka kwa Mtume -Sala na Amani ziwe juu yake- amesema: "Msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, wala nyumba zenu kuwa makaburi, na nitakieni rehma, kwani dua zenu hunifikia popote mlipo" Kaipokea katika kitabu Al Mukhtara.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya za suratu baraa.
La pili: Kuwaweka kwake mbali umma wake katika mpaka huu umbali mkubwa.
La tatu: kutajwa kwa pupa yake juu yetu na upole wake na huruma yake.
La nne: Katazo lake kuhusu ziara ya kaburi lake kwa namna maalum pamoja nakuwa kulizuru ni katika amali bora.
La tano: katazo lake juu ya kukithirisha kulizuru
La sita: Kuhimiza kwake juu ya kuswali swala za sunna nyumbani.
La saba: Nikuwa hili linafahamika kwao kuwa hakuna kuswali juu ya makaburi.
La nane: kutaja kwake sababu kuwa maombi na salamu ya mtu juu yake yeye humfikia hata kama akiwa mbali, hakuna haja ya kile anachokidhania yule anayetaka ukaribu.
La tisa: Nikuwa huko huko katika maisha yake ya Barzakh (kaburini) Mtume Sala na Amani ziwe juu yake hufunuliwa matendo ya umma wake pale wanapomuombea Sala na Amani juu yake.
Mlango wa yaliyokuja kuwa baadhi ya umma huu wanaabudu masanamu:
Na kauli ya Allah Mtukufu: "Je hukuwaona wale waliopewa sehemu katika kitabu wanaamini masanamu na mashetani" [An nisaa: 51]
Na kauli ya Allah Mtukufu: Sema ewe MUHAMMAD je nisikuelezeni shari kuliko hiyo mafikio mabaya mbele ya ALLAH yule atakaye laaniwa na ALLAH na akamkasirikia juu yake na ALLAH akawafanya kuwa ni nyani na nguruwe na waabudiwa miungu isiyo kuwa ALLAH." [Al Maaidah: 61].
Na kauli ya Allah Mtukufu: "Wakasema wale wenye kusikilizwa maneno yao na wenye uwezo miongoni mwao, «Tutatengeneza mahali pao hapo msikiti wa kufanya ibada.» [Al kahf: 21].
kutoka kwa Abuu Saidi Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Hakika mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu, kama nyoya linavyoufuata mshale (Hatua kwa hatua) hata kama wataingia katika shimo la kenge nanyi mtaingia".
Wakasema: Ewe Mjumbe wa ALLAH, (Unakusudia) Mayahudi na Manaswara?
Akasema: (Ni akina nani) kama si hao? Wameipokea Maimamu wawili.
Na kwa Imamu Muslim kutoka kwa Thauban -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Hakika ALLAH alinikunjiulia Ardhi nikaona Mashariki yake na Magharibi yake, na hakika umma wangu utafikia Ufalme wake kiasi hicho nilichokunjiwa"
Na nimepewa hazina mbili: Nyekundu na Nyeupe.
Na mimi nilimuomba Mola wangu kwa umma wangu asiuangamize kwa ukame wote mara moja, na asiwasalitishie adui asiyetokana na wao, akahalalisha (akaumaliza) umoja wao.
Na hakika Mola wangu alisema: Ewe Muhammadi ninapolihukumu jambo basi hilo huwa halirudishwi, na hakika mimi nimekupa kwa umma wako nisiwaangamize kwa ukame wote mara moja, na nisiwasalitishie adui asiyekuwa katika wao akahalalisha (kuumaliza) umoja wao, hata kama wangewakusanyikia katika miji yao, mpaka ikafikia baadhi yao wanawauwa baadhi na baadhi yao wakiwafanya mateka baadhi yao"
Ameipokea Al Barqaaniy katika sahihi yake, na akaongeza: "Na hakika ninacho ogopea katika umma wangu ni viongozi wapotofu,na likishuka panga juu yao halitonyanyuliwa mpaka siku ya qiyamah,na hakitosimama qiyamah mpaka mmoja katika umma wangu waungane na washirikina,na mpaka liabudu kundi katika umma wangu masanamu,na hakika watapatikana waongo thelathini katika umma wangu wote wanadai kuwa ni manabii,na mimi ni wa mwisho katika manabii,hakuna Nabii baada yangu,na halitoacha kuwepo katika haki kundi katika umma likinusuriwa kwa haki hiyo, halidhuriki na yeyote mwenye kuwasaliti mpaka itakapokuja amri ya ALLAH Mtukufu".
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya ya suratun nisaai.
La pili Tafsiri ya aya ya suratul maaidah.
La tatu: Tafsiri ya aya ya suratul kahf.
La nne: Nalo ndiyo la muhimu kuliko yote, ni nini maana ya kuamini masanamnu na matwaghuti kati
sehemu hii?
Je ni itikadi ya moyo?
au ni kuendana na watu wenye kuyafanya hayo pamoja na kuyachukia na kujua ubatili wake?
La tano: kauli yao: hakika makafiri wanaoujua ukafiri wao wameongoka njia zaidi kuliko waumini.
La sita: Ndiyo lengo la tafsiri kuwa hili lazima lipatikane katika umma huu kama ilivyothibiti katika hadithi ya Abuu Saidi.
La saba: Kuwekwa wazi kutokea kwake- Nakusudia ibada za masanamu- katika umma huu tena katika kundi kubwa.
La nane: Laa ajabu zaidi ni kujitokeza mwenye kudai utume kama Mukhtari pamoja na kutamka kwake shahada mbili na kuweka kwake wazi kuwa hili litakuwa katika umma huu, nakuwa Mtume ni wa kweli na Qur'ani ya kweli, na ndani kumeelezwa kuwa Muhammadi ni Mtume wa mwisho, lakini pamoja na hayo anaaminiwa pamoja nakuwa ni wazi yuko kinyume, na alijitokeza Mukhtari katika zama za mwisho wa Maswahaba na likamfuata kundi kubwa.
La tisa: Kuna habari njema kuwa haki haiondoki kama ilivyo ondoka zamani, bali bado kuna kundi linalo fuata haki.
La kumi: Muujiza mkubwa kuwa pamoja na uchache wao, lakini hatowadhuru mwenye kuwasaliti wala mwenye kupingana nao.
La kumi na moja: Nikuwa hilo ni sharti mpaka QIYAMAH kisimame.
La kumi na mbili: Ni yale yaliyomo katika alama kubwa: Miongoni mwazo ni kueleza kwake kuwa ALLAH Alimkunjuliaa Mashariki na Magharibi, na akaeleza maana ya hayo, na ikatokea kama alivyoeleza tofauti na kusini na kaskazini, na kueleza kwake kuwa amepewa hazina mbili, na akaeleza kuwa yalipokelewa maombi yake kwa umma wake katika mambo mawili, na akaeleza kuwa alinyimwa la tatu, na kueleza kwake kuwa litashuka panga (vitatokea vita) na kwamba halitonyanyuliwa litakaposhuka, na akaeleza baadhi ya watu kuwaangamiza wengine, na wengine kuwafanya mateka baadhi yao,na hofu yake kwa umma wake juu ya viongozi wapotofu, na kueleza kwake juu ya kujitokeza wenye kujipa utume katika umma huu, na akaeleza juu ya kubaki kwa kundi lenye kunusuriwa, na yote haya yametokea kama alivyoeleza, pamoja nakuwa kila moja katika hayo linaweza kuwa mbali katika akili ya baadhi ya watu.
La kumi na tatu: Kuieleza kwake kwa ujumla hofu yake juu umma wake kutokana viongozi wapotofu.
La kumi na nne: Tahadhari ya maana ya kuyaabudu masanamu.
HUU NI MLANGO ULIO KUJA KUELEZEA UBAYA WA UCHAWI
Na amesema ALLAH Mtukufu: "Na hakika walijua kuwa mwenye kuyachagua hayo hana fungu lolote huko Akhera" [Al Baqara: 102].
na kauli yake: "Wanaamini Masanamu na Mashetani" [An nisaa: 51]
Amesema: Omari: (Masanamu: Hapa inamaana ya uchawi, na Twaghuti ni shetani).
Na amesema Jaabiri: (Twaghuti ni Makuhani walikuwa mashetani wakiwateremkia, katika kila mtaa anashuka mmoja).
kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza"
Wakasema: Ewe Mjumbe wa ALLAH,Ni yapi hayo?
"Akasema: Ni kumshirikisha ALLAH, na uchawi, na kuuwa nafsi aliyoiharamisha ALLAH isipokuwa kwa haki, na kula riba, na kula mali ya yatima, na kukimbia siku ya mapambano, na kuwazulia machafu wanawake waumini wenye kujihifadhi wenye kujizuia na machafu".
Na kutoka kwa Jundabu Hadithi Marfu'u: "Hukumu ya Mchawi ni kupigwa upanga" Kaipokea Tirmidhiy na akasema: (kiusahihi nikuwa hadithi hii ni mauquf, haifanyiwi kazi)
Na katika sahihi Bukhari imepokelewa kutoka kwa Bajala bin Abda Amesema: (Aliandika ujumbe Omari bin Khattwab yakuwa muuweni kila mchawi wa kiume na wa kike, Anasema: Tukawaua wachawi watatu).
(Na imethibiti kutoka kwa Hafswa radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yakwamba yeye aliamrisha kuuliwa kijakazi wake aliyemroga, na akauliwa)
Na vile vile imethibiti kutoka kwa Jundab.
Amesema Ahmad: (Kutoka kwa watu watatu katika maswahaba wa Mtume ALLAH na Amani ziwe juu yake).
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya ya suratul Baqara.
La pili Tafsiri ya aya ya suratun nisaai.
La tatu: Tafsiri ya Jibti na Twaghuti na tofauti kati yake.
La nne: Nikuwa Twaghuti (shetani) anaweza kuwa katika majini, na anaweza kuwa miongoni mwa watu.
La tano: Kuyajua mambo saba yenye kuangamiza yaliyotajwa maalumu katika katazo.
La sita: Nikuwa mchawi anakufuru.
La saba: Nikuwa kisheria anauawa na wala hapewi muda wa kutubia.
La nane: Kupatikana jambo hili kwa waislamu wa zama za Omari je hali iko kwa wale walio baada yake?.
Mlango wa kubainisha sehemu miongoni mwa aina za uchawi:
Amesema Ahmad: Alituhadithia Muhammadi bin Ja'far, alitusimulia Auf, Alituhadithia Hayyan bin Alaa, alituhadithia Qatwan bin Qabiiswa, kutoka kwa baba yake, yakwamba yeye alimsikia Mtume Sala na Amani ziwe juu yake akisema: "Hakika (kuamini mikosi ya) sauti za ndege, na kupiga ramli na mikosi ni katika uchawi"
Amesema Aufu: (Iyafa: ni sauti ya ndege, na Twarq: ni mchoro huchorwa ardhini)
Na jibtu:
Amesema Hasan: (Ni Mlio wa shetani).
Isnadi yake ni nzuri, na imepokelewa kwa Abuudaudi na Nasaai na bin Hibban katika sahihi yake inayonasibishwa kwake.
Na kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mtume wa ALLAH -Sala na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Atakayejifunza sehemu katika elimu ya nyota; basi atakuwa kajifunza sehemu katika uchawi, amezidisha anavyozidisha." Imepokelewa na Abuu Daud na Isnad yake ni sahihi.
Na imenukuliwa kutoka kwa Nasaai katika hadithi ya Abuu Huraira Radhi za ALLAH ziwe juu yake: "Atakayefunga fundo lolote kisha akalipulizia basi atakuwa ameroga, na atakayeroga atakuwa kafanya shirki, na atakayetundika imani yake katika kitu basi atawakilishwa kwacho"
Na kutoka kwa bin Mas'udi Yakwamba Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Je nisikufahamisheni nini Adh-hu? ni umbea, kuhamisha hamisha maneno ya fitna baina ya watu." Imepokelewa na Imamu Muslim
Na imepokelewa kutoka kwa Ibnu omar -Radhi za mwenyezi mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa ALLAH-Sala na Amani ziwe juu yake na amani- amesema: (Hakika katika ufasaha kuna uchawi".
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Hakika (kuamini mikosi ya) sauti za ndege, na kupiga ramli na mikosi ni katika uchawi
La pili Tafsiri ya mikosi ya sauti za ndege, kupiga ramli, na mikosi.
La tatu: Nikuwa elimu ya nyota ni katika uchawi.
La nne: Nikuwa kufunga na kupuliza ni katika uchawi pia.
La tano: Nikuwa kusengenya ni katika hayo.
La sita: Nikuwa miongoni mwa hayo ni baadhi ya ufasaha.
Mlango wa yaliyokuja kuhusu makuhani na Mfano wake.
Amepokea Muslim katika sahihi yake kutoka kwa baadhi ya wake wa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake, Kutoka kwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake Amesema: "Atakayemuendea mpiga ramli akamuuliza kuhusu lolote, akamsadikisha haitokubaliwa kwake swala yoyote siku arobaini."
Na kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Atakayemuendea kuhani na akamsadikisha kwa yale anayoyasema basi atakuwa amekufuru yale yaliyoteremshwa kwa Muhammadi Sala na Amani ziwe juu yake" Imepokelewa na Abuu Daud
Na imepokelewa kwa Maimamu wanne na imamu Hakim pia.
Na akasema ni hadithi sahihi: Ambayo iko katika sharti zao (Bukhari na Muslim) kuhusu "Atakayemuendea mpiga ramli au kuhani na akamsadikisha kwa yale anayoyasema basi atakuwa amekufuru yale yaliyoteremshwa kwa Muhammadi Sala na Amani ziwe juu yake"
Na imepokelewa kutoka kwa Abuu Ya'laa
Kwa isnadi jayyid, kutoka kwa bin Mas'udi hadithi mfano wake ambayo ni Marfu'u:
Na kutoka kwa Imran bin Huswain Radhi za ALLAH ziwe juu yake Hadithi Marfu'u: "Si miongoni mwetu mwenye kuitakidi mikosi kupitia ndege, au mwenye kuwa kuhani au akafanyiwa ukuhani, au akafanya uchawi, au akataka afanyiwe uchawi, na atakaye mwendea kuhani na akamsadikisha ayasemayo, basi huyo kayakufuru aliyokuja nayo Muhammad -Sala na amani ziwe juu yake. kaipokea Al Bazzaru kwa Isnadi Jayyid.
Na kaipokea Twabaraaniy katika kitabu (Al Ausat) kwa Isnad Hasan katika hadithi za bin Abbas: bila kuwa na kauli yake (Na atakayemuendea kuhani) mpaka mwisho.
Amesema Al Baghawiy: (Mpiga ramli: Ni yule anayedai kujua mambo kwa kutumia viashiria anavyovitumia kama hoja kwa yule aliyeibiwa na mahala kilipo kilichopotea na mfano wa hayo)
Na inasemekana maana yake ni Kuhani, Na kuhani ni yule anayetoa habari za mambo yaliyofichikana yatakayotokea baadaye.
Na inasemekana ni yule anayeeleza yaliyoko moyoni.
Na amesema Abul Abbas bin Taimiya: (Mpiga ramli: ni jina na kuhani na mtazamia nyota na mpiga bao na mfano wao miongoni mwa wale wanaozungumzia kujua mambo kupitia njia hizi)
Na alisema bin Abbas kuhusu watu wanaoandika Alfabeti za kiarabu na wanatazamia nyota: (Sioni kama mwenye kufanya hivyo kama anafungu lolote mbele ya ALLAH).
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Nikuwa havikai pamoja kumuamini kuhani na imani ya Qur'ani.
La pili Kumewekwa wazi kuwa huo ni ukafiri.
La tatu: Kutajwa mwenye kufanyiwa ukuhani.
La nne: Kutajwa mwenye kutazamiwa mikosi.
La tano: Kutajwa mwenye kufanyiwa uchawi.
La sita: Ametajwa mwenye kujifunza kupiga ramli kwa Alfabeti za kiarabu.
La saba: Kumetajwa tofauti kati ya kuhani na mpiga ramli.
HUU NI MLANGO ULIO KUJA KUELEZEA UHARANU WA KUONDOA UCHAWI MWILINI KWA KUTUMIA UCHAWI.
Kutoka kwa Jaabiri: yakwamba Aliulizwa Mtume Salana Amani ziwe juu yake kuhusu kutibu uchawi kwa uchawi, Akasema: "Akasema hiyo ni katika kazi za shetani" kaipokea Ahmad kwa isnadi Jayyid, na Abuudaud, na akasema: aliulizwa Ahmadi kuhusu hili akasema: bin Mas'udi alikuwa akilichukia hili.
Na katika sahihi Bukhari kutoka kwa qatadah: nilisema kumwambia Abul Musayyib: (kwa mfano mtu kapatwa na uchawi, au kafungwa kumwendea mkewe, je afunguliwe au aondolewe uchawi kwa uchawi?
Akasema: (Hakuna tatizo, kwani watu hutafuta kwa mambo hayo kutengeneza, ama yenye manufaa hayakukatazwa) Mwisho wa kunukuu.
Na imepokelewa kutoka kwa Hassan yakwamba yeye amesema: "Hauondoi uchawi ila mchawi".
Na amesema ibnul Qayyim: (Nushra: Maana yake: Ni kuondoa uchawi kwa aliyerogwa, nayo ina aina mbili:
Ya kwanza: Kuuondoa kwa uchawi mfano wake, ambayo ni katika matendo ya shetani,na kwa hili ndiyo inafasiriwa kauli ya Hasan, utakuta anajikurubisha mfanyaji wake na yule mwenye kuzinguliwa (mwenye kutibiwa) kwa shetani kwa yale anayoyapenda basi hapo ndiyo anabatilisha kazi aliyoifanya kwa huyu aliyerogwa.
Ya pili: Kuuondoa uchawi kwa kutumia Ruqya (kisomo) na kinga za dua na dawa na maombi ya halali hili linafaa kisheria)
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Katazo la kuondoa uchawi kwa uchawi.
La pili Tofauti kati ya yaliyokatazwa na yaliyoruhusiwa ni katika mambo yanayoondoa utata.
Mlango wa yaliyokuja katika kuamini mikosi.
Na amesema ALLAH Mtukufu: {Tambueni kuwa hakika mambo yenu yote yako kwa Allah, lakini wengi wao hawajui} [Al A'raf:131].
na kauli yake: Wakasema mikosi ipo pamoja na nyie hata kama mkikatazwa isipokuwa nyie ni watu waovu. [Yasin: 19].
Na kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume ALLAH na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Hakuna kuambukizana maradhi wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, wala mkosi wa Bundi, na aina zingine za ndege, wala kutuhumu kuwa mwezi wa safari unamikosi, au maradhi ya tumbo yanayompata ngamia." Wameitoa hadithi hii Maimamu wawili.
Akaongeza Muslim: "(Na wala hakuna kuamini mikosi ya nyota wala mikosi ya baadhi ya wanyama).
Na wamepokea maimamu wawili kutoka kwa Anasi Amesema , Amesema Mtume Sala na Amani zimfikie: "Hakuna kuambukizana maradhi, wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, na kinachonipendeza zaidi ni kujipa matumaini. Wakasema: Ni nini matumaini?
Akasema: (Ni neno jema)
Na imepokelewa kwa Abuudaud kwa Isnadi Sahihi kutoka kwa Uqba bin Aamir Amesema: Lilitajwa swala la mikosi kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: (Kilichobora zaidi ni kujipa matumaini, na wala mikosi haiwezi kumrudisha muislamu, atakapoona mmoja wenu anachokichukia basi na aseme: Ewe ALLAH hakuna aletaye mazuri ila wewe, na wala hakuna azuiaye mabaya ila wewe, na hakuna ujanja wala nguvu ila kwako).
Na kutoka kwa bin Mas'udi hadithi Marfu'u: "Mikosi ya ndege ni shirki, na hakuna yeyote miongoni mwetu isipokuwa (ana chembe ya hilo), lakini ALLAH huliondoa kwa kumtegemea" kaipokea Abuudaud na Tirmidhiy na akaisahihisa, na akafanya mwisho wa hadithi hii ni katika kauli za bin Mas'udi.
Na imenukuliwa kutoka kwa Ahmad katika hadithi za bin Amri: "Itakayemrudisha imani ya mkosi wa ndege akaacha shida yake basi atakuwa amefanya shirki", wakasema: Ni ipi kafara ya hilo? Akasema: "ni useme: Ewe Mwenyezi Mungu hakuna kheri ila kheri yako, na hakuna ndege isipokuwa ndege wako, na hakuna Mola zaidi yako."
Na pia Kutoka kwa Fadh-li bin Abbas -Radhi za ALLAH ziwe juu yake- "Hakika imani ya mikosi ni kila kitakachokufanya uende ama urudi"
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Tahadhari juu ya kauli yake: (Tambueni kuwa mambo yao yote yako kwa ALLAH) pamoja na kauli yake: (Ukorofi wenu uko pamoja nayi)
La pili kukanushwa kuambukizana.
La tatu: Kukanushwa mikosi ya ndege.
La nne: Kukanushwa mikosi ya bundi.
La tano: Kukanushwa mikosi ya mwezi swafar au mwezi wowote.
La sita: Nikuwa kujipa matumaini si katika hayo.
La saba: tafsiri ya neno matumaini.
La nane: Nikuwa kinachojitokeza nyoyoni pamoja nakuwa hakipendezi lakini hakidhuru imani ya mtu, bali anakiondosha ALLAH kwa kumtegemea.
La tisa: Kumeelezwa ni yapi ya kusema atakayejihisi hivyo.
La kumi: Kumewekwa wazi kuwa mikosi ni katika ushirikina.
La kumi na moja: Tafsiri ya imani ya mikosi iliyokatazwa
HUU NI MLANGO ULIO KUJA KUKATAZA UBAYA WA KUPIGA RAMLI KUPITIA NYOTA.
Amesema Bukhari katika kitabu chake (Sahihi) Amesema Qatada: "Aliziumba ALLAH nyota hizi kwa malengo matatu: Pambo la mbingu, na kwa kuwapigia mashetani, na alama za kuongozea wasafiri, atakayetafsiri katika nyota hizo tofauti na hapo atakuwa kakosea na atakuwa kapoteza fungu lake, na atakuwa kajilazimisha mambo asiyo na elimu nayo" Imeishia hapo.
Na alichukizwa Qatada kujifunza mashukio ya nyota, na hakuliruhusu hilo bin Uyaina, ametaja hayo Harbu kutoka kwao wawili.
Na akaruhusu Ahmad na is-haka kujifunza mashukio.
Na kutoka kwa
Abuu Musa Amesema , Amesema Mtume Sala na Amani zimfikie: "Watu wa aina tatu hawatoingia peponi: Mlevi kupindukia, na mwenye kukata udugu, na mwenye kusadikisha uchawi" kaipokea Ahmad na bin Hibban katika sahihi yake.
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Hekima ya kuumbwa nyota.
La pili Kumjibu mwenye kudai matumizi tofauti na hayo.
La tatu: Kutajwa kwa tofauti za mitazamo katika swala la kujifunza mashukio ya nyota.
La nne: Ahadi ya adhabu kwa atakayesadikisha chochote katika uchawi, hata kama atajua kuwa ni batili.
HUU NI MLANGO ULIO KUJA KUELEZEA UBAYA WA KUOMBA MVUA KWA KTUMIA NYOTA.
Na amesema ALLAH Mtukufu: "Na je mnaifanya shukrani yenu kwa neema za Mola wenu ni kuwa nyinyi mnazikanusha. [Al Waaqiya: 82].
Na kutoka kwa Abuu Maaliki Al Ash'ariy Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Mambo manne ndani ya umma wangu ni katika mambo ya zama za ujinga hawatoyaacha: kujifaharisha kwa vyeo, na kutukana koo, na kuomba mvua kupitia nyota, na kuomboleza".
Na akasema: (Muombolezaji kama hatotubia kabla ya kifo chake atasimamishwa siku ya kiyama akiwa na kanzu ya uji wa shaba iliyoyeyushwa na ngao ya ukurutu (yaani ngozi yake itakuwa mfano wa mwenye ugonjwa wa kupukutika ngozi). Imepokelewa na Imamu Muslim
Na wamepokea kutoka kwa Zaidi bin Khalid Radhi za ALLAH ziwe juu yake Amesema: (Alitusalisha Mtume Sala na Amani ziwe juu yake swala ya Alfajiri tukiwa Hudaibiya baada ya mvua ya usiku, alipomaliza swala akawageukia watu na akasema: "Hivi mnajua ni nini kasema Mola wenu?" wakasema: (ALLAH na Mtume ndio wajuzi zaidi) Akasema: "kumekuwa katika waja wangu na mwenye kuniamini mimi na mwenye kunikufuru, ama aliyesema: Tumenyeshelezewa kwa fadhila za ALLAH na Rehema zake huyo ndiyo mwenye kuniamini mimi na kupinga imani ya nyota, na ama aliyesema: Tumenyeshelezewa kwa nyota kadhaa wa kadhaa, basi huyo ndiyo mwenye kunikufuru mimi mwenye kuziamini nyota)
Na wamepokea pia katika hadithi za
bin Abbas maana yake, "Wakasema baadhi yao: Hakika imesema kweli nyota kadhaa wa kadhaa, akateremsha ALLAH aya hizi: ALLAH Anaapa kwa maporomoko ya nyota nyakati za kuzama kwake mbinguni." Nacho ni kiapo kikubwa lau mnajua kadiri yake. Hakika hiyo ni quran tukufu. iliyo ndani ya kitabu cha asili. Hawaigusi quran isipokuwa walio kuwa wasafi. ni uteremkaji kutoka kwa mlezi wa viumbe hivi mzungumzo hayo nyie mnayapinga. na mnajalia kuwa riziki zenu kuwa nyie mwazipinga. [Al waaqi'a: 75-82]
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya ya suratul waaiqai'a.
La pili Kumetajwa mambo manne ambayo ni katika mambo ya zama za ujinga
La tatu: kutajwa baadhi ya ukafiri
La nne: Nikuwa katika ukafiri upo usiomtoa mtu katika uislamu.
La tano: Kauli yake: (kumekuwa katika waja na mwenye kuniamini mimi na mwenye kunikufuru mimi) kwa sababu ya kushukiwa na neema.
La sita: Kuwa makini na maswala ya imani katika maeneo haya.
La saba: kuwa makini na swala la ukafiri katika maeneo haya.
La nane: kuwa makini katika kauli yake {Hakika imesema kweli nyota kadhaa wa kadhaaa}
La tisa: Mwalimu kumpa elimu mwanafunzi kwa njia ya swali; kwa kauli yake: (Hivi mnajua ni nini kasema Mola wenu?)
La kumi: Ahadi ya adhabu kwa mpiga mayowe kwa kuomboleza.
HUU NI MLANGO WA KAULI YAKE ALLAH MTUKUFU. "Na miongoni mwa watu, wako wanaojifanyia kinyume na ALLAH miungu wengine wanawapenda kama wanavyompenda ALLAH," [Baqara: 165].
Na kauli yake: Sema ewe MUHAMMAD kama ikiwa baba zenu na watoto wenu na ndugu zenu na wake zenu na familia zenu na mali mlizo zichuma na biashara mnazo ogopa kupata hasara na makazi mnayo yaridhia yanapendeza zaidi kuliko ALLAH na mtume wake na kupigania jihad katika njia yake basi subirini mpaka ALLAH alete jambo lake ALLAH hawaongozi watu wachafu. [Tauba: 24].
Na kutoka kwa Anasi: Yakwamba Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hawezi kuamini mmoja wenu mpaka niwe napendeka kwake zaidi kuliko mtoto wake, na mzazi wake, na watu wote." Wameitoa hadithi hii Maimamu wawili.
Na wamepokea maimamu wawili kutoka kwa Anasi Amesema , Amesema Mtume Sala na Amani zimfikie: "Mambo matatu yatakayokuwa kwake basi atapata kwa mambo hayo ladha ya imani: Awe ALLAH na Mtume wake wanapendeka zaidi kwake kuliko yeyote asiyekuwa wao, na ampende mtu si kumpenda kwa lolote ila ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na achukie kurudi katika ukafiri baada ya ALLAH kumuokoa kama anavyochukia kutupwa motoni"
Na katika upokezi (Hawezi kupata yeyote ladha ya imani mpaka) Mpaka mwisho wa hadithi
Na Kutoka kwa bin Abbas- Radhi za Allah ziwe juu yao amesema: "Atakayependa kwa ajili ya ALLAH, na akachukia kwa ajili ya ALLAH, na akafanya urafiki kwa ajili ya ALLAH, na akafanya uadui kwa ajili ya ALLAH, kwani hakika hupatikana mapenzi ya ALLAH kwa mambo hayo, na hatopata mja utamu wa Imani hata kama swala zake na swaumu zake zitakuwa nyingi mpaka awe hivyo, na hakika leo hii umekuwa urafiki wa watu wengi ni kwa ajili ya mambo ya kidunia na hilo haliwapatishi chochote wafanyaji wake" Imepokelewa na Ibnu Jariri
Na Amesema bin Abbasi katika kauli yake Mtukufu: "Na zikakatikakatika kwao sababu zote" Anasema: Maana yake ni (mapenzi).
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya ya suratul Baqara.
La pili Tafsiri ya aya za suratu baraa.
La tatu: Ulazima wa kumpenda Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kuliko hata nafsi na familia na mali.
La nne: Nikuwa kukanushwa (kuwa hana imani) hakumaanishi ni kutoka katika uislamu.
La tano: Nikuwa kumbe Imani ina utamu anaweza kuupata mtu, na anaweza kuukosa pia.
La sita: Matendo ya moyo manne yaliyotajwa ambayo haupatikani ukaribu na ALLAH isipokuwa kwa mambo hayo,na wala hawezi kupata yeyote utamu wa Imani isipokuwa kwa mambo hayo.
La saba: Uelewa wa maswahaba juu ya hali halisi ya mazingira: kuwa urafiki mwingi ni katika mambo ya kidunia.
La nane: Tafsiri ya (Na zikakatikakatika kwao sababu zote).
La tisa: Nikuwa miongoni mwa washirikina wapo wanaompenda Mwenyezi Mungu mapenzi makubwa.
La kumi: Ahadi ya adhabu kali kwa ambaye mambo manane yatapendeka zaidi kwake kuliko dini yake.
La kumi na moja: Nikuwa yeyote atakayefanya mshirika ambaye mapenzi yake yatakuwa sawa na mapenzi ya ALLAH basi atakuwa kafanya shirki kubwa.
MLANGO HUU UMEKUJA KUELEZEA KAULI YAKE ALLAH MTUKUFU: shani ya jambo ilivyo huyo nishetani anawahofisha vipenzi wake basi msimuogope niogopeni ikiwa nyinyi ni waumini. [Al-Imran: 175].
Na kauli yake ALLAH MTUKUFU: Shani ya jambo ilivyo anae imarisha misikiti ya ALLAH ni yule aliye muamini ALLAH na siku ya mwisho na akatoa zaka na hakuogopa isipokuwa ALLAH hakika hao watakuwa miongoni mwa walio ongoka. [Tauba: 18].
na kauli yake: kuna miongoni ya watu anasema ameamini anapo pewa maudhi kwa ajili ya ALLAH analinganisha fitna za watu mfano wa adhabu za ALLAH" [Al Ankabut: 10].
Kutoka kwa Abuu Saidi Radhi za Allah ziwe juu yake Hadithi Marfu'u: "Hakika katika udhaifu wa yakini ni kuwaridhisha watu kwa kumchukiza ALLAH, na kuwashukuru juu ya riziki ya ALLAH, na kuwasema vibaya kwa kile ambacho hajakupa ALLAH, na hakika riziki ya ALLAH haivutwi na pupa ya mwenye kupupia na wala haizuiliwi na chuki ya mwenye kuchukia".
Na imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za ALLAH ziwe juu yake -kwamba Mtume wa ALLAH-Sala na amani za ALLAH ziwe juu yake - amesema: "Atakayetafuta kumridhisha Mwenyezi Mungu kwa kuwachukiza watu basi ALLAH atamridhia na watu watamridhia, na atakayetafuta kuwaridhisha watu kwa kumchukiza Mwenyezi Mungu basi ALLAH atamchukia na watu watamchukia" Kaipokea Ahmad na bin Hibban katika sahihi yake.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya ya suratul Al imran.
La pili Tafsiri ya aya za suratu baraa.
La tatu: Tafsiri ya aya ya suratul Ankabut.
La nne: Nikuwa yakini hudhoofika na kuimarika.
La tano: Alama za kudhoofika kwake na miongoni mwazo ni mambo haya matatu.
La sita: Nikuwa kutakasa hofu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni katika mambo ya lazima.
La saba: Kutajwa kwa malipo ya mwenye kulifanya hilo.
La nane: Kutajwa kwa adhabu ya mwenye kuliacha hilo.
HUU NI MLANGO ULIYO KUJA KUELEZEA KAULI YAKE ALLAH MTUKUFU. Na tegemeeni kwa ALLAH ikiwa ni waumini. [Maaida: 23].
Na kauli yake ALLAH MTUKUFU: Si vinginevyo hakika waumini ni wale ambao anapotajwa ALLAH inapata uwoga mioyo yao na wanapo somewa juu yao aya zetu zinawazidishia imani na kwa MOLA wao wanategemea. [Al-anfaal: 2]
na kauli yake ALLAH: Ewe Nabii akutosha ALLAH na wale ambao walio kufuata miongoni mwa waumini" [Anfal: 64].
na kauli yake ALLAH MTUKUFU Na mwenye kumtegemea ALLAH basi ALLAH ni mwenye kumtosha. [Twalaq: 3].
Na Kutoka kwa bin Abbas- Radhi za Allah ziwe juu yao amesema: "Anatutosha ALLAH na yeye ndiye mbora wa kutegemewa" Neno hili alilisema Ibrahim Amani ALLAH iwe juu yake pindi alipotupwa motoni, na alilisema Muhammadi pindi waliposema kumwambia: Hakika watu wamejikusanya kwa ajili yenu waogopeni ikawazidishia imani na wakasema anatutosha ALLAH na ndiye mbora wa kutegemewa" [Al-Imran: 173]. Ameipokea Bukhari na Al- nasaai.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Nikuwa; kumtegemea ALLAH ni katika mambo ya lazima.
La pili Nikuwa hilo ni katika sharti za Imani.
La tatu: Tafsiri ya aya ya suratul Anfal.
La nne: Tafsiri ya aya kuwekwa mwisho wake.
La tano: Tafsiri ya aya ya suratu Twalaqa.
La sita: Ukubwa wa swala la neno hili, nakuwa ni miongoni mwa kauli za Ibrahim Amani iwe juu yake na Muhammadi Sala na Amani ziwe juu yake wakati wa matatizo.
HUU NI MLANGO ULIO KUJA KUELEZEA KAULI YAKE ALLAH MTUKUFU: hivi wanajiaminisha na vitimbi vya ALLAH hakuna anaye jiaminisha na vitimbi vya ALLAH isipokuwa watu walio pata hasara. [A'raf: 99].
Na kauli yake ALLAH mtukufu: Hakuma anaye kata tamaa na huruma za MOLA wake isipokuwa wapotevu. [Al Hijri: 56].
Kutoka kwa bin Abbas: yakwamba Aliulizwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake kuhusu madhambi makubwa, Akasema: "Ni kumshirikisha ALLAH na kitu kingine, na kukata tamaa na rehema za ALLAH, na kujiaminisha na adhabu za ALLAH"
Kutoka kwa Ibnu Masoud- Radhi za Allah ziwe juu yake alisema: "Madhambi makubwa kuliko yote: Ni kumshirikisha ALLAH, na kujiaminisha na adhabu za ALLAH, na kukata tamaa na rehema za ALLAH, Na kufa moyo katika huruma za ALLAH" Imepokelewa na Abdurazaq.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya ya suratul A'raf.
La pili Tafsiri ya aya ya suratul Hijri.
La tatu: Ahadi ya adhabu kali kwa atakayejiaminisha na adhabu za ALLAH.
La nne: Ahadi ya adhabu kali katika kukata tamaa.
MLANGO HUU UMEKUJA KUELEZEA NI SEHEMU YA IMANI KUFANYA SUBRA JUU YA MAKADIRIO YA ALLAH.
Na kauli ya Allah Mtukufu: "Na atakayemuamini ALLAH atauongoza moyo wake na Mwenyezi Mungu kwa kila kitu ni Mjuzi" [Attaghaabun: 11].
Amesema Alqama: (Ni mtu kupatwa na msiba na akajua kuwa umetoka kwa ALLAH akaridhia na akakubaliana na hilo)
Na katika sahihi (Muslim) kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Mambo mawili kwa watu hayo kwao ni ukafiri: Kutukana ukoo, na kulia kwa kumuomboleza maiti"
Na Imepokelewa kwa Bukhari na Muslim kutoka kwa bin Mas'udi Hadithi Marfu'u: "Si miongoni mwetu atakayepiga mashavu, na akachana mifuko ya nguo, na akalalamika kwa malalamiko ya zama za ujinga"
Na imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za ALLAH ziwe juu yake -kwamba Mtume wa ALLAH-Rehema na amani za ALLAH ziwe juu yake - amesema: "Anapotaka ALLAH kwa mja wake kheri humharakishia mateso duniani, na anapotaka kwa mja wake shari humzuilia dhambi lake ili amlipe kwalo siku ya qiyamah"
Amesema Mtume Sala na Amani za ALLAH ziwe juu yake: "Hakika ukubwa wa malipo huendana sawa pamoja na ukubwa wa matatizo, na hakika ALLAH Mtukufu anapowapenda watu huwapa mtihani; atakayeridhia atapata radhi, na atakayechukia atapata hasira. Kaifanya kuwa Hadithi Hasan Imamu Tirmidhi.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya ya suratu ttaghaabun.
La pili Nikuwa hili ni katika kumuamini ALLAH.
La tatu: Kutukana ukoo.
La nne: Ahadi ya adhabu kali kwa atakayepiga mashavu, na akachana mifuko ya nguo, na akalalamika kwa malalamiko ya zama za ujinga.
La tano: Alama ya ALLAH kumtakia mja wake kheri.
La sita: Na alama ya ALLAH kumtakia shari.
La saba: Alama ya ALLAH kumpenda mja.
La nane: kuharamishwa kuchukia na kulalamika.
La tisa: Malipo ya kuridhia mtihani.
MLANGO HUU UNAZUNGUMZIA UBAYA WA KUJIONESHA:
Na amesema ALLAH Mtukufu: Sema ewe MUHAMMAD hakika si vinginevyo mimi ni mtu mfano wenu nimeshushiwa ufunuo hakika MOLA wenu ni MUNGU MMOJA basi atakaye tarajia kukutana na MOLA wake basi afanye matendo mazuri na wala asishirikishe katika ibada ya MOLA wake na kitu chochote. [Al Kahf: 110].
Na hadithi imepokelewa kutoka kwa abuu Huraira - Mar-fuu. (Amesema ALLAH Mtukufu: Mimi nimejitosheleza na washirika juu ya kushirikishwa; atakayefanya jambo lolote akamshirikisha pamoja nami mwingine nitamuacha na shirki yake. Imepokelewa na Imamu Muslim
Na hadithi imepokelewa kutoka kwa abuu Saidi- Mar-fuu. (Je nisikuelezeni ninachokihofia zaidi kwenu nyinyi kuliko hata Masihi Dajali?)
Wakasema: (Tueleze Ewe Mjumbe wa ALLAH). Akasema: (Ni shirki iliyofichikana, anasimama mtu kuswali anaipendezesha swala yake kwakuwa anaona kuna mtu anamtazama). Imepokelewa na Ahmad
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya ya suratul kahf.
La pili Hapa kuna jambo kubwa nalo ni kurejeshwa amali njema itakapoingiliwa na kitu kinyume na ALLAH.
La tatu: Kutajwa kwa sababu inayopelekea hilo nalo ni kukamilika kwa kujitosheleza.
La nne: Nikuwa miongoni mwa sababu: Nikuwa yeye ni mbora wa washirika.
La tano: Hofu ya Mtume Sala na Amani zimfikie kwa maswahaba zake kutokana na riyaa.
La sita: Nikuwa yeye alilitafsiri hilo kuwa ni mtu kuswali kwa ajili ya ALLAH lakini anaipendezesha kwa kile anachokiona kama mtu kumtazama.
HUU NI MLANGO UNAO ELEZEA KUWA KUTOKANA NA USHIRIKINA NI MTU KUTAKA KWA MATENDO YAKE YA KIDUNIA:
Na kauli ya Allah Mtukufu: Ambaye anataka maisha ya dunia na mapambo yake tutawapa matendo yao na wao hawato punjwa Hao ndio ambao hawana wao siku ya qiyamah isipokuwa moto na yameporomoka yote waliyo yafanya ndani ya dunia na yamekuwa ni batili yote waliyo yafanya. [Hud: 15-16].
Na imepokelewa katika sahihi Bukhari kutoka kwa Abuu Huraira Amesema , Amesema Mtume Sala na Amani zimfikie: "Amepata hasara mtumwa wa dunia, amepata hasara mtumwa wa Dirham.
Amepata hasara mja wa mavazi.
Amepata hasara mja wa misitu
akipewa anaridhia na asipopewa ana chukia, amepata hasara na mambo yamemwendea mrama, na hata akichomwa mwiba hawezi kuutoa.
Pongezi kwa mja atakayechukua kamba ya farasi wake kwenda katika njia ya ALLAH, kichwa chake kikitimka vumbi, nyayo zake zikiwa zimejaa vumbi.
Akiwa katika ulinzi basi anasimamia vizuri ulinzi.
Na akiwa mwisho jeshi basi anasimamia vizuri pia
Hata akiomba ruhusa haruhusiwi, na hata akimtetea yeyote hasikilizwi"
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Mtu kutaka maslahi ya dunia kwa amali ya Akhera.
La pili Tafsiri ya aya ya suratu Hud.
La tatu: kuitwa mtu muislamu kuwa ni mtumwa wa dinari (pesa) na dirham na mavazi.
La nne: Kutafsiriwa hilo kuwa yeye akipewa huridhia na asipopewa huchukia.
La tano: kauli yake (Amepata hasara na mambo yake yamemwendea mrama)
La sita: kauli yake: (Na hata akichomwa mwiba hawezi kuutoa)
La saba: kusifiwa kwa mpigana jihadi mwenye kusifika na sifa hizo.
MLANGO UNAO ZUNGUMZIA UHARAMU WA KUWATII WANAZUONI NA VIONGOZI KATIKA KUHARAMISHA ALIYO HALALISHA ALLAH AU KUHALALISHA ALIYO HARAMISHA ALLAH HAKIKA WAMEWAFANYA KUWA NI MIUNGU KINYUME NA ALLAH:
Na amesema Ibni Abas: "Inahofiwa kushukiwa na mawe juu yenu kutoka mbinguni nina waambia Alisema Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake,na nyie mnasema alisema Abubakar na Omar.
Na amesema Ahmad bin Hanbal: (Nawashangaa watu waliojua usahihi wa mapokezi ya maneno ya Mtume Sala na Amani ziwe juu yake wanafanyia kazi rai ya Sufyani, na ALLAH Mtukufu anasema: "Basi nawatahadharisha wanao halifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu." [An Nur 63] Hivi mnajua fitina ni ipi? Fitina maana yake ni Shirki huwenda akipinga baadhi ya maneno ya Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake ikaingia katika moyo wake shaka ikawa ni sababu ya kuangamia."
Kutoka kwa Adiy bin Haatim: Yakwamba yeye alimsikia Mtume Sala na Amani ziwe juu yake akisoma aya hii: Wamewafanya wanazuoni wao na mapadri wao kuwa ni miungu kinyume na ALLAH na ISSAH mwana wa MARIAM na hawakuamrishwa isipokuwa wamuabudu mungu mmoja[ALLAH] hakuna wa kuabudiwa isipokuwa yeye utakasifu ni wake kwa yote wanayo mshirikisha. [At Tauba: 31]. Nilisema: nikasema kumwambia: Hakika sisi hatuwaabudu wao.
Akasema: "Hivi kwani hawaharamishi aliyoyahalalisha ALLAH nanyi mkayaharamisha, na wakahalalisha aliyoyaharamisha ALLAH nanyi mkahalalisha?"
Nikasema: Ndivyo.
Akasema: "Basi huko ndiko kuwaabudu" Ameipokea Ahmad na Tirmidhiy na akaifanya kuwa hadithi Hasan.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya ya suratu nnur.
La pili Tafsiri ya aya za suratu baraa.
La tatu: Tahadhari juu ya maana ya ibada aliyoikanusha Adiy.
La nne: Kupiga mfano bin Abbas wa Abuubakar na Omar, na kupigia mfano Ahmad wa Sufyani.
La tano: Kubadilika kwa hali kutoka katika malengo haya mpaka ikawa kwa watu wengi ni ibada ya kuwaabudu watu wema katika dini yao, na likaonekana hilo kuwa ndiyo jambo bora, na linaitwa ni kutaka mapenzi na ukaribu kwao, na ibada ya kuwaabudu wanavyuoni ni kwa elimu na utambuzi, kisha hali ikabadilika mpaka kufikia kuabudiwa kinyume na ALLAH ambao si katika watu wema, na kuabudiwa kwa maana ya pili ni kuwaabudu hao wanavyuoni mtu ambaye ni miongoni mwa wajinga.
Mlango wa kauli ya ALLAH Mtukufu: Umepata kuona ewe MUHAMMAD kwa wale ambao wanadai kuwa wao wameamini yale uliyo teremshiwa juu yako na yale yaliyo teremshwa kabla yake wanataka wakahukumiane kwa miungu na hakika wameamrishwa waipinge hiyo miungu na anataka shetani awapoteze kupotea kwa mbali. Wanapo ambiwa wao njooni kwa yale yaliyo teremsha ALLAH na kwa MTUME utwaona ewe MUHAMMAD wanajizuia kwako kujizuia kweli kweli. Itakuwaje watakapo potwa na matatizo kwa yale yaliyo tangulizwa na mikono yao kisha wakakujia wakimuapa ALLAH hatuja kusudia -hayo-isipokuwa ni wema na kupata kuwafiqishwa. [An nisaa: 60-62].
na kauli yake: "Wanapopewa nasaha wakome kufanya uharibifu katika ardhi kwa kukanusha na kuasi kutoa siri za Waumini na kuwategemea makafiri, huwa wakisema kwa uongo na kubisha, “Sisi ndio watu wakutengeneza.” [Al baqara: 11].
na kauli yake: Na wala msifanye ufisadi katika ardhi baada ya kutengamaa na muombeni[ALLAH]kwa kuogopo na kutamani hakika huruma ya ALLAH ipo karibu na wafanyao vizur. [Al A'raf: 56].
na kauli yake: Hivi hukmu za kijinga ndio wanazitaka na ninani aliye mbora wa kuhukumu kuliko ALLAH kwa watu wenye yaqini. [Al-maida 50].
kutoka kwa Abdillah bin Amri Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hatokuwa na imani mmoja wenu mpaka yale matamanio yake ni yenye kufuata yale niliyokujua nayo"
Amesema Imamu Nawawi: (Hadithi hii ni sahihi, tumeipokea kutoka katika kitabu (Al Hujja) kwa isnadi sahihi).
Na amesema Sha'biy: (Kulitokea Ugomvi kati ya mtu mmoja mnafiki na mwingine Yahudi).
Akasema yule Yahudi: Twende tukahukumiane kwa Muhammad.
Yahudi alijua kuwa Muhammadi hapokei Rushwa.
Akasema Yule mnafiki: Tukahukumiane kwa Yahudi, kwakuwa alijua huwa wanachukua rushwa.
Wakakubaliana waende kwa kuhani mmoja maeneo ya Juhaina, akahukumiana kwake basi ikateremka: "Kwani hukujua, ewe Mtume, mambo ya wale wanafiki wenye kudai" mpaka mwisho wa aya. [An nisaa: 60-62].
Na inasemekana: (Iliteremka kwa sababu ya watu wawili waligombana, akasema mmoja wao: (Tupelekane kwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake) Na akasema mwingine: (Twende kwa Ka'bu bin Ashraf) kisha wakapelekana kwa Omar, mmoja akamueleza kisa kilivyokuwa.
Omari akasema kumuuliza yule ambaye hakuridhishwa na hukumu ya Mtume Sala na Amani ziwe juu yake: (Ndiyo hivyo anavyosema ndugu yake?)
Yule bwana akasema: (ndiyo); Basi Omar akampiga panga akamuuwa).
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya ya suratun nisaa, pamoja msada uliko wa kuifahamu maana ya Twaghuti.
La pili Tafsiri ya aya Suratul Baqara: (Na wanapoambiwa msifanye uharibifu katika ardhi}.
La tatu: Tafsiri ya aya ya suratul A'raaf: {na wala msifanye uharibifu katika ardhi baada ya kutengemaa kwake}.
La nne: Tafsiri ya {Hivi hukumu za kijinga ndizo wanazotaka}
La tano: Ni yale aliyoyasema Sha'biy katika sababu ya kuteremka aya ya kwanza.
La sita: Tafsiri ya imani ya kweli na ya uongo.
La saba: Kisa cha Omar pamoja na mnafiki.
La nane: Kuwa imani haiwezi kupatika kwa yeyote mpaka yawe matamanio yake ni yenye kufuata yale aliyokuja nayo Mtume Sala na Amani ziwe juu yake.
MLANGO UNAO ELEZEA HUKMU YA ATAKAYE PINGA CHOCHOTE MIONGONI MWA MAJINA YA ALLAH.
Na amesema ALLAH Mtukufu: Na wao wao wanampinga ARHMANI[mwingi wa huruma]sema ewe MUHAMMAD ndiye MOLA wangu hapana MOLA apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye juu yake nimetegemea na kwake yeye ndio marejeo. [Al Ra'd: 30].
Na katika sahihi Bukhari amesema Ally: (Waelezeni watu mambo wanayoyafahamu, hivi mnataka apingwe ALLAH na Mtume wake)
Na amepokea Abdulrazzaq kutoka kwa Ma'mar, kutoka kwa Twaus, kutoka kwa baba yake, Kutoka kwa bin Abbasi -Radhi za ALLAH ziwe juu yao- yakwamba yeye alimuona mtu alishituka aliposikia mazungumzo kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika sifa (za Allah) -akafanya kama ishara ya kulipinga hilo- akasema: "Ni nini kinachowaogopesha hawa? wanapatwa na ulaini (wanazikubali) aya zilizo wazi, na wanaangamia katika aya zinazotatiza". mwisho
Na walipomsikia Makuraishi Mtume Sala na Amani ziwe juu yake akimtaja Al Rahmaan -Mwingi wa HURUMA- walilipinga hilo, kateremsha ALLAH kuhusiana nao: {Na hali wao wanamkurufu Al Rahmaan -Mwingi wa HURUMA} [Al Ra'd: 30].
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Kukosekana kwa Imani kwa kitendo cha kupinga chochote katika majina na sifa.
La pili Tafsiri ya aya ya suratul Ra'd.
La tatu: Kuacha kuzungumza mambo ambayo hayaelewi msikilizaji.
La nne: Kutajwa sababu ya hilo nikuwa hupelekea kupingwa ALLAH na Mtume wake, hata kama mpingaji atakuwa hajakusudia.
La tano: Maneno ya bin Abbas kwa yeyote atakayepinga chochote katika hayo nakuwa hilo litamuangamiza.
MLANGO WA KAULI YAKE ALLAH MTUKUFU: Wana fahamu neema za ALLAH kisha wanazipinga na wengi wao ni makafiri. [An Nahli: 83].
Amesema Mujahidi katika maneno ambayo maana yake ni: (Ni kauli ya mtu kusema: Hii ni mali yangu nimeirithi toka kwa baba zangu).
Na amesema 'Aun bin Abdillah: (wanasema: Lau kama si fulani basi isingekuwa kadhaa).
Na amesema bin kutaiba: (wanasema: Limetokea hili kwa sababu ya utetezi wa miungu yetu).
Na amesema Abul Abbas baada ya mazungumzo ya Zaidi bin Khalid ambayo ndani yake kuna: nikuwa ALLAH Mtukufu amesema: "kumekuwa miongoni mwa waja wangu na mwenye kuniamini na mwenye kunikufuru" mpaka mwisho wa hadithi na tumeshaitaja mwanzoni
Na mifano kama hii ni mingi sana katika Qur'ani na sunna, anamkemea ALLAH Mtukufu kila mwenye kuziegemeza neema zake kwa asiyekuwa yeye na akamshirikisha na kitu kingine.
wamesema baadhi ya wema waliotangulia: (Hii ni kauli ya baadhi ya watu: Upepo ulikuwa mzuri, na Nahodha pia alikuwa mahiri, na mfano wa hayo miongoni mwa yale ambayo yamezoeleka katika ndimi za watu wengi).
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Tafsiri ya kukiri neema na kuikanusha kwake.
La pili Kujua kuwa swala hili limezoeleka katika ndimi za watu.
La tatu: kuitwa maneno haya kuwa ni kukufuru neema.
La nne: kukusanyika kwa vitu viwili vinavyokinzana katika moyo.
MLANGO WA KAULI YAKE ALLAH MTUKUFU: "Basi msimfanyie ALLAH washirika na hali nyinyi mnajua" [Al Baqara 22]
Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbasi kuhusu aya hii: (washirika: ni shirki iliyofichikana kuliko hata unyayo wa sisimizi katika jiwe jeusi tena katika giza nene la usiku).
Nayo ni kusema: Namuapa ALLAH na maisha yako ewe fulani. Naapia maisha yangu.
Na kusema: Lau kama si kijimbwa hiki wezi wangetujia.
Na lau kama si bata hawa hapa nyumbani wezi wangekuja.
Na kauli ya mtu kumwambia mwenzie: Akitaka ALLAH na ukataka wewe.
Na kauli ya mtu laiti kama si ALLH na fulani, usimchanganye hapo fulani hii yote ni shirki. Imepokelewa na bin Abii Hatim
Na kutoka kwa Omar bin Khattwab Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Mwenye kumuapia asiyekuwa Allah atakuwa amekufuru au kamshirikisha Allah." kaipokea Tirmidhiy na akaifanya kuwa hadithi Hasan na akaisahihisha Al Haakim.
Na amesema bin Mas'udi: (kuapa kwangu kwa jina la ALLAH kwa uongo napenda zaidi kuliko kuapa kwa jina la asiyekuwa ALLAH nikisema ukweli"
Na imepokelewa kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za ALLAH ziwe juu yake -kwamba Mtume wa ALLAH-Rehema na amani za ALLAH ziwe juu yake - amesema: (Msiseme: Ni matakwa ya ALLAH na matakwa ya fulani, lakini semeni: Ni matakwa ya ALLAH kisha akataka fulani) Imepokelewa na Abuu Daud na Isnad yake ni sahihi.
Na kutoka kwa Ibrahim An Nakhaiy yakwamba yeye anachukia kauli ya kusema: Najilinda kwa ALLAH na kwako, lakini inafaa kusema: Najilinda kwa ALLAH kisha kwako, Amesema: na kisha mtu aseme: Lau kama si ALLAH kisha fulani, na wala usiseme: Lau kama si ALLAH na fulani.
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya ya suratul Baqara katika maana ya Andaad -washirika-.
La pili Nikuwa maswahaba wanaitafsiri aya iliyoteremka katika shirki kubwa kuwa inakusanya mpaka shirki ndogo.
La tatu: Nikuwa kuapa kwa siyekuwa ALLAH ni shirki.
La nne: Nikuwa mtu akiapa kwa jina la asiyekuwa ALLAH hali yakuwa ni mkweli basi hilo ni dhambi kubwa kuliko kuapa kwa jina la ALLAH na akaongopa.
La tano: Tofauti kati ya kiunganishi 'Na' na 'Kisha' katika matamshi.
MLANGO ULIO KUJA KUELEZEA YULE AMBAYE HAKUTOSHEKA KUMUAPIA ALLAH.
Na imepokelewa kutoka kwa Ibnu omar -Radhi za ALLAHziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za ALLAH ziwe juu yake - amesema: "Msiape kwa majina ya baba zenu, na atakayeapa kwa jina ALLAH basi na aseme ukweli, na atakayeapiwa kwa jina la ALLAH basi na aridhie, na ambaye hatoridhia basi huyo si miongoni mwa (waja) wa ALLAH". Ameipokea bin Maaja kwa isnad nzuri
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: katazo la kuapa kwa majina ya baba.
La pili Kuamrishwa mwenye kuapiwa kwa jina la ALLAH aridhie.
La tatu: Ahadi ya adhabu kwa ambaye hatoridhia.
MLANGO UNAO ELEZEA UBAYA WA KUSEMA AKITAKA ALLAH NA UKITAKA WEWE.
Imepokelewa kutoka kwa Kutaiba yakwamba Yahudi mmoja alikuja kwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake akasema: Hakika nyinyi mnamshirikisha ALLAH.
Mnasema: Akitaka ALLAH na ukitaka wewe:
Na mnasema: Naapa kwa jina la Al-kaaba.
Akawaamrisha Mtume Sala na Amani ziwe juu yake wanapotaka kuapa basi waseme: (Namuapia Mola wa Al-kaaba.
Na waseme: Akitaka ALLAH kisha wewe) Kaipokea Nasaai na akaisahihisha.
Na amepokea pia kutoka kwa bin Abbas: Yakwamba mtu mmoja alisema kumwambia Mtume Sala na Amani ziwe juu yake: Akitaka ALLAH na ukitaka wewe, basi akasema: (Hivi umenifanya mimi kwa ALLAH kuwa mshirika? bali: akitaka ALLAH peke yake).
Na imepokelewa kutoka kwa bin Maajah kutoka kwa Tufaili kaka yake Aisha upande wa mama yake amesema: (Niliota kuwa nimekwenda kwa kundi la Mayahudi.
Nikasema: Hakika nyinyi ni watu sahihi kabisa laiti msingekuwa mnasema: Uzeiri ni mtoto wa ALLAH.
Wakasema: Hata nyinyi ni watu sahihi kabisa laiti kama msingekuwa mnasema Akitaka ALLAH na akataka Muhammad.
Kisha nikapita katika kundi la wakristo: Nikasema: Hakika nyinyi ni watu sahihi laiti kama msingekuwa mnasema: Masihi ni mwana wa mungu.
Wakasema: Hata nyinyi ni watu sahihi kabisa laiti kama msingekuwa mnasema Akitaka ALLAH na akataka Muhammad.
Palipopambazuka nilimueleza ndoto hiyo niliyeweza kumueleza.
Kisha nikamuendea Mtume -Sala na Amani za ALLAH ziwe juu yake- Nikamueleza:
Akasema: (Je ushamueleza yeyote?)
Nikasema: Ndiyo, Akasema:
(Akamshukuru ALLAH na akamsifu,kisha akasema: Baada ya hayo:
Hakika Tufaili ameota ndoto kamueleza aliyemueleza miongoni mwenu.
Na hakika nyinyi mmesema neno ambalo kilinizuia kitu fulani kukukatazeni.
Msiseme: Ni matakwa ya ALLAH na matakwa ya Muhammadi, lakini semeni: Ni matakwa ya ALLAH peke yake.)
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Mayahudi kuijua shirki ndogo.
La pili Kumjua mtu ikiwa kama ana matamanio.
La tatu: kauli yake Sala na Amani ziwe juu yake: (Hivi umenifanya mimi kwa ALLAH kuwa mshirika?) ni vipi kwa atakayesema:
Sina mwingine ninayemtegemea zaidi yako. Na maneno mfano wa hayo?
La nne: Nikuwa hili si katika shirki kubwa kwa kauli yake: (Kilizuia kitu fulani).
La tano: Nikuwa ndoto njema ni sehemu ya wahyi.
La sita: Nikuwa ndoto zinaweza kuwa sababu ya kuletwa baadhi ya sheria.
MLANGO UNAOELEZEA ATAKAYE TUKANA ZAMA HAKIKA AMEMUUDHI ALLAH.
Na amesema ALLAH Mtukufu: Wakasema hayakuwa haya isipokuwa ni maisha yetu ya dunia tunakufa na tunapata uhai na hakuna cha kutumaliza isipokuwa ni zama na hawana wao kwa kauli hiyo ujuzi hawakuwa wao isipokuwa wanadhania. [Al Jaathiya: 24].
"Na katika Sahihi Al-Bukhari pia kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: (Amesema ALLAH: Ananiudhi mimi mwanadamu, anatukana nyakati na mimi ndiye nyakati, ninaugeuza usiku na mchana).
Na katika riwaya nyingine: (Msitukane nyakati; kwani ALLAH ndiye nyakati).
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Katazo la kutukana nyakati.
La pili Kuitwa kuwa ni kumuudhi ALLAH.
La tatu: Kuizingatia kauli yake: (kwani ALLAH ndiye nyakati).
La nne: Nikuwa inaweza kuwa ni matusi hata kama mtu hajakusudia kutoka moyoni mwake.
MLANGO UNAO KATAZA KUJIITA HAKIMU WA MAHAKIMU.
Na katika Sahihi Al-Bukhari kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Hakika jina la udhalili zaidi mbele ya ALLAH ni mtu kajiita Mfalme wa Wafalme, hakuna Mfalme isipokuwa ALLAH"
Amesema Sufyani: Mfano: (Shahan shahan -Yaani: Mfalme wa wafalme).
Na katika riwaya nyingine: (Ni Mtu anayechukiza zaidi kwa ALLAH siku ya kiyama na ni mtu dhalili zaidi).
kauli yake: (Dhalili) yaani: Mwenye Fedheha.
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Katazo la kujiita Mfalme wa wafalme.
La pili Nikuwa maneno yenye kuendana na haya ni yale aliyoyasema sufyani.
La tatu: Kuwa makini katika hili lililotiliwa uzito mkubwa na mfano wake pamoja nakuelezwa wazi kuwa moyo haukukusudia maana hiyo.
La nne: Kuwa makini kuwa hili ni kwa ajili ya kumtukuza ALLAH Mtukufu.
MLANGO UNAO ELEZEA ULAZIMA WA KUHESHIMU MAJINA YA ALLAH MTUKUFU NA KUBADILISHA JINA KWA AJILI HIYO.
Kutoka kwa Abuu Shuraihi: Yakwamba yeye alikuwa akiitwa Abuul Hakam (baba wa mahakimu), Mtume Sala na Amani ziwe juu yake akasema kumwambia: (Hakika ALLAH ndiye Hakimu na kwake ndiyo kuna hukumu).
Akasema: Hakika watu wangu walihitilafiana katika jambo wakanijia nikawahukumu kati yao zikaridhia pande zote mbili.
Akasema: (Uzuri ulioje wa jambo hili! Je una mtoto?).
Nikasema: Shuraihi na Muslim na Abdallah.
Akasema: (Ni yupi mkubwa kati yao?)
Nikasema: Shuraihi.
Akasema: "Basi wewe ni Abuu Shuraihi" kaipokea Abuudaud na wengineo.
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Kuheshimu majina ya ALLAH na sifa zake, hata kama mtu hajakusudia maana hiyo.
La pili Kubadili jina kwa ajili hiyo.
La tatu: Kumchagua mkubwa katika watoto kwa ajili ya kutumia jina lake.
MLANGO UNAO ELEZEA UBAYA WA MTU ATAKAYE PUUZA KITU NDANI YAKE KUNA UTAJO WA ALLAH AU QURAN AU MTUME.
Na amesema ALLAH Mtukufu: Na kama utawauliza hakika watasema si vinginevyo tuliku tunajilewaza na tunacheza sema ewe MUHAMMAD hivi ALLAH na aya zake na MTUME wake ndio mlikuwa mnavifanyia mizaha. [Tauba: 65].
Kutoka kwa bin Omar na Muhammad bin ka'bu, na zaidi bin Aslam, na Katada -Hapa mizungumzo yao yaliingiliana- Yakwamba mtu mmoja alisema katika vita vya Tabuk: Hatujawahi kuona watu mfano wa wasomi wetu hawa hakuna walafi (wanaopenda kula sana) kama wao, na waongo kama wao, na wala hakuna waoga katika vita kama wao -Yaani wakimkusudia Mtume Sala na Amani ziwe juu yake na maswahaba zake wasomi, akasema Aufu bin Maaliki: We muongo na bali wewe ni mnafiki, na hakika nitamueleza maneno hayo Mtume Sala na Amani ziwe juu yake.
Akaenda Aufu kwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake ili amueleze akakuta tayari Qur'ani ishamtangulia.
Akaja yule bwana kwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake akiwa tayari ameshajiandaa na amepanda Ngamia wake.
Akasema: Ewe Mjumbe wa ALLAH hakika tulikuwa tukifanya mzaha tu na tukizungumza mazunguzo ya wasafiri ili kukata uchovu wa safari njiani, Anasema bin Omar: "Kana kwamba namuona alivyokuwa ameshikilia kamba ya Ngamia ya Mtume Sala na Amani ziwe juu yake na mawe yakimgonga miguuni mwake na huku akisema: Hakika tulikuwa tukifanya mzaha na mchezo tu, Na Mtume Sala na Amani ziwe juu yake akisema: «Je ni ALLAH na aya zake na Mtume Wake mlikuwa mkimfanyia mzaha? hakika mmekufuru baada ya kuamini kwenu» Huku Mtume Sala na Amani ziwe juu yake akiwa hamuangalii wala hazidishi neno zaidi ya hayo)
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: -Nalo ndiyo kubwa- Nikuwa atakayefanya mzaha kwa haya basi atakuwa kafiri.
La pili: Nikuwa hii ndiyo tafsiri ya aya kwa yeyote atakayefanya hivyo, yeyote yule atakayekuwa.
La tatu: Tofauti kati ya kusengenya na nasaha kwa ajili ya ALLAH na Mtume wake.
La nne: Tofauti kati ya msamaha anaoupenda ALLAH na kati ya ukali kwa maadui wa ALLAH.
La tano: Nikuwa katika uadui uko ambao haufai kufumbiwa macho.
MLANGO WA KAULI YAKE ALLAH MTUKUFU: Na kama tungewaonjesha huruma kutoka kwetu baada ya madhara yaliyo mpata hakika angesema haya ni yangu na sidhani kuwa qiyamah ni chenye kusimama na hata kama tarejeshwa kwa MOLA wangu hakika ninayo mema kwakwe yeye hakika tutawaeleza wale ambao walio kufuru kwa yale waliyo yafanya na hakika tutawaonjesha kutokana na adhabu nzito. [Fuswilat: 50].
Amesema Mujaahidi: (Haya nimeyapata kwa kazi zangu na mimi ninastahiki kuyapata).
Amesema bin Abbas (Anakusudia nimeyapata kwa ujanja wangu)
Na kauli yake ALLAH: {Husema hakika haya nimepewa kwa sababu ya elimu yangu (ya utafutaji) Amesema katada: (Yaani kwa ujuzi wangu wa njia za utafutaji riziki)
Na wakasema wengineo: (Kwa elimu ya ALLAH kujua kuwa mimi ndiye ninayestahiki).
Na hii ndiyo maana ya kauli ya Mujaahidi: (Nimepewa kwa sababu ya cheo).
Na kutoka kwa Abuu Huraira Hakika yeye alimsikia Mtume wa Allah Sala na amani za Allah ziwe juu yake akisema: Yakwamba watu watatu katika wana wa Israeli: Mwenye ugonjwa wa ngozi na mwenye kipara (aliyenyonyoka nywele za kichwa kwa ugonjwa) na kipofu.
ALLAH akataka kuwapa mtihani, akawatumia Malaika.
Akamuendea mwenye ugonjwa wa ngozi (mbaranga) akasema: Ni kitu gani unapenda zaidi maishani mwako?.
Akasema: Napenda Rangi nzuri, na ngozi nzuri, na iniondokee hii ambayo inafanya watu waninyanyapae.
Akasema: Malaika akamfuta: basi ule uchafu wake wote ukaondoka; akapewa rangi nzuri na ngozi nzuri.
Akasema Malaika kumuuliza: Ni mali gani unapenda sana maishani mwako?
Akasema: Napenda kufuga Ngamia au Ng'ombe -hapa kuna shaka ya mpokezi, je Mtume alisema Ngamia au Ng'ombe?- Basi akapewa Ngamia aliyenona.
Malaika akasema: Allah akubariki katika Ngamia huyu.
Mtume anasema: Malaika akamuendea Mwenye ugonjwa wa kipara.
akasema: Ni kitu gani unapenda zaidi maishani mwako?.
Akasema: Napenda nywele nzuri, na iniondokee hali hii ambayo inafanya watu waninyanyapae.
Malaika akamfuta ile hali ikamuondokea, na kapewa nywele nzuri.
Akasema Malaika kumuuliza: Ni mali gani unapenda sana maishani mwako?
Akasema: Napenda Ng'ombe au Ngamia, basi akapewa Ng'ombe mwenye mimba.
Malaika akasema: Allah akubariki katika Ng'ombe huyu.
Basi akamuendea yule kipofu.
akasema: Ni kitu gani unapenda zaidi maishani mwako?.
Akasema: Ni ALLAH kunirudishia macho yangu ili na mimi niwaone watu, Malaika akamfuta na Mwenyezi Mungu akamrudishia macho yake.
Akasema Malaika kumuuliza: Ni mali gani unapenda sana maishani mwako?
Akasema: Napenda kufuga mbuzi.
Akapewa mbuzi mwenye mtoto akawazalisha mbuzi hawa na huyu akazaa sana.
Basi akawa yule bwana wa kwanza anamiliki bonde zima la Ngamia, na huyu wa pili pia bonde zima la Ng'ombe, na huyu wa tatu pia bonde zima la Mbuzi.
Akasema: Kisha Malaika akamjia yule aliyekuwa na ugonjwa wa mbaranga akiwa katika sura kama yake na muonekano kama wake, akasema: Mimi ni mtu masikini, na mpita njia na nimekatikiwa na kila kitu katika safari yangu hii, sina namna yoyote yakuweza kufika isipokuwa namtegemea Mwenyezi Mungu kisha wewe.
Nakuomba kwa jina la yule aliyekupa rangi nzuri, na ngozi nzuri, na mali, nisaidie Ngamia moja nimtumie kufika safari yangu.
Yule bwana akasema: Nina majukumu mengi.
Malaika akamwambia: kana kwamba nakufahamu, hivi hukuwa na ugonjwa wa ngozi wewe watu wakikunyanyapaa, tena ukiwa fakiri masikini Mwenyezi Mungu akakupa mali?
Yule bwana akasema: Hizi mali nimerithi kutoka vizazi na vizazi.
Malaika akasema: Ikiwa kama unasema uongo basi ALLAH akugeuze urudi ulivyokuwa.
Mtume akasema: Malaika akamuendea yule aliyekuwa na ugonjwa wa kipara katika sura yake na muonekano wake.
Akasema kumwambia: kama alivyomwambia yule wa kwanza, naye akamjibu kama alivyomjibu yule wa kwanza.
Malaika akasema: Ikiwa kama unasema uongo basi Mwenyezi Mungu akugeuze urudi ulivyokuwa.
Akasema: Kisha Malaika akamjia yule aliyekuwa kipofu akiwa katika sura kama yake na muonekano kama wake, akasema: Mimi ni mtu masikini, na mpita njia na nimekatikiwa na kila kitu katika safari yangu hii, sina namna yoyote yakuweza kufika isipokuwa namtegemea ALLAH kisha wewe.
Nakuomba kwa jina la yule aliyekurejeshea macho yako mbuzi mmoja nimtumie kufika safari yangu.
Yule bwana akasema: Nikweli nilikuwa kipofu ALLAH akanirudishia macho yangu; hivyo chukua ukitakacho, na uache ukitakacho; Wallahi -Namuapa ALLAH hakuna kitu chochote ninachoweza kukuzuia utakachokichukua kwa ajili ya ALLAH.
Malaika akasema: Hapana, baki na mali yako, hakika nyinyi mmepewa mtihani na hakika ALLAH ameridhika na wewe na amewakasirikia jamaa zako wale wawili) Wameitoa Maimamu wawili.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya.
La pili: Nini maana ya: (Hakika atasema hizi ni za kwangu).
La tatu: Nini maana ya kauli yake: {Hakika haya nimepewa kwa ujuzi wangu}.
La nne: Ni mambo ya kustaajabisha yaliyoko ndani ya kisa hiki miongoni mwa hayo ni mazingatioa makubwa.
Mlango wa kauli ya ALLAH Mtukufu: ALLAH Alipowaruzuku, yule mume na mke, mtoto mwema walimfanyia ALLAH washirika katika mtoto yule ambaye ALLAH Alipwekeka katika kumuumba wakamfanya ni mja wa asiyekuwa Mwenyezi Mungu; Ametukuka ALLAH na Ameepukana na kila mshirika." [A'raf: 190].
amesema Ibni Hazmi: (Wamekubaliana kuliharamisha kila jina ambalo litafanywa kuwa ni utumwa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu kama Abdi Omar, mja wa Omar, na abdil ka'aba na mfano wa hayo kasoro Abdul Muttwalibu).
Na kutoka kwa bin Abbasi katika aya hii amesema: (Alipomuingilia Adamu Hawa akabeba ujauzito aliwajia ibilisi akasema: mimi ndiye jamaa yenu niliyewatoa peponi, sasa, ima mnitii au nimuwekee mapembe tena na meno yaliyotokeza, ili atoke tumboni mwako yamuhangaishe.
Na hakika nitafanya kadha wa kadhaa, akiwatisha.
Muiteni mja wa mkulima.
Wakakataa kumtii mtoto akazaliwa akiwa maiti.
Kisha Hawa akabeba tena ujauzito akawajia tena akawaambia kama alichowaambia mara ya kwanza; wakakataa kumtii mtoto akazaliwa akiwa maiti.
Kisha akabeba ujauzito mara nyingine akawajia akawaeleza yakawaingia mapenzi ya mtoto ikabidi wamuite Abdul Harith.
Na hiyo ndiyo kauli yake (wanamfanyia mshirika katika kile alichowapa) Imepokelewa na bin Abii Hatim
Na amepokea pia kwa isnadi sahihi kutoka kwa Katada amesema: (washirika katika kumtii yeye, na si katika ibada zake)
Na pia amepokea kwa isnadi sahihi kutoka kwa Mujaahidi katika kauli yake: {Ikiwa utatupa mtoto mwema} amesema: (Tunataraji awe mwanadamu).
Na ametaja maana yake kutoka kwa Hasan Al baswariy na Saidi na wengine.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Kuharamishwa kila jina lililofanywa utumwa kwa siyekuwa ALLAH.
La pili Tafsiri ya Aya
La tatu: Nikuwa shirki hii ni katika majina tu tena ambayo hayakukusudiwa uhalisia wake.
La nne: Nikuwa zawadi ya ALLAH kumpa mwanaume mtoto wa kike aliyesalama ni katika neema.
La tano: Ni wema waliotangulia kutaja tofauti kati ya shirki ya kutii na shirki katika ibada.
MLANGO UNAO ELEZEA KAULI YAKE ALLAH: Na majina mazuri ni yake ALLAH basi muiteni kwa majina hayo na waacheni wale ambao wanakengeuka katika majina yake. [Suratul Al-A'raf 180]
Ametaja bin Abii Hatim kutoka kwa bin Abbas (wanaogeuza majina yake) yaani (wanaofanya shirki)
Na kutoka kwake pia: (waliliita sanamu Lata kutoka katika jina Ilaahi -Mola- Na uzza kutoka katika jina Aziizi).
Na kutoka kwa A'mashi: (Wanaingiza katika majina yake yasiyofaa)
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Kuthibitisha majina.
La pili Nikuwa ni majina mazuri mno.
La tatu: Amri ya kumuomba kupitia majina hayo.
La nne: Kumuacha yeyote mwenye kuyapinga miongoni mwa wajinga katika wapagani na wapingaji.
La tano: Tafsiri ya kupinga.
La sita: Ahadi ya adhabu kwa atakaye pinga.
MLANGO ULIO KUJA KUKATAZA KUSEMA'AMANI IWE JUU YA ALLAH.
katika sahihi Bukhari kutoka kwa bin Mas'udi Radhi za ALLAH juu yake amesema: Tulikuwa tunapokuwa na Mtume Sala na Amani ziwe juu yake katika swala, tunasema: Amani iwe juu ya ALLAH toka kwa waja wake, Amani iwe juu ya fulani na fulani, Akasema Mtume Sala na Amani ziwe juu yake: "Msiseme Amani iwe juu ya ALLAH kwani ALLAH yeye ndiye Amani"
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya salam (Amani)
La pili Nikuwa hiyo ni salamu.
La tatu: Nikuwa haifai kwa Mwenyezi Mungu.
La nne: sababu ya hilo.
La tano: kujifunza kwao salamu inayofaa kwa Mwenyezi Mungu.
MLANGO UNAO KATAZA KUSEMA EWE ALLAH NISAMEHE UKITAKA.
katika Sahihi Al-Bukhari kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Asiseme mmoja wenu : Ewe Allah nisamehe ukipenda, Ewe Allah nirehemu ukipenda, bali aazimie katika maombi, kwani Allah hakuna wa kumtenza nguvu".
Na imepokelewa toka kwa Muslim: "Na awe na shauku ya kuomba mambo makubwa; kwani ALLAH hakuna kitu chochote kwake kikubwa atampa".
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Katazo la kuweka shaka katika dua.
La pili sababu ya hilo.
La tatu: kauli yake: "Na aazimie maombi"
La nne: Kuwa na shauku ya kuomba makubwa.
La tano: Sababu ya jambo hilo.
Mlango mtu asiseme: Mja wangu na mjakazi wangu:
katika sahihi Bukhari kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Asiseme mmoja wenu: Mlishe Mola wako, mtie udhu Mola wako, na aseme: bwana wangu na bosi wangu, na asiseme mmoja wenu mja wangu na mjakazi wangu na aseme: kijana wangu na binti yangu".
Hapa kuna maswala:
La kwanza: katazo la kusema: Mja wangu na mjakazi wangu.
La pili Asiseme mtumwa: Mola wangu na asiambiwe: Mlishe mola wako.
La tatu: Mafundisho ya kwanza: kauli ya kijana wangu na binti yangu.
La nne: Mafundisho ya pili ni kauli ya: bwana wangu na bosi wangu.
La tano: tahadhari ya makusudio ya hilo, nayo ni kuithibitisha Tauhidi hata katika matamshi.
MLANGO UNAO ELEZEA KUTOKATALIWA MAOMBI ATAKAOMBA KWA AJILI YA ALLAH.
kutoka kwa bin Omar -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mtume wa ALLAH -Rehema na amani za ALLAH ziwe juu yake- Atakayeomba kinga kwa jina la ALLAH basi mkingeni,na atakayeomba kitu kwa jina la ALLAH basi mpeni,na atakayekuiteni basi mjibuni,na atakayekutendeeni wema basi mlipeni,ikiwa hamtopata cha kumlipa basi muombeeni dua mpaka muonyeshe kuwa tayari mmemlipa" Imepokelewa na Abuu Daud na nasaai kwa Isnad sahihi.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: kumpa hifadhi mwenye kuomba kinga kwa jina la ALLAH.
La pili. kumpa aliyeomba kwa jina la ALLAH.
La tatu: kuitika wito.
La nne: Kulipa juu ya kitendo chema.
La tano: Nikuwa dua ni malipo kwa ambaye hatoweza kumlipa.
La sita: kauli yake: "Mpaka muonyeshe kuwa mmemlipa".
Hakuombwi kwa uso wa ALLAH isipokuwa pepo:
Na kutoka kwa Jabiri Amesema , Amesema Mtume rehema na Amani zimfikie: "Hakuombwi kwa uso wa ALLAH isipokuwa pepo" Imepokelewa na Abuu Daud
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Katazo la kuombwa kwa uso wa ALLAHisipokuwa lengo kuu la mwisho.
La pili kuthibitisha sifa ya uso.
MLANGO ULIYO KUJA KUELEZEA UBAYA WA KUSEMA LAITI.
Na amesema ALLAH Mtukufu: {Wanasema lau kama tungelikuwa na maamuzi ya yoyote basi tusingeliuawa hapa} [Al-Imran: 154].
na kauli yake: "wale waliosema kuwaambia ndugu zao nao wakakaa wakaacha kwenda vitani, lau wangelitusikiliza wasingeuawa" [Al-Imran: 16].
katika sahihi Bukhari kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Sala na amani za ALLAH ziwe juu yake alisema: "Pupia yenye manufaa na wewe, na utake msaada kwa ALLAH na wala usishindwe,na likikusibu jambo usiseme: Lau ningefanya kadha basi ingelikuwa kadha na kadha, lakini sema: Hii ni Qadari ya ALLAH naye hufanya alitakalo, maana neno " Lau" linafungua matendo ya shetani."
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya mbili katika suratul Al Imrani.
La pili katazo la wazi la kauli ya: (Lau) kinapokupata kitu.
La tatu: sababu ya jambo hilo nikuwa hilo linafungua amali ya shetani.
La nne: kuelekezwa katika maneno mazuri.
La tano: kuamrishwa kupupia yenye manufaa pamoja na kutaka msaada kwa ALLAH.
La sita: Katazo la kinyume chake nalo ni kushindwa.
MLANGO UNAO ELEZEA UBAYA WA KUTUKANA UPEPO.
kutoka kwa Ubayya bin kaabu Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Msiutukane upepo, mkiona yanayo kuchukizeni katika upepo basi semeni: Ewe Allah tunaomba kheri za upepo huu na kheri zilizomo, na kheri ambazo kwazo umeamrishwa upepo huu, na tunataka hifadhi na ulinzi kutokana na shari zake, na shari ambazo kwa sababu yake umeamrishwa." Ameisahihisha Tirmidhiy
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Katazo la kutukana upepo.
La pili Kuelekezwa katika maneno yenye manufaa anapoona mtu anayoyachukia.
La tatu: Maelekezo kuwa upepo huo umeamrishwa.
La nne: Nikuwa unaweza kuamrishwa kwa kheri na unaweza kuamrishwa kwa shari.
MLANGO UNAO ELEZEA KAULI YAKE ALLAH MTUKUFU. Wanadhania kwa ALLAH bila ya haki kudhania kwa ujinga wanasema "hivi sisi tunajambo katika kitu" sema ewe MUHAMMAD hakika jambo lote ni lake ALLAH wanaficha yaliyo ndani ya nafsi zao yale wasiyo yadhihirisha kwako wanasema "laiti tungelikuwa na jambo lolote basi tusinge uwawa hapa"sema ewe MUHAMMAD laiti mngelikuwa ndani ya majumba yenu hakika wangefikiwa wale ambao wamepangiwa kifo kwenye vitanda vyao na awajaribu ALLAH yale yaliyomo ndani ya vifua vyenu na achambue yale yaliyo ndani ya mioyo yenu na ALLAH ni mjuzi kwa yale yaliyomo ndani ya vifua. [Al-Imran: 154].
na kauli yake: Wamdhaniao kwa ALLAH dhana mbaya juu yao kuna mwisho mbaya na ALLAH amewakasirikia na amewalaani na amewaandalia wao moto wa jahannama na yamekuwa mafikio mabaya. [Al Fathi: 6]
Amesema binil Qayyim katika aya ya kwanza: (Imefasiriwa dhana hii kuwa;ALLAH Mtukufu hatomnusuru Mtume wake nakuwa jambo lake litatoweka, na imefasiriwa kuwa yaliyompata hayakuwa kwa makadirio ya ALLAH na hekima zake, ikafasiriwa kuwa ni kupinga hekima na kupinga makadirio, na nikupinga kuwa hatolitimiza jambo la Mtume wake, nakuwa hatoidhihirisha ikawa juu ya dini zote, na hii ndiyo dhana mbaya, ambayo walidhania wanafiki na washirikina katika suratul Fat'hi, bali hii imekuwa ni dhana mbaya kwa sababu ni kudhania kile kisichomstahiki Aliyetakasika na kutukuka, na wala haiendani na hekima zake na sifa zake njema na ahadi zake za kweli.
Atakayedhania kuwa anaipeleka taratibu batili katika haki kupeleka ambako ni endelevu basi ajue haki itaporomoka pamoja na batili, au akapinga yanayotokea kuwa hayajatokea kwa maamuzi yake na makadirio yake Mtukufu, au akapinga kuwa makadirio yake na hekima zake hazina maana wala hekima ya ndani kiasi ambacho zinastahiki kumshukuru ALLAH, bali akadhani kuwa hayo yametokea kwa matakwa tu ambayo hayana lolote, basi hiyo ndiyo dhana ya makafiri, na ole wao waliokufuru kutokana na adhabu ya moto, na watu wengi wanamdhania ALLAH dhana mbaya katika yale anayohusika nayo mwenyewe, na katika yale anayowafanyia wasiokuwa wao, na hili hakuna anayesalimika nalo isipokuwa yule aliyemtambua ALLAH na majina yake na sifa zake, na yale yanayokusudiwa katika hekima zake na shukrani zake.
Basi ajikite mwenye akili na uelewa na nafsi yake katika jambo hili, na atubie kwa Mwenyezi Mungu na amuombe msamaha kwa kumdhania kwake Mola wake dhana mbaya.
Na hata ukimchunguza yeyote unayeweza kumchunguza; basi utamuona anachembe ndogo ya kupinga makadirio na anakiashiria hicho, na hali yakuwa alistahiki awe kadhaa wa kadhaa, yuko ambaye nafsi yake imetulizana na yuko ambaye hudadisi kwa wingi, na ichunguze nafsi yako, Je, wewe umesalimika?.
ikiwa utasalimika na hilo basi utakuwa umesalimika na jambo kubwa na vinginevyo basi mimi sikuoni kama umesalimika)
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya aya ya suratul Al imran.
La pili Tafsiri ya aya ya suratul Fat-hi.
La tatu: Kuelezwa kuwa kuna aina nyingi ambazo hazihesabiki.
La nne: Nikuwa hasalimiki na hilo ila yule aliyeyafahamu majina na sifa na akajitambua.
MLANGO UNAO ELEZEA UBAYA WA ANAYE PINGA QADARI.
Na amesema bin Omar: (Namuapa yule ambaye nafsi ya bin Omar iko mkononi mwake, laiti watu angemiliki mmoja wao dhahabu mfano wa Mlima Uhudi, kisha akaitoa katika njia ya ALLAH basi ALLAH asingeikubali toka kwake, mpaka aamini makadirio, kisha bin Omar akatoa ushahidi wa kauli ya Mtume Sala na Amani ziwe juu yake: "Ni kumuamini ALLAH na Malaika wake na vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho na kuamini Qadari kheri yake na shari yake." Imepokelewa na Imamu Muslim
Kutoka kwa Ubada bin Swamit yakwamba yeye alisema kumwambia mwanaye: "Ewe mwanangu hakika wewe hutopata utamu wa imani mpaka ujue kuwa yaliyokupata hayakuwa ni yenye kukukosa, na yaliyokukosa hayakuwa ni yenye kukupata, nilimsikia Mtume Sala na Amani ziwe juu yake akisema: "Hakika kitu cha kwanza alichoumba ALLAH ni kalamu akasema kuiambia: Andika, ikasema: Ewe Mola niandike nini?
Akasema: Andika makadirio ya kila kitu mpaka kiyama kusimama"
Ewe mwanangu, Nilimsikia Mtume wa Allah Sala na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Atakayekufa katika imani tofauti na hii basi huyo si miongoni mwangu"
Na katika mapokezi ya Ahmad: "Hakika kitu cha kwanza alichokiumba allah Mtukufu ni kalamu akaiambia: Andika, basi yakafanyika katika saa hiyo yale yote yatakayokuwa katika maisha mpaka siku ya kiyama".
Na katika iriwaya ya bin Wahab, Amesema Mtume Sala na Amani zimfikie: "Yeyote ambaye hatoamini makadirio heri yake na shari yake basi ALLAH atamchoma kwa moto".
Na katika kitabu cha Al Musnadi, kutoka kwa bin Dailamiy Amesema: Nilimwendea Ubayya bin Ka'bu nikasema: Katika nafsi yangu kuna shaka kidogo na hii Qadar (Mipango ya ALLAH) Hebu nisimulie kitu ambacho huenda ALLAH akaniondoshea hilo moyoni mwangu. Akasema: "Laiti ungelitoa (sadaka) ya dhahabu mfano wa (mlima) Uhudi basi asingeikubaliALLAH kwako mpaka uamini (Qadari) Mipango ya ALLAH,na ujue kuwa yaliyokupata hayakuwa ni yenye kukukosa, na yaliyokukosa hayakuwa ni yenye kukupata, na laiti ungelikufa (katika imani) tofauti na hii basi ungelikuwa ni katika watu wa motoni"
Anasema: Nikamuendea Abdallah bin Mas'udi, na Hudhaifa bin Yamani, na Zaidi bin Thabiti, wote hao wakanihadithia mfano wa maneno hayo kutoka kwa Mtume -Sala na Amani ziwe juu yake-." Hadithi ni sahihi kaipokea Al Hakim katika sahihi yake.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Kubainishwa ulazima wa kuamini makadirio.
La pili Kubainishwa namna ya kuyaamini.
La tatu: Kuporomoka kwa matendo ya yeyote ambaye hatoyaamini.
La nne: Kumeelezwa kuwa yeyote hatopata ladha ya imani mpaka ayaamini.
La tano: Kutajwa kiumbe cha kwanza kuumbwa.
La sita: Nikuwa yaliandikwa makadirio katika wakati ule mpaka siku ya kiyama.
La saba: Kujitenga kwake Mtume Sala na Amani ziwe juu yake na yule ambaye hatoamini makadirio.
La nane: Kawaida ya wema waliotangulia kuondoa utata kwa kuwauliza wasomi.
La tisa: Nikuwa wanachuoni walimjibu kwa majibu yaliyomuondolea utata wake, na hii ni pale walipoyanasibisha maneno kwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake pekee.
MLANGO ULIO KUJA KUELEZA UBAYA WA WAPIGA PICHA.
Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa ALLAH-Sala na Amani za ALLAH ziwe juu yake: "Amesema ALLAH Mtukufu: Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule aliyekwenda kuumba kama kuumba kwangu, basi na waumbe punje, au waumbe mbegu, au waumbe ngano" Wameitoa hadithi hii Maimamu wawili.
Na katika sahihi mbili kutoka kwa Aisha -Radhi za ALLAH ziwe juu yake -kwamba Mtume wa ALLAH-Sala na Amani za ALLAH ziwe juu yake na amani- amesema: "Watu wenye adhabu kali zaidi siku ya kiyama ni wale wanaoigiza vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu"
Na kutoka kwa Ibnu Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Kila mwenye kupiga picha atakwenda motoni, atawekewa nafsi katika kila picha aliyoipiga atakuwa akiadhibiwa nayo katika moto wa Jahanamu"
Na kutoka kwao wawili wameipokea kutoka kwake mar'fuu "Atakayepiga picha yoyote duniani, atalazimishwa aipulizie roho na hali yakuwa hawezi"
Na katika sahihi Muslim kutoka kwa Abul Hayyaji Amesema: "Alisema Ally kuniambia": "Je nikuagize katika yale aliyoniagiza kwayo Mjumbe wa ALLAH Sala na Amani ziwe juu yake? Usiache picha yoyote isipokuwa umeifuta, wala kaburi lililonyanyuliwa isipokuwa umelisawazisha."
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Kutiwa mkazo mkubwa kwa wapiga picha.
La pili Kutanabahishwa juu ya sababu, nayo ni kutokuwa na adabu na ALLAH, kwa kauli yake: "Na ni nani dhalimu mkubwa zaidi kuliko yule aliyekwenda akiumba kama kuumba kwangu".
La tatu: kutanabahishwa juu ya uwezo wake na kushindwa kwao hao, kwa kauli yake: "basi na waumbe punje, au, mbegu, au ngano".
La nne: Kuwekwa wazi kuwa wao ndiyo watakuwa watu wenye adhabu kali zaidi
La tano: Nikuwa ALLAH ataumba nafsi kwa idadi ya zile picha atakuwa akimuadhibu nazo mpiga picha katika moto wa jahanamu.
La sita: Nikuwa yeye atalazimishwa azipulizie roho.
La saba: Amri ya kuzifuta zinapopatikana.
MLANGO ULIO KUJA KUBAINISHA UBAYA WA KUKITHIRISHA VIAPO.
Na amesema ALLAH Mtukufu: "Na hifadhini viapo vyenu". [Maaida: 89].
kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Kiapo hupambia bidhaa, lakini hufuta baraka za kipato" Wameitoa hadithi hii Maimamu wawili.
Na kutoka kwa Salman Yakwamba Mtume Sala na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Watu wa aina tatu hatowasemesha ALLAH na wala hatowatakasa na watakuwa na adhabu iumizayo; Mzee mzinifu, na masikini jeuri, na mtu aliyemfanya ALLAH kuwa ndiyo bidhaa yake; hanunui isipokuwa kwa kiapo chake na wala hauzi isipokuwa kwa kiapo chake" Imepokelewa na Twabaraniy na Isnad yake ni sahihi.
Na katika sahihi Bukhari, kutoka kwa Imran bin Huswain -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa ALLAH-Sala na amani za ALLAH ziwe juu yake- "Watu bora katika umma wangu ni karne yangu, kisha wale wanaowafuatia, kisha wale wanaowafuatia, Anasema Imrani: Sijui alitaja baada ya karne yake mara mbili au tatu, kisha baada yenu watakuja watu, wanatoa ushahidi wala hawaombwi kutoa ushahidi, na watafanya hiyana wala hawatoaminiwa, na wataweka nadhiri wala hawatimizi, na utadhihiri kwao unene.
Na kutoka kwa Ibnu masoud pia -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika MtumeSala na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Watu bora ni karne yangu, kisha wale wanaowafuatia, kisha wale wanaowafuatia, kisha watakuja watu kiapo cha mmoja wao kitatangulia ushahidi wake, na ushahidi wake kiapo chake".
Amesema Ibrahim: "Walikuwa wakitupiga juu ya swala la ushahidi na Ahadi wakati tukiwa wadogo".
Hapa kuna maswala:
La kwanza: usia wa kuhifadhi viapo.
La pili Kuelezwa kuwa kiapo hupambia bidhaa itoke lakini kinaondosha baraka.
La tatu: Ahadi ya adhabu kali kwa yule ambaye hauzi wala hanunui mpaka kwa kiapo chake.
La nne: Kutahadharishwa kuwa dhambi inazidi kuwa kubwa kadiri sababu ya kuapia inavyozidi kuwa ndogo.
La tano: Kukemewa wale wanao apia bila kutakwa kuapia.
La sita: Kuzisifia kwake Mtume Sala na Amani ziwe juu yake karne nne bora, na kutajwa kile kitakachotokea baada yao.
La saba: Kukemewa wale wanao toa ushahidi bila kutakwa kutoa ushahidi.
La nane: Nikuwa wema waliotangulia walikuwa wakiwapiga watoto wadogo kwa sababu ya kuwakemea kutoa ushahidi na kutoa ahadi.
HUU NI MLANGO ULEZEA KUWA NDANI YA DHIMA YA ALLAH NA DHIMA YA NABII WAKE.
Na kauli yake ALLAH. Na tekelezeni ahadi za ALLAH mnapo ahidi na wala msitengue viapo baada ya kuvithibitisha na hakika mmemjalia ALLAH kuwa kwenu ni mdhamini hakika ALLAH anajua yote mnayo yafanya. [Nahli 91].
Na imepokelewa kutoka kwa Buraida Amesema: Alikuwa Mtume -Sala na Amani ziwe juu yake- anapomteua kiongozi katika jeshi au kikosi anamuusia kumcha ALLAH, na kwa wale alionao katika waislamu kuwatendea wema, akasema: "Piganeni kwa jina la ALLAH, piganeni na aliyemkufuru ALLAH, piganeni na wala msiibe wala msifanye hiyana, na wala msimsulubu mtu (kumuua kinyama), na wala msiue mtoto mdogo, na ukikutana na adui yako katika washirikina basi walinganie katika mambo matatu, kwa lolote watakalo kukubalia basi nawe wakubalie na usiwapige, kisha waite kuingia katika uislamu, ikiwa watakukubalia basi wakubalie hilo. Kisha waamrishe kubadili makazi kutoka katika makazi yao kwenda katika makazi ya waliohama (Muhajirina), na uwaeleze kuwa ikiwa kama watalikubali hilo watapewa haki sawa na haki za waliohama na watahusika katika majukumu sawa na yale waliyonayo waliohama, ikiwa kama watakataa kubadili makazi basi waeleze kuwa na wao watakuwa ni kama waarabu wa vijijini wa kiislamu, zitawahusu kwao hukumu za ALLAH, na wala hawatostahiki kupata chochote katika ngawira wala faiy (mali iliyopatikana bila vita) isipokuwa kama nao watapigana pamoja na waislamu, na ikiwa watayakataa yote hayo basi waombe kutoa kodi, na ikiwa watalikubali hilo basi wakubalie na wala usiwapige, na ikiwa kama watakataa basi omba msaada kwa Mwenyezi Mungu na upigane nao. Na ukiwazingira watu wa ngome yoyote na wakataka uwawekee dhima ya ALLAH na dhima ya Mtume wake, basi usiwawekee dhima ya ALLAH wala dhima ya Nabii wake, bali wawekee dhima yako na dhima ya watu wako; kwani kuvunja kwenu dhima yenu (Makubaliano) na dhima ya watu wenu hilo lina nafuu zaidi kuliko kuvunja dhima ya ALLAH na dhima ya Nabii wake, Na ikiwa utawazingira watu wa ngome fulani na wakataka uwaweke katika hukumu ya Mwenyezi Mungu basi usifanye hivyo, bali waweke katika hukumu yako, kwani we huwezi kujua kuwa je utapatia kwao hukumu ya ALLAH au la?". Imepokelewa na Imamu Muslim
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tofauti kati ya dhima ya ALLAH na dhima ya Nabii wake, na dhima ya waislamu. (dhima: maana yake: ni jukumu)
La pili Kuelekezwa katika jambo ambalo lina hatari ndogo kuliko jingine.
La tatu: Kauli yake: "piganeni kwa jina la ALLAH katika njia ya ALLAH"
La nne: Kauli yake: "Piganeni na yule aliyemkufuru Mwenyezi Mungu".
La tano: kauli yake: "Taka msaada kwa ALLAH na upigane nao".
La sita: Tofauti kati ya hukumu ya ALLAH na hukumu ya wanachuoni.
La saba: Nikuwa swahaba anahukumu wakati ambao kuna haja ya kuhukumu na hajui je ataafikiana na hukumu ya ALLAH au la?.
MLANGO UNAO KATAZA KUAPA JUU ALLAH.
Na kutoka kwa Jundabu bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa ALLAH -Rehema na amani za ALLAH ziwe juu yake- ((Mtu mmoja alisema: Wallahi ALLAH hatomsamehe fulani, akasema ALLAH aliyetakasika na kutukuka: Ni nani huyo anayepata ujasiri wa kuapia juu yangu kuwa sitomsamehe fulani? Basi mimi nimemsamehe na nimeporomosha matendo yako)) Imepokelewa na Imamu Muslim
Na imekuja katika hadithi ya Abuu Huraira kuwa muapaji alikuwa ni mtu mchamungu, akasema Abuu Huraira: "Alizungumza neno ambalo liliteketeza dunia yake
Na Akhera yake".
Hapa kuna Maswala:
La kwanza: Tahadhari ya kuapia juu ya Mwenyezi Mungu.
La pili Nikuwa kumbe moto uko karibu sana na mmoja wetu kuliko hata kisigino cha kiatu chake.
La tatu: Nikuwa hata pepo pia hivyo hivyo.
La nne: Hapa kuna ushahidi wa kauli yake: "Hakika mtu anaweza kuzungumza neno bila kujali." mpaka mwisho wa hadithi.
La tano: Nikuwa mtu anaweza kusamehewa kwa sababu mambo aliyoyafanya yalikuwa yakimchukiza zaidi hata kwake.
MLANGO UNAO ELEZEA HAKUNA KUOMBA UTETEZI KWA ALLAH JUU YA VIUMBE WAKE.
Kutoka kwa Jubair bin Mutwi'm -Radhi za ALLAH ziwe juu yake- Amesema: "Alikuja bedui mmoja kwa Mtume -Sala na Amani ziwe juu yake- Akasema: Ewe Mjumbe wa ALLAH,nafsi zimedhoofika,na familia zina njaa na mali zimeangamia,tuombee sisi mvua kwa Mola wako, kwani sisi tunaomba utetezi kwaALLAH kupitia kwako,akasema Nabii-Sala na Amani ziwe juu yake-: "Sub-haanallaah! Sub-haanallaah! -Yaani: Ametakasika Mwenyezi Mungu- akaendelea kuleta tasbihi -yaani kusema neno hilo- mpaka likajulikana hilo katika nyuso za maswahaba zake, kisha akasema: una nini wewe hivi unayajua ya Mwenyezi Mungu? Hakika jambo la ALLAH ni kubwa kuliko hilo, hakika hauombwi utetezi kwa ALLAH juu ya yeyote" Na akaitaja hadithi kuwa imepokelewa na Abuudaudi.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Kumkemea kwake aliyesema: ((Kwani sisi tunaomba utetezi kwa ALLAH juu yako)).
La pili Kubadilika kwake kubadilika ambako kulijulikana katika nyuso za maswahaba kwa sababu ya neno hili.
La tatu: Nikuwa hakumkemea aliposema kauli yake: (Tunataka ututetee kwa ALLAH).
La nne: Ukumbusho juu ya tafsiri ya neno Sub-haana llaah -Ametakasika ALLAH-.
La tano: Nikuwa waislamu walikuwa wakimuomba Mtume wa Allah Sala na amani za Allah ziwe juu yake: awaombee mvua.
HUU NI MLANGO UNAO ELEZEA MTUME SALA NA AMANI ZIWE JUU YAKE KULINDA TAUHEED NA KUZUIA KWAKE NJIA ZA USHIRIKINA.
Kutoka kwa Abdillah bin Shikhir Radhi za ALLAH ziwe juu yake Amesema: Niliondoka nikiwa katika kundi la bani Aamiri kwenda kwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake: Tukasema: Wewe ndiye Bwana wetu.
Akasema: ((Bwana ni Allah aliyetakasika na kutukuka))
Tukasema: Wewe ndiye mbora zaidi na ndiye Mtukufu wetu hata kwa uwezo.
Akasema: ((Semeni kwa kauli zenu, au baadhi ya kauli zenu, na wala asijekukukoteni shetani)) Imepokelewa na Abuu Daud na Isnad yake ni Jayyid.
Kutoka kwa Anasi Radhi za ALLA ziwe juu yake: Yakwamba watu walisema: Ewe Mjumbe wa ALLAH, Ewe Mbora wetu, na mtoto wa mbora wetu, na bwana yetu, na mtoto wa bwana yetu. Akasema: ((Enyi watu, semeni kwa kauli zenu na wala asikuporomosheni shetani, Mimi ni Muhammad Mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake, sipendi mninyanyue zaidi ya nafasi yangu ambayo kaniweka ALLAH Aliyetakasika na kutukuka)) Imepokelewa na Nasaai na Isnad yake ni Jayyid.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Kuwatahadharisha watu na kuchupa mipaka.
La pili Anachotakiwa akiseme mwenye kuambiwa: Wewe ndiye Bwana wetu.
La tatu: Kauli yake: ((Asijekukuvuteni shetani)) pamoja nakuwa hawakusema isipokuwa kweli.
La nne: Kauli yake: ((Sipendi mninyanyue juu zaidi ya nafasi yangu)).
MLANGO UNAO ELEZEA KAULI YA ALLAH MTUKUFU. Na hawakutukuza ALLAH ukweli wa kumtukuza na ardhi yote allah ameikamata siku ya qiyamah na mbingu saba ni zenye kukunjwa kwa mkono wake wa kulia utakasifu ni wake ALLAH kunako yote wanayo mshirikisha. [Azzumar: 67].
Kutoka kwa bin Mas'udi Radhi za ALLAH ziwe juu yake Amesema: "Alikuja Padri miongoni mwa mapadri kwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake akasema: "Ewe Muhammadi hakika sisi tunapata katika vitabu vyetu kuwa ALLAH ataziweka mbingu juu ya kidole, na Ardhi juu ya kidole, na miti juu ya kidole, na maji juu ya kidole, na udongo juu ya kidole, na viumbe vingine juu ya kidole, kisha atasema: Mimi ndiye Mfalme" Basi akacheka Mtume Sala na Amani ziwe juu yake mpaka yakaonekana magego yake kwa kuisadikisha kauli ya Padri kisha akasoma: "Na hawa washirikina hawakumuadhimisha ALLAH vile Anavyostahiki kuadhimishwa, kwa kuwa wamemuabudu asiyekuwa Yeye pamoja na Yeye miongoni mwa wale wasionufaisha wala kudhuru, wakamfanya muumbwa, pamoja na uelemevu wake, kuwa ni sawa na Muumba Mtukufu, Ambaye kotokana na uweza Wake mkubwa ni kwamba ardhi yote itakuwa iko mkononi Mwake Siku ya Kiyama"
Na katika mapokezi ya Muslim: (Na Milima na Miti juu ya kidole, kisha atavitikisa na aseme: Mimi ndiye Mfalme, Mimi Ndiye Allah".
Na katika mapokezi ya Bukhari: (Ataziweka mbingu juu ya kidole, na maji na udongo juu ya kidole, na viumbe vilivyobakia juu ya kidole) Wameitoa hadithi hii Maimamu wawili.
Na Imepokelewa kwa Muslim kutoka kwa bin Omari Hadithi Marfu'u: ALLAH Mtukufu atazikunja Mbingu siku ya Kiyama, kisha azichukue kwa mkono wake wa kulia kisha aseme: Mimi ndiye Mfalme wako wapi majabali (wenye jeuri)? wako wapi wenye kiburi?. kisha atazikunja ardhi kushotoni kwake, kisha aseme: Mimi ndiye Mfalme wako wapi majabali (wenye jeuri)? wako wapi wenye kiburi?"
na Imepokelewa kutoka kwa bin Abbasi Amesema: "Si chochote mbingu saba na ardhi saba katika kiganja cha Ar-Rahmaani -Mwingi wa rehema- isipokuwa ni kama punje ya ulezi katika mkono wa mmoja wenu"
Na akasema bin Jariri: Amenisimulia Yunus, Alitusimulia bin Wahab, Amesema: Alisema bin Zaidi: Alinisimulia baba yangu: Akasema: Amesema Mtume Sala na Amani ziwe juu yake: "Si chochote mbingu saba katika Kursiy ila ni kama Dirham (fedha za sarafu) saba zilizotupwa katika Ardhi ya tambarare pana"
Na amesema: Amesema Abuu Dhari -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Sala na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Si chochote kursiy (Mahala anapoweka miguu Ar-Rahmani) katika Arshi isipokuwa ni kama bangili la chuma lililowekwa katika ardhi ya jangwa"
Na kutoka kwa bin Mas'udi Amesema: (Kati ya Mbingu ya Dunia na ile inayofuata ni mwendo wa miaka mia tano, na kati ya mbingu na mbingu ni mwendo wa miaka mia tano, na kati ya mbingu ya saba na Kursiy ni mwendo wa miaka mia tano, na kati ya kursiy na maji ni mwendo wa miaka mia tano, na Arshi iko juu ya maji, na Allah yuko juu ya Arshi, hakifichikani kwake chochote katika matendo yenu) Kaitoa hadithi hii bin Muhdiy kutoka kwa Hammad bin Salama, kutoka kwa Aaswim, kutoka kwa Zari, kutoka kwa Abdillah, na akapokea yenye mfano kama hii Al Mas'udiy kutoka kwa Aaswim, kutoka kwa Abuu Waail, kutoka kwa Abdillah, Amesema maneno haya Al hafidh Adh-dhahabiy ALLAH Mtukufu Amrehemu- Amesema: na imepelekewa kwa njia nyingi pia.
Na kutoka kwa Al Abbas bin Abdil Muttwalib Radhi za ALLAH ziwe juu yake Amesema: Amesema Mtume Sala na Amani ziwe juu yake: (Hivi mnajua kuna umbali gani kati ya mbingu na Ardhi?) Tukasema:ALLAH na Mtume wake ndio wajuzi zaidi, akasema: (Kati yake kuna mwendo wa miaka mia tano, na kutoka mbingu moja kwenda nyingine ni mwendo wa miaka mia tano, na unene wa kila mbingu ni mwendo wa miaka mia tano, na kati ya mbingu ya saba na Arshi kuna Bahari, kutoka chini yake mpaka juu yake ukubwa wake ni kama masafa ya mbingu na Ardhi, na ALLAH Mtukufu yuko juu ya hayo, na wala hakifichiki kwake chochote katika matendo ya wanadamu).
Kaitoa Abuudaudi na wengineo.
Hapa kuna maswala:
La kwanza: Tafsiri ya kauli yake Mtukufu: {Na Ardhi yote itakunjwa mkononi mwake siku ya kiyama}
La pili Nikuwa elimu kama hizi na mfano wake zilibakia kwa Mayahudi waliokuwa katika zama zake Mtume Sala na Amani ziwe juu yake hawakuzipinga na wala hawakuzibadilisha.
La tatu: Nikuwa padri alipoeleza kwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake alimsadikisha, na ikateremka Qur'ani kulikubali hilo.
La nne: Kutokea swala la kucheka kutoka kwa Mtume Sala na Amani ziwe juu yake pale alipotaja Padri elimu hii tukufu.
La tano: Kumeelezwa wazi kutajwa kwa mikono miwili, nakuwa mbingu ziko katika mkono wa kulia na Ardhi ziko katika mkono mwingine.
La sita: Kumewekwa wazi kuwa umeitwa kuwa ni mkono wa kushoto.
La saba: kutajwa majabari na wenye kiburi wakati huo.
La nane: Kauli yake: ni kama punje ya ulezi katika kiganja cha mmoja wenu.
La tisa: Ukubwa wa Kursiy ukilinganisha na mbingu.
La kumi: Ukubwa wa Arshi ukilinganisha na Kursiy.
La kumi na moja: Nikuwa Arshi ni tofauti na Kursiy na Maji.
La kumi na mbili: Kuna masafa gani kati ya mbingu na Ardhi.
La kumi na tatu: kuna masafa gani kati ya mbingu ya saba na Kursiy.
La kumi na nne: kuna masafa gani kati ya Kursiy na maji.
La kumi na tano: Nikuwa Arshi iko juu ya maji.
La kumi na sita: Nikuwa ALLAH yuko juu ya Arshi.
La kumi na saba: kuna masafa gani kati ya mbingu na Ardhi.
La kumi na nane: Unene wa kila mbingu ni miaka mia moja.
La kumi na tisa: Nikuwa Bahari iliyoko mbinguni chini yake na juu yake ni mwendo wa kutembea miaka mia tano, Na Allah ndiye Mjuzi zaidi.
kimetimia kitabu cha Tauhidi kwa Fadhila za Allah Mtukufu: