Mwanachuoni Muhammad bin Abdil Wahhab -Mwenyezi Mungu Amrehemu
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu.
Namuomba Mwenyezi Mungu Mkarimu Mola wa Arshi tukufu akusimamie duniani na Akhera.
Na akufanye kuwa mwenye kubarikiwa popote utakapokuwa, na akufanye kuwa ni mtu ambaye ukipewa unashukuru, ukijaribiwa unasubiri, na ukifanya dhambi unaomba msamaha. Kwani mambo haya matatu ndiyo anuani ya furaha.
Tambua, akuongoze Mwenyezi Mungu katika utiifu wake: Yakuwa utakasifu ndiyo dini ya Ibrahim: Nao ni kumuabudu Mwenyezi Mungu, yeye pekee kwa kumtakasia dini, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:"Na sikuumba majini na binadamu isipokuwa kwa lengo tukufu, nalo niabudiwe mimi peke yangu, na sio asiyekuwa mimi".[A Dhariyati: 56].Unapotambua kuwa Mwenyezi Mungu kakuumba kwa ajili ya kumuabudu yeye; basi tambua kuwa ibada haiitwi ibada isipokuwa mpaka iwe na tauhidi (yaani kumpwekesha Mwenyezi Mungu) kama ambavyo swala haiitwi swala ila mpaka iwe na twahara, Na pindi inapoingia shirki katika ibada, ibada hiyo inaharibika, kama hadathi (kutokuwa na udhu) kunavyokuwa katika twahara, unapofahamu kuwa shirki ikiingia katika ibada inaiharibu, na inaporomosha amali, na anakuwa mfanyaji wake ni katika watu wenye kukaa milele motoni. Basi hapo utajua kuwa jambo la msingi zaidi kwako ni kulijua hilo (yaani kuifahamu tauhiidi), huenda Allah akakuepusha na mtego huu, nao ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu ambako Mwenyezi Mungu alisema ndani yake:"Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi Madhambi ya kushirikishwa naye, na husamehe madhambi mengine yote yasiyokuwa ushirikina kwa anayemtaka".[An nisaai: 116].Na hili ni kwa kuijua misingi minne aliyoitaja Mwenyezi Mungu katika kitabu chake:
Na uombezi uliokubaliwa: Ni ule unaoombwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na muombaji awe ni mtu aliyepewa utukufu wa kuombea, na mwenye kuombewa awe ni katika wale ambao Mwenyezi Mungu ameridhia kauli zake na matendo yake baada ya idhini yake; kama alivyosema Mtukufu:"Ni nani awezaye kuombea kwake maombi yoyote isipokuwa kwa idhini yake"[Al Baqara: 255].
Na imesimuliwa kutoka kwa Abuu Waaqid Al laithiy Amesema Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Tulitoka pamoja na Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kwenda katika vita vya Hunain, na sisi tukiwa ni wageni hatuna muda mrefu tangu kutoka katika ukafiri, na washirikina wakawa wana mti wa mkunazi ambao wanauzunguka kwa ibada na wanatundika hapo silaha zao, Mti huo ukiitwa (Dhaata anwaatwi) Yaani mahali pa kutundikia, Tukaupita mti mwingine wa mkunazi nasi tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tuwekee na sisi mahala pa kutundikia kama wao walivyo na mahala pa kutundikia, mpaka mwisho wa hadithi.
Imamu Muhammad Bin Abdul Wahaab ulinganizi wake na Historia yake.
11 lugha
Imamu Muhammad Bin Abdul Wahaab ulinganizi wake na Historia yake.
Utunzi wa Shekh Abdul Aziz Bin Abdillahi Bin Baaz Sifa zote njema anastahiki ALLAH Mola wa viumbe wote, sala na salam na baraka ziwe juu ya mja wake na Mtume wake mbora wa viumbe bwana wetu na kiongozi wetu Muhammad bin Abdillahi, na watu wake na Swahaba zake na wenye kufuata nyayo zao. Ama baada ya hayo: Enyi ndugu zangu watukufu, Enyi wanangu watukufu, muhadhara huu mfupi nauleta mbele yenu ili kuzinawirisha fikra, pamoja na kuweka wazi uhakika wa mambo, na kuwanasihi waja kwa ajili ya ALLAH, na kutekeleza baadhi ya mambo yanayo niwajibikia miongoni mwa haki, na muhadhara huu anuwani yake…
Kitabu hiki kinazungumzia mambo ya msingi ambayo yampasa Muislamu kujifunza: Kumjua Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuijua dini ya Uislamu, na kumjua Mtume Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake-, na kinaweka mkazo juu ya umuhimu wa mambo haya ya msingi katika kujenga imani na matendo mema kwa kutegemea ushahidi kutoka katika Qur'an tukufu na Sunna za Mtume.
Imamu Muhammad Ibnu Abdil Wahaab. Mlango wa Ulazima wa Kuufuata Uislamu. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na Mwenye kutafuta dini isiyokuwa dini ya Kiislamu, ambayo ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kumpwekesha na kumfuata kwa kumtii na kumdhalilikia, na kwa Mtume wake aliye Nabii wa mwisho Muhammad, Rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa kumuamini na kumfuata na kumpenda kwa dhahiri na kwa siri, basi hiyo haitakubaliwa kwake, na yeye Akhera atakuwa ni miongoni mwa wenye kupata hasara ambao walizifanyia ubahili nafsi zao kwa kuzinyima mambo yenye kuzinufaisha". [Al-Imran:…