Skip to content
Orodha ya Sura /

النَّحل

النَّحل is chapter 16 of the Quran and has 128 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

128 Aya Sura Na. 16
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

أَتَىٰٓ أَمۡرُ ٱللَّهِ فَلَا تَسۡتَعۡجِلُوهُۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Amri ya Mwenyezi Mungu itafika tu. Basi msiihimize. Ametakasika na Ametukuka na wanayo mshirikisha nayo.

Explanation & meanings · 1
  1. Enyi washirikina! Kuweni na yakini kwamba aliyo kuahidini Mwenyezi Mungu kuwa yatakuwa Siku ya Kiyama yapo karibu kutokea bila ya shaka. Basi msifanye maskhara kwa kuyahimiza yatokee. Mwenyezi Mungu ametakasika na kuwa na mshirika wa kuabudiwa badala yake. Na hiyo miungu mnayo mshirikisha naye haiwezi jambo lolote.

يُنَزِّلُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ بِٱلرُّوحِ مِنۡ أَمۡرِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦٓ أَنۡ أَنذِرُوٓاْ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱتَّقُونِ

Huwateremsha Malaika na Roho kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake ili nyinyi muonye kwamba hapana mungu ila Mimi, basi nicheni Mimi.

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu huteremsha Malaika kwa yanayo huisha nyoyo katika Wahyi wake (ndio hiyo Roho) juu ya anaye mkhiari kumpa Utume katika waja wake, ili watu wajue kwamba hapana mungu wa kuabudiwa kwa Haki ila Mimi. Basi jitengeni na yanayo nikasirisha na yatayo kuleteeni adhabu. Na shikamaneni na ut'iifu ili ukukingeni na adhabu.

خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۚ تَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Ametukuka na wanayo shirikisha.

Explanation & meanings · 1
  1. Yeye ameumba mbingu na ardhi kwa mujibu wa hikima. Ametakasika kuwa na mshirika wa kufanya lolote katika utawala wake, au wa kuabudiwa kama Yeye.

خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِن نُّطۡفَةٖ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٞ مُّبِينٞ

Amemuumba mtu kwa tone la manii. Naye mara amekuwa mshindani dhaahiri.

Explanation & meanings · 1
  1. Amemuumba kila mmoja katika wanaadamu kutokana na maji maji yasiyo shikamana, nayo ni manii. Kutokana na hayo ndio anakuwa mtu mwenye nguvu za kujitetea nafsi yake, mshindani na makhasimu zake, mwenye kuweka wazi hoja zake.

وَٱلۡأَنۡعَٰمَ خَلَقَهَاۖ لَكُمۡ فِيهَا دِفۡءٞ وَمَنَٰفِعُ وَمِنۡهَا تَأۡكُلُونَ

Na nyama hoa amekuumbieni. Katika hao mna vifaa vya kutia joto,na manufaa mengineyo, na baadhi yao mnawala.

Explanation & meanings · 1
  1. Enyi waja! Mwenyezi Mungu amekufadhilini - amekuumbieni nyama hoa, wanyama wa kufuga, kama ngamia, na ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, ili mpate kutokana na sufi zao na manyoa yao vifaa vya kukupatieni joto kujihifadhi na baridi, na mle nyama yao mhifadhi uhai wenu.