Skip to content
النَّحل /

Aya 123

16 : 123
النَّحل Aya 128
Sura · النَّحل
Kiswahili · Barawani
16 : 123

ثُمَّ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ أَنِ ٱتَّبِعۡ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Kisha tukakufunulia ya kwamba ufuate mila ya Ibrahim, mwongofu,wala hakuwa miongoni mwa washirikina.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Nabii! Baada ya Ibrahim kwa karne nyingi, tulikupa Wahyi wewe, na tukakuamrisha umfuate Ibrahim katika wito wake wa kulingania Tawhid, na fadhila njema, na kujiepusha na dini za uwongo. Kwani yeye hakuwa katika wanao mshirikisha Mwenyezi Mungu, kama wanavyo msingizia hawa washirikina.