Skip to content
النَّحل /

Aya 62

16 : 62
النَّحل Aya 128
Sura · النَّحل
Kiswahili · Barawani
16 : 62

وَيَجۡعَلُونَ لِلَّهِ مَا يَكۡرَهُونَۚ وَتَصِفُ أَلۡسِنَتُهُمُ ٱلۡكَذِبَ أَنَّ لَهُمُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ لَا جَرَمَ أَنَّ لَهُمُ ٱلنَّارَ وَأَنَّهُم مُّفۡرَطُونَ

Na wanampa Mwenyezi Mungu wanavyo vichukia wao, na ndimi zao zinasema uwongo kwamba wao watapata mema. Hapana shaka hakika wamewekewa Moto, nao wataachwa humo.

Explanation & meanings · 1
  1. Na washirikina wanamnasibisha Mwenyezi Mungu mabinti na ushirika mambo ambayo wao wanayachukia. Na ndimi zao zinatamka uwongo wanapo dai ya kwamba, kama walivyo kuwa na utajiri na utawala duniani, basi kadhaalika Akhera nao watapata malipo mema kwa Mwenyezi Mungu watapo fufuliwa; nayo ni Pepo! Hapana shaka hao watatiwa Motoni, nao watasukumwa huko kabla ya wengineo.