Skip to content
النَّحل /

Aya 97

16 : 97
النَّحل Aya 128
Sura · النَّحل
Kiswahili · Barawani
16 : 97

مَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَلَنُحۡيِيَنَّهُۥ حَيَوٰةٗ طَيِّبَةٗۖ وَلَنَجۡزِيَنَّهُمۡ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini,tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika mwenye kutenda mema duniani, sawa sawa akiwa mwanamume au mwanamke, akajiingiza katika huo wema kwa nguvu za imani, kwa kila linalo wajibika kwa kuliamini, basi Sisi hatuna budi kumfanya aishi maisha mazuri yasiyo kuwa na machungu, yenye ndani yake ukinaifu na kuridhika na kuvumilia masaibu ya dunia, na shukrani kwa neema anazo zipata kwa Mwenyezi Mungu. Na Akhera hapana budi ya kuwa tutawalipa watu wa namna hii bora ya malipo kwa kuzidi marudufu kwa vitendo vyao vya duniani.