Skip to content
النَّحل /

Aya 37

16 : 37
النَّحل Aya 128
Sura · النَّحل
Kiswahili · Barawani
16 : 37

إِن تَحۡرِصۡ عَلَىٰ هُدَىٰهُمۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي مَن يُضِلُّۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّٰصِرِينَ

Hata ukiwa na pupa ya kutaka kuwaongoa, lakini Mwenyezi Mungu hamwongoi yule anaye shikilia kupotea. Wala hawatapata wa kuwanusuru.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Nabii! Ikiwa una hamu mno ya kuwaongoa washirikina katika watu wako, kwa kutumia ukomo wa juhudi yako, basi usiihiliki nafsi yako kwa huzuni ikiwa hayo uyatakayo hayawi. Kwani hao wamekwisha milikiwa na matamanio. Na Mwenyezi Mungu hawalazimishi kuongoka walio khiari upotovu na wakaushikilia, kwani Yeye huwaacha wajichagulie wenyewe, nao watapata malipo yao, nayo ni adhabu kubwa. Na wala hawatapata Siku ya Kiyama wa kuwanusuru na kuwalinda na adhabu ya Mwenyezi Mungu.