Skip to content
النَّحل /

Aya 60

16 : 60

Aya 60 of النَّحل (16 : 60). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النَّحل Aya 128
Sura · النَّحل
Kiswahili · Barawani
16 : 60

لِلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ مَثَلُ ٱلسَّوۡءِۖ وَلِلَّهِ ٱلۡمَثَلُ ٱلۡأَعۡلَىٰۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Hali ya wasio iamini Akhera ni ovu; na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye sifa tukufu. Naye ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.

Explanation & meanings · 1
  1. Ni hali mbaya ya wasio amini Akhera na yote yaliyoko huko ya thawabu na adhabu, nayo ni ile haja ya kutaka watoto wa kiume na kuchukia watoto wa kike. Na Mwenyezi Mungu ana sifa tukufu. Yeye ni Mkwasi, hahitajii kitu, wala hana haja ya mtoto. Naye ni Mwenye kushinda, Mwenye nguvu, wala hana haja ya msaidizi.