Skip to content
النَّحل /

Aya 25

16 : 25

Aya 25 of النَّحل (16 : 25). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النَّحل Aya 128
Sura · النَّحل
Kiswahili · Barawani
16 : 25

لِيَحۡمِلُوٓاْ أَوۡزَارَهُمۡ كَامِلَةٗ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَمِنۡ أَوۡزَارِ ٱلَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيۡرِ عِلۡمٍۗ أَلَا سَآءَ مَا يَزِرُونَ

Ili wabebe mizigo yao kwa ukamilifu Siku ya Kiyama, na sehemu ya mizigo ya wale wanao wapoteza bila ya kujua. Angalia, ni maovu mno hayo wanayo yabeba!

Explanation & meanings · 1
  1. Wanasema hayo ili wawazuie watu wasimfuate Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na mwisho wa kuishia mambo yao ni kuwa wataadhibiwa Siku ya Kiyama kwa adhabu ya upotovu wao kwa ukamilifu, na adhabu ya baadhi ya watu walio kuwa wakiwakhadaa na kuwadanganya mpaka wakapotea bila ya ilimu wala kuchungua! Zingatia, ewe mwenye kusikia, kwa huu uovu wa madhambi wanayo yafanya, vipi ukali wa adhabu watayo pata!