Skip to content
النَّحل /

Aya 43

16 : 43

Aya 43 of النَّحل (16 : 43). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النَّحل Aya 128
Sura · النَّحل
Kiswahili · Barawani
16 : 43

وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ إِلَّا رِجَالٗا نُّوحِيٓ إِلَيۡهِمۡۖ فَسۡـَٔلُوٓاْ أَهۡلَ ٱلذِّكۡرِ إِن كُنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ

Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi(Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.

Explanation & meanings · 1
  1. Na kabla ya kukutuma wewe, ewe Nabii, kwa umma wako, hatukuwatuma kwa kaumu zilizo tangulia ila watu wanaume tulio wafunulia kwa Wahyi yale tunayo yataka wawafikishie. Wala hatukuwatuma Malaika kama watakavyo makafiri wa kaumu yako. Basi, enyi makafiri, waulizeni wenye kuvijua Vitabu vya mbinguni, kama nyinyi hamyajui hayo. Watajua kuwa Mitume wote wa Mwenyezi Mungu hawakuwa ila wanaadamu, wala si Malaika.