Skip to content
النَّحل /

Aya 111

16 : 111

Aya 111 of النَّحل (16 : 111). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النَّحل Aya 128
Sura · النَّحل
Kiswahili · Barawani
16 : 111

۞ يَوۡمَ تَأۡتِي كُلُّ نَفۡسٖ تُجَٰدِلُ عَن نَّفۡسِهَا وَتُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا عَمِلَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Siku ambayo kila nafsi itakuja jitetea, na kila nafsi italipwa sawa sawa na a'mali ilizo zifanya, nao hawatadhulumiwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Nabii! Watajie watu wako, kwa kuwahadharisha, Siku ambayo kila mtu atakuwa hana linalo mshughulisha ila kujitetea nafsi yake. Hayamshughulishi ya mzazi wala mwana. Siku hiyo ndiyo Siku ya Kiyama! Na Mwenyezi Mungu siku hiyo atailipa kila nafsi malipo ya vitendo iliyo tenda, ikiwa kheri au shari. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu hata mtu mmoja.