16 : 32
ٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ طَيِّبِينَ يَقُولُونَ سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمُ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema, wanawaambia:Amani iwe juu yenu! Ingieni Peponi kwa sababu ya yale mliyo kuwa mkiyatenda.
Explanation & meanings · 1
- Na ndio hao Malaika huzichukua roho zao na hali wamesafika na uchafu wa ushirikina na maasi. Na Malaika watawaambia kwa kuwatuza: Amani kwenu itokayo kwa Mwenyezi Mungu! Baada ya hii leo hamtopata la karaha. Na ifurahieni Pepo mtakayo ingia kwa sababu ya vitendo vyema mlivyo vitanguliza katika dunia yenu.