Skip to content
النَّحل /

Aya 127

16 : 127

Aya 127 of النَّحل (16 : 127). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النَّحل Aya 128
Sura · النَّحل
Kiswahili · Barawani
16 : 127

وَٱصۡبِرۡ وَمَا صَبۡرُكَ إِلَّا بِٱللَّهِۚ وَلَا تَحۡزَنۡ عَلَيۡهِمۡ وَلَا تَكُ فِي ضَيۡقٖ مِّمَّا يَمۡكُرُونَ

Na subiri. Na kusubiri kwako kusiwe ila kwa sababu ya MwenyeziMungu tu. Wala usiwahuzunikie; wala usiwe katika dhiki kwa hila wanazozifanya.

Explanation & meanings · 1
  1. Na ewe Nabii! Subiri! Kwani hivyo ndio yatakusahilikia mengi katika mashaka ya maisha, na yataondoka matatizo yake. Wala usisikitike kwa kuwa watu wako hawaitikii Wito wako, na hawakuamini. Wala usione dhiki kifuani mwako kwa hila zao na vitimbi vyao vya kuukaba roho Wito wako. Kwani vitendo vyao havitakudhuru kitu. Na wewe umekwisha tekeleza waajibu wako, na umemcha Mola wako Mlezi.