Skip to content
النَّحل /

Aya 70

16 : 70

Aya 70 of النَّحل (16 : 70). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النَّحل Aya 128
Sura · النَّحل
Kiswahili · Barawani
16 : 70

وَٱللَّهُ خَلَقَكُمۡ ثُمَّ يَتَوَفَّىٰكُمۡۚ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰٓ أَرۡذَلِ ٱلۡعُمُرِ لِكَيۡ لَا يَعۡلَمَ بَعۡدَ عِلۡمٖ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٞ قَدِيرٞ

Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni; kisha anakufisheni. Na miongoni mwenu wapo wanao rudishwa kwenye umri mbaya kabisa, hata akawa asijue kitu baada ya ujuzi alio kuwa nao. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi na Mweza.

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu amekuumbeni, na amekujaalieni kila mtu na ajali yake. Kati yenu wapo wanao kufa mapema, na wengine wanao fikia ukongwe wakarejea katika hali ya udhaifu. Wakawa wanadhoofika kidogo kidogo, zikipungua nguvu zao za mwili, na mifupa na viungo na mishipa. Mwisho wao wakawa hawajiwezi kujifanyia lolote liwapasalo! Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa siri za kuumba kwake, ni Muweza wa kutimiza alitakalo.