Skip to content
النَّحل /

Aya 126

16 : 126
النَّحل Aya 128
Sura · النَّحل
Kiswahili · Barawani
16 : 126

وَإِنۡ عَاقَبۡتُمۡ فَعَاقِبُواْ بِمِثۡلِ مَا عُوقِبۡتُم بِهِۦۖ وَلَئِن صَبَرۡتُمۡ لَهُوَ خَيۡرٞ لِّلصَّٰبِرِينَ

Na mkilipiza basi lipizeni sawa na vile mlivyo adhibiwa. Na ikiwa mtasubiri, basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanao subiri.

Explanation & meanings · 1
  1. Enyi Waislamu! Mkitaka kuwaadhibu wale wanao kufanyieni uadui wakakuvamieni, basi waadhibuni kwa kadiri walivyo kutendeeni, wala msizidishe kuliko hivyo. Na kuweni na yakini kwamba mkistahamili, msijilipizie kisasi, itakuwa ni kheri zaidi kwenu hapa duniani na Akhera. Basi toeni adhabu kwa ajili ya Haki, wala msiadhibu kwa ajili ya nafsi zenu.