Skip to content
النَّحل /

Aya 107

16 : 107

Aya 107 of النَّحل (16 : 107). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النَّحل Aya 128
Sura · النَّحل
Kiswahili · Barawani
16 : 107

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ ٱسۡتَحَبُّواْ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا عَلَى ٱلۡأٓخِرَةِ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Hayo ni kwa sababu wameyapenda zaidi maisha ya duniani kuliko ya Akhera, na kwa sababu Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri.

Explanation & meanings · 1
  1. Na hiyo ghadhabu na adhabu waliyo stahiki kuipata, ni kwa sababu ya kupenda kwao mno neema za duniani na starehe zake za kupita njia, hata zikawaweka mbali na Haki, na zikawatia upofu wasiione kheri. Basi Mwenyezi Mungu akawaachilia mbali na huo ukafiri wanao upenda. Huo ndio mwendo wake anavyo watendea viumbe vyake, huwaacha kama hawa, na huwaacha asiwahidi kwa sababu ya ufisadi wao wenyewe, na kukakamia katika upotovu.