Skip to content
النَّحل /

Aya 59

16 : 59
النَّحل Aya 128
Sura · النَّحل
Kiswahili · Barawani
16 : 59

يَتَوَٰرَىٰ مِنَ ٱلۡقَوۡمِ مِن سُوٓءِ مَا بُشِّرَ بِهِۦٓۚ أَيُمۡسِكُهُۥ عَلَىٰ هُونٍ أَمۡ يَدُسُّهُۥ فِي ٱلتُّرَابِۗ أَلَا سَآءَ مَا يَحۡكُمُونَ

Anajificha asionekane na watu kwa ubaya wa aliyo bashiriwa! Je,akae naye juu ya fedheha hiyo au amfukie udongoni? Tazama uovu wa wanavyohukumu!

Explanation & meanings · 1
  1. Anajaribu kujificha watu wasiione huzuni ya machungu yaliyo mpata kwa kupewa khabari ya binti aliye zaliwa. Anatapatapa: amwache hai juu ya fedheha anayo iona, kama anavyo jigamba? Au amzike katika udongo naye yuhai mpaka afe? Ewe msikilizaji! Zingatia uwovu wa vitendo vya watu hawa! Na uovu gani wa kumhukumia Mwenyezi Mungu mabinti ambao wao wanawachukia!