10 : 81
فَلَمَّآ أَلۡقَوۡاْ قَالَ مُوسَىٰ مَا جِئۡتُم بِهِ ٱلسِّحۡرُۖ إِنَّ ٱللَّهَ سَيُبۡطِلُهُۥٓ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُصۡلِحُ عَمَلَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ
Walipo tupa, Musa alisema: Mliyo leta ni uchawi. Hakika Mwenyezi Mungu haitengenezi kazi ya waharibifu.
Explanation & meanings · 1
- Walipo tupa kamba zao na fimbo zao, Musa aliwaambia: Huo mlio fanya ni uchawi kweli, na Mwenyezi Mungu Subhanahu atauvunja kwa mkono wangu! Hakika Mwenyezi Mungu hawasahilishii mafisadi vitendo vyao vikawa vizuri na vyenye nafuu.