Skip to content
Yunus /

Aya 57

10 : 57

Aya 57 of Yunus (10 : 57). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Yunus Aya 109
Sura · Yunus
Kiswahili · Barawani
10 : 57

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَتۡكُم مَّوۡعِظَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَشِفَآءٞ لِّمَا فِي ٱلصُّدُورِ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ

Enyi watu! Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na poza kuponyesha yaliyomo vifuani, na uwongofu, na rehema kwa Waumini.

Explanation & meanings · 1
  1. Enyi watu! Kimekujieni kwa ulimi wa Mtume Muhammad Kitabu kilicho toka kwa Mwenyezi Mungu. Ndani yake mna makumbusho ya Imani, na ut'iifu, na mawaidha ya kuhimiza kheri, na kukataza vitendo viovu, na kueleza mzingatie khabari za walio kutangulieni, na kukutakeni muangalie utukufu wa uumbaji ili mpate kuuelewa utukufu wa Muumba. Na ndani ya Kitabu hicho mna dawa ya maradhi ya nyoyo zenu, maradhi ya shirki na unaafiki; na mna uwongofu wa kuendea Njia Iliyo Nyooka. Na yote hayo ni rehema kwa Waumini wanao itikia wito.