Skip to content
البَقَرَة /

Aya 186

2 : 186

Aya 186 of البَقَرَة (2 : 186). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 186

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌۖ أُجِيبُ دَعۡوَةَ ٱلدَّاعِ إِذَا دَعَانِۖ فَلۡيَسۡتَجِيبُواْ لِي وَلۡيُؤۡمِنُواْ بِي لَعَلَّهُمۡ يَرۡشُدُونَ

Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka.

Explanation & meanings · 1
  1. Na Mimi nawajua vyema waja wangu, na najua wanayo yafanya na wanayo yawacha. Na Ewe Muhammad! Wakikuuliza waja wangu wakasema: Hivyo Mwenyezi Mungu yupo karibu nasi hata ajue tunayo yaficha na tunayo yatangaza na tunayo yawacha? Waambie: Mimi ni karibu nao zaidi kuliko wanavyo dhani. Na dalili ya hayo ni kuwa ombi la mwenye kuomba linafika wakati huo huo, na Mimi ndiye ninaye pokea hayo maombi wakati huo huo vile vile. Ilivyo kuwa Mimi nimewaitikia maombi yao basi na wao waniitikie Mimi kwa kuamini na kut'ii, kwani hiyo ndiyo njia ya kuongoka kwao na kusibu kwao.