Skip to content
Orodha ya Sura /

المؤمنُون

المؤمنُون is chapter 23 of the Quran and has 118 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

118 Aya Sura Na. 23
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

قَدۡ أَفۡلَحَ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

HAKIKA wamefanikiwa Waumini!

Explanation & meanings · 1
  1. Kumethibiti kufanikiwa kwa Waumini wanao muamini Mwenyezi Mungu na waliyo kuja nayo Mitume; na wamefuzu kwa wayatakayo.

ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي صَلَاتِهِمۡ خَٰشِعُونَ

Ambao ni wanyenyekevu katika Swala zao!

Explanation & meanings · 1
  1. Hao ambao wameambatisha juu ya Imani yao vitendo vyema. Basi hao katika Swala zao humuelekea Mwenyezi Mungu kwa nyoyo zenye kumkhofu na kumnyenyekea, wanahisi unyenyekevu wa mwisho kwake Yeye .

وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَنِ ٱللَّغۡوِ مُعۡرِضُونَ

Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi!

Explanation & meanings · 1
  1. Hao wanashughulikia mambo ya maana, wanapuuza vitendo na maneno yasiyo na kheri ndani yake.

وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِلزَّكَوٰةِ فَٰعِلُونَ

Na ambao wanatoa Zaka!

Explanation & meanings · 1
  1. Nao wanashikilia kutoa Zaka kuwapa wanao stahiki. Kwa hivyo wanakusanya ibada ya mwili na ibada ya mali, na baina ya kujisafisha nafsi na kuyasafisha mali. "Na ambao wanatoa Zaka,": Huu waajibu wa kutoa Zaka unapelekea kujenga mashikamano ya umoja baina ya Waislamu, na kutia katika moyo wa kila mtu kuwa ana jukumu kwa nduguye, anahisi kama anavyo hisi yeye, na anaungulika kama anavyo ungulika yeye. Kwa hivyo ni waajibu wake kufanya awezavyo kumkinga na balaa za kilimwengu, na machungu ya ukosefu. Kwa hivyo fakiri au masikini hatomchukia tajiri, bali wote watahisi kama ni ukoo mmoja unao saidiana na wenye kushikamana na Kamba ya Mwenyezi Mungu. Wala mwenye deni hakati tamaa kuweza kulipa deni lake lilio bakia ikiwa hana cha kumalizia hilo deni. Wala haianguki chini azma ya mujaahidi anaye pigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuinusuru Dini yake na kukomboa nchi yake kwa sababu ya kukosa mali ya kutimizia makusudio yake. Wala msafiri au mgeni mhitaji aliye mbali na mali yake hakosi wa kumkidhia haja zake kwa kumsaidia mpaka afike kwake. Na juu ya haya Zaka ilikuwa ni njia moja katika njia kubwa ulio chukua Uislamu kukombolea mateka na wafungwa na kuondoa utumwa. Na Uislamu umeongeza kutimiza malengo yake ya kijamii kwa ulimwengu mzima ikatupilia mbali chuki zinazo chusha za kidini, na ikatoa ruhusa Zaka wapewe makafiri ikihitajia haja kuwakopesha. Hali kadhaalika hupewa wale wanao itumikia Zaka, kama kuikusanya na kuigawa. Pia waandishi, na wasafiri, na wanao khasiri kwa ajili ya kupatanisha wenye kugombana, na wanao wasaidia Waislamu katika vita. Ama makusudio ya kiuchumi ya Zaka ni kuondoa ufakiri popote ulipo, na kumsaidia kila mwenye haja kama ilivyo kwisha tangulia.

وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِفُرُوجِهِمۡ حَٰفِظُونَ

Na ambao wanazilinda tupu zao!

Explanation & meanings · 1
  1. Nao wanajihifadhi nafsi zao wasiingiane na wanawake. "Na ambao wanazilinda tupu zao, isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa. Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka." Aya hizi zinaambatana na Aya nyengine ziliomo katika Suratun Nur zilio anzia: "Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mpigeni kila mmoja wao bakora mia." Hakika Aya hizi tukufu zilizo tajwa zinaashiria maovu ya katika umma yanayo tokea kwa uzinzi. Ama katika umma ni kuvurugika nasaba ya watoto isijuulikane, ama katika siha ni sehemu mbili. KWANZA ni katika mwili, mfano wa kisonono, tego, AIDS n.k. Kisonono huweza kuzalisha maradhi ya urithi kwa watoto hata huweza kuleta upofu. Ama tego (Syphilis) huenea katika mishipa ya damu na ya hisiya na huweza kuishia wazimu, na pia huenea mpaka kwa vizazi, na huenda mtoto akafa tumboni au akatoka na kilema. Ama maradhi ya AIDS (Ukimwi) hayo ni maafa yasiyo semeka, Mwenyezi Mungu atulinde nayo. PILI ni kuathirika mishipa ya hisiya na akili, kwani uzinzi huweza kuathiri dhamiri ya mtu, na kuadhibika nayo, na hata mwishoe huweza kuingia wazimu.