23 : 87
سَيَقُولُونَ لِلَّهِۚ قُلۡ أَفَلَا تَتَّقُونَ
Watasema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, hamwogopi?
Explanation & meanings · 1
- Watakiri kuwa huyo ni Mwenyezi Mungu. Basi waambie: Je! Hamwogopi matokeo ya ushirikina wenu na ukafiri wenu na kumuasi kwenu Mwenye uumbaji huu wote mkubwa?