23 : 47
فَقَالُوٓاْ أَنُؤۡمِنُ لِبَشَرَيۡنِ مِثۡلِنَا وَقَوۡمُهُمَا لَنَا عَٰبِدُونَ
Wakasema: Je, tuwaamini wanaadamu wawili hawa kama sisi, na ambao watu wao ni watumwa wetu?
Explanation & meanings · 1
- Wakasema kwa mastaajabu na kukanya: Je, tuuamini wito wa watu wawili walio ni wanaadamu kama sisi, na tena watu wao hawa Wana wa Israili ni wenye kutunyenyekea sisi na kutut'ii kama ni watumwa?