23 : 51
يَٰٓأَيُّهَا ٱلرُّسُلُ كُلُواْ مِنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ وَٱعۡمَلُواْ صَٰلِحًاۖ إِنِّي بِمَا تَعۡمَلُونَ عَلِيمٞ
Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa mnayo yatenda.
Explanation & meanings · 1
- Tumewaambia Mitume wawafikishie watu wao: Kuleni vyakula vya kila namna vya halali na vizuri, na stareheni na ishukuruni neema yangu kwa vitendo vyema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa myatendayo na nitakulipeni kwayo.