Skip to content
المؤمنُون /

Aya 101

23 : 101

Aya 101 of المؤمنُون (23 : 101). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

المؤمنُون Aya 118
Sura · المؤمنُون
Kiswahili · Barawani
23 : 101

فَإِذَا نُفِخَ فِي ٱلصُّورِ فَلَآ أَنسَابَ بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَئِذٖ وَلَا يَتَسَآءَلُونَ

Basi litapo pulizwa baragumu hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo, wala hawataulizana.

Explanation & meanings · 1
  1. Ukifika wakati wa kufufuliwa tutawafufua kutoka makaburini kwao. Na hayo ni kwa mfano wa kupulizwa tarumbeta watafufuka nao wamefarikiana. Hapana mtu utaomfaa ujamaa wake na fulani. (Ujamaa Kiswahili maana yake makhusiano ya nasaba, sio usoshalisti.) Wala hapana mtu atae muomba mtu kitu cha kumfaa. Kwani kila mmoja wao siku hiyo atakuwa kashughulika na lake.