Skip to content
المؤمنُون /

Aya 44

23 : 44

Aya 44 of المؤمنُون (23 : 44). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

المؤمنُون Aya 118
Sura · المؤمنُون
Kiswahili · Barawani
23 : 44

ثُمَّ أَرۡسَلۡنَا رُسُلَنَا تَتۡرَاۖ كُلَّ مَا جَآءَ أُمَّةٗ رَّسُولُهَا كَذَّبُوهُۖ فَأَتۡبَعۡنَا بَعۡضَهُم بَعۡضٗا وَجَعَلۡنَٰهُمۡ أَحَادِيثَۚ فَبُعۡدٗا لِّقَوۡمٖ لَّا يُؤۡمِنُونَ

Kisha tukawatuma Mitume wetu, mmoja baada ya mmoja. Kila umma alipo wafikia Mtume wao walimkanusha. Tukawafuatanisha hawa baada ya hawa, na tukawafanya ni hadithi za kusimuliwa. Wakapotelea mbali watu wasio amini.

Explanation & meanings · 1
  1. Kisha tukawatuma Mitume wetu wakifuatana, kila mmoja kwa kaumu yake. Kila akija Mtume kwa kaumu yake waliukadhibisha wito wake. Nasi tukawateketeza mfululizo, na tukazifanya khabari zao ni hadithi za watu kusimuliana na kuzistaajabia. Basi hao kaumu wasio isadiki Haki wala hawaifuati wametengeka mbali na rehema, na wamehiliki.