23 : 118
وَقُل رَّبِّ ٱغۡفِرۡ وَٱرۡحَمۡ وَأَنتَ خَيۡرُ ٱلرَّٰحِمِينَ
Nawe sema: Mola wangu Mlezi! Samehe na urehemu nawe ni Mbora wa wanao rehemu.
Explanation & meanings · 1
- Na sema, ewe Nabii, ukimlingania Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea: Ewe Mola wangu Mlezi! Nisamehe dhambi zangu, na nirehemu. Kwani Wewe ni Mbora wa wanao rehemu, kwa sababu rehema yako imeenea na ipo karibu kwa watendao mema.