Skip to content
Orodha ya Sura /

آل عِمران

آل عِمران is chapter 3 of the Quran and has 200 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

200 Aya Sura Na. 3
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

الٓمٓ

Alif Laam Miim.

Explanation & meanings · 1
  1. "Alif Laam Miim", yaani "A.L.M." ni harufi za kutamkwa na kusikilizana kwa sauti. Zimeletwa kubainisha kuwa hii Qur'ani ya miujiza imetokana na hizi hizi harufi zinazo tamkwa, ili watu watanabahi na wasikilize.

ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَيُّ ٱلۡقَيُّومُ

Mwenyezi Mungu, hakuna mungu ila Yeye Aliye Hai, Msimamizi wa yote milele.

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu ni Mmoja, hapana mungu isipo kuwa Yeye. Na kila kiliomo ulimwenguni kinashuhudia hayo kwa namna ya kilivyo umbika na kushikamana, katika umbo na kazi, na viumbe vyenginevyo. Na Yeye Mwenyezi Mungu ni Yuhai, hafi. Ni Mwenye kusimamia na kuendesha mambo yote ya ulimwengu. Yeye ndiye Mwenye kuyadabiri (kuyaendesha) na kuyasarifu.

نَزَّلَ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَأَنزَلَ ٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَ

Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili .

Explanation & meanings · 1
  1. Umeteremshiwa wewe, Muhammad, hii Qur'ani yenye kukusanya ukweli wa misingi yote ya Sharia ya Mbinguni iliomo katika Vitabu vilivyo tangulia. Na hakika kabla ya Qur'ani Mwenyezi Mungu alikwisha teremsha Taurati kwa Musa, na Injili kwa Isa.

مِن قَبۡلُ هُدٗى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ ٱلۡفُرۡقَانَۗ إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ لَهُمۡ عَذَابٞ شَدِيدٞۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٞ ذُو ٱنتِقَامٍ

Kabla yake, ziwe uwongofu kwa watu. Na akateremsha Furqani (Upambanuo). Hakika walio zikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu watakuwa na adhabu kali. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye kulipa.

Explanation & meanings · 1
  1. Ameziteremsha hizo kabla ya Qur'ani ili kuwaongoa watu. Walipo kengeuka akaiteremsha Qur'ani ipambanue baina ya Haki na baat'ili, baina ya kweli na uwongo, baina ya uwongofu na upotovu. Basi hii Qur'ani ni Kitabu cha kweli, chenye kudumu milele. Na kila mwenye kuacha aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu na akazikanya Aya zake, Ishara zake, atapata adhabu iliyo kali. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza, hashindwi na kitu, na Mwenye kuwalipa wanao stahiki kulipwa.

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَخۡفَىٰ عَلَيۡهِ شَيۡءٞ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِي ٱلسَّمَآءِ

Hakika Mwenyezi Mungu hakifichiki chochote kwake, duniani wala mbinguni.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. Kwa hivyo hapana kinacho fichika kwake katika Ardhi na hata katika Mbingu, kikiwa kidogo au kikubwa, kinacho onekana na kisicho onekana.