Skip to content
آل عِمران /

Aya 19

3 : 19

Aya 19 of آل عِمران (3 : 19). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

آل عِمران Aya 200
Sura · آل عِمران
Kiswahili · Barawani
3 : 19

إِنَّ ٱلدِّينَ عِندَ ٱللَّهِ ٱلۡإِسۡلَٰمُۗ وَمَا ٱخۡتَلَفَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلۡعِلۡمُ بَغۡيَۢا بَيۡنَهُمۡۗ وَمَن يَكۡفُرۡ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika Dini ya Haki aliyo iridhi Mwenyezi Mungu ni Dini ya Tawhidi, ya Mungu Mmoja, na kumnyenyekea Yeye kwa usafi wa moyo. Mayahudi na Wakristo wamekhitalifiana na Dini hii, wakazua na wakabadilisha. Na wala kukhalifu kwao hakukuwa kwa kudanganyikiwa au kwa ujinga ilipo wajia ilimu, bali yalikuwa hayo kwa uhasidi na ushindani tu. Na mwenye kupinga Ishara za Mwenyezi Mungu, basi na angojee hisabu ya Mwenyezi Mungu, nayo yenda kasi mno.