Skip to content
آل عِمران /

Aya 90

3 : 90

Aya 90 of آل عِمران (3 : 90). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

آل عِمران Aya 200
Sura · آل عِمران
Kiswahili · Barawani
3 : 90

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بَعۡدَ إِيمَٰنِهِمۡ ثُمَّ ٱزۡدَادُواْ كُفۡرٗا لَّن تُقۡبَلَ تَوۡبَتُهُمۡ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلضَّآلُّونَ

Hakika wale walio kufuru baada ya kuamini kwao, kisha wakazidi kukufuru, toba yao haitakubaliwa, na hao ndio walio potea.

Explanation & meanings · 1
  1. Kukubaliwa toba na kupata rehema ya maghfira kunashurutishwa mtu adumu juu ya Imani. Wanao ipinga Haki baada ya ut'iifu na kusadiki, na wakazidisha upinzani na ufisadi na kuwaudhi Waumini, Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la hatokubali toba yao. Haiwezi kuwa toba yao hiyo ni kweli na safi na hali wanaendelea na vitendo vyao, wapo mbali na Haki na wanaigeuzia nyuso zao.