Skip to content
آل عِمران /

Aya 187

3 : 187

Aya 187 of آل عِمران (3 : 187). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

آل عِمران Aya 200
Sura · آل عِمران
Kiswahili · Barawani
3 : 187

وَإِذۡ أَخَذَ ٱللَّهُ مِيثَٰقَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ لَتُبَيِّنُنَّهُۥ لِلنَّاسِ وَلَا تَكۡتُمُونَهُۥ فَنَبَذُوهُ وَرَآءَ ظُهُورِهِمۡ وَٱشۡتَرَوۡاْ بِهِۦ ثَمَنٗا قَلِيلٗاۖ فَبِئۡسَ مَا يَشۡتَرُونَ

Na pale Mwenyezi Mungu alipo fungamana na walio pewa Kitabu kuwa: Lazima mtawabainishia watu, wala hamtokificha, walikitupa nyuma ya migongo yao, na wakanunua kwacho thamani duni. Basi ni kiovu hicho walicho nunua.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Nabii! Kumbuka na utaje pale Mwenyezi Mungu alipo chukua ahadi madhbuti kwa Watu wa Kitabu, kuwa wayaeleze wazi maana ya Kitabu chao, na wala wasiwafiche watu chochote, na wao wakakitupilia mbali nyuma ya migongo yao, na badala yake wakatafuta starehe za dunia. Na starehe za dunia kama zitakavyo kuwa ni kitu chenye thamani duni kabisa kulinganisha na uwongofu na uwongozi. Ama wamejua kutenda uovu! (Hayo yalikuwa zamani na bado yanaendelea. Kuficha na kugeuza na kupotosha Biblia hakusiti. Vipo vitabu vyao vinavyo itwa "Apokrifa", maana yake "Vilivyo fichwa", kwa kuwa hivyo ni marfuku visisomwe ila na mapadri tu, na vingine vimeteketezwa. Miongoni mwa hivyo ni Injili ya Barnaba.)