Skip to content
آل عِمران /

Aya 21

3 : 21
آل عِمران Aya 200
Sura · آل عِمران
Kiswahili · Barawani
3 : 21

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَيَقۡتُلُونَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ بِغَيۡرِ حَقّٖ وَيَقۡتُلُونَ ٱلَّذِينَ يَأۡمُرُونَ بِٱلۡقِسۡطِ مِنَ ٱلنَّاسِ فَبَشِّرۡهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ

Hakika wanao zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakawauwa Manabii pasipo haki, na wakawauwa watu waamrishao Haki wabashirie adhabu kali.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika wale wanao zipinga Ishara za Mwenyezi Mungu katika uumbaji na hizi zilizo teremka, na wakawauwa Manabii alio watuma Mwenyezi Mungu waje kuwaongoa - bila ya haki kabisa, na hiyo ni dhulma kubwa mno - na wakawauwa wale wanao waita watu wafanye haki na uadilifu, watu hao wanastahiki adhabu kali. Basi wabashirie adhabu hiyo!