Skip to content
آل عِمران /

Aya 79

3 : 79

Aya 79 of آل عِمران (3 : 79). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

آل عِمران Aya 200
Sura · آل عِمران
Kiswahili · Barawani
3 : 79

مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُؤۡتِيَهُ ٱللَّهُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحُكۡمَ وَٱلنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُواْ عِبَادٗا لِّي مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِن كُونُواْ رَبَّٰنِيِّـۧنَ بِمَا كُنتُمۡ تُعَلِّمُونَ ٱلۡكِتَٰبَ وَبِمَا كُنتُمۡ تَدۡرُسُونَ

Haiwezi kuwa mtu aliye pewa na Mwenyezi Mungu Kitabu na hikima na Unabii kisha awaambie watu: Kuweni wa kuniabudu mimi badala ya Mwenyezi Mungu. Bali atawaambia: Kuweni wenye kumuabudu Mola Mlezi wa viumbe vyote, kwa kuwa nyinyi mnafundisha Kitabu na kwa kuwa mnakisoma.

Explanation & meanings · 1
  1. Si akili wala haimfalii mwanaadamu aliye teremshiwa Kitabu na Mwenyezi Mungu na akapewa ilimu ya manufaa na kuweza kuzungumza mambo yanayo tokana na Mwenyezi Mungu, tena awatake watu wamuabudu yeye badala ya kumuabudu Mwenyezi Mungu. Lakini linalo ingia akilini, na lifaalo, ni kuwa yeye awatake watu wamsafie ibada Mola wao Mlezi aliye waumba kwa mujibu alivyo wafunza kutokana na ilimu ya Kitabu na kwa mujibu ya wanayo soma.