3 : 173
ٱلَّذِينَ قَالَ لَهُمُ ٱلنَّاسُ إِنَّ ٱلنَّاسَ قَدۡ جَمَعُواْ لَكُمۡ فَٱخۡشَوۡهُمۡ فَزَادَهُمۡ إِيمَٰنٗا وَقَالُواْ حَسۡبُنَا ٱللَّهُ وَنِعۡمَ ٱلۡوَكِيلُ
Walio ambiwa na watu: Kuna watu wamekukusanyikieni, waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa.
Explanation & meanings · 1
- Hao ndio walio tiwa khofu na watu kwa kuwaambia: Maadui zenu wamekusanya jeshi kubwa kukupigeni, basi waogopeni. Na wao hawakudhoofika wala hawakulegea, bali walizidi Imani ya Mwenyezi Mungu na wakawa na moyo kuwa atawanusuru. Jawabu yao ikawa: Mwenyezi Mungu anatutosheleza. Yeye ndiye aliye tawala mambo yetu. Na Yeye ndiye anaye tegemezwa mambo yote.