Skip to content
آل عِمران /

Aya 185

3 : 185
آل عِمران Aya 200
Sura · آل عِمران
Kiswahili · Barawani
3 : 185

كُلُّ نَفۡسٖ ذَآئِقَةُ ٱلۡمَوۡتِۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوۡنَ أُجُورَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۖ فَمَن زُحۡزِحَ عَنِ ٱلنَّارِ وَأُدۡخِلَ ٱلۡجَنَّةَ فَقَدۡ فَازَۗ وَمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَآ إِلَّا مَتَٰعُ ٱلۡغُرُورِ

Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kaamili Siku ya Kiyama. Na atakaye epushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu.

Explanation & meanings · 1
  1. Hapana hivi wala hivi, kila nafsi lazima ionje Mauti. Na ikiwa hapa duniani mtapata machungu basi Siku ya Kiyama mtalipwa thawabu kwa ukamilifu. Na mwenye kuukaribia Moto akaepushwa nao basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe yenye kupita, haina dawamu.