Skip to content
آل عِمران /

Aya 38

3 : 38

Aya 38 of آل عِمران (3 : 38). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

آل عِمران Aya 200
Sura · آل عِمران
Kiswahili · Barawani
3 : 38

هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُۥۖ قَالَ رَبِّ هَبۡ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةٗ طَيِّبَةًۖ إِنَّكَ سَمِيعُ ٱلدُّعَآءِ

Pale pale Zakariya akamwomba Mola wake Mlezi, akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unaye sikia maombi.

Explanation & meanings · 1
  1. Zakariya a.s. alipo iona neema ya Mwenyezi Mungu kwa Maryamu alimwelekea Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu akimwomba kwa fadhila yake na ukarimu wake na uwezo wake, naye ampe mtoto mwanamume. Kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia maombi ya mwenye kuomba kwake kwa unyenyekevu. Naye ni Muweza wa kuitikia maombi na hata zinge kuwapo pingamizi za kikawaida kama ukongwe na utasa.