Skip to content
آل عِمران /

Aya 39

3 : 39

Aya 39 of آل عِمران (3 : 39). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

آل عِمران Aya 200
Sura · آل عِمران
Kiswahili · Barawani
3 : 39

فَنَادَتۡهُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَهُوَ قَآئِمٞ يُصَلِّي فِي ٱلۡمِحۡرَابِ أَنَّ ٱللَّهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحۡيَىٰ مُصَدِّقَۢا بِكَلِمَةٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَسَيِّدٗا وَحَصُورٗا وَنَبِيّٗا مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Alipo kuwa kasimama chumbani akiswali, Malaika kamnadia: Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya, ataye kuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni bwana na mt'awa na Nabii kwa watu wema.

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu aliitikia dua yake. Malaika akamnadia naye kasimama pahala pake pa ibada akimwelekea Mola wake Mlezi kumbashiria mtoto mwanamume jina lake Yahya, atakaye muamini Isa a.s. ambaye atazaliwa kwa kauli ya Mwenyezi Mungu kwa njia isiyo ya dasturi. Na Yahya atawahimiza kaumu yake kushika ilimu na kuswali, na atakataza mambo ya pumbao na matamanio, na atamfanya awe miongoni mwa Manabii na watu wema.