Skip to content
آل عِمران /

Aya 36

3 : 36
آل عِمران Aya 200
Sura · آل عِمران
Kiswahili · Barawani
3 : 36

فَلَمَّا وَضَعَتۡهَا قَالَتۡ رَبِّ إِنِّي وَضَعۡتُهَآ أُنثَىٰ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا وَضَعَتۡ وَلَيۡسَ ٱلذَّكَرُ كَٱلۡأُنثَىٰۖ وَإِنِّي سَمَّيۡتُهَا مَرۡيَمَ وَإِنِّيٓ أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ

Basi alipo mzaa alisema: Mola wangu Mlezi! Nimemzaa mwanamke - na Mwenyezi Mungu anajua sana aliye mzaa - Na mwanamume si sawa na mwanamke. Na mimi nimemwita Maryamu. Nami namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde na Shet'ani aliye laaniwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Alipo jifungua mimba akasema kwa kujiudhuru kumwambia Mola wake Mlezi: Niliye mzaa ni mwanamke - na Mwenyezi Mungu anajua vilivyo alicho kizaa, na kuwa mwana wenyewe ni mwanamke ni bora kuliko alivyo taka mama kuwa awe mwanamume. Akasema yule mama: Mimi nimemwita Maryamu, na mimi nakuomba umlinde yeye na ukoo wake na uharibifu wa Shetani maluuni.