Skip to content
آل عِمران /

Aya 31

3 : 31

Aya 31 of آل عِمران (3 : 31). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

آل عِمران Aya 200
Sura · آل عِمران
Kiswahili · Barawani
3 : 31

قُلۡ إِن كُنتُمۡ تُحِبُّونَ ٱللَّهَ فَٱتَّبِعُونِي يُحۡبِبۡكُمُ ٱللَّهُ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡ ذُنُوبَكُمۡۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu.

Explanation & meanings · 1
  1. Sema: Ikiwa nyinyi ni wakweli katika madai yenu, kuwa mnampenda Mwenyezi Mungu na mnataka Mwenyezi Mungu akupendeni, basi nifuateni mimi kwa ninayo kuamrisheni na ninayo kukatazeni. Kwani mimi nimetumwa na Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu atakupendeni kwa hivyo, na atakulipeni kwa kukufanyieni hisani na kusamehe makosa yenu. Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kuwasamehe na kuwarehemu waja wake.