Skip to content
آل عِمران /

Aya 146

3 : 146

Aya 146 of آل عِمران (3 : 146). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

آل عِمران Aya 200
Sura · آل عِمران
Kiswahili · Barawani
3 : 146

وَكَأَيِّن مِّن نَّبِيّٖ قَٰتَلَ مَعَهُۥ رِبِّيُّونَ كَثِيرٞ فَمَا وَهَنُواْ لِمَآ أَصَابَهُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَمَا ضَعُفُواْ وَمَا ٱسۡتَكَانُواْۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلصَّٰبِرِينَ

Na Manabii wangapi walipigana na pamoja nao Waumini wengi wenye ikhlasi! Hawakufanya woga kwa yaliyo wasibu katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawakudhoofika wala hawakuwa wanyonge. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wanao subiri.

Explanation & meanings · 1
  1. Na Manabii wangapi wamepigana vita na pamoja nao Waumini wengi wenye ikhlasi kwa Mola wao Mlezi! Nyoyo zao hazikuingia woga, wala azma zao hazikudahadari, wala hawakuwanyenyekea maadui zao kwa sababu ya masaibu yaliyo wapata katika Sabili Llahi, Njia ya Mwenyezi Mungu. Haya ni kwa sababu wamo katika ut'iifu wake, na Mwenyezi Mungu huwalipa wanao vumilia ikiwafika balaa.