3 : 16
ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَآ إِنَّنَآ ءَامَنَّا فَٱغۡفِرۡ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ
Ambao husema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumeamini, basi tufutie madhambi yetu, na tuepushe na adhabu ya Moto,
Explanation & meanings · 1
- Malipo haya watayapata wale ambao nyoyo zao zimejaa Imani, na wakatangaza kwa ndimi zao wakisema kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu: Mola Mlezi wetu! Hakika sisi tumeamini kwa kuitikia wito wako. Basi tusamehe dhambi zetu, na utuhifadhi na adhabu ya Moto.