3 : 108
تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱللَّهِ نَتۡلُوهَا عَلَيۡكَ بِٱلۡحَقِّۗ وَمَا ٱللَّهُ يُرِيدُ ظُلۡمٗا لِّلۡعَٰلَمِينَ
Hizi ni Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki. Na Mwenyezi Mungu hataki kuwadhulumu walimwengu.
Explanation & meanings · 1
- Na hizo Aya zilizo kuja za kueleza kuwa mwema na mwovu watalipwa tunakusomea, nazo zimekusanya haki na uadilifu. Na Mwenyezi Mungu hataki kumdhulumu yeyote kati ya watu na majini.